Madhabahu
ni nini?
Ni
daraja la kuunganisha katika ya ulimwengu wa roho wa Mungu au shetani.
Kuna
aina 2 za madhabahu, Madhabahu ya MUNGU (Nuru)na madhabahu ya shetani (giza)
***MADHABAHU
YA MUNGU
Watu/watumishi
wa Mungu katika Biblia walianza kwa kujenga madhabahu kabla ya kufanya chochote
NUHU
– Mwanzo 8:20“Nuhu akamjengea Bwana madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye
safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya
madhabahu.”
MUSA
– Kutoka 17:15“Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake Yehova-nisi;”
YOSHUA
– Yoshua 8:30“Ndipo Yoshua alijenga madhabahu kwa Bwana, Mungu wa Israeli
katika mlima Ebali.”
GIDEONI
– Waamuzi 6:24“Ndipo Gideoni akamjengea Bwana madhabahu hapo, akaiita jina
lake, Yehova-Shalomu; hata hivi leo iko huko katika Ofra ya Waabiezeri.”
SAMWELI
– 1 Samweli 7:17“Na kurudi kwake kulikuwa mpaka Rama; maana ndipo ilipokuwa
nyumba yake; nako ndiko alikowaamua Israeli; na huko akamjengea Bwana madhabahu.”
***MADHABAHU
YA SHETANI
shetani
na watumishi wake wana madhabahu ambayo hutumia kupitisha mambo mabaya/maovu
kutoka katika ulimwengu wa roho (giza) kuingia katika ulimwengu wa mwili.
Kutoka
34:11-13 “11 Liangalie neno hili ninalokuamuru leo; tazama, mbele yako namtoa
Mwamori, na Mkanaani, na Mhiti, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi. 12 Ujihadhari
nafsi yako, usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi ile unayoiendea, lisiwe
mtego katikati yako. 13 Bali utabomoa madhabahu zao, na kuvunja-vunja nguzo zao,
na kuyakata-kata maashera yao.”
Mungu
anawaagiza wana wa Israeli wasifanye maagano na wenyeji bali wabomea madhabahu
zao kwani matatizo ili yakupate lazima yatokee katika madhabahu ya shetani.
Kumb
12:2-3 “2 Vunjeni kabisa mahali pote walipokuwa wakiitumikia miungu yao mataifa
mtakayoyamiliki, juu ya milima mirefu, na juu ya vilima, na chini ya kila mti
wenye majani mabichi; 3 nanyi zivunjeni madhabahu zao, zibomoeni nguzo zao, na
maashera yao yateketezeni kwa moto, na sanamu za kuchonga za miungu yao zikateni;
na jina lao lifutilieni mbali na mahali hapo.”
MAMBO
MUHIMU YANAYOUNDA MADHABAHU
1. Mungu wa madhabahu
2. Kuhani wa madhabahu
3. Washirika wa madhabahu
4. Kafara ya madhabahu
5. Nguvu ya madhabahu
1. MUNGU WA MADHABAHU
Neno
“mungu” ni nafasi au cheo kama ilivyo kwa Rais. Kwa maana hiyo unapotaja jina
la mungu inakubidi uainishe ni mungu yupi unayemtaja.
Kutoka
6:1-3“1 Bwana akamwambia Musa, Sasa utaona nitakavyomtenda Farao; maana kwa
mkono hodari atawapa ruhusa kwenda zao, na kwa mkono hodari atawafukuza katika
nchi yake. 2 Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA; 3 nami
nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina
langu YEHOVA sikujulikana kwao.”
**MUNGU
WA MADHABAHU ZA KISHETANI
shetani
ndiye mungu wa madhabahu za wachawi, waganga wa kienyeji, wasoma nyota na
mawakala wote wa mauti.
2Kor
4:4“ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini,
isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.”
1Wafalme
16:32“31 Ikawa, kama ingalikuwa neno dogo tu kuyaendea makosa ya Yeroboamu
mwana wa Nebati, akamwoa Yezebeli binti Ethbaali, mfalme wa Wasidoni, akaenda
akamtumikia Baali, akamsujudia. 32 Akamjengea Baali madhabahu katika nyumba ya
Baali, aliyoijenga huko Samaria.”
*****FANYA
MAOMBI YA KUWAANGAMIZA MIUNGU WA MADHABAHU ZA KISHETANI*****
2. KUHANI WA MADHABAHU
Kuhani
wa madhabahu ni mtu mwenye uwezo wa kuleta mambo kutoka ulimwengu wa roho
kuingiza katika ulimwengu wa mwili.
Mwanzo
14:18 “Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa
kuhani wa Mungu Aliye juu sana.”
**KUHANI
WA MADHABAHU ZA KISHETANI
1
Samweli 5:5 “Kwa hiyo makuhani wa Dagoni, na mtu awaye yote aingiaye nyumbani
mwa Dagoni, hawakanyagi kizingiti cha nyumba ya Dagoni huko Ashdodi, hata leo.”
1Wafalme
18:25-26 “25 Eliya akawaambia manabii wa Baali, Jichagulieni ng'ombe mmoja,
mkamtengeze kwanza; maana ninyi ndio wengi; mkaliitie jina la mungu wenu, wala
msitie moto chini. 26 Wakamtwaa yule ng'ombe waliyepewa, wakamtengeza,
wakaliitia jina la Baali tangu asubuhi hata adhuhuri, wakisema, Ee Baali,
utusikie. Lakini hapakuwa na sauti, wala aliyejibu. Nao wakaruka-ruka juu ya
madhabahu waliyoifanya.”
****
FANYA MAOMBI YA KUWAANGAMIZA MAKUHANI WA MADHABAHU ZA KISHETANI
3. KAFARA YA MADHABAHU
Madhabahu
haiwezi kukamilika kama hakuna kafara kwasababu kila mungu wa madhabahu
huhitaji kafara.
Walawi
2:2“kisha atauleta kwa wana wa Haruni, hao makuhani; naye atatwaa konzi moja
katika huo unga mwembamba, na katika mafuta yake, na huo ubani wote; kisha
kuhani atauteketeza kuwa ndio ukumbusho wake juu ya madhabahu, ni kafara ya
kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana;”
Zaburi
40:6“6 Dhabihu na matoleo hukupendezwa nazo, Masikio yangu umeyazibua, Kafara
na sadaka za dhambi hukuzitaka.”
Zaburi
50:8“Sitakukemea kwa ajili ya dhabihu zako, Na kafara zako ziko mbele zangu
daima.”
**KAFARA
KWENYE MADHABAHU YA KISHETANI
Zaburi
106:36-38“36 Wakazitumikia sanamu zao, Nazo zikawa mtego kwao. 37 Naam, walitoa
wana wao na binti zao Kuwa dhabihu kwa mashetani. 38 Wakamwaga damu isiyo na
hatia, Damu ya wana wao na binti zao, Waliowatoa dhabihu kwa sanamu za Kanaani;
Nchi ikatiwa unajisi kwa damu.”
Yeremia
32:35“Tena walijenga mahali palipoinuka kwa Baali, palipo katika bonde la mwana
wa Hinomu, ili kuwapitisha wana wao na binti zao katika moto kwa ajili ya
Moleki, jambo nisilowaagiza; wala halikuingia moyoni mwangu kwamba walitende
chukizo hilo; wapate kumkosesha Yuda.”
****MAOMBI
YA KUANGAMIZA KAFARA ZA MADHABAHU ZA KISHETANI
4. WASHIRIKA WA MADHABAHU
Washirika
wa madhabahu ni watu muhimu sana kwenye madhabahu. Kama vile wewe ulivyo ni
mshirika wa kanisa Fulani vivyo hivyo kila madhabahu ya kishetani inayo
washirika wake.
Eliya
alifahamu umuhimu wa kuwa na washirika. 1Wafalme 19:9-10“9 Akafika kunako
pango, akalala ndani yake. Na tazama, neno la Bwana likamjia, naye akamwambia,
Unafanya nini hapa, Eliya? 10 Akasema, Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya Bwana
Mungu wa majeshi; kwa kuwa wana wa Israeli wameyaacha maagano yako, na
kuzivunja madhabahu zako, na kuwaua manabii wako kwa upanga; nami nimesalia,
mimi peke yangu; nao wanitafuta roho yangu, waiondoe.”
Mungu
anamtoa Eliya hofu 1Wafalme 19:18“Pamoja na hayo nitajisazia katika Israeli
watu elfu saba, kila goti lisilomwinamia Baali, na kila kinywa kisichombusu.”
**WASHIRIKA
WA MADHABAHU ZA KISHETANI
Hawa
ni watu hatari sana, kwakuwa matatizo yote huanzia kwenye madhabahu za
kishetani, wanao peleka jina lako/kazi yako/ndoa yako/elimu yako…… ni washirika
wa madhabahu ili lijadiliwe kwa lengo la kuharibu maisha yako.
Washirika
wa madhabahu ya kishetani mara zote ni watu wako wa karibu
Waamuzi
16:5 “Nao wakuu wa Wafilisti wakamwendea, wakamwambia, Mbembeleze, upate kujua
asili ya nguvu zake nyingi, na jinsi tutakavyoweza kumshinda, tupate kumfunga
na kumtesa; nasi tutakupa kila mtu fedha elfu na mia moja.”
Mathayo
10:36“na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake.” Na Mika 7:5-6“5 Msimwamini
rafiki, msimwekee kiongozi tumaini; ilinde milango ya midomo ya kinywa chako
ili mkeo alalaye kifuani mwako asijue habari. 6 Kwa maana mwana humwaibisha
babaye, na binti huondoka ashindane na mamaye; na mwanamke aliyeolewa
hushindana na mavyaaye; adui za mtu ni watu wa nyumbani mwake mwenyewe.”
****MAOMBI
YA KUWAANGAMIZA WASHIRIKA WA MADHABAHU ZA KISHETANI
5. NGUVU YA MADHABAHU
Nguvu
ya madhabahu inategemea mambo yote yanayounda
madhabahu yaani Mungu wa madhabahu, kuhani wa madhabahu, kafara ya
madhabahu na washirika wa madhabahu.
Mashetani
walio katika madhabahu wanao mfumo wa uongozi wa kifalme. Imeandikwa Waefeso
6:12 “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya
falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya
katika ulimwengu wa roho.”
****FANYA
MAOMBI YA KUHARIBU NGUVU YA MADHABAHU ZA KISHETANI
Isaya
47:9-12 “9 lakini mambo haya mawili yatakupata katika dakika moja siku moja,
kufiwa na watoto, na ujane; yatakupata kiasi kitimilifu, uchawi wako ujapokuwa
mwingi, na uganga wako mwingi mno. 10 Maana umeutumainia ubaya wako; umesema,
Hapana anionaye; hekima yako, na maarifa yako yamekupotosha, nawe umesema
moyoni mwako, Mimi ndiye, wala hapana mwingine zaidi yangu mimi. 11 Kwa sababu
hiyo ubaya utakupata; wala hutajua kutopoa kwake; na msiba utakuangukia;
hutaweza kuuondoa; na ukiwa utakupata kwa ghafula, usioujua. 12 Simama sasa na
uganga wako, na wingi wa uchawi wako, uliojitaabisha nao tangu ujana wako;
labda utaweza kupata faida, labda utaweza kushinda.”
Ezekiel
13:17-22“17 Na wewe, mwanadamu, kaza uso wako juu ya binti za watu wako,
watabirio kwa akili zao wenyewe; ukatabiri juu yao, 18 useme, Bwana MUNGU asema
hivi; Ole wao wanawake wale, washonao hirizi katika viungo vyote vya mikono,
wawekao leso juu ya vichwa vya kila kimo, ili wawinde roho za watu; je!
Mtaziwinda roho za watu wangu, na kuzihifadhi hai roho zenu wenyewe? 19 Nanyi
mmeninajisi kati ya watu wangu, kwa ajili ya makonzi ya shayiri na vipande vya
mkate, ili kuziua roho za watu ambao haiwapasi kufa, na kuzihifadhi hai roho za
watu ambao haikuwapasa kuwa hai, kwa kuwaambia uongo watu wangu wasikilizao
uongo. 20 Basi Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni kinyume cha hirizi zenu,
ambazo kwa hizo mnaziwinda roho za watu kama ndege, nami nitazitoa katika
mikono yenu kwa nguvu; nami nitaziachilia roho zile mnazoziwinda kama ndege. 21
Na leso zenu nazo nitazirarua, na kuwaokoa watu wangu katika mikono yenu, wala
hawatakuwa katika mikono yenu tena kuwindwa; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi
Bwana. 22 Kwa kuwa ninyi mmemhuzunisha moyo mwenye haki kwa uongo, ambaye mimi
sikumhuzunisha; na kuitia nguvu mikono ya mtu mbaya, hata asigeuke, na kuiacha
njia yake mbaya, na kuhifadhika; 23 basi, kwa sababu hiyo ninyi hamtaona tena
ubatili, wala kutabiri mambo; nami nitawaokoa watu wangu katika mikono yenu;
nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.”
0 Comments