MAMBO YA KUFANYA ILI FIKRA ZAKO ZITUMIKE KUFANIKISHA MAISHA YAKO_

Na Mwl Christopher Mwakasege.



*Lengo la Somo:*
_Kutambua maarifa ya kutumia fikra zako kupata Mafanikio maishani._

*MSINGI WA SOMO.*
Mithari 23:7a
*_Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo._*

*Omba MUNGU akusaidie uweze kupata kutoka kwenye vitabu maarifa unayoyahitaji ili uhitajike.*
Danieli 12:4
4" Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka.

1. Ni vyepesi mtu kuhitajika akiwa ana maarifa yanayohitajika katika kipindi husika. 
Danieli 1:17~21
17' Basi, kwa habari za hao vijana wanne, Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; Danieli naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto.18' Hata mwisho wa siku zile alizoziagiza mfalme za kuwaingiza, mkuu wa matowashi akawaingiza mbele ya mfalme Nebukadreza.
19' Naye mfalme akazungumza nao; na miongoni mwao wote hawakuonekana waliokuwa kama Danieli, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria; kwa hiyo wakasimama mbele ya mfalme.20' Na katika kila jambo la hekima na ufahamu alilowauliza mfalme, akawaona kuwa walifaa mara kumi zaidi ya waganga na wachawi waliokuwa katika ufalme wake.21' Tena, Danieli huyo akadumu huko hata mwaka wa kwanza wa mfalme Koreshi.

*Watu wanapata shida sana wakidhani wakiwa na elimu ni guarantee kupata kazi lakini kiuhalisia sio hivo. Kina Daniel walilipiwa na serikali ya kina Nabukadreza na walilipiwa wengi lakini walikuja kuchaguliwa wanne tu. Ni vyepesi sana mtu kuhitajika akiwa na maarifa ya kipindi husika kupata kazi.*
Daniel 1:3~4
3' Mfalme akamwambia Ashpenazi, mkuu wa matowashi wake, awalete baadhi ya wana wa Israeli, wa uzao wa kifalme, na wa uzao wa kiungwana;4' vijana wasio na mawaa, wazuri wa uso, wajuzi wa hekima, werevu kwa sababu ya maarifa yao, wenye kufahamu elimu, watakaoweza kusimama katika jumba la mfalme; tena alimwambia awafundishe elimu ya Wakaldayo, na lugha yao.

2. Kuna vitabu vilivyobeba maarifa yanayotakiwa kwa muda husika.(Daniel 12:4)
*Muda ndo unaoamua maarifa yanayotakiwa maana Biblia inasema kuna majira na nyakati kwa kila jambo.* 
Mwanzo 1:1
1' Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.

[HAPO MWANZO] ðŸ‘‰MUNGU aliumba muda kwanza kabla ya mbingu na nchi, maana anaishi katika umilele ingawa yeye ni Alfa na Omega. 
Daniel 1:4
4' vijana wasio na mawaa, wazuri wa uso, wajuzi wa hekima, werevu kwa sababu ya maarifa yao, wenye kufahamu elimu, watakaoweza kusimama katika jumba la mfalme; tena alimwambia awafundishe elimu ya Wakaldayo, na lugha yao.

*Hawa watu walikuwa na maarifa kwa kiwango flani lakini sio ya muda ule ndo mana ilibidi waingizwe shule tena. Fikra zao hazikuwa zinaweza kubeba mambo ya muda ule. Maarifa ambayo mfalme alikuwa anataka si yale yaliyotoka sehemu nyingine.*
Maarifa yanaenda na Lugha, na maarifa yako yanaenda na kupata kazi pia. Ndo mana ukitaka kwenda Germany lazima usome kijerumani mwaka ili maarifa unayoenda kupata huko uweze kuyaelewa.
Ayubu 35:16, 34:35
Sio kila kitabu chenye maneno kina maarifa. Au kina uweze wa kutoa maarifa. Kinaweza kukusaidia kufauli mtihani
3. Vitabu vilivyobeba maarifa vingine vinafungwa visitoe maarifa mpaka muda mwingine wa kuhitajiwa hayo maarifa au muda utakapokuwa umekaribia au umewadia.
Daniel 9:1~3
1' Katika mwaka wa kwanza wa Dario, mwana wa Ahasuero, wa uzao wa Wamedi, aliyetawazwa kuwa mfalme juu ya milki ya Wakaldayo;2' katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danieli, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la BWANA lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini.3' Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu.

#Kitabu chochote ambacho muda wa kuachilia maarifa ukifika, wewe ambaye umesoma utaanza kuweka kwenye matendo kile ambacho umesoma kwenye kile kitabu#
#Ukinunua kitabu lazima uombe sana, ili MUNGU akupe kitabu ambacho maarifa yake utahitaji hapo badae. Unaweza usisome wakati huo, ila utakihitaji hapo badae#
4. Muhimu kwa kitabu kufunguliwa na akili za msomaji kufunguliwa kwa pamoja ili maarifa yaliyomo ndani ya kitabu yawe msaada katika muda husika kwa ajili ya huyo msomaji.
Luka 24:44~49
44' Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi.45' Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko.46' Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu;47' na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu.48' Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya.49' Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.

Katika mistari ya Luka hapo juu kitabu kilikuwa kimefunguliwa ila akili zao zilikuwa zimefungwa, kwa sababu walikaa na YESU muda mwingi ila hawakuelewa. 
5. Muombe MUNGU akukutanishe na vitabu vilivyobeba maarifa unayohotaji na avifungue kama bado vimefungwa ili upate maarifa unayotakiwa kuwa nayo.
Katika kitabu cha Ufunuo 5:1~5, Ufunuo 10:1~11 vinaelezea vizuri kuhusu vitabu. 
*Kitabu kinaweza kikafungwa na ukaomba kikafunguliwa, na kama kikifunguliwa ukiwa huelewi omba MUNGU akupe maarifa yaliyopo kwenye kitabu hicho*
*Muda unaweza ukafika na ukawa unahitaji hayo maarifa na yakawa yamefungwa. Umewahi kufikiri kwanini watu wengi wamesoma lakini sio wabunifu?*
*MUNGU anatafuta kwa namna ambayo watu wawe wanapata maarifa ya ubunifu kwa watu wote

Post a Comment

0 Comments