UNAPOHITAJI MFANIKIO TAFADHARI ACHANA NA MAMBO HAYA HARAKA SANA.

1. Acha kutegemea mafanikio ya haraka.Mara nyingi hizi ndizo zimekuwa ndoto nyingi za watu wengi kutaka kuona mafanikio makubwa na ya haraka. Mafanikio yoyote huwa yanajengwa hatua kwa hatua. Tena kuna wakati huwa ni hatua za kutambaa mithili ya mtoto mdogo. Kama utategemea mafanikio ya haraka zaidi katika maisha yako hutayapata zaidi ya kujidanganya wewe mwenyewe. Acha kung’angania mafanikio ya haraka, utakwama. Jiwekee malengo kisha songa mbele. SOMA; Jinsi Ya Kuweka Malengo Utakayoyafikia. 2. Acha kuwa mtu wa visingizio.Hili ni jabo mojawapo ambalo umekuwa ukiling’ang’ania mara kwa mara katika maisha yako. Umekuwa ni mtu wa visingizio kwa kudai kuwa huwezi kufanikiwa kwa sababu hukusoma, huna mtaji ama umetoka katika familia maskini. Kutokana na visingizio hivyo umekuwa huchukui hatua yoyote zaidi ya kuzidi kufanya maisha yako kuwa magumu. Ili uweze kufanikiwa, achana na kung’ang’ania visingizio kama mkombozi wako. Badala yake, chukua hatua juu ya maisha yako. S...