Posts

Showing posts from October, 2018

JINSI WACHAWI WANAVYOWEZA KUIBA NYOTA YAKO

Image
Salam wapendwa katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo. Leo nipo hapa kuwaletea topic mpya kabisa ambayo wachungaji wengi hawaifundishi makanisani na yamkini baadhi yao hawaijui.kama kichawa cha habari kinavyosema, leo nataka kuzungumza juu ya wachawi.kunawatu wengi sana Duniani wanalia kila wanavyojaribu kuyakwamua maisha yao inashindikana, lakini hawajui ni kwa nini? nataka nikuambie leo, wapo watu ambao Mungu ameamua kuwanyima mali kwa makusudi anayoyajua yeye mwenyewe, na kuna watu ambao Mungu hakuwanyima mali mpango wa mungu ni kwamba watu hawa wapate mali lakini hawana! hapa ni kwamba shetani huamua kuwaonea na kuwadhulumu watu hawa. Unajua kila mmoja wetu anakitu alichopewa na Mungu ili kuweza kuzikamilisha shughuli za ulimwengu huu. ngoja nikupe siri moja kuu sana, kila mwanadamu anapozaliwa huwa anakitu kinachoitwa nyota, kitu hiki ni ishara au ni kitambulisho cha mtu huyo katika ulimwengu wa roho ya kuwa yeye kapewa nini hapa duniani,soma mathayo 2:1-5.biblia inas...

KUBOMOA MADHABAHU ZA SHETANI(Samson Mollel – Uzima wa Milele International Ministries) (Somo limefundishwa na Bishop J. Gwajima – Kitabu cha Maombi ya Kubomoa Madhabahu)

Image
Madhabahu ni nini? Ni daraja la kuunganisha katika ya ulimwengu wa roho wa Mungu au shetani. Kuna aina 2 za madhabahu, Madhabahu ya MUNGU (Nuru)na madhabahu ya shetani (giza) ***MADHABAHU YA MUNGU Watu/watumishi wa Mungu katika Biblia walianza kwa kujenga madhabahu kabla ya kufanya chochote NUHU – Mwanzo 8:20“Nuhu akamjengea Bwana madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.” MUSA – Kutoka 17:15“Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake Yehova-nisi;” YOSHUA – Yoshua 8:30“Ndipo Yoshua alijenga madhabahu kwa Bwana, Mungu wa Israeli katika mlima Ebali.” GIDEONI – Waamuzi 6:24“Ndipo Gideoni akamjengea Bwana madhabahu hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu; hata hivi leo iko huko katika Ofra ya Waabiezeri.” SAMWELI – 1 Samweli 7:17“Na kurudi kwake kulikuwa mpaka Rama; maana ndipo ilipokuwa nyumba yake; nako ndiko alikowaamua Israeli; na huko akamjengea Bwana madhab...

SEMINA YA KUPANDA NA KUVUNA 2017

Image
SADAKA INAYOMFANYA MUNGU AKUKUMBUKE *NA MWL MWAKASEGE* >>Katika kujifunza somo hili nataka tuangalie point kama tano hivi. *1 KUNA SADAKA UNAYOWEZA KUMPA MUNGU NA IKAWA UKUMBUSHO MBELE ZAKE ILI AWE ANAITUMIA KUKUMBUKA* _’’Matendo ya mitume 10:1-4, 31 Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia, mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima. Akaona katika maono waziwazi, kama saa tisa ya mchana, malaika wa Mungu, akimjia na kumwambia, Kornelio! Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu. akasema, Kornelio, kuomba kwako kumesikiwa, na sadaka zako zinakumbukwa mbele za Mungu’’_ >>Hii si sadaka kama zilivyonyingine maana Mungu huwa anaitumia kukumbuka. *2 KUNA VITABU VILIVYOKO MBINGUNI AMBAKO KUNA ANDIKWA VITU AMBAVYO MUNGU ANATAKA VIWE KUMBUKUMBU KWA AJI...

NYOTA KIBIBLIA :ASKOFU GWAJIMA

Image
UTANGULIZI: Huu ni mwendelezo wa somo la Nyota na Maisha mtu aliyonayo. Mathayo 2:1; Kama tulivyoona tangu mwanzo kuwa nyota ni kipawa, uweza, hatma au hali ya mtu ya baadaye. Tukaona nyota ya Yesu ilionekana kabla Yesu hajazaliwa na mamajusi wa mashariki walimwona kama Mfalme. MAANA YA NYOTA: Kama tulivyooa sehemu ya kwanza kuwa nyota ni kiashiria cha rohoni, kinachoonesha mtu atakuwa nani baadaye, mafanikio ya mtu au hatma ya mtu. Viashiria hivi ndivyo vinavyoitwa nyota. NYOTA KATIKA BIBLIA : Hesabu 24:14-17 Baraki alikuwa mfalme, na alipoona kuwa wanaisrael wanakuja ili kushambulia ufalme wake, akamtafuta Balaam amtabirie. Hayo ni maneno ya Balaamu aliyoona, Hivyo Balaamu alipoangalia taifa la Israel akaona nyota, kimsingi nyota ya mtu inaonyesha jinsi mtu atakavyokuwa baadaye. Hivyo balaamu aliweza kumuona Yesu tangu mwanzo na ndio maana mamajusi wa mashariki nao pia walimwona Yesu kama nyota. Nyota yaweza kuonyesha kusudi la maisha ya mtu, na ndio maana ingawa Sul...

SEMINA YA NENO LA MUNGU NA MWL. CHRISTOPHER MWAKASEGE (Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam) SOMO: UPONYAJI KWA WALIOVUNJIKA MOYO NA WALIO NA HAJA YA KUPONA.

Image
SIKU YA NANE Mistari ya kusimamia:  Isaya 61:1   “ Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. ”  Luka 9:11   “Na makutano walipojua walimfuata; akawakaribisha, akawa akisema nao habari za ufalme wa Mungu, akawaponya wale wenye haja ya kuponywa.”  Yeremia 6:14   “Wameiponya jeraha ya watu wangu kwa juu juu tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani.” SOMO LA LEO: UPONYAJI KWA WALIOVUNJIKA MOYO KWASABABU YA KUCHOKA MOYONI KULE KUNAKOLETA KUKATA TAMAA. 1.       Nini maana ya kuchoka moyoni kunakoleta kukata tamaa? Ø    Kukata tamaa ni maneno mawili. Kukata. Tamaa. Ø    Tamaa maana yake ni hamu, kiu, msukumo, kiu  kutoka moyoni wa kutaka kupata unachotaka kukipata. Ø    Kukata ni kuachanisha au...