
MAOMBI YA KUMUOMBA MUNGU ILI AFANYE JAMBO JIPYA. Na Peter M Mabula. Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU. BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU na kisha tuombe maombi ya ushindi sana. Leo tunamuomba MUNGU afanye jambo jipya katika maisha yetu. Kama magonjwa yalitutawala leo MUNGU BABA anafanya jambo jipya kwa kuleta uponya wake. Isaya 43:19 '' Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani.'' MUNGU wetu anaenda kufanya jambo jipya, Hata baraka ambazo tuliziona haziwezekani kwetu leo kwa maombi yetu kupitia jina la YESU KRISTO tunaenda kufanikiwa. Kwanini MUNGU afanye jambo jipya? Ni kwa sababu '' hakuna neno lisilowezekana kwa MUNGU.-Luka 1:37'' Kwanini JEHOVAJ MUNGU wetu atende jambo jipya? Yeye MUNGU anakuuliza wewe akisema; '' Tazama, mimi ni BWANA, MUNGU wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisilol...