MANENO NA MISEMO YA MAISHA KUTOKA KWA WATU KUMI MASHUHURI DUNIANI
Hekima huja sio tu kwa kuona
matendo yasiyo na busara ndani yake. Bali hekima hujipambanua katika umbo la
uelewa na ufahamu ,pale tu uwapo tayari kusikiliza sauti mhimu toka
moyoni mwako.Miongoni mwa sauti hizi ni pamoja na ile nia ya kutafuta
ukweli wa jambo, kutafta maamuzi sahihi na kupata mawazo endelevu ,
na yakinifu. Endapo mmoja ana kiu katika kuona matunda ya sauti hizi,
huyu mtu ni wazi kuwa ana chemichemi za hekima ndani yake. Kama ilivyo kwa ufahamu,
hekima halikadharika hupatikana kwa mtu yeyote aliye na nia kama zilizotajwa
hapo juu. Huyu mtu wa hekima na busara hutoka katika tabaka la aina
yeyote.Kuanzia kwa wazee, vijana, wanaume, wanawake, mabwana,
watumwa, tajiri, masikini, wasomi hadi wasiosoma .Matabaka haya ya watu
katika jamii hayahukumu mgawanyo wa hekima na busara ndani ya vichwa vya
wanajamii.Hugawanya tu mitazamo yao. Kutokana na hali hii tunapata misemo,
maneno, nahau na methati juu ya maisha, kazi, dini , tamaduni na vitu chungumzima
vinavyosukuma gurudumu la jitihada katika maendeleo ndani na nje ya jamii zetu
. Misemo, maneno na aina nyingi za fasihi simulizi mara nyingi zimekuwa
haziathiriwi na vipindi, nyakati hata muda. Ni kwa kuwa fikira pevu,chanya na
yakinifu zilitumika kuchimbua mizizi ya hekima iliyokuwa imejificha chini sana.
Na hizi fikira ni matokeo ya ugumu na urahisi wa mapambano ya kila
siku zidi ya maisha , yanaoibua uzoefu wa kukabiliana na changamoto za
mara kwa mara au zile zinazofanana. Hapa ni maneno na misemo ya maisha toka kwa
watu kumi mashuhuri duniani.
1.''Maisha ni kile kinachokutatiza
wakati unapangilia mikakati yako ''John Lennon(mwanamziki)
2.''Maisha ni asilimia 10 ya kile kinachonipata na asilimia 90 ni
kile nikifanyacho katika kukabiliana na hiyo hali'' Charles
Swindolls(mchungaji)
3.''Muda wako unakikomo, kamwe usipote kwa kujaribu kuishi maisha ya mtu
mwingine''Steve Job(mhasisi wa Kampuni ya Apple )
4.’’Maisha huchanua na kusinyaa kutokana na ujarisi wa mtu husika''Anais Nin(mwandishi wa kihispania)
5.''Enenda wima katika ndoto zako,na utaishi maisha uliotaraji''Henry David Thoreau(mwandishi wa kimarekani)
6.''Maisha hayapimwi kwa idadi ya
pumzi tuivutayo ,hupimwa kwa idadi za hatua zichuako pumzi zetu''Maya
Angelou(mshairi)
7.''Changamoto hupendezesha maisha,na kukabiliana nazo ndio maana halisi ya maisha''Joshua J Marine(mtoa nukuu)
8.''Mtu hata badili maisha yake
kama hakuanza na kubadiri fikira zake''William James(mwanasaikolojia)
9.''Kwa kutazama tu ulichonacho maishani ,kila siku utahisi unazaidi,ila
kwa kutazama unachokosa maishani kamwe hutokuwa na zaidi''Oprah
Winfrey(muongozaji wa maonyesho ya televisheni)
10.''Maisha ni kile ukitendacho,ipo hivyo.itakuwa hivyo''Grandma
moses(msanii wa vitu asili katika umri mkubwa)
barikiwa mtumishi
ReplyDeleteMaisha yetu hapa duniani yanatanabaishwa saana na hulka tuliyoamua kuiishi, ukitenda mema, utavuna mema, ukitenda mabaya utavuna mabaya, ukifanya kazi kwa bidii utafaidi matunda ya bidii yako
ReplyDeleteEngineer Elisony mtoto wa Mweladzi
ok asanteh kwa maneno ya faraja aseeee
Deletemaneno mazuri
ReplyDeleteYako powa
ReplyDeleteSaf sana
ReplyDeletemungu yupo tayari kumuongoza yeyote yule anayemwomba usaidizi. yaani yeye yupo tayari ni mimi na wewe ndio hatupo tayari.
ReplyDelete