Na Peter Mabula. Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU. BWANA YESU atukuzwe. Karibu tujifunze na tuombe maombi ya ushindi sana. Yeremia 15:20-21 '' Nami nitakufanya kuwa kama ukuta wa boma la shaba juu ya watu hawa; nao WATAPIGANA NAWE; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, ili nikuokoe, na kukuponya, asema BWANA. Nami nitakuokoa na mkono wa watu wabaya, nami nitakukomboa katika mkono wao wenye kutisha. ' ' Neno la MUNGU linasema kwamba adui zako katika ulimwengu wa roho watapigana na wewe. Maana yake wewe na adui zako kwenye ulimwengu wa roho mtapigana. Katika mapigano au vita kuna mambo mawili; kuna kushinda na kuna kushindwa. Lakini ashukuriwe MUNGU maana ukiwa katika wokovu wake utashinda. Ukiwa muombaji sahihi hakika utashinda. Changamoto ya wakristo wengi huwa hawapigani na adui kimaombi bali wanamkemea tu adui. Kwenye ndoto najua kabisa ni mara nyingi sana umeonyeshwa juu ya vita inayokukabili. Najua kabisa kwenye ...
Na Peter M Mabula. Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU. BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Kanisa ni jumuia ya Wakristo. Kanisa ni watu walioitwa na kutengwa na mambo ya dhambi. 1 Kor 6:17-18 '' Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema BWANA, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa BABA kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,'' Maandiko hayo ni sehemu tu ndogo ya maandiko yanayolitambulisha Kanisa la KRISTO duniani. Kanisa hai wametengwa na uovu wa dhambi na wametengwa na mambo ya kidunia yaliyo machukizo(Machafu). Ndio maana huwezi kumuona Askofu akiwa disko akicheza. Huwezi kumuona Mkristo aliyeokoka akiwa kwa mganga wa kienyeji. Huwezi kumuona Mchungaji anatoa talaka. Huwezi kumuona Mteule wa MUNGU akivuta sigara wala bangi na tena huwezi kumuona mteule wa KRISTO akitumia madawa ya kulevya. Huwezi kuona kanisa wakichukua mapanga na mikuki wakienda kul...
Salam wapendwa katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo. Leo nipo hapa kuwaletea topic mpya kabisa ambayo wachungaji wengi hawaifundishi makanisani na yamkini baadhi yao hawaijui.kama kichawa cha habari kinavyosema, leo nataka kuzungumza juu ya wachawi.kunawatu wengi sana Duniani wanalia kila wanavyojaribu kuyakwamua maisha yao inashindikana, lakini hawajui ni kwa nini? nataka nikuambie leo, wapo watu ambao Mungu ameamua kuwanyima mali kwa makusudi anayoyajua yeye mwenyewe, na kuna watu ambao Mungu hakuwanyima mali mpango wa mungu ni kwamba watu hawa wapate mali lakini hawana! hapa ni kwamba shetani huamua kuwaonea na kuwadhulumu watu hawa. Unajua kila mmoja wetu anakitu alichopewa na Mungu ili kuweza kuzikamilisha shughuli za ulimwengu huu. ngoja nikupe siri moja kuu sana, kila mwanadamu anapozaliwa huwa anakitu kinachoitwa nyota, kitu hiki ni ishara au ni kitambulisho cha mtu huyo katika ulimwengu wa roho ya kuwa yeye kapewa nini hapa duniani,soma mathayo 2:1-5.biblia inas...
Comments
Post a Comment