SOMO: WOKOVU MKUU



 
WARUMI 5 –8

UTANGULIZI

•Kwakuwa Mungu ametumia gharama kubwa kuleta wokovu duniani, katika huo, imeachiliwa nguvu inayo weza kuleta faida kubwa katika maisha ya mwanadamu
•Ili tuweze kupokea faida  inayo ambatana na wokovu, lazima tuujali na kuuishi katika wokovu halisi katika maisha yetu.
•Itakuwa rahisi kwetu kuujali wokovu kama tutatambua gharama iliyotumika kuleta wokovu

MAANA YA WOKOVU

1.    WOKOVU NI ZAWADI YA MUNGU KWA WAMINIO

Tofauti na mshahara (dhawabu) ambayo hutolewa kulingana na kazi ya mtu na kwa makubaliano, zawadi hutolewa kwa mtu kulingana na furaha ya yule anayetoa na sio kwa kazi ya yule anayepokea. Wokovu ni zawadi ya Mungu inayotokana na furaha yake kwetu tunapomwamini yeye, na Yesu kristo aliyemtuma. Kama ingetokana na kazi hakuna mtu angeyeweza kufanya kazi ya kustahili ijara inayolingana na thamani ya wokovu. Hivyo Wokovu si matokeo ya matendo mema, kusali, kufunga wala kutoa sadaka nyingi bali ni matokeo ya kuukubali upendo wa Mungu kwetu na kuiamini kazi ya Yesu Kristo msalabani.

Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu(Efe 2:8-9).
2.    Wokovu ni badiliko la kudumu la mtu wa ndani

Neno la kiingereza lilotumika ni “trans-formation”maana yake ni mabadiliko yasiyoweza kurudia hali yake ya kwanza. Ni mfano wa kuchoma karatasi na kupata majivu ambayo hayawezi kuwa tena karatasi na sio mfano wa maji yanayoganda kuwa barafu na baadaye kuyeyeuka tena kuwa maji. Mtu aliyepata wokovu halisi na kuonja wema wa Mungu hapaswi kuwa na kigeugeu wala ndoto ya kurudi nyuma.

Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu(Rum 12:2).
  
3.    Wokovu ni kuhamishwa

Kabla ya kuokoka ulikuwa unaendeshwa na ufalme wa giza kwa kumtii shetani na matakwa ya nafsi na mwili. Kuokoka ni kukubali KUENDESHWA na Neno la Mungu. Maanake ni kuishi kwa kukataa matakwa yako na kufuata matakwa ya Mungu. Kumtii Mungu kunakoambatana na kukana matakwa ya adui apitiaye nafsi na miili yetu tutafunga mlango wa kuonewa na ibilisi na kufungulia baraka za Mungu(Yak 4:7). Kwa hakika wokovu unatutoa kutoka mahali pabaya na kutuweka katika ulimwengu salama ndani ya Kristo Yesu katika Ulimwengu wa roho
 
Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake (Kol 1:13)

4.    Wokovu ni kukombolewa

Wakati mwingi tumesita kutumia neno “ukombozi”kwa sababu ya matumizi mabaya yaliyozoeleka hivi sasa. Lakini ni moja ya neno kuu sana katika wokovu wetu.

Neno “ukombozi”limetukaje vibaya?

(A).Kwa kutumia Neno kukombolewa kama njia ya kutoka kwenye magonjwa na shida mbali mbali.
(B).Kwa kudai sadaka au tendo fulani kama vile kufunga kama njia ya kuleta ukombozi


Matumizi sahihi ya neno “kukombolewa”ni yapi?

(a) Ni kibali cha kutolewa kwenye hukumu ya Mungu. Neno sahihi kwa habari ya kutolewa kwenye magonjwa na shida/madhaifu mengine ni kuponywa.
(b) Ni tendo linatokana na sadaka pekee na moja tu ya mauti ya Kristo na kumwagika kwa damu yake msalabani.

Je, kuna tofauti gani kati ya wokovu na ukombozi?

Wokovu ni matokeo ya ukombozi kamili. Baada tu ya mwanadamu kuanguka pale Edeni pale pale iliandikwa hati ya mashitaka kwa wanadamu wote mbele za Mungu na nakala (copy/kivuli) zikatumwa duniani. Naye shetani akazichukua kama ushahidi kwamba hakuna mwanadamu atakayekwenda Mbinguni, Na hiyo ndiyo ilkuwa hukumu, yaani kutengwa na Mungu(mauti ya milele).Watakatifu wa zamani walipolala walizuiwa kuingia Mbinguni kwa sababu ile hati.Walisubiri ukombozi wao wakiwa kifuani kwa Ibrahimu (Ebr 11:13). Hata baada ya kufufuka kwao walisubiria siku tatu hapa hadi hati ilipofutwa (Mt 27:52-53)

Je, kuna tofauti gani kati ya wokovu na ukombozi?

Kwa muda wote huo alikuwa natafutwa mtu ambaye angeweza kuingia maeneo yote matatu ili kuzifuta hati zote za mashitaka. Ndio maana baada tu ya Bwana Yesu kumwaga damu yake alienda nayo patakatifu pa hapa duniani(kitambaa cha hekalu kilipasuka) ili kufuta nakala ya hati ya mashitaka, kisha akaenda kuzimu nako akabatilisha ushahidi uliokuwemo na hatimaye akaenda hadi Mbinguni ilimokuwa hati halisi akaifuta kwa damu yake, kisha akaandika hati nyingine pale pale ya kutangaza ukombozi kwa wanadamu wote tangu Adamu  (Ebr 9:22-24, Kol 2:14-15, 1Pet 18-19, Ufu 5:1-10). Haya yatufanye kujua kwamba wokovu tuliopewa ni mkuu sana (Ebr 2:3)

Wokovu ni ukombozi

Kwa hiyo ukombozi ni kitendo cha kufutwa kwa hati ya uadui kati ya Mungu na mwanadamu na kuandikwa kwa hati ya kukubaliwa na Mungu. Wokovu ni kitendo cha kukubali/kupokea ukombozi wa Yesu kristo katika maisha ya mtu binafsi. Kitendo cha Yesu kufa msalabani na kufuta hati ya mashitaka na nakala zake kilitangaza majira ya ukombozi kwa wanadamu wote, na kutoa nafasi kwa kila mtu kuokoka. Kinachopaswa ni kusaini hati hiyo kwa kumwamini Yesu kristo (Lk 4:18-19).

Wokovu ni kukombolewa

Ukombozi manake ni kulipiwa deni na deni tulilopiwa ni kutolewa kwenye hukumu ya Mungu(1Pet 1:18-19). Mkataba wa ukombozi ni kwamba baada ya kulipiwa deni tunakuwa mali ya yule aliyetununua yaani Yesu Kristo na hivyo tunarudi kwa Mungu na muumba wetu, naam (1Kor 6:19). Kwa njia hiyo, yanarejeshwa mahusiano yaliyokuwa yamevunjika wakati wa anguko la Edeni

Wokovu ni mchakato wa MATENGENEZOya mfumo mpya wa maisha

Ili tuweze kudumisha wokovu wetu Lazima kilasiku tu elekeze nia zetu katika kuvua matendo yazamani na kujivika tabia mpya za waenda Mbinguni.Njia yakujithibitisha katika wokovu ni kuhakikisha kuwa kilasiku, katika maeneo yote ya maisha yako, kuna mabadiliko endelevu katika mtazamo wako, vipaumbele vyako, usemi, matendo, utoaji, huduma, ibada, kusomaneno, maombi nk.

Mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani,unao haribika kwa kuzifuata tama zenye kudanganya;na mfanywewapya katika roho ya nia zenu; mkavae utu mpya, ulio umbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wakweli (Efe4:22-24)

Post a Comment

0 Comments