Posts

UNAPOHITAJI MFANIKIO TAFADHARI ACHANA NA MAMBO HAYA HARAKA SANA.

Image
1. Acha kutegemea mafanikio ya haraka.Mara nyingi hizi ndizo zimekuwa ndoto nyingi za watu wengi kutaka kuona mafanikio makubwa na ya haraka. Mafanikio yoyote huwa yanajengwa hatua kwa hatua. Tena kuna wakati huwa ni hatua za kutambaa mithili ya mtoto mdogo. Kama utategemea mafanikio ya haraka zaidi katika maisha yako hutayapata zaidi ya kujidanganya wewe mwenyewe. Acha kung’angania mafanikio ya haraka, utakwama. Jiwekee malengo kisha songa mbele. SOMA; Jinsi Ya Kuweka Malengo Utakayoyafikia. 2. Acha kuwa mtu wa visingizio.Hili ni jabo mojawapo ambalo umekuwa ukiling’ang’ania mara kwa mara katika maisha yako. Umekuwa ni mtu wa visingizio kwa kudai kuwa huwezi kufanikiwa kwa sababu hukusoma, huna mtaji ama umetoka katika familia maskini. Kutokana na visingizio hivyo umekuwa huchukui hatua yoyote zaidi ya kuzidi kufanya maisha yako kuwa magumu. Ili uweze kufanikiwa, achana na kung’ang’ania visingizio kama mkombozi wako. Badala yake, chukua hatua juu ya maisha yako. S...

SOMO: WOKOVU MKUU

Image
  WARUMI 5 –8 UTANGULIZI •Kwakuwa Mungu ametumia gharama kubwa kuleta wokovu duniani, katika huo, imeachiliwa nguvu inayo weza kuleta faida kubwa katika maisha ya mwanadamu •Ili tuweze kupokea faida   inayo ambatana na wokovu, lazima tuujali na kuuishi katika wokovu halisi katika maisha yetu. •Itakuwa rahisi kwetu kuujali wokovu kama tutatambua gharama iliyotumika kuleta wokovu MAANA YA WOKOVU 1.      WOKOVU NI ZAWADI YA MUNGU KWA WAMINIO Tofauti na mshahara (dhawabu) ambayo hutolewa kulingana na kazi ya mtu na kwa makubaliano, zawadi hutolewa kwa mtu kulingana na furaha ya yule anayetoa na sio kwa kazi ya yule anayepokea. Wokovu ni zawadi ya Mungu inayotokana na furaha yake kwetu tunapomwamini yeye, na Yesu kristo aliyemtuma. Kama ingetokana na kazi hakuna mtu angeyeweza kufanya kazi ya kustahili ijara inayolingana na thamani ya wokovu. Hivyo Wokovu si matokeo ya matendo mema, kusali, kufunga wala kutoa sadaka nyingi bali ni m...

MAOMBI MAKALI YAKUOMBA NA KUFUNGULIWA.

*MUNGU akukumbuke. BWANA akutendee muujiza mkuu. MUNGU ayakumbuke machozi yako. Kwa jina la YESU KRISTO umeshinda. BWANA YESU alisema kwamba kila tutakalolifunga duniani na mbinguni limefungwa Mathayo 18:18. Hivyo tunawafunga wachawi wanaokusumbua na watakimbia wenyewe. Kwa jina la YESU KRISTO. umeshindaaaaaaaaa kwa jina la YESU KRISTO. *Nakuombea Masikio yako yafunguke, kifungo cha ulimi wako kilegee uisemee haki yako. Mwili, nafsi na roho yako vifunguliwe na kila aina ya vifungo vya mawazo, maneno na matendo kwa jina na damu ya YESU KRISTO na kwa neno la MUNGU kama lilivyoandikwa katika Marko 7:34-35 '' YESU akatazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia, Efatha, maana yake, Funguka.Mara masikio yake yakafunguka, kifungo cha ulimi wake kikalegea, akasema vizuri.''Mungu akubariki. * Jiwe lililokuwa kizuizi cha kumzuia BWANA kutoka kaburini, liliondolewa na malaika. Na leo wapo watu wengi leo mawe yamewakalia katika maisha yao, kuna mawe yamekalia bi...

mafundisho yenye makosa, yanayowaongoza watu katika uzoefu udanganyao.

Hatari za Mafundisho ya Kisasa – mafundisho yenye makosa, yanayowaongoza watu katika uzoefu udanganyao. Wanasema kuwa aina hii ya “mapambano ya kiroho” ni muhimu kwa ajili ya mafanikio ya Injili. Pasipo shaka yoyote huo ni udanganyifu. Lakini tena wanatuambia kuwa kutakuwa na “majeruhi” miongoni mwa Wakristo, kwa sababu Wakristo wengi “hawana silaha zifaazo” kwa ajili ya aina hii ya mapambano au hawajafahamu “jinsi ya kupigana” aina hii ya vita! Lakini wazo la kuwa mtu anajishughulisha na vita vya kweli vya kiroho inaweza kumletea matokeo ya roho chafu kukushambulia na kuharibu maisha ya familia yake ni mafundisho yasiyo na maana na yasiyo ya Kibiblia. Hii ni zaidi ya aina fulani ya mafundisho ya ulozi ambayo yanaweza tu kuwaletea watu hofu katika mioyo yao. Hata kama chanzo cha majanga ambayo tunaelewa yanawaangukia wakristo, yanaweza kuwa ni kutokana na kujihusisha kwao na aina hii ya vita vya kiroho ambavyo sio vya Kibiblia, hii ni hoja ya kuijadili kama nilivyokwisha sema...