ZIJUE SIRI ZA UFALME WA GIZA!.
ZIJUE SIRI ZA UFALME WA GIZA!. Na Nickoso Mabena Bwana Yesu asifiwe Mtu wa Mungu Popote pale Ulipo, ninayo furaha leo hii kukuletea Ujumbe wa Neno la Mungu, Ujumbe huu ni Muhimu sana kwa Kila Mwanadamu aweze kuupata. Ninamshukuru Mungu pia kwa ajili ya watu wake aliowatumia kuniuliza Maswali, na wengine kunishauri niandae Somo kama hili, na hiyo yote ilikuja Baada ya Siku Moja kuandika Ujumbe Uliohusu UPASUAJI NA MATATIZO YA MATUMBO KWA WANAWAKE, na Niliandika kwenye ujumbe ule ya Kwamba hizo ni roho kutoka Kuzimu!. Watu wengi walinitaka nielezee maana ya roho kutoka kuzimu.. Somo hili nimeliita Zijue Siri za Ufalme wa Giza, na leo hii nataka nianze na Utangulizi tu wa Somo hili, ili upate Picha japo kwa kidogo, vitu nitakavyofundisha! NAMUOMBA MUNGU KWA AJILI YAKO ILI UPATE UFAHAMU WA KIROHO 👉Tunapaswa kujua ya Kwamba kuna Falme kuu Mbili katika Ulimwengu wa roho, 1.Ufalme wa Nuru 2.Ufalme wa Giza Falme hizi zinatenda Kazi na kuratibu Mambo mengi sana tunayoyaona na...