UNAPOHITAJI MFANIKIO TAFADHARI ACHANA NA MAMBO HAYA HARAKA SANA.






1. Acha kutegemea mafanikio ya haraka.Mara nyingi hizi ndizo zimekuwa ndoto nyingi za watu wengi kutaka kuona mafanikio makubwa na ya haraka. Mafanikio yoyote huwa yanajengwa hatua kwa hatua. Tena kuna wakati huwa ni hatua za kutambaa mithili ya mtoto mdogo. Kama utategemea mafanikio ya haraka zaidi katika maisha yako hutayapata zaidi ya kujidanganya wewe mwenyewe. Acha kung’angania mafanikio ya haraka, utakwama. Jiwekee malengo kisha songa mbele.
SOMA; Jinsi Ya Kuweka Malengo Utakayoyafikia.

2. Acha kuwa mtu wa visingizio.Hili ni jabo mojawapo ambalo umekuwa ukiling’ang’ania mara kwa mara katika maisha yako. Umekuwa ni mtu wa visingizio kwa kudai kuwa huwezi kufanikiwa kwa sababu hukusoma, huna mtaji ama umetoka katika familia maskini. Kutokana na visingizio hivyo umekuwa huchukui hatua yoyote zaidi ya kuzidi kufanya maisha yako kuwa magumu. Ili uweze kufanikiwa, achana na kung’ang’ania visingizio kama mkombozi wako. Badala yake, chukua hatua juu ya maisha yako.
SOMA; Mambo 7  Yanayo kufanya  Ushindwe  Kutimiza  Ndoto  Zako.

3. Acha kuogopa sana kushindwa.Kushindwa ni hatua mojawapo muhimu ya kuweza kukufikisha kwenye njia halisi ya mafanikio. Unaposhindwa unakuwa unajifunza kutokana na makosa unayoyafanya na kisha kuendelea zaidi. Kama utaendelea kuogopa kujaribu mambo mapya kila siku kwa sababu ya kushindwa, tambua hutaweza kufanikisha mambo makubwa katika maisha yako. Ili uweze kufikia mafanikio makubwa hutakiwi kuogopa kushindwa kwa namna yeyote ile. Unatakiwa kuachana na woga huu mara moja ili kufikia mafanikio makubwa.
SOMA; Jiulize “Kwa Ni Nini Maisha Yangu Yako Hivi”

4. Acha kufanya kazi kutegemea pesa.Kama utaendelea kufanya kazi na kuwaza pesa! Pesa Pesa!, hutaweza kufika mbali sana. Fanya kazi kwa lengo la kujifunza na kisha baada ya hapo pesa ndiyo ifuate. Ukiwa unafanya kazi kwa lengo la kupata pesa utajikuta unafanya mambo yako mengi sana chini ya ufanisi. Badili fikra zako na acha kung’ang’ania kufanya kazi kwa kutaka pesa tu. Ukitengeneza huduma iliyobora zaidi pesa kama pesa itake isitake itakufuata tu huko ulipo.
SOMA; FEDHA; Kama Unataka KuwaTajiri, Acha Kufanya Makosa Haya Unapokuwa Na Pesa.

5. Acha kuwa Kufikiria sana makosa yaliyopita.Kwa kuendelea kufikiri sana makosa uliyoyafanya hiyo itakufanya uzidi kupoteza mwelekeo wa mafanikio yako. Njia sahihi ya kufanikiwa ni kuachana na kufikiria makosa hayo. Vinginevyo utakuwa unapoteza nguvu zako nyingi kun’gang’ania jambo ambalo haliwezi kukufikisha kwenye mafanikio ya kweli. Hili ni jambo mojawapo ambalo unatakiwa kuliacha mara moja ili uweze kufanikiwa.

Kwa vyovyote vile, kwa kadri unavyozidi kun’gang’ania mambo hayo ndivyo ambavyo unajikuta unazidi kuharibu maisha yako bila kujua. Ili kuweza kufanikiwa na kutimiza ndoto zako halisi ulizojiwekea, unatakiwa kushika wajibu mmoja tu. Huu ni wajibu wa kuweza kun’gang’ania mambo yatakayokusaidia na kubadili maisha yako kabisa. Kwa kifupi, hayo ndiyo mambo unayotakiwa kuyaacha mara moaj ili uweze kufanikiwa

Post a Comment

0 Comments