Posts

SOMO: KWANINI TUYAOMBEE TUNAYOTAKA KUYAFANYA WAKATI TUNAWEZA KUYAFANYA BILA KUYAOMBEA

MWL. CHRISTOPHER MWAKASEGE UTANGULIZI Wafilipi 4:6-7 “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.” Swali ninalotaka kujibu ni hili linalosema “KWANINI TUYAOMBEE TUNAYOTAKA KUYAFANYA WAKATI TUNAWEZA KUYAFANYA BILA KUYAOMBEA?” Kwa sababu una malengo yako mwaka huu (biashara, kazi fulani, masomo). Ni mara nyingi watu wengi huombea vile vitu ambavyo hawana uwezo wa kuvifanya hapo  ndipo huona  kuwa wanamhitaji Mungu. Lakini mambo mengine huwa hawaombi na kama wanaomba basi ni watu wachache sana ambao wanaombea kila jambo. Lakini huo mstari unasema tusijisumbue na neno lolote, bali katika kila neno (kila tunachokifanya). Hii ni kati ya mistari iliyonisumbua tokea pale nilipookoka miaka ile ya 1980s na Mungu alinisukuma sana hasa kwenye heshima ya neno la Mungu na suala la maombi. Kwa hi...

JINSI WACHAWI WANAVYOWEZA KUIBA NYOTA YAKO

Image
Salam wapendwa katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo. Leo nipo hapa kuwaletea topic mpya kabisa ambayo wachungaji wengi hawaifundishi makanisani na yamkini baadhi yao hawaijui.kama kichawa cha habari kinavyosema, leo nataka kuzungumza juu ya wachawi.kunawatu wengi sana Duniani wanalia kila wanavyojaribu kuyakwamua maisha yao inashindikana, lakini hawajui ni kwa nini? nataka nikuambie leo, wapo watu ambao Mungu ameamua kuwanyima mali kwa makusudi anayoyajua yeye mwenyewe, na kuna watu ambao Mungu hakuwanyima mali mpango wa mungu ni kwamba watu hawa wapate mali lakini hawana! hapa ni kwamba shetani huamua kuwaonea na kuwadhulumu watu hawa. Unajua kila mmoja wetu anakitu alichopewa na Mungu ili kuweza kuzikamilisha shughuli za ulimwengu huu. ngoja nikupe siri moja kuu sana, kila mwanadamu anapozaliwa huwa anakitu kinachoitwa nyota, kitu hiki ni ishara au ni kitambulisho cha mtu huyo katika ulimwengu wa roho ya kuwa yeye kapewa nini hapa duniani,soma mathayo 2:1-5.biblia inas...

KUBOMOA MADHABAHU ZA SHETANI(Samson Mollel – Uzima wa Milele International Ministries) (Somo limefundishwa na Bishop J. Gwajima – Kitabu cha Maombi ya Kubomoa Madhabahu)

Image
Madhabahu ni nini? Ni daraja la kuunganisha katika ya ulimwengu wa roho wa Mungu au shetani. Kuna aina 2 za madhabahu, Madhabahu ya MUNGU (Nuru)na madhabahu ya shetani (giza) ***MADHABAHU YA MUNGU Watu/watumishi wa Mungu katika Biblia walianza kwa kujenga madhabahu kabla ya kufanya chochote NUHU – Mwanzo 8:20“Nuhu akamjengea Bwana madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.” MUSA – Kutoka 17:15“Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake Yehova-nisi;” YOSHUA – Yoshua 8:30“Ndipo Yoshua alijenga madhabahu kwa Bwana, Mungu wa Israeli katika mlima Ebali.” GIDEONI – Waamuzi 6:24“Ndipo Gideoni akamjengea Bwana madhabahu hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu; hata hivi leo iko huko katika Ofra ya Waabiezeri.” SAMWELI – 1 Samweli 7:17“Na kurudi kwake kulikuwa mpaka Rama; maana ndipo ilipokuwa nyumba yake; nako ndiko alikowaamua Israeli; na huko akamjengea Bwana madhab...