Posts

Showing posts from March, 2019

SOMO: KWANINI TUYAOMBEE TUNAYOTAKA KUYAFANYA WAKATI TUNAWEZA KUYAFANYA BILA KUYAOMBEA

MWL. CHRISTOPHER MWAKASEGE UTANGULIZI Wafilipi 4:6-7 “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.” Swali ninalotaka kujibu ni hili linalosema “KWANINI TUYAOMBEE TUNAYOTAKA KUYAFANYA WAKATI TUNAWEZA KUYAFANYA BILA KUYAOMBEA?” Kwa sababu una malengo yako mwaka huu (biashara, kazi fulani, masomo). Ni mara nyingi watu wengi huombea vile vitu ambavyo hawana uwezo wa kuvifanya hapo  ndipo huona  kuwa wanamhitaji Mungu. Lakini mambo mengine huwa hawaombi na kama wanaomba basi ni watu wachache sana ambao wanaombea kila jambo. Lakini huo mstari unasema tusijisumbue na neno lolote, bali katika kila neno (kila tunachokifanya). Hii ni kati ya mistari iliyonisumbua tokea pale nilipookoka miaka ile ya 1980s na Mungu alinisukuma sana hasa kwenye heshima ya neno la Mungu na suala la maombi. Kwa hi...