Salam
wapendwa katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo.
Leo
nipo hapa kuwaletea topic mpya kabisa ambayo wachungaji wengi hawaifundishi
makanisani na yamkini baadhi yao hawaijui.kama kichawa cha habari kinavyosema,
leo nataka kuzungumza juu ya wachawi.kunawatu wengi sana Duniani wanalia kila
wanavyojaribu kuyakwamua maisha yao inashindikana, lakini hawajui ni kwa nini?
nataka nikuambie leo, wapo watu ambao Mungu ameamua kuwanyima mali kwa makusudi
anayoyajua yeye mwenyewe, na kuna watu ambao Mungu hakuwanyima mali mpango wa
mungu ni kwamba watu hawa wapate mali lakini hawana! hapa ni kwamba shetani
huamua kuwaonea na kuwadhulumu watu hawa. Unajua kila mmoja wetu anakitu
alichopewa na Mungu ili kuweza kuzikamilisha shughuli za ulimwengu huu. ngoja
nikupe siri moja kuu sana, kila mwanadamu anapozaliwa huwa anakitu kinachoitwa
nyota, kitu hiki ni ishara au ni kitambulisho cha mtu huyo katika ulimwengu wa
roho ya kuwa yeye kapewa nini hapa duniani,soma mathayo 2:1-5.biblia inasema
“Yesu alipozaliwa zamani za mfalme herode mamajusi wa mashariki walikwenda
kumwona, na walipofika wakauliza yuko wapi aliyezaliwa mfalme maana tuliiona
nyita yake nasi tumekuja kumsujudia. Ukisikia mamajusi ujue si watu wema.
kasome biblia ya kiingereza imesema ‘Astrologers’ yaani wabashiri au wanaanga.
pia biblia ya NIV imesema Maggi, yaani washirikina, biblia nyinge imesema the
Meggicians yaani wachawi.kwa tafsri hizi moja kwamoja tunatambua kwamba hawa
mamajusi kuwa ni wachawi. Sasa rejea katika kauli yao walipofika kwa Yesu
walisema “Yuko wapi waliyezaliwa mfalme maana tuliiona nyota yake nasi tumekuja
kumsujudia” mpendwa wangu sasa naomba ufungue akili yako ili Mungu akusaidie.
watu hawa ni wachawi, lakini cha ajabu wanasema wameiona nyota ya Yesu wakajua
ya kuwa aliyezaliwa ni mfalme. kwa hiyo tunajifunza kwamba kumbe wachawi
wanauwezo wa kutazama katika ulimwengu wa roho na kutambua kwamba wewe unanyota
gani katika maisha yako.
Si
kwamba walikosea kwa Yesu kusema kwamba Yesu ni mfalme, walisema kweli kabisa
rejea kauli za Bwana wetu alipokuwa kwa pilato aliulizwa wewe ndiye mfalme wa
wayahudi hakukataa bali alijibu wewe wasema.pia akaongeza kusema kwamba ufalme
wangu si dunia hii. kwa hiyo ni mfalme. pia ukirejea katika Isaya 9:6 biblia
inasema na uweza wakifalme utakuwa mabegani mwake; Hivyo basi wachawi
wakishatazama katika ulimwengu wa roho na kuona nyota yako kuwa ni ya kifalme
kama ya Yesu au labda nyota yako ni Biashara, au Elimu, au Ajira,nk.
wanachokifanya ni kwamba wanaiba ile nyota na kuiweka kwa mtu mwingine au
wakaiacha tu.
Kuna
dalili za kutambua nyota yako ni ipi hasa ni rahisi sana kutambua nyota ya
mtoto mdogo. kwa mfano: mtoto akiwa na nyota ya uongozi,utambua hivi watafute
wanapokuwa wanacheza watoto wengi kwa pamoja, kisha angalia vizuri kaa utulie
usipige kelele kisha uangalie vizuri ni lazima atakuwepo mtoto atakayewadhibiti
wenzake na kuwalazimisha kufanya anavyotaka yeye na lazima watafanya, kwamfano
anawezakusema nyamazeni na wote kweli wakanyamaza, au twendeni na wote kweli
wakamfuata.
Pia
dalili za kutambua Nyota iliyoibiwa ni hizi, kwa mfano mtoto alikuwa anafanya
vizuri kabisa darasani lakini sasa hivi anazidi kudidimia wala hapendi kusoma,
ukiona hivyo ujue tayari wameshachukua wanjanja! pia kwa mtu mzima unaweza
kukuta kwamba unaandaa mipango lakini haitimii mipango yako.unapanga mwaka huu
lazima nitafungua Duka lakini utashangaa linazuka tatizo hutafungua hilo duka
mpaka mwaka utaisha. au unaandaa mpango mzuri kabisa lakini utashangaa unamwona
mwenzako tayari ameshaanzisha mpango uleule kama ulivyokuwa unapanga. au kama
ni biashara utaona mwingine kaanzisha vilevile kama ulivyokuwa unafikilia hapo
ujue Nyota yako inatumiwa na mwingine. Unajua nyota hizi huambatana na mawazo
yako. jinsi mawazo yako yalivyo ndivyo na nyota yako ilivyo hawezi mtu
akaitumia nyota yako pasipo mawazo yako.utajikuta kwamba wakati mwingine
unapoteza fahamu kama hujielewi vizuri vile. hapo ujue kuna kitu.
SASA
TUNAKWENDA KURUDISHA HIYO NYOTA YAKO KUTOKA KWA WACHAWI:
sali
sala hii kwa bidii:
Baba
katika Jina la Yesu kristo nimetambua kama kunawizi wa nyota uliyonipa katika
maisha yangu sasa kwa Jina lako naiamuru Nyota yangu kokote iliko irudi.katika
jina la Yesu ninakuja kinyume na kila nguvu za shetani nazikata kamba zashetani
nilizofungwa katika jina la yesu.asante bwana kwa kurudisha nyota yangu.
SASA
SHIKA MKONO WAKO KATIKA SCREEN YAKO NIKUOMBEE:
Baba
katika Jina la Yesu asante Mungu kwa sababu wewe ni mkuu kuliko wote.kwaJina
lako Mungu ninaamuru Nyota iliyoibiwa ya mtoto huyu, mama huyu,kijana huyu,
binti huyu irudi mara moja na taabu iwapate hao waliomwibia nyota yake mtu huyu
katika jina la Yesu.
na
baada ya hapo ni lazima utajiona tofauti katika mawazo yako, umekuwa na mawazo
tofauti hii ni ishara kwamba nyota yakko imerudi,kama hutaona hizo dalili hizi
ni ishara kwamba nyota yako haijarudi tafadhali rudia tena sala hii usichoke
mpka uzione dalili hizi.
bwana
akubariki.
2 Comments
Ningependa kujua ninini nnacho faakuepuka ikiwa Niko karibu ama kila siku napatana na alieiba nyota yangu na namjua?
ReplyDeleteMimi napenda kuuliza nina marafiki zangu mmoja nilkua naishi naye usiku saa nane nilimkuta ananikuna nyayo mwingine rafiki yangu pia nilimkuta ananikuna na kidole gumba cha mguu nilikuwa nimelala je hiyo inahusiano na maswala ya kuibiwa kwa yota yako na ni kwann wananifanyia mm watu wawili tofaut?
Delete