Utume
wa Kanisa unafupishwa kwa maneno ya Kristo katika Injili ya Marko
anaposema “Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila
kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa” (Mk
16:15 – 16). Utume huu si jambo jingine bali ni uendelezaji wa habari
njema ya wokovu ambayo Bwana wetu Yesu Kristo kwa hiyo aliutwaa
ubinadamu wetu na kukaa katikati yetu. Habari hiyo ni “kuwahubiria
maskini habari njema ... kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao na
vipofu kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa na kutangaza mwaka wa Bwana
uliokubaliwa (Lk 4:18 – 19). Hii inamaanisha kwamba utume wa Kanisa
unapaswa kujikita katika kumwangalia mwanadamu aliyejeruhiwa, kumganga
na kumfanya apate nafuu na kuiona tena huruma ya Mungu. Wajibu huu kama
tunavyosisitiziwa sana katika mwaka huu wa Jubilei ya huruma ya Mungu
huonekana vizuri zaidi kwa kuwaangalia wale waliosukumiziwa pembezoni na
ambao sauti zao haziwezi kusikika. Mfano wa hawa ni yatima, wajane na
wanyonge wengi katika jamii ya mwanadamu.
Somo la Injili la Dominika hii lina tuwekea tukio hilo la kutumwa.
Yesu anawatuma watu sabini mbili wamtangulie kule ambapo anakusudia
kwenda. Hii ni ishara nzuri ya utume wa Kanisa kwamba unaanzia kwa Mungu
mwenyewe na lengo lake ni kwenda kumfanyia makao huko anapotuma.
“Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana
wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake”. Huu ndiyo wito kwa
Kanisa katika kuwaunda watenda kazi ambao watatumwa kuvuna shambani mwa
Bwana. Jamii ya mwanadamu inayo mahitaji mengi ambayo bado yanahitaji
kuipokea habari njema, kufunguliwa na kupewa mwanga na zaidi wanahitaji
kuuona uso wa Mungu wenye huruma. Jukumu linalotolewa kwa Kanisa ni
kuutangaza Ufalme wa Mungu hapa duniani, ufalme ambao ni wa amani,
ufalme wenye nguvu, ufalme wa haki na wa milele (Rej Is 9:6 – 7). Kanisa
linatumwa kufanya utume wa kuukarabati ubinadamu uliochakaa.
Somo la Injili linaendelea kuonesha mazingira halisi ya utume huo.
“Enendeni, angalieni, nawatuma kama Kondoo kati ya mbwa-mwitu”. Muktadha
huu unatudai sisi kama Kanisa kuwa na ujasiri na uangalifu. Ni
mazingira kinzani ambapo tunaelekezwa kuutekeleza huu utume wetu. Adui
shetani hana raha tena kwa sababu ya Ufalme huu unaoletwa duniani na
zaidi anatutambua sisi wanadamu katika udhaifu wetu. Pengine udhaifu wa
kukata tamaa mapema, au kupenda zaidi mali, vyeo, madaraka na pesa.
Kristo anatutaadharisha kwamba “angalieni”. Tambueni nguvu mlizo nazo
kama Kondoo na hivyo mbele ya mbwa-mwitu mnahitaji nguvu za ziada. Pia
anawaambaia kuwa mbele ya mbwa-mwitu ni ujasiri tu wa kipekee
unahitajika kusudi kuweza kusonga mbele. Hapa inadokezwa nafasi ya
msaada wa kimungu ambao ni neema zake zitakazotupatia ujasiri wa kusonga
mbele na kuutimiza utume huu. Hivyo agizo hili “angalieni” ni wito wa
kubaki tumeungana na Mungu katika Neno lake, Sala na Sakramenti. Tukio
hili la Kondoo kupambana na mbwa-mwitu si la kawaida lakini kwa uwezo wa
Mungu tutashinda.
Ujumbe tunaotumwa kuutangaza ni amani. “Na nyumba yoyote
mtakayoingia, semeni kwanza Amani iwemo nyumbani humu”. Amani
wanayotumwa kuitangaza ni amani ya Kristo Mfufuka. Amani hiyo si kama
ile ya ulimwengu ambayo imejikita katika vitu, madaraka na umaarufu wa
kibinadamu bali ni amani ile ya kuwa na Mungu ndani mwako. Amani
tunayopewa na Kristo inaambatana na Upendo na huruma yake. Ni amani
ambayo inatupatanisha tena na Mungu na mwanadamu mwenzetu na hivyo
kutufanya kuishi kindugu kweli kweli bila kujali kupata kitu kuzidi
wengine. Ni amani ambayo daima inanuia mema kwa wengine. Hiyo ndiyo
amani inayoletwa na Kristo na ambayo tunatumwa kwenda kuitangaza, na
hiyo ndiyo amani ambayo mwanadamu katika hali ya dhambi ameipoteza na
yupo katika hamu kubwa ya kuwa na amani hiyo.
Uthabiti katika mafundisho ni muhimu sana kwa sisi kama wanakanisa
katika kuutekeleza utume wetu. “Msihame-hame kutoka nyumba hii kwenda
nyumba hii”. Pale mtume wa Kristo anaposhindwa kueleweka kama kweli yeye
ni wa moto au wa baridi hapo ndipo anapoteza sifa ya kuwa mtumishi
mwaminifu. Hatupaswi kuwa kama bendera inayofuta upepo. Leo hii unasema
hili na kesho unatenda hili. Hili ni onyo la kuepa kufanya utume kwa
ajili kuwafurahisha wale unaowatumikia. Mara nyingi sisi kama wanakanisa
huingia katika vishawishi vya kutaka kusawazisha mapokeo au mazoea
mahalia na Injili ya Kristo kwa kusudi tu na kuepuka mafarakano nao.
Injili tunayoitangaza inakosa nguvu kwani leo tunaipambanua katika namna
hii na kesho kwa namna ile. Namna hii ya utumishi haitatupatia ufanisi
wa kweli.
Mwisho Injili ya leo inatutaka kushirikiana na tunaowahudumia katika
maisha yao ya kila siku. “Na mji wowote mtakaouingia, wakiwakaribisha,
vileni vyakula viwekwavyo mbele yenu; wapoozeni wagonjwa waliomo,
waambieni, Ufalme wa Mungu umekaribia”. Hii inaunganika vizuri na
tunaloambiwa katika somo la kwanza la leo, juu ya Yerusalemu mpya ambayo
ni sababu ya furaha kwa wote. Kanisa linakuwa kama Yerusalemu mpya pale
tu linapoingia katika maisha ya kawaida ya mwanadamu na kumgusa katika
maisha yake ya kawaida kwa kumfunulia ufalme wa mbinguni. Ndiyo hiyo
habari njema ambayo wanahitaji kuisikia wanadamu na kwa habari hiyo
kweli watapata kufurahi na kushangilia, kunyonya na kushibishwa kwa
maziwa ya faraja zake na kukama na kufurahiwa kwa wingi wa utukufu wake.
Somo hilo la kwanza linatuwekea taswira mbalimbali ambazo zinapaswa
kuambatana na utume wetu. Moja ya taswira hiyo ni “mfano wa mama
anayefariji mtoto wake juu ya magoti yake”. Hivyo utangazaji wetu wa
ufalme wa Mungu katikati ya jamii ya mwanadamu inapaswa kujikita katika
kuwaganga wagonjwa wa kiroho na kimwili, kuwafungua waliofungwa na
kongwa la utumwa wa shetani na kuwaangazia wale ambao wapo katika giza
na wamepoteza kabisa matumaini. Tuingie nyumbani mwao na kula
vinavyowekwa mbele yetu, yaani tupokee hayo machungu yao na kuyahisi
sawasawa ndani mwetu na kisha tuwasadie kuwatoa huko na hilo ndilo
tangazo letu kwao ya kwamba ufalme wa Mungu umekaribia.
Mtume Paulo katika somo la pili anatupatia msingi ambao ni Msalaba wa
Kristo. “Mimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu chochote ila msalaba
wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambao kwa huo ulimwengu unasulubiwa kwangu,
na mimi kwa ulimwengu”. Watakatifu wengi walichota nguvu zao za
kuutekeleza utume wao kupitia juhudi zao za kujiunganisha na msalaba wa
Kristo. Padre Pio aliwahi kusema maneno haya juu ya msalaba: “Jambo hili
nimelitamani kwa moyo wangu wote, kuujua, kuupenda na kuuishi msalaba.
Kwa maana katika msalaba kuna wokovu”. Kadiri ya mafundisho ya Mtakatifu
Thomaso wa Akwino tunaambiwa kwamba katika msalaba tunajifunza fadhila
za unyenyekevu, utii, uvumilivu, msamaha, ujasiri na katika ujumla wake
upendo. Ni kwa njia ya faadhila hizi ndipo tunaweza kupata ujasiri wa
kutoka kama Kondoo na kupita kati ya mbwa-mwitu na kuwatangazia watu
kwamba Ufalme wa Mungu umekaribia.
Tuombe neema ya Mungu katika Dominika hii kusudi kwa msaada wake
tuweze kweli kuwa mawe hai ya kuijenga Yerusalemu mpya, yaani Kanisa, na
hivyo kuutangaza Ufalme wake kwa watu wote.
Kutoka studio za Radio Vatican ni mimi Padre Joseph Mosha.
Na Peter Mabula. Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU. BWANA YESU atukuzwe. Karibu tujifunze na tuombe maombi ya ushindi sana. Yeremia 15:20-21 '' Nami nitakufanya kuwa kama ukuta wa boma la shaba juu ya watu hawa; nao WATAPIGANA NAWE; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, ili nikuokoe, na kukuponya, asema BWANA. Nami nitakuokoa na mkono wa watu wabaya, nami nitakukomboa katika mkono wao wenye kutisha. ' ' Neno la MUNGU linasema kwamba adui zako katika ulimwengu wa roho watapigana na wewe. Maana yake wewe na adui zako kwenye ulimwengu wa roho mtapigana. Katika mapigano au vita kuna mambo mawili; kuna kushinda na kuna kushindwa. Lakini ashukuriwe MUNGU maana ukiwa katika wokovu wake utashinda. Ukiwa muombaji sahihi hakika utashinda. Changamoto ya wakristo wengi huwa hawapigani na adui kimaombi bali wanamkemea tu adui. Kwenye ndoto najua kabisa ni mara nyingi sana umeonyeshwa juu ya vita inayokukabili. Najua kabisa kwenye ...
Na Peter M Mabula. Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU. BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Kanisa ni jumuia ya Wakristo. Kanisa ni watu walioitwa na kutengwa na mambo ya dhambi. 1 Kor 6:17-18 '' Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema BWANA, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa BABA kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,'' Maandiko hayo ni sehemu tu ndogo ya maandiko yanayolitambulisha Kanisa la KRISTO duniani. Kanisa hai wametengwa na uovu wa dhambi na wametengwa na mambo ya kidunia yaliyo machukizo(Machafu). Ndio maana huwezi kumuona Askofu akiwa disko akicheza. Huwezi kumuona Mkristo aliyeokoka akiwa kwa mganga wa kienyeji. Huwezi kumuona Mchungaji anatoa talaka. Huwezi kumuona Mteule wa MUNGU akivuta sigara wala bangi na tena huwezi kumuona mteule wa KRISTO akitumia madawa ya kulevya. Huwezi kuona kanisa wakichukua mapanga na mikuki wakienda kul...
0 Comments