KAMA UMEZALIWA, UNATAKIWA KUKUA

KAMA UMEZALIWA, UNATAKIWA KUKUA

Na Mwl Nickson Mabena

Bwana Yesu asifiwe, karibu kwenye mada inayosema JINSI YA KUUKULIA WOKOVU, 
Hapa nitakushirikisha kidogo, vitu vichache vitakavyokusaidia kufanya tathimini ya UKUAJI WAKO!. 
Kicha cha ujumbe, nimekwambia KAMA UMEZALIWA, UNATAKIWA KUKUA!. 
Biblia inatufundishwa kwamba, Mwanadamu baada ya Kuzaliwa mara ya kwanza, anatakiwa kuzaliwa mara ya pili, 
"Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu" YOHANA 3:3
" *Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho*". YOHANA 3:6, 
Roho ndiye anaizaa roho yako kwa NENO la Kweli, 
Ile siku unaokoka, 
Kama hujaokoka, maana yake, umezaliwa na MWILI, bado unatakiwa kuzaliwa tena mara ya pili, 
Ndio maana kuokoka ni LAZIMA, 
Ndio Maana Kuokoka sio Dhehebu, 
Ndio Maana hauokoki kwa sababu umerithi kwa Wazazi, 
KUOKOKA NI KUZALIWA MARA YA PILI, 
Angalia, "Kwa kupenda kwake mwenyewe *alituzaa* sisi kwa neno pa kweli, tuwe kama limbuko la viumbe vyake" YAKOBO 1:18
Angalia, " *Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili*; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele." 1PETRO 1:23
Si tayari umeshaelewa kwamba UMEZALIWA?,
Kama umekubali kwamba Umezaliwa, Ukae ukijua UNATAKIWA KUKUA..

Ngoja tuangalie, kuhusu KILICHOZALIWA NA MWILI.
Siku Ulipozaliwa, Wazazi/walezi wako walikuwa wanafanya Juhudi Kubwa ili UKUE KIMWILI, 
Mzazi ataenda Clinic, kuangalia Ukuaji wa Mtoto, kama Ukuaji ni Mbaya, Madaktari watamshari Mzazi, KUHUSU AINA YA VYAKULA VYA KUMLISHA MTOTO HUYO, 
Hali ikiwa mbaya ZAIDI MTOTO ANAWEZA AKALAZWA 
(Kama unataka ujue maendeleo ya Ukuaji wako ulipokuwa mdogo, kaitafute kadi yako ya kliniki uangalie),
Mzazi hayupo tayari kuona Miaka inaenda, lakini mtoto wake HAKUI NA KUONGEZEKA, 
Hayupo tayari Mtoto wake ale chakula chochote tu, ilimradi ameshiba!. 
Mzazi mwingine, hakubali Mtoto wake akakae kwa Ndugu, kwa sababu akienda kwa ndugu, anarudi amekonda, au anaumwa!. 
Nakumbuka, wakati nasoma, kila nikirudi nyumbani likizo, Mama akinipokea, ananiangalia kama NIMENENEPA KWA AFYA,
Kwa sababu nilikua nasoma Bweni, mara zote nilikua narudi nimeisha kweli, 
Alichokua anakifanya, ananitengenezea *Special diet* ili kurudisha Afya!.
MZAZI YUPO TAYARI KUINGIA GHARAMA KUBWA, KUSAFIRI UMBALI MREFU, KUWATAFUTA WATAALAMU, ILI KUCHEKI UKUAJI WA MTOTO WAKE!. 
Ok,
Kama hivyo, tunafanya Kwa ajiki ya Mambo ya MWILINI TU, 

Twende rohoni kidogo,
Wewe si umezaliwa mara ya pili?, roho yako si imezaliwa upya?,
Je! Ni lini ulipohangaika ili UKUE?, 
Pengine UMEDUMAA, Umri wa kuzaliwa mara ya pili ni mwingi, Kuliko, UKUAJI WAKO, 
Pengine Ulikua, alafu ukapungua/ukashuka!.
Pengine ukuaji wako ni wa spidi ndogo sana, 

Pengine, hata hujui kama umezaliwa au bado,
JE! UMERIDHIKA NA UKUAJI WAKO KIROHO?
JE! UMEFIKA MWISHO WA KUKUA KWAKO?
NAJUA WAKRISTO WENGI HAWANA TABIA YA KUJIFANYIA CHECKUP YA KIROHO, 
WAMERIDHIKA TU, KISA WANAVIDHEHEBU VYAO, 
WAPOWAPO TU, KISA WANAIMBISHA MAKANISANI, 
Hebu jikague kague na wewe, upo kundi gani?
Nimesukumwa sana nikwambie, 
*KAMA UMEZALIWA, UNATAKIWA KUKUA!.*
Tukutane sehemu ijayo, nikusaidie kujua JINSI YA KUUKULIA WOKOVU!.
Naitwa,
Mwl. Nick
0712265856
(WhatsApp#)

Post a Comment

1 Comments

  1. Ubarikiwe Pia ni vizuri watu kufahamu namna ya kuongeza nguvu za rohoni...Kwa maelezo mapana tembelea link hii >>> https://wingulamashahidi.org/2019/06/17/nitaongezaje-nguvu-zangu-za-rohoni/

    ReplyDelete