Posts

Showing posts from June, 2016

MFALME ALIYEKUWA NA MBWA WAKALI KUMI

 MFALME ALIYEKUWA NA MBWA WAKALI KUMI Kulikuwa na mfalme mmoja aliyekuwa na mbwa kumi wakali sana. Alipenda kuwatumia mbwa hawa pindi akitaka kumuadhibu mtumwa aliyekosea. Mbwa hawa waliwatesa watumwa kwa kuwararua na meno yao makali! Wakati mwingine watumwa waliokutana na adhabu hii walipoteza uhai. Siku mtumwa aliyemtumikia mfalme kwa miaka kumi alitoa wazo baya ambalo halikumpendeza mfalme, ikaamriwa akamatwe na kutupwa katika banda la mbwa. Mtumwa alinung'unika na kusema :"nimekutumikia kwa miaka 10, na leo wanitenda hivi? Naomba unipe walau siku 10 kabla hujanitupa baniani! " Mfalme akakubali. Katika siku izo 10, mtumwa alimfuata mlinzi wa banda la mbwa na kumuomba ampe nafasi kuwahudumia mbwa wale. Mlinzi alistaajabu ila akakubali. Mara moja mtumwa akaanza kazi ya kuwapa mbwa chakula, kuwaogesha na kila aina ya faraja ambazo wanyama huhitaji. Siku 10 zikaisha, mfalme akaamuru mtumwa atupwe bandani kutumikia adhabu yake. Hilo likafanyika kwa hara...

KUMFANYIA SHINGO NGUMU NA KUMPINGA ROHO MTAKATIFU.

Bibilia inatuambia sisi watu ambao tumeamua kumpokea na kumwamini Yesu na kumfanya Bwana na Mwokozi wa maisha yetu: “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;” (YN. 1:12 SUV). Kwa hiyo kila mmoja wetu aliyempokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yake amepewa uwezo wa kufanyika mtoto wa Mungu. Huu uwezo unajidhihirisha katika huduma na kazi ya Roho Mtakatifu katika maisha ya mwamini. Moja ya majina ambayo Roho Mtakatifu anaitwa kwayo ni "ROHO WA KUTIFANYA WANA." Maandiko yanasema: “Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba.” (RUM. 8:15 SUV). Huyu Roho wa kufanywa wana anayetajwa katika huu mstari ni Roho Mtakatifu. Kwa kadiri mimi na wewe tunavyoitikia huduma na kazi ya Roho Mtakatifu maishani mwetu tunaudhihirisha uwana katika maisha yetu. Ndo maana maandiko yanasema: “Kwa kuwa wote wanaoongo...