MAOMBI YA KUTUMA MAPIGO KWA WACHAWI WANAOKUTESA.


Na Peter Mabula. Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.


BWANA YESU atukuzwe.
Karibu tujifunze na tuombe maombi ya ushindi sana.
 Yeremia 15:20-21 ''Nami nitakufanya kuwa kama ukuta wa boma la shaba juu ya watu hawa; nao WATAPIGANA NAWE; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, ili nikuokoe, na kukuponya, asema BWANA. Nami nitakuokoa na mkono wa watu wabaya, nami nitakukomboa katika mkono wao wenye kutisha. ''

 Neno la MUNGU linasema kwamba adui zako katika ulimwengu wa roho watapigana na wewe. Maana yake wewe na adui zako kwenye ulimwengu wa roho mtapigana.
Katika mapigano au vita kuna mambo mawili; kuna kushinda na kuna kushindwa. Lakini ashukuriwe MUNGU maana ukiwa katika wokovu wake utashinda.
Ukiwa muombaji sahihi hakika utashinda.
Changamoto ya wakristo wengi huwa hawapigani na adui kimaombi bali wanamkemea tu adui.
Kwenye ndoto najua kabisa ni mara nyingi sana umeonyeshwa juu ya vita inayokukabili.
Najua kabisa kwenye ndoto au maono umeonyeshwa juu ya maadui wanaokutesa lakini wengi wenu mmekuwa watu wakupuuzia tu ndoto hizo na kuja kujuta baadae.
Biblia hapo juu inasema kwamba adui atapigana na wewe yaani na wewe utakuwa katika mapigano na adui, lakini ahadi ya MUNGU kwako uliye upande wake ni kwamba utashinda kwa jina la YESU KRISTO.

Ufunuo 12:11 '' Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.''

Utamshinda shetani kwa damu ya YESU KRISTO.
Kumshinda adui yako hakuishii tu katika kumfukuza.
Kuwashinda wachawi wanaokusumbua hakuishii tu katika kuwakemea bali kuwapiga kabisa kiroho.
Kuwashinda waganga wanaokusumbua hakuishii tu kuwaambia ''tokaa'' bali kuwapiga pia.
Washirikina wanaokutesa wanahitaji mapigo makuu kutoka kwako ndipo watasalimu amri.
Kuwashinda mawakala wa shetani wanaukusumbua hakuishii tu katika kuwaondoa katika eneo lako.
Kumshinda  adui wa rohoni wakati mwingine kunaambata na  kumuua ili asiwepo tena au asikusumbue tena.
Wabaya wako hutoa kafara za wanyama au ndege ili tu kukuharibia maisha yako.
Walio wehu au vichaa  leo sio wote walizaliwa hivyo bali wengine walirogwa. Sasa kama wewe unawahurumia wakuu wa giza wanaokusumbua basi ni hatari kwako.
Wao wanaamuru mapigo kwa kutumia kafara ya damu za kuku au mbuzi, wewe amuru mapigo kwako kwa kutumia damu ya YESU KRISTO ya ushindi na isiyoweza kushinda na mganga yeyote.
Wachawi hupanga kukuua lakini wewe siku zote umeishia tu kuwafukuza kimaombi.
waganga wanapanga uwe kichaa lakini wewe kwa maombi yako unaishia tu kuwafukuza kwenye eneo lako.
Ni kweli kabisa wakristo huwa hatupigani na maadui zetu kwa damu na nyama bali vita vyetu ni katika ulimwengu wa roho tu.
Huko katika ulimwengu wa roho tuna nguvu na tukiweza kuzitumia vizuri nguvu zetu zilizo katika jina la YESU hakika tutashinda kila ushetani unaonyemelea maisha yetu, biashara zetu, ndoa zetu, kazi zetu, uchumi wetu, vipato vyetu, chumba zetu na kila kitu chetu.

Hatuwezi kuwa na huruma kuliko MUNGU  ambaye ndiye alituambia kwamba tusiwaache wachawi kuishi.
Kutoka 22:18 ''Usimwache mwanamke mchawi kuishi.''

Hatuwaui wachawi kwa hali ya kimwili bali kwa maombi kupitia jina la YESU KRISTO.
Ukimfuata mchawi kumpiga kimwili MUNGU atakuacha na utaishia kupigwa au kuuawa kabisa maana ulinzi wa MUNGU juu yako utaondoka. MUNGU anataka uwapige wachawi wanaokusumbua, uwapige kwa maombi kupitia jina la YESU KRISTO.
Hakikisha kwa maombi yako hakuna mchawi anayekusumbua tena.
Wapige wachawi kwa moto wa jina la YESU KRISTO.
Kwa hiyo kumshinda adui wako aliye wakala wa shetani hakutakiwi tu  kuishia kwenye kumfukuza bali mpige kwa mapigo kwa damu ya YESU KRISTO kama yeye naye alivyokuwa anakupiga kwa mapigo.

Kumbukumbu 28:7 '' BWANA atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.''

MUNGU BABA kupitia maombi yako ya imani katika jina la YESU KRISTO atawafanya adui zako kupigwa mbele zako.
Sio kufukuzwa ila kupigwa.
Sio kuondolewa kwenye baraka yako tu au kuondolewa kwenye mtaa tu bali kupigwa kabisa. 
Kama umezoea kuwafukuza tu wachawi au majini  wanaoharibia ndoa yako, uchumba wako, biashara yako, maisha yako au kazi yako, naomba leo anza kuomba maombi ya kuwashushia mapigo mabaya hao mawakala wa shetani wanaokusumbua katika maisha yako.
Kama umezoea tu kusema ''Enyi washirikina mshindwe kwa jina la YESU'' Anza sasa kusema ''Enyi washirikina wote nawateketeza kwa moto wa jina la YESU KRISTO''
Mimi Peter Mabula Kijijini kwetu sisi nilikokulia ni wakulima. Siku za kula wali tulikuwa tunaanika mpunga kwenye ngozi ya ng'ombe, ili mpunga huo uwe vizuri tayari kwa kuwekwa kwenye kinu ili kutwangwa na kupembuliwa ili kupata mchele safi tayari kwa kupikwa. Kwa sababu vijana tulikuwa wengi nyumbani ndio tulikuwa wakati mwingine tunatwanga mchele huo na kupembua vizuri. Kwanini nasema haya hapa? nataka ujifunze kitu kuhusu maadui ambao umezoea tu kuwafukuza na sio kuwapiga.
Wakati tumeanika mpunga kwenye ngozi ya ng'ombe tulitakiwa pia kuulinda mpunga huo maana ndege walikuwa wanautaka sana kuula hivyo ukizubaa kidogo tu ndege wanaweza kumaliza mchele wote. Ndege wale tulikuwa tunawafukuza kila wakija kwenye mchele wetu tulioanika. Ndege wale tulikuwa tunasumbuka sana kuwafukuza maana kila  wakija tunafukuza na wanaenda jirani tu na eneo hilo, tukizubaa kidogo wanakuja haraka na kuchukua mchele., unawafukuza tena ila wameshakutia hasara tayari. Ikafika kipndi  Tukatengeneza manati ili ndege wakija  unampiga mmoja na kumuumiza au kumuua ndipo watakimbia wale ndege na utawaona tena.
 Ndivyo alivyo adui  anayekutesa maishani mwako. Kama umezoea kumfukuza tu au kumkemea tu adui yako hakika atakuwa  anarudi na kurudi na kurudi ili kukusumbua.
Lakini ukimuua kwa maombi au ukiua kazi zake zote kwa maombi hakika adui huyo hutamuona tena akikisumbua.
Ongeza tu imani na utakatifu na maombi ya vita katika jina la YESU KRISTO.
Yeremia 1:10 ''angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.''

Utamshinda adui yako katika ulimwengu wa roho kwa damu ya YESU KRISTO.
 Kwa damu ya YESU KRISTO utamshinda adui yako kwa kumng'oa katika eneo lako.
Kwa damu ya YESU KRISTO utamshinda adui yako kwa kumbomoa.
Kwa damu ya YESU KRISTO utamshinda adui yako kwa kumharibu.
Kwa damu ya YESU KRISTO utamshinda adui yako kwa kumwangamiza.
 Yeremia 5:14 ''Kwa sababu hiyo BWANA, MUNGU wa majeshi, asema hivi, Kwa sababu mnasema neno hili, tazama, nitafanya maneno yangu katika kinywa chako kuwa moto, na watu hawa kuwa kuni, nao moto utawala. ''

MUNGU atalifanya neno lake ndani yako kuwa moto wakati ukitamka katika maombi yako kwa ajili ya mawakala wote wa shetani wanaokusumbua. Neno linasema adui zako watakuwa kama kuni na maneno yako kama moto na moto huo utawala maadui zako. Hiyo ndio vita ya kiroho unayotakiwa kuifanya dhidi ya wakuu wa giza, wachawi, majini, mizimu, waganga na washirikina wote na kila anayekunenea laana au ajali.
Leo kwa maombi pambana ukimwangamiza adui yako wa rohoni  kwa jina la YESU KRISTO.
Wamezoea kukunenea mabaya ili ufe au uugue au ufukuzwe kazi na wametumia kafara  za wanyama ili jambo walilokusudia kwako likupate, Leo ita damu ya YESU KRISTO ukiamuru mapigo kwao na hakika watapondwa.
Ninazo shuhuda nyingi sana juu ya wachawi  waliopondwa kwa jina la YESU KRISTO ila nafasi hapa ni ndogo kueleza yote.
MUNGU akubariki sana na nakuomba sana unichangie mchango wako wa hiari ili niweza kuchapisha vitabu 2000 vya masomo ya maombi na vijana kuelekea ndoa. Namba yangu ni 0714252292 na jina la namba hiyo ya tigo pesa ni Peter Mabula.
Nitaandika jina lako kwenye orodha ya watu wa kuwaombea na kitabu kikitoka nitakujulisha mwanzo kabisa.
Ubarikiwe sana 
Baada ya kujitakasa kwa toba ya kweli naomba uombe maombi haya kwa wewe ambaye ni muombaji mchanga ila kwa muombaji mzoefu najua kabisa kulijua tu somo kunaweza kukufanya uombe kuliendea hitaji lako na utashinda.

MAOMBI YA KUTUMA MAPIGO KWA WACHAWI WANAOKUTESA.

 JEHOVAH  MUNGU wangu uliyeniumba ninakuja mbele zako kama nilivyo.
Naomba unisamehe dhambi zangu zote na unitakase ili niwe chombo chako kikali cha kuuangamiza utawala wa shetani katika maeneo yangu.
Nakushukuru kwa wokovu mkuu kwangu kupitia BWANA wangu na Mwokozi wangu YESU KRISTO mfalme wa uzima.
Asante kwa ROHO MTAKATIFU kwa ufunuo huu kwangu.
Niko mbele zako MUNGU wangu nikiharibu kila uchawi ulioelekezwa kwangu na katika familia yangu au ndoa yako, Nauharibu uchawi huo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Walizoea wachawi kunirushia mishale yao na mapigo yao lakini leo kwa jina la YESU KRSTO nawarushia mapigo wao na kuwaangamiza wote.
Maadui wote waliotuma kwangu magonjwa leo naamuru magonjwa yaleyale waliyayaelekeza kwangu yawapate sasa wao kwa damu ya YESU KRISTO.
Ewe adui unaniletea balaa na mikosi nakupiga pigo la upofu na vidonda mwili mzima, nakupiga kwa jina la YESU KRISTO.
Ewe mchawi nakupiga kwa pigo la uvimbe shingoni mwako na watu wote watauona huo uvimbe, nakupiga kwa pigo hilo kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Mlizoea kuroga familia yangu na uchumba wangu na ndoa yangu lakini leo kwa mamlaka ya jina la YESU KRISTO nawapiga kwa mapigo makuu. Kila pigo baya liwapate enyi washirikina na mashetani,  pigo hilo liwapige wote kwa jina la YESU KRISTO.
Mapigo yenu yote mliyoyatuma kwangu mwaka huu wote nayakamata kama yalivyo na kuwatupia ninyi na yanaangamize wote.
Sitamuacha mchawi aiishi wala kazi zake hazitafanya kazi tena kwa jina la YESU KRISTO.
Uliyeroga ndoa yangu hata migogoro imetawala nakupiga kwa pigo la vidonda mwili mzima, nakupiga kwa jina la YESU KRISTO.
Wewe mchawi unayetaka kunifukuzisha kazi nakupiga kwa pigo na uchawi wako ukurudie wewe kukuangamiza, nakupiga kwa jina la YESU KRISTO.
 Kila aina ya pigo lililotumwa kwangu nawarudishia waliolituma, Nawarudishia kwa jina la YESU KRISTO.
Kila aliyenilaani kwa kinywa chake, mabaya na yampige kwa jina la YESU KRISTO.
Kuanzia leo hakuna pigo la mchawi litakalonipa, najifunika kwa damu ya YESU KRISTO na familia yangu yote naifunika kwa damu ya YESU KRISTO. Mapigo wakiyatuma yatakuwa yanawarudia wao kwa jina la YESU KRISTO.

Kila aina ya pigo la ugongwa walilolipanga linipige, leo linawapiga wao kwa jina la YESU KRISTO.
Umasikini walionipangia uwapate wao miaka 50 kwa jina la YESU KRISTO.
Nakushukuru MUNGU wangu maana kila pigo lililokusudiwa linipate sasa litawapata wote waliotuma pigo hilo.
Nitawaona kwa macho yangu wakidhurika kwa mapigo niliyowapiga leo.
Asante MUNGU wangu wa mbinguni kwa kunishindia.
Katika jina la YESU KRISTO najifunika kwa damu ya YESU, nafunika kazi yangu kwa damu ya YESU, nafunika biashara yangu kwa damu ya YESU, nafunika uchumba wangu kwa jina la YESU na nafunika kila mali yangu kwa jina la YESU KRISTO.
Hakika nimeshinda katika jina la YESU KRISRO aliye hai.
Nimeomba haya na kupokea ushindi katika jina la YESU KRISTO.
Amen Amen.

Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.

Je, Umejiandaaje?

Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili

Post a Comment

2 Comments