Posts

Image
wakati mwingine tunahisi hatumuoni Mungu wala hasikii maombi yetu,lalin kumbe ni sisi wenyewe tunashindwa kujitathimin na kujiweka vizuri na Mungu .Lakini vitu vinavyokwamisha maombi yetu yasiwe na majibu/manufaa 1.MAOVU     Isaya 59:1-2  maovu yetu ndiyo sababu kubwa  Mungu anashindwa kujidhihirisha  kwetu maovu yetu yanatufarakanisha na uso wa Mungu 2.KUKATA TAMAA   Roho ya kukata tamaa ni kizuizi kikubwa katika maisha yetu. 3.LENGO BAYA Maombi ya kujisifu Mungu hawezi kujidhihirisha (TUFANYE MAOMBI KWA AJILI YA UTUKUFU WA MUNGU NA KUMWINUA) na Mungu atajidhihirisha kwetu. 4.KIBURI Luka 18:10-14 Kuomba kwa kutokuangalia hali ya kimaisha utajiri,umaskini na mengineyo. 5.MAOMBI Mambo katika ulimwengu wa Roho hayaendi pasipo imani 6. KUSAMEHE Watu wengi tunashindwa kusamehe tunashindwa kujiachilia tunabeba vitu vizito moyoni mwetu (uchungu) Mungu anaangalia moyo wa mtu,Mungu hakai mahali penye huzuni jifunze kusamehe.Marko 5:21-27 ...
    JIFUNZE KUUTAFUTA USO WA MUNGU Nimesoma kitabu cha kutoka ...nimejifunza vitu vingi sana juu ya safari ya wana waisrael jinsi ambavyo  Mungu alikuwa pamoja nao kwa sababu walikua n wana wa agano.  Lakin mejifunza zaidi katika KUTOKA 33:12-------  Licha ya kwamba neeema ya Mungu  ilikuwa juu ya Musa  hakuacha kujiona anamhitaji Mungu  wakati wote na Mungu wakati wote. Na  Mungu  akamuahidi kwa uso wake utakwenda pamoja na yeye.Musa hakuona kuwa kuambiwa na Mungu tu imetosha. KUTOKA 33:15 Musa akasema  USO WAKO USIPOKWENDA NA MIMI USITUCHUKUE KUTOKA HAPA . Ni maneno yenye nguvu sana.  Nilichojifunza  kuwa hata kama unakubalika kiasi gan mbele za Mngu kuutafuta uso wa MUNGU  au uwepo  wake katika maisha yetu ni kitu cha lazima.Tunahitaji kutembea katika ktk nguvu/uwepo wa Mungu  wakati wote haijalishi Mungu amekuahidi nini tafuta uso wa Mungu mahali popote  uendako. Musa aliona bila...

MSINGI IMARA

uimara wa nyumba siku zote na pahala popote  upo  kenye MSINGI. hivyo ni vizuri sana kuimarisha msingi kama unataka kuwa na nyumba imara  isiyo teteleka. BAHATI NZURI TUNAFAHAMU KUWA YESU NI MSINGI IMARA HIVYO TUJENGE MAMBO YETU  HAPO ILI TUSITETELEKE . ENDELEA  KUBARIKIWA SANA

MTAZAME BWANA

unapoona ukiyainua macho yako na kutazama milima kasha ukajiuliza msaada wangu utatoka wapi?  JIBU ni moja MSAADA WAKO U KATIKA BWANA. IMETUPASA KUMTUMAINI BWANA SIKU ZOTE NA KUMPENDA MAANA YEYE ALITUPENDA KWANZA

REHEMA NA FADHILI

REHEMA NA FADHILI ZA BWANA HUTUFUATA SIKU ZOTE. NDIO MAANA ANAFIKA MAHALA ANASEMA NITAKUONESHA NJIA  UTAKAYOIENDEA  JICHO LANGU  LIKIKUTAZAMA. HIVYO TEMBEA UKIWA NA UHAKIKA KWAMBA MUNGU  ANAKUPENDA SANA
MUNGU NI MKUU YATUPASA KUMWABUDUU YEYE PEKEE. UWE NA WAKATI MWEMA. ENDELEA KUTAFAKARI  WEMA WA BWANA

ALFA NA OMEGA

MUNGU  ni ALFA na OMEGA. hivyo hakuna siku atakuacha uangamie wala upotee kwa sababu AMEKUGHARAMIA KWA DAMU YA MWANAKONDOO. Hivyo mwite YEYE siku zote za maisha yako. YESU AENDELEE KUKUBARIKI.