Posts

UPENDO KWA YESU

KWA MWAKA MZIMA YESU  AMEKUWA MWAMINIFU. NI VEMA   UKIPATA NEEMA YA KUINGIA MWAKA MPYA  UKAIMARISHA UPENDO WAKO KWAKE

UWEZA WA DAMU YA YESU KUTATUA MATATIZO YA KURITHI (1) – MWL MWAKASEGE

Image
LENGO LA SOMO. kujifunza namna ya kutumia  Damu ya Yesu katika kutatua matatizo ya kurithi. Kila siku Mungu atakuwa anaongeza kitu ndani yako ili uwezo kuitumia Damu ya Yesu kwa ajili ya kuchukua hatua ili kuomba. Kwa hiyo tutakuwa tunajifunza na kuomba hapa ili kuweka kwenye matendo kile tunachojifunza. Kwa hiyo tutakuwa tunajifunza hapa na itakusaidia kuomba kwa ajili yako na mtu mwingine. Hamna sababu ya kusoma shule kama huna mpango wa kutumia unachosoma ina maana unapoteza muda kama hutatumia hicho ulichojifunza hapa. Mungu kakuleta mahali hapa chini ya Mwalimu ina maana unatakiwa kujifunza ili utumie maarifa haya.  Kwa sababu umepata hii nafasi itumie vizuri kujifunza na kuweka kwenye matendo kile ulichojifunza. MTIRIRIKO WA SIKU YA LEO WAKATI TUNAWEKA MSINGI NATAKA TUANGALIE POINT KADHAA HAPA 1. Kurithi ni kitendo cha kupokea kitu kwa kuwa umechaguliwa uwe mrithi wa hicho kitu. Maana kurithi si kwa kila mtu maana tunapewa kuri...

KAZI KUMI(10) ZA MUNGU KAMA MTETEZI WAKO IKIWA UNA SIFA ZA KUTETEWA NA YEYE.

Image
Na Peter M Mabula. Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Leo tunaangalia baadhi ya kazi za MUNGU akiwa kama mtetezi wako, lakini tu ukiwa na sifa za yeye MUNGU kukutetea wewe. Siku moja wachawi walikuja katika eneo ambalo nilikuwa nimelala, ghafla ROHO wa MUNGU akaniondolea usingizi nikajikuta nimeamka na nikagundua kabisa natakiwa niombe japokuwa nilikuwa sijaona chochote. Niliomba kidogo kisha nikalala, baada ya muda nikasikia sauti tena ikisema ''Amka uombe'' nikaamka na kuomba kidogo kisha nikalala, baadae tena nikasikia sauti ikisema ''Amka uombe, nikaamka na na kujikuta naangalia nje ya dirisha maana lilikuwa dirisha la wazi kiasi unaweza kuona kila kitu nje. Nilipotazama niliona wachawi wawili wanaume na wananirushia moto lakini moto ule kila wakirusha unatoka mwingi kisha kabla haujanifikia unazima, wanakazana na huku wakiongea maneno ya kunifunga na kuchochea ...

MAMBO YALIYOTOKEA BAADA YA YESU KRISTO KUPANDISHWA MSALABANI.

Image
Na Peter M Mabula. Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU Bwana YESU atukuzwe sana. Karibu tujifunze ujumbe mfupi huu. Luka 19:10 '' Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea. ''   Hilo ndilo kusudi kuu la Bwana YESU kuja duniani. Yohana 3:16-21 ''Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU. Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa. Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendw...
Image
wakati mwingine tunahisi hatumuoni Mungu wala hasikii maombi yetu,lalin kumbe ni sisi wenyewe tunashindwa kujitathimin na kujiweka vizuri na Mungu .Lakini vitu vinavyokwamisha maombi yetu yasiwe na majibu/manufaa 1.MAOVU     Isaya 59:1-2  maovu yetu ndiyo sababu kubwa  Mungu anashindwa kujidhihirisha  kwetu maovu yetu yanatufarakanisha na uso wa Mungu 2.KUKATA TAMAA   Roho ya kukata tamaa ni kizuizi kikubwa katika maisha yetu. 3.LENGO BAYA Maombi ya kujisifu Mungu hawezi kujidhihirisha (TUFANYE MAOMBI KWA AJILI YA UTUKUFU WA MUNGU NA KUMWINUA) na Mungu atajidhihirisha kwetu. 4.KIBURI Luka 18:10-14 Kuomba kwa kutokuangalia hali ya kimaisha utajiri,umaskini na mengineyo. 5.MAOMBI Mambo katika ulimwengu wa Roho hayaendi pasipo imani 6. KUSAMEHE Watu wengi tunashindwa kusamehe tunashindwa kujiachilia tunabeba vitu vizito moyoni mwetu (uchungu) Mungu anaangalia moyo wa mtu,Mungu hakai mahali penye huzuni jifunze kusamehe.Marko 5:21-27 ...
    JIFUNZE KUUTAFUTA USO WA MUNGU Nimesoma kitabu cha kutoka ...nimejifunza vitu vingi sana juu ya safari ya wana waisrael jinsi ambavyo  Mungu alikuwa pamoja nao kwa sababu walikua n wana wa agano.  Lakin mejifunza zaidi katika KUTOKA 33:12-------  Licha ya kwamba neeema ya Mungu  ilikuwa juu ya Musa  hakuacha kujiona anamhitaji Mungu  wakati wote na Mungu wakati wote. Na  Mungu  akamuahidi kwa uso wake utakwenda pamoja na yeye.Musa hakuona kuwa kuambiwa na Mungu tu imetosha. KUTOKA 33:15 Musa akasema  USO WAKO USIPOKWENDA NA MIMI USITUCHUKUE KUTOKA HAPA . Ni maneno yenye nguvu sana.  Nilichojifunza  kuwa hata kama unakubalika kiasi gan mbele za Mngu kuutafuta uso wa MUNGU  au uwepo  wake katika maisha yetu ni kitu cha lazima.Tunahitaji kutembea katika ktk nguvu/uwepo wa Mungu  wakati wote haijalishi Mungu amekuahidi nini tafuta uso wa Mungu mahali popote  uendako. Musa aliona bila...

MSINGI IMARA

uimara wa nyumba siku zote na pahala popote  upo  kenye MSINGI. hivyo ni vizuri sana kuimarisha msingi kama unataka kuwa na nyumba imara  isiyo teteleka. BAHATI NZURI TUNAFAHAMU KUWA YESU NI MSINGI IMARA HIVYO TUJENGE MAMBO YETU  HAPO ILI TUSITETELEKE . ENDELEA  KUBARIKIWA SANA