SOMO: KWANINI TUYAOMBEE TUNAYOTAKA KUYAFANYA WAKATI TUNAWEZA KUYAFANYA BILA KUYAOMBEA



MWL. CHRISTOPHER MWAKASEGE
UTANGULIZI
Wafilipi 4:6-7
“Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.”
Swali ninalotaka kujibu ni hili linalosema
“KWANINI TUYAOMBEE TUNAYOTAKA KUYAFANYA WAKATI TUNAWEZA KUYAFANYA BILA KUYAOMBEA?”
Kwa sababu una malengo yako mwaka huu (biashara, kazi fulani, masomo). Ni mara nyingi watu wengi huombea vile vitu ambavyo hawana uwezo wa kuvifanya hapo  ndipo huona  kuwa wanamhitaji Mungu. Lakini mambo mengine huwa hawaombi na kama wanaomba basi ni watu wachache sana ambao wanaombea kila jambo.
Lakini huo mstari unasema tusijisumbue na neno lolote, bali katika kila neno (kila tunachokifanya). Hii ni kati ya mistari iliyonisumbua tokea pale nilipookoka miaka ile ya 1980s na Mungu alinisukuma sana hasa kwenye heshima ya neno la Mungu na suala la maombi. Kwa hiyo hili jambo nilienda nalo kwa muda mrefu sana hasa katika uhusiano kati ya mtu na Roho Mtakatifu na kujua Mungu anataka nijue  nini kuhusu maisha.
Kwa hiyo kuna mambo manne yaliyonisumbua sana tangu wakati huo Nilipo okoka.
Nikiwa nasoma kuhusu maombi mstari wa Wafilipi 4:6 - 7  ulinisumbua sana kuelewa kwa sababu Biblia inasema  “kila neno kwa kusali”. Unaombaje kila wakati na kila leo? Ukisoma mahali pengine panasema “dumuni/kesheni katika kuomba”. Ningekuwa nafikiri kibinadamu ingekuwa tabu sana maana sasa  nina  ufahamu kidogo na kupata kusoma mistari mbalimbali kwenye Biblia na kuelewa maana yake nini.
Nilijiuliza, unadumuje kwenye maombi wakati unafanya kazi?. Kwa maana hiyo ni rahisi sana ukaacha kazi na kukaa kwenye maombi ukafikiri ndio Mungu anataka. Roho Mtakatifu anaweza akakuambia unatega kazi “nenda kafanye kazi”.
Tunapo omba maombi ya mwaka huu 2019, natamani tupate angalau majibu machache kuwa “kwa nini tuombee kila tunalotaka kufanya 2019? Na kwa nini tusiyafanye bila kuombea kila jambo?” Ziko sababu nyingi sana ndani ya Biblia lakini mimi nataka nikupe nne tu ambazo Mungu amenipa. Sababu hizo ni:-
SABABU YA KWANZA
1. BILA MSAADA WA MUNGU, HATUWEZI KUFANYA TUNACHOFANYA KWA KIWANGO CHAKE MUNGU
Yohana 15:5
“Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.”
Waefeso 2:10
“Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.”
Hapo kwenye Yohana 15:5 Yesu mwenyewe amesema “pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.” na hakusema pasipo mimi kuna mambo mengine mtafanya lakini tunajua kuna vitu vingi tunafanya na Yesu hahusiki.
Kama umesoma Biblia yako utakuwa unaelewa Waefeso 2:10 ukiunganisha na Yohana 15:5 vitu vilivyozungwa hapo. Ukianza na hiyo juu ya vitu ambavyo Waefeso 2:10 inazungumzia kuwa kuna mambo ambayo tuliumbiwa nayo yaani Mungu kaweka ndani yetu na hatuyakuti hapa duniani; tuliumbiwa tuenende nayo, tulitengenezwa maalumu kwa ajili ya vitu fulani yaani aina fulani ya maisha. Ni sawa na Matendo ya Mitume 17:28
“Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake.”
Kwa hiyo kuna vitu tuliumbiwa kitabia na kikazi.
Kwenye Yohana 15:5 inamaanisha hakuna mwanadamu aliyeumbwa akae nje ya Yesu halafu anafikiri atafanikiwa. Kila kitu kiliumbwa katika Kristo lakini tuna muunganiko na Yesu ambapo hutaweza kuta muunganiko huo katika mimea, ndege, wadudu na wanyama. Binadamu ni kiumbe ambacho Mungu alikiumba kwa mfano wake kwa kumwekea sura na roho yake.
Mwanadamu haku umbwa ili ajitengeneze au amtengeneze mwanadamu mwingine; Mungu tayari ameshaweka sura na roho yake ndani ili mwanadamu anapozaa azae mtu ambaye ana sura na mfano wa Mungu na kupaswa kuenenda Ki-Mungu na kwa kiwango cha Mungu.
Dhambi ilipoingia kitu kibaya kimojawapo iliichofanya  ni kutunyang'anya uso na mfano wa Mungu ndani yetu. Kwa kutunyang'anya vitu tunavyovifahamu kama uzima wa milele na uzima wa Mungu ndani yetu lakini Yesu alipokuja alisema katika
 Yohana 10:10
“mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.”
Uzima ni maisha ya Mungu ndani ya mtu iliyodhihirishwa ndani ya Kristo. Huwezi kupata huo uzima kama hutamjua huyo Mungu katika Kristo Yesu sawa na Yesu alivyosema katika
 Yohana 17:3
“Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.”
Kwa hiyo huwezi kuwa na uzima wa milele kama hujamjua Mungu katika Kristo Yesu. Na huu uzima wa milele ni Uungu ndani ya mtu. Ni uzima wa Mungu ndani ya mtu ambao dhambi ilipoingia iliondoa ndani ya mtu, na baada ya kuondolewa ndani ya mtu kukatokea kitu kinaitwa udhaifu ndani ya mwanadamu.
Tangu wakati huo mwanadamu bila Mungu hawezi kufikia kiwango kile ambacho Mungu alimkusudia kukifikia, ni Adamu peke yake mpaka wakati huo ambao Yesu alipozaliwa na alipokufa msalabani na akafufuka na watu wakaanza kuokoka na Yesu akaanza kuingia ndani yao ndio kidogo kidogo tunaanza kuonja maana yake nini Mungu alikuwa amekikusudia ndani ya Adam kabla dhambi haijaingia. Kwa sababu tulikuwa hatufahamu na sidhani kama tumefikia hiyo picha kwamba mwanadamu aliumbwa na kitu cha namna gani na Mungu alimuwekea kitu gani ndani yake na faida ya kuwa na Mungu katika maisha ni nini na hasara za kutokuwa naye ni nini.
Kuna namna ambavyo Mungu alimuumbia mtu na akibadilisha vitu vyovyote ndani yake kila kitu kinaharibika. Mfano mzuri ni kutumia gari ya diesel kuweka mafuta ya petrol. Na ndivyo mwanadamu alivyofanya alikataa Roho ya Mungu akachukua roho ya shetani halafu anaendelea na maisha akifikiri yuko sahihi. Vile vitu ambayo havikuwa vya kawaida vimekuwa vya kawaida. Mungu anapotutazama anatutazama katika kiwango ambacho tulitakiwa tuwe  na twende nacho
Hivyo ni muhimu sana uweze kujua hili ya kwamba dhambi ilipoingia ilitunyang’anya uzima wa Mungu ndani yetu, maana yake maisha ya Mungu ndani yetu ambayo kwa sasa tunayapata ndani ya Kristo. Ndiyo maana tunapokuwa ndani ya Kristo tumesulubiwa pamoja na Kristo siyo sisi tunaoishi bali Kristo ndani yetu, uhai tulionao tunauona katika imani ya Mwana wa Mungu aliye hai aliyekufa na kufufuka kwa ajili yetu. Unapokuwa ndani ya Kristo huwezi tena kuishi kwa ajili yako mwenyewe bali unaishi kwa ajili yake yeye aliyekufa kwa ajili yako.
Ndiyo maana Biblia inasema kwenye
 Luka 9:23 ya kwamba
“Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate.”
Maana yake ni kwamba huwezi tena ukaishi kibinafsi, nafsi yako haiwezi tena kuwa na agenda yoyote kwenye maisha yako bali agenda yako inapotea saa ile unapomkaribisha Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako, agenda yako inaisha na ndani yako inaanza agenda ya Yesu. Agenda ya Yesu ni ile ambayo tokea awali alikuumbia ili uweze kuenenda nayo ya kwamba utakapokuwa pamoja naye ufanye yale yake na yale yote akuagizayo.
Kwa hiyo sababu mojawapo ya kuingia kwenye maombi ni kumwambia Mungu;
pasipo wewe siwezi kufikia kiwango unachotaka,
pasipo wewe siwezi kufikia kiwango ulichoweka juu yangu
Hakuna mwanadamu ambaye anaweza kukuwekea hicho kiwango, kiwango kipo ndani ya Biblia, na utakikuta ndani ya Kristo na ndiyo maana Biblia inasema “kuweni mpaka mfikie kimo cha utimilifu wake Kristo" huwezi kukipata kiwango hiki nje ya Kristo bali utakipata ndani ya Kristo.
Kumbuka kuna kimo/kiwango Mungu alikikusudia katika jambo lolote unalolifanya. Huwezi kukipata mahala pengine isipokuwa ndani ya Kristo. Na unapoingia kwenye maombi ni ishara ya kumwambia Mungu ninahitaji mkono wako katika hili maana pasipo wewe mimi siwezi kufanya katika kiwango unachotaka.
SABABU YA PILI
2. MAOMBI YANAMPA MUNGU NAFASI YA KUWA MTENDA KAZI PAMOJA NAWE/NASI
1Wakorintho 3:9
“Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu.”
Waefeso 3:20
“Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;”
Yesu anapoingia ndani yako  hakupi tu uzima wa milele wala kuishi tu ndani yako bali anataka aishi pamoja na wewe. Kwa hiyo anakuwa mtendaji pamoja na wewe. Tabia unayokuwa nayo ya ki-Mungu siyo yako ni ya Mungu lakini Mungu anataka ujue namna ya kushirikiana na hiyo mbegu ya tabia iliyoko ndani yako. Anataka ujue namna ya kushirikiana na Roho Mtakatifu aliye ndani yako ili usifanye kitu peke yako wala kwa nguvu zako mwenyewe bali mshirikiane kufanya jambo analotaka mfanye pamoja.
Na kwa sababu  unapozaliwa mara ya pili nguvu za Mungu  na Roho Mtakatifu anapokaa ndani yako, Mungu anakupa nafasi ya kuingia na kuendelea kukaa hapa duniani. Roho Mtakatifu atakufundisha kujifunza, kutenda, kutembea na kuishi pamoja na Yesu kila siku za maisha yako.
Waefeso 3:20 inaeleza namna ambavyo Mungu anajibu kuliko yale tuyaombayo au tuyawazayo. Kwa sababu unaweza uka tune mawazo yako yakaa kimaombi au kukaa kiuhitaji kumhitaji Mungu masaa yote. Kwa sababu Yesu  anaishi ndani yako ataona ndani yako kabla ya kusikia kwenye mdomo wako wakati unaomba kwa sababu sio wewe unayeishi ila yeye anaishi ndani yako. Kwa maana mawazo yanayokuja ndani yako ya  ni yake, Lakini kama mawazo mengo yanayokuja ndani yako ni ya Shetani unahitaji kusoma Biblia vizuri ili ujue kwanini mawazo mengi yanayokujia ni mabaya!.
Kama umeokoka wazo linalokuja ndani yako jifunze kulipa nafasi ya kwanza na kama bado unapambana huko ndani hakikisha una Neno la kutosha kwa sababu Neno linakusaidia kukarabati nafsi yako ubadilishe namna kufikiri ili uweze kufikiri jinsi Mungu alivyokuuumba anatengeneza utu mpya na utu wa kale unaondolewa.
Neno la Mungu linakusaidia kukukarabati na kuweka ndani yako mtazamo mpya na fikra mpya. Ukiona mawazo yanakusumbua tatitizo sio kwamba hujaokoka ila huna Neno ndani na kama lipo basi hujalipa heshima linalostahili kwenye maisha yako. Kwa sababu kama umekufa ndani ya kristo wazo la kwanza halitakuwa la kwako litakuwa la Yesu na kama Yesu yupo ndani yako shetani hawezi kuanza kabla ya Yesu.
Ndio maana anasema kabla hujanena alisikia na kujibu alisikia lini na wapi? Alisikia moyoni mwako! Kwa sababu anajua nini unachohitaji kabla hujaomba lakini kwanini anataka uombe ni kwa sababu ya shida iliyotokea kwenye bustani ya Edeni!
Mwandamu alimkataa Mungu na hapo ndipo haja ya maombi ilipokuja kabla dhambi haijaingia maombi hayakuwepo. Kulikuwa na fellowship (ushirika) hatukuhitaji barua ya appointment kumsikia Mungu hatukuhitaji itifaki ya kwenda mbinguni kuzungumza na Mungu, tulikuwa watoto wake, ndio maana watoto wako hawana haja ya itifaki kuja kukuona. Kuna namna watakuja kwa kuwa wanajua huyu ni baba na huyu ni mama si kwamba hawata kuheshimu hapana bali wanajua huyu ni mzazi wetu. Ni tofauti sana na mtoto ambaye alikukosea anapokuja kwa sababu kwanza hana uhakika kama utamkubalia kwa hiyo inabidi ataengeneze itifaki ya namna ya kuja ili apate msaada kutoka kwako.
Tangu tulipomkataa Mungu mwanadamu akitaka msaada wa Mungu lazima apeleke ombi kwamba Mungu nahitaji msaada ndipo apewe msaada. Hapo  ndipo maombi yalikotoka yakaja yakasambaa kwa style tofauti tofauti. Maana yake Mungu anasema mlinikataa kama mnanihitaji mtaniita na akaweka itifaki kwenye Biblia ya kukubalia na kuja kufanya kazi pamoja na wewe kwa maombi kwanza.
Ukisoma kitabu cha Mwanzo  humuoni Adamu akimuita Mungu kuja kwenye bustani lakini sasa tunamuita Mungu kuja kwenye ibada, ofisini, kwenye semina, ndoa, kazi nk. Baada ya kumkataa Mungu adamu alifukizwa kwenye bustani na Malaika wakawekwa kulinda. Tangu wakati huo  kama unamtaka Mungu ni lazima ufuate utaratibu, lazima upeleke request, ndio maana maombi yanampa Mungu nafasi ya kuwa mtenda kazi pamoja na wewe.
Ukishaokoka kuna watu wengi wanaacha baadhi ya maombi kwa sababu wanafikiri wana kila kitu na ni kwa sababu hawajui ngazi tofauti tofauti za maombi yana.  Kwa sababu kuna maombi ya kusema nataka Mungu uende namni katika hili au hili lakini kadri unavyoendelea kukua huwezi kuomba  kama unavyotaka. Maana utakuwa unaomba namna ya kuombea mapenzi ya Mungu kwanza katika maisha au mwaka ulionao. Hii ni kwa sababu unatafuta kwanza mapenzi yake  na si ya kwako.
Pamoja na kwamba Mungu amesema omba  lolote nami nitakupa kuna ngazi    huwezi kuomba lolote kwa sababu utakuwa mwangalifu sana unapoomba. Si kila kitu unachoomba ni mapenzi yake akupe mengine amekupa kwa sababu umeng’ang’ania tu, uking’ang’ana unapewa lakini si kila kitu unachoomba ni mapenzi ya Mungu. Wana wa Israel waling’ang’ana wapewe nyama lakini  akawakondesha mioyo yao.
Kwa hiyo kuna ngazi tofauti za maombi kadri unavyokua kiroho maombi yanabadilika. Hata watoto wako kadri wanavyo kua na wanaendelea kukufahamu kitu wanachokuja kuzungumza na wewe kina badilika ndipo inakuja ile
Waefeso 3:20
Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;
Kwa hiyo kuna maombi ambavyo siyo kwa ajili ya kuzungumza na Mungu lakini ni maombi ya kuhakikisha nguvu zilizoko ndani yako zinaingia kazini zinaenda kwenye eneo lile unaloliombea na kutengeneza hicho kitu ambacho unakiombea na kukusaidia.
Mungu hajibu kwa kadri ya nguvu inayotoka mbinguni anajibu kwa kadri ya nguvu inayotenda kazi ndani yako.
Kwa hiyo kama una upako 100% na unaotenda kazi ni 10% majibu ya maombi yako yatatokana na 10% haijalishi 90% uliyonayo ndani yako.
Mfano Tanesco wanaku charge kwa umeme unaotumia sio umeme unaoingia ndani yako na kukaa tu na umeme usio tumia hauna faida kwa Tanesco na hauna faida kwako maana hautumiki.
Upako usioutumia hauna faida kwako na  kwa Mungu. Njia mojawapo ya kufanya upako ufanye kazi ndani yako ni maombi. Kama unataka kumuona Mungu katika kila jambo unalofanya unahitaji kufanya maombi kulingana na nguvu itendayo kazi ndani yako
Ukisoma kama ninavyosoma utaanza kuona heshima ya Mungu kila eneo. Haijalishi niwe nahubiri au niwe nimesimama kwenye vikao vya umoja wa mataifa ninazungumza habari za uchumi maombi ninayoomba hapa ni sawa sawa na maombi ninayoomba minaposimama na wataalam wa uchumi kule.
Wakinitazama wakati naongea wanajua ninajua kila kitu lakini kumbe ninae Mungu aliye hai ambaye ananipa kitu cha kusema .Nikimaliza kuongea waandishi wa habari wananizunguka wanaanza kuuliza umetokea wapi! sasa tukuitaje doctor! Wanatafuta kila cheo kinachoendana na kitu nilichosema halafu wanashangaa nakataa kila cheo na wanasema haiwezekani. Kwa sababu ninacho zungumza wakati huo ni cha ngazi ya juu sana.


USHUHUDA
Niliandika siku moja andiko la kuweka changamoto juu ya watalaamu wa uchumi ulimwenguni waliobuni  mbinu mbali mbali za kukuza uchumi wa  nchi tofauti tofauti na likasambaa kwenye vyombo vya uchumi huko Duniani.
Baada ya muda nikapigiwa simu kuwa natakiwa niende Washington DC  Marekani kwa ajili ya kwenda “kupresent” kila nilichoandika kwenye lile andiko maana kutakuwa na mkutano wa wataalaam wa uchumi duniani.
Wakanitumia makaratasi ya watu watakao hudhuria kikao hicho. Nilishangaa sana maana kulikuwa na watu ambao ndio watu walioandika Vitabu vya uchumi na ndio waliobuni uchumi wa Marekani na World bank na Nchi tofauti tofauti duniani hata nchi zetu zinazoendelea. Na mimi nilikuwa miongoni mwa wazungumzaji wa siku hiyo.
Sasa hapo niliomba  kuliko kufikiri.  Japo nilikuwa nasoma maana Biblia inasema fanya bidii kusoma kwa sababu Roho Mtakatifu hakocopy na kupaste. Lakini unaweza ukasoma na usielewe na ukaelewa na ukashindwa kujieleza. Hapo ndipo unahitaji msaada wa Mungu.
Kwa hiyo niliomba sana kumkaribisha Mungu anisaidie katika kueleza maswali niliyouliza na kwanini nimepinga hili kwanini haliwezi kufanikiwa labda liende kwa style nyingine.
Nilipoenda kwenye mkutano niliomba Mungu na niliweza kuongea kitu ambacho Mungu alinipa kuongea na nilijibu Maswali yao yote. Nilipokuwa nimesima pale alikuwa Yesu ndani yangu anaongea na kilitoka kiingereza safi kabisa hata mimi nilishangaa. Wale watalaam walinitazama sana na walishangaa sana.
Nilipomaliza mtu mmoja akaniuliza unafanya kazi serikalini? nikamjibu hapana. Wakauliza tena sasa unapofuatalia sana masuala ya uchumi wakati wewe hufanyi kazi serikalini sasa umetumwa na nani?. Huwa nawajibu kuwa mimi ni mtumishi wa Mungu na kazi mojawapo ambayo Mungu kanipa ni kufuatilia masuala ya uchumi.
Mtu ambaye ni Dereva na akajifunza kumuomba Mungu aingie kazini anapokuwa anaendesha gari. Huwa hachoki akiwa kazini anachoka wakati kamaliza kuendesha maana kuna kitu kinamshikilia maana nguvu za Mungu zinatenda kazi ndani yake.
Yesu anapokuwa ndani yako, ukajifunza kuomba aachilie nguvu ndani yako katika kile unachofanya utaona msaada mkubwa saba.
SABABU YA TATU.
3. MAOMBI NI ISHARA KWA MUNGU KUWA UNAHITAJI REHEMA ZAKE KILA SIKU
Maombolezo 3:22
Ni huruma za Bwana kwambahatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi.Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu.Bwana ndiye fungu langu, husema nafsi yangu, Kwa hiyo nitamtumaini yeye.
Rehema sio neema. Biblia inasema katika
Waebrania 11:6
Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.

Mtu yeyote aliye na Mungu anajua umuhimu wa imani katika kutembea na Mungu na katika kupokea majibu ya maombi yake. Imani ina sehemu kubwa.
Sasa inapokuja kuwa imani imepotea, imani imetindika na umekata tamaa kabisa au umepita mahali pagumu na pamenyang’anya imani yako kabisa Lakini Biblia inasema Pasipo Imani haiwezekani kumpendeza Mungu.
Kama una mstari mmoja kwenye Biblia inatosha kukukatisha usiombe tena. Kuna kitu kinaitwa rehema.  Rehema ni huruma  na uaminifu wa Mungu kwa agano lake.
Kuna wakati unapita mahali pagumu ambapo pananyang’anya kabisa imani yako na unakata tamaa huoni kama Mungu anakusikia. Au kuna jambo unaomba na  huoni kama Mungu hakusikii lakini huwezi kuishi bila Mungu.
Biblia inasema rehema zake ni mpya kila siku maana yake ni rehema ni za kila siku. Sasa si kila wakati zinakuja maana ni lazima awepo mtu anayeomba. Akiomba kuwa Mungu naomba umrehemu huyu akisha sema namna hiyo maana yake anamwambia Mungu tazama uaminifu wako uliomwachia mwanao pale msalabani Damu yake ikamwagika, ulimfia hajakujua, ulimsamehe na hajaomba msahama ulikuwa tayari kumpokea wakati yeye bado hajakukubali. Ee Mungu naomba kumbuka rehema zako naomba umrehemu.
Mungu ukishamweleza  namna  hiyo maana ana fadhili zake , rehema zake siku kwa siku. Ukishamweleza namna hiyo Mungu anatazama rehema zake za siku hiyo na anatuma Malaika kusema teremka nenda kamsaidie yule. Wewe ndani yako  unasaidiwa hadi unatikisa kichwa.
“Mtu mwingine anasema Mungu yani simuelewi maana imani yangu ilikuwa imeisha kabisa”. Katika hali ya namna hiyo huwezi kuhesabia kuwa imani yako imekusaidia maana ni rehema za Mungu zimeingia kazini.
Ndio maana kama imani yako imetindika na unaona kabisa kama Mungu hakusikii usiache kupiga kelele kuwa ee mwana wa Daudi unirehemu. Kama umeishiwa kuomba usiku wewe sema tu ee Mwana wa Daudi unirehemu na funga macho yako. Na ukiamka asubuhi sema tena ee mwana wa Daudi unirehemu atakusaidia siku hiyo maana ana wingi wa Rehema zakw siku kwa siku.
SABABU YA NNE.
4. UNAWEZA KUTUMIA MAOMBI KUISAIDIA NCHI NA WATU WENGINE
Ezekieli 22:30-31
30 Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu. 31 Kwa sababu hiyo nimemwaga ghadhabu yangu juu yao; nimewateketeza kwa moto wa hasira yangu; nami nimeileta njia yao wenyewe juu ya vichwa vyao, asema Bwana MUNGU.
Mungu anasema Nami nikatafuta mtu hasemi watu bali anatafuta mtu ambaye atambebesha mzigo kwa ajili ya nchi isije ikaangamia.
Ni upendo wa ajabu sana kuwa unamkorofisha Mungu  hataki kukuangamiza na anatafuta mtu wa kukuombea wewe kabla haujaangamia. Inawezekana kakutafuta wewe mwenyewe uombe na hujaomba sasa anatafuta mtu mwingine akuombee
Huu ni moyo wa tofauti sana na huwa nauona kwa wayahudi peke yake  kwenye jeshi lao. Ni jeshi pekee duniani  ambalo likitaka kupiga nyumbani ya mtu mahali huwa wanatoa taarifa dakika kumi kabla kuwa wataangamiza nyumba fulani kwa hiyo walipo pale wajisalimishe.Wakijisalimisja wanapona na wasipofanya hivyo baada ya dakika kumi nyumba zao zinapigwa mabomu.
Wakitaka kuangamiza mji wanapitisha ndege dakika kumi kabla  ili kurusha makaratasi ya taarifa kuwa wanakuja kuangamiza mji huo. kwa hiyo watu wajisalimishe baada ya hapo wanakuja kweli kuangamiza.   sasa huwa nawaza kuwa wakitoa taarifa ni kuwa wanatala kuja kugombana na watu au na majumba?
Lakini ni roho ya ajabu sana wanayo maana wakipiga watu kwa mabomu na watu wakajeruhiwa huwa wanawapeleka hospitali kuwatibu.
Biblia inasema Mungu anatafuta mtu ambaye kama kuna shida nyumbani kwenu au kazini au kwenye nchi ambaye yuko tayari kukaa kuomba toba kwa ajili ya nchi au mahali anapotaka ukae kuomba.
Mungu anamuweka kila mtu kwa maksudi kwa sababu Mungu hakumpamga kila mtu aliyeokoka atoke kesho aende kuhubiri. Biblia inasema kila alie na mwana anao ushuhuda  kushuhudia sio kuhubiri maana maisha yetu ni ushuhuda. Kushuhudia ni kwa kila aliye na mwana na kuhubiri ni kwa kila aliyepangiwa kuhubiri kwa hiyo  kama ndani yako unapangiwa kushuhudia haina maana uende kuhubiri. Ushuhudie kile ambacho Yesu alikutendea maana ni ushuhuda kwako na kinatosha kuwavuta watu kuja kwa Yesu. Kwa sababu kazi ya kuwaleta watu kwa Yesu sio kazi ya wahubiri tu na mikutano bali ni kazi ya kila mmoja wetu.
Kwa hiyo maneno yetu yanatakiwa yawavute watu kwa Yesu. Haitoshi tu kuwaleta watu kwenye mikutano na kanisani ili waongozwe sala ya toba bali tunatakiwa  tuwaongoze sala ya toba. Maana kama hujui kumwongoza mtu sala ya toba andika kwenye karatasi na kila ukimpata mtu msomee au unamwambia soma hapa.
Hayo ndio mazoezi yenyewe maana si wote waliokutana na watu na kuwaongoza sala ya toba kwani walikuwa wanajua? Maana mara nyingine walikuwa hata hawajui hata kuongoza sala ya toba. Lakini walianza kidogo kidogo na wakaweza.
Sasa katika malengo ya mwaka huu unakuta hata hujaweka lengo na kutaka Mungu akusaidie kuwaleta watu kwa Yesu. Utakuwa umeweka malengo ya kuomba hela lakini hili hujaweka. Hakikisha mwaka huu lengo mojawapo la kwako ni kuwaleta watu kwa Yesu.
Inapofika kwenye maombi Mungu anatafuta watu waliotayari kuomba maana yake atakuwa anateremsha mzigo wa maombi ndani yao kama wako tayari kubeba.  Unakuta mtu anapata mzigo wa kuomba na haombi muda huo anaanza kuwaza kuwa hili ntalipeleka kwenye kikundi cha maombi.  Ikifika asubuhi ule mzigo wa maombi hana tena na anaanza kusema jana nilikuwa na mzigo wa kuomba ila sasa umetoweka. Mungu hatafuti kikundi bali anatafuta mtu maana ulihitaji kusema ee Bwana niko hapa  nisaidie niombe.
Sasa unapoanza kuomba Mungu atakusaidia maana hata kama  utashirikisha wengine lakini ndani yako unakuja tayari umejiweka sawa kuomba maana wanaweza kuja  wenzio na agenda za kwao za kuombea na usipojua namna ya kusimamia agenda ambayo Mungu kakupa unajikuta umehama kwenye kusudi.
Mungu anataka kukuambia kuwa kwa maombi yako Sekta, Nchi itapona. Ukiona sekta inaangamia  na wewe uko pale ujue hujawa chumvi inayotakiwa.
Suala la maombi ni mfumo wa maisha maana ni mawasiliano yako na Mungu kila wakati. Kuna saa unaacha kila kitu unaomba. Ile kwamba umemaliza kuomba haina maana hutaomba tena maana  maombi ni mfumo wa maisha.


Post a Comment

0 Comments