Nimesoma kitabu cha kutoka ...nimejifunza vitu vingi sana juu ya safari ya wana waisrael jinsi ambavyo Mungu alikuwa pamoja nao kwa sababu walikua n wana wa agano. Lakin mejifunza zaidi katika KUTOKA 33:12-------
Licha ya kwamba neeema ya Mungu ilikuwa juu ya Musa hakuacha kujiona anamhitaji Mungu wakati wote na Mungu wakati wote. Na Mungu akamuahidi kwa uso wake utakwenda pamoja na yeye.Musa hakuona kuwa kuambiwa na Mungu tu imetosha.KUTOKA 33:15 Musa akasema USO WAKO USIPOKWENDA NA MIMI USITUCHUKUE KUTOKA HAPA.Ni maneno yenye nguvu sana.
Nilichojifunza kuwa hata kama unakubalika kiasi gan mbele za Mngu kuutafuta uso wa MUNGU au uwepo wake katika maisha yetu ni kitu cha lazima.Tunahitaji kutembea katika ktk nguvu/uwepo wa Mungu wakati wote haijalishi Mungu amekuahidi nini tafuta uso wa Mungu mahali popote uendako.
Musa aliona bila uwepo wa Mungu yeye si chochote.
Tujifunze kuutafuta uso wa Mungu kwa hali yeyote ile...........TO WALK IN HIS PRESENCE TO THE MAXIMUM, kaa magotini kwake kam ni kuomba omba,funga kwa Maombi,soma neno lake utaona udhihirisho wa MUNGU katika maisha yako.Na Mungu atajitukuza kupitia sisi.
Na Peter Mabula. Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU. BWANA YESU atukuzwe. Karibu tujifunze na tuombe maombi ya ushindi sana. Yeremia 15:20-21 '' Nami nitakufanya kuwa kama ukuta wa boma la shaba juu ya watu hawa; nao WATAPIGANA NAWE; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, ili nikuokoe, na kukuponya, asema BWANA. Nami nitakuokoa na mkono wa watu wabaya, nami nitakukomboa katika mkono wao wenye kutisha. ' ' Neno la MUNGU linasema kwamba adui zako katika ulimwengu wa roho watapigana na wewe. Maana yake wewe na adui zako kwenye ulimwengu wa roho mtapigana. Katika mapigano au vita kuna mambo mawili; kuna kushinda na kuna kushindwa. Lakini ashukuriwe MUNGU maana ukiwa katika wokovu wake utashinda. Ukiwa muombaji sahihi hakika utashinda. Changamoto ya wakristo wengi huwa hawapigani na adui kimaombi bali wanamkemea tu adui. Kwenye ndoto najua kabisa ni mara nyingi sana umeonyeshwa juu ya vita inayokukabili. Najua kabisa kwenye ...
Na Peter M Mabula. Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU. BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Kanisa ni jumuia ya Wakristo. Kanisa ni watu walioitwa na kutengwa na mambo ya dhambi. 1 Kor 6:17-18 '' Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema BWANA, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa BABA kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,'' Maandiko hayo ni sehemu tu ndogo ya maandiko yanayolitambulisha Kanisa la KRISTO duniani. Kanisa hai wametengwa na uovu wa dhambi na wametengwa na mambo ya kidunia yaliyo machukizo(Machafu). Ndio maana huwezi kumuona Askofu akiwa disko akicheza. Huwezi kumuona Mkristo aliyeokoka akiwa kwa mganga wa kienyeji. Huwezi kumuona Mchungaji anatoa talaka. Huwezi kumuona Mteule wa MUNGU akivuta sigara wala bangi na tena huwezi kumuona mteule wa KRISTO akitumia madawa ya kulevya. Huwezi kuona kanisa wakichukua mapanga na mikuki wakienda kul...
0 Comments