MAOMBI MAKALI YAKUOMBA NA KUFUNGULIWA.
*MUNGU akukumbuke. BWANA akutendee muujiza mkuu. MUNGU ayakumbuke machozi yako. Kwa jina la YESU KRISTO umeshinda. BWANA YESU alisema kwamba kila tutakalolifunga duniani na mbinguni limefungwa Mathayo 18:18. Hivyo tunawafunga wachawi wanaokusumbua na watakimbia wenyewe. Kwa jina la YESU KRISTO. umeshindaaaaaaaaa kwa jina la YESU KRISTO. *Nakuombea Masikio yako yafunguke, kifungo cha ulimi wako kilegee uisemee haki yako. Mwili, nafsi na roho yako vifunguliwe na kila aina ya vifungo vya mawazo, maneno na matendo kwa jina na damu ya YESU KRISTO na kwa neno la MUNGU kama lilivyoandikwa katika Marko 7:34-35 '' YESU akatazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia, Efatha, maana yake, Funguka.Mara masikio yake yakafunguka, kifungo cha ulimi wake kikalegea, akasema vizuri.''Mungu akubariki. * Jiwe lililokuwa kizuizi cha kumzuia BWANA kutoka kaburini, liliondolewa na malaika. Na leo wapo watu wengi leo mawe yamewakalia katika maisha yao, kuna mawe yamekalia bi...