BWANA
YESU atukuzwe ndugu yangu.
Kwa
furaha kubwa nakukaribisha tujifunze faida za maombi ya kufunga.
Marko
9:23 ‘’ YESU akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye.‘’
-Kwanini
Mengine yanashindwa kuwezekana?
Ni
kwa sababu hatufungi na hata tukifunga basi tunafunga bila kuomba na hata
tukiomba tunaomba kidogo sana.
Baada
ya mimi kuokoka nilikaa siku kadhaa bila hata kuwaza kama huwa kuna kufunga.
Lakini siku moja kwa neema ya ajabu nikasikia sauti ikisema ‘’ Mtu hataishi kwa
mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha MUNGU.’’ Na baada tu
kusikia sauti hiyo nikapata msukumo wa ajabu wa kufunga. Niliazimia kufunga
siku 3 hata hivyo sikuzimaliza. Lakini baadae nilizoea na wakati mwingine
nilikuwa naweza kufunga siku 3 bila kula chochote na kazi mbalimbali nafanya
lakini hawezi kujua mtu yeyote. Maombi ya kufunga ni muhimu sana kwa kila
Mkristo. Kuna watumishi hufunga siku hata zaidi ya 7 bila kula chochote
wakiomba kwa BWANA.
2
Petro 1:10 ‘’ Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na
uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe. ‘’
Kunahitajika
juhudi na nguvu ili tusijikwae. juhudi hizo na nguvu hizo wakati mwingine
zinahitaji kufunga na kuomba.
Luka
2:37 ‘’ Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila
huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba. ‘’
-Maombi
ni maisha kwa mkristo.
-Maombi
ni mkono mrefu wa kupokea kutoka kwa MUNGU.
-Kwa
sababu maombi ni maisha tambua jambo hili kwamba maombi ya kufunga ni sehemu ya
maombi ambayo maombi hayo ni maisha.
-Mama
huyu kweli andiko hapo juu alikuwa na miaka 84 lakini alikuwa akifunga na
kumwomba MUNGU. Kumbe kufunga ni muhimu sana kwako, kama watu wa miaka 84
wanafunga unadhani kuna udhuru utatoa wewe mwenye miaka chini ya 40. Kila mtu
anatakiwa kuomba na wakati mwingi kuomba maombi ya kufunga.
FAIDA
SABA ZA MAOMBI YA KUFUNGA.
1.
Maombi ya kufunga yanaweza kukufanya uongezeke kiimani.
Mathayo
17:21 ‘’ [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.] ‘’
-Kwa
sababu kuna mambo ambayo yatawezekana tu baada ya kufunga, naamini imani yako
itaongezeka kupitia matokeo ya kufunga kwako.
Mfano.
Ulikuwa ukihitaji kupata kazi kwa muda mrefu sana. Uliomba maombi ya kawaida na
bado hukufanikiwa kupata kazi, baada ya kuamua kufunga siku 5 ukajikuta unapata
kazi na pia ukawa unapigiwa simu kwamba unahitajika katika kazi 3 tofauti.
MUNGU amekujibu ombi lako la kupata kazi na nahakika imani yako itaongezeka
sana. Ndio maana nasema hivi maombi ya kufunga yanaweza kusababisha imani yako
ikue, hiyo ndio sifa ya kufunga na kuomba kisha kupokee kutoka kwa BWANA.
2.
Macho yako ya ndani yatakuwa yanaona vizuri.
Zaburi
119:18 ‘’ Unifumbue macho yangu niyatazame Maajabu yatokayo katika sheria yako.
‘’
-Mambo
mengine ya kiroho kuyajua ni lazima ufumbuliwe macho ndipo utaona na kujua.
-Kuna
vitu vingi sana ambavyo sikuwahi kuvijua wala kuviona lakini baada ya maombi ya
kufunga niliona na kushangaa sana.
-Biblia
inaposema kwamba ''Unifumbue macho yangu nitazame'' maana yake mwanzo hakuweza
kutazama na kuelewa hata kama macho anayo ila macho ya ndani yalikuwa yamezibwa
ndio maana hakuona, na katika hilo tunarudi pale pale kwamba ''Mengine
yatawezekana tu baada ya kufunga na kuomba''
-Maombi
ya kufunga yatafungua macho yako ya ndani na na utaona hata maadui walio sirini
ambao wamekutesa kwa muda mrefu.
.
3. Mwili wako utakuwa umetiishwa.
Wakolosai
3:5 ‘’ Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu,
tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;‘’
-Ndugu
yangu, kuutiisha mwili wakati mwingine hauhitaji tu kujaribu kuishi maisha
matakatifu bali ni kuishi maisha matakatifu huku ukiomba na maombi ya kufunga
ndio yaliyo na nguvu zaidi za kukusaidia katika hilo.
-Unapofunga
na kuomba hata kama hukuombea kutiisha mwili wako lakini lazima tu mwili wako
utiishwe kutokana na maombi uliyoomba hata kama hukuombea jambo hilo.
-Maombi
ya kufunga ni tiba kuu ya vitu vinavokutesa ambavyo viko katika mwili wako.
-Kama
unateswa na mwili wako kwa kuwaka tamaa ya ngono, basi funga na kuomba na mwili
wako uttiishwa.
-Kama
mawazo mabaya yanakutesa basi funga na kuomba yataondoka.
-Kitu
chochote ambacho kinakuendesha bila hata wewe binafsi kutaka, lakini unajikuta
tu ukikitii kitu hicho ambacho ni machukizo, basi funga na kuomba utashinda.
1
Thesalonike 5:17 ''ombeni bila kukoma;''
-Njia
mojawapo ya kuutiisha mwili wako hata usinaswe na dhambi wala tamaa mbaya ni
kwa njia ya kufunga.
-Kama
umekuwa unateswa na mawazo machafu yanayokunajisi basi ukifunga na ukaomba
kweli katika kufunga kwako hakika mawazo hayo machafu yataondoka.
-Kufunga
ni muhimu sana kwa wewe ambaye dhambi za zamani zinataka kukuteka tena. Funga
na omba hakika utabaki mshindi daima.
Marko
11:24 ''Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba
mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.''
4.
Kupokea maana ni ahadi ya MUNGU kujibu maombi yako.
Yeremia
29:13 ‘’Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.''
Tena Biblia inasema ''Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni,
nanyi mtafunguliwa;-Mathayo 7:7'' na kwa sababu MUNGU analiangalia neno lake
alitimize basi hata aliposema tuombe ni hakika atajibu maana yeye hajipingi na
Neno lake, labda tu sisi tuombe vibaya na tupungukiwe na imani katika maombi
yetu.
1
Yohana 5:14-15 ''Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu
sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho
chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.''
-Maombi
ya kufunga ni mkono mrefu wa kupokea kutoka kwa MUNGU.
Waebrania
4:16 ''Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na
kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji. ''
5.
Utamruhusu ROHO MTAKATIFU kukutumia.
1
Kor 12:11 ‘’ lakini kazi hizi zote huzitenda ROHO huyo mmoja, yeye yule,
akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye. ‘’
-ROHO
MTAKATIFU humgawia kila mtu huduma kama atakavyo yeye ROHO lakini wakati
mwingine huduma unayo lakini haiendelei kwa sababu huombi ndio maana BWANA YESU
akasema '' Mengine yatawezekana kwa wewe kufunga na kuomba''
-Maombi
ya kufunga ni muhimu sana na inakuwa rahisi zaidi ROHO MTAKATIFU kukutumia
maana hata wewe unakuwa rohoni.
-ROHO
pia anaweza kukutumia kwa maombi.
Warumi
8:26-27 ''Kadhalika ROHO naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba
jinsi itupasavyo, lakini ROHO mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza
kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya ROHO ilivyo, kwa kuwa
huwaombea watakatifu kama apendavyo MUNGU''.
6.
Utatumika kwa MUNGU vizuri
Matendo
13:2-3 ‘’Basi hawa walipokuwa wakimfanyia BWANA ibada na kufunga, ROHO
MTAKATIFU akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia. Ndipo
wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende
zao.’’
-Maombi
ya kufunga yalifungulia njia ya watumishi hawa kuitwa na kupewa jukumu na
MUNGU.
-Hata
wewe unaweza kuwa katika kufunga na MUNGU akasema na wewe jambo fulani ambalo
unatakiwa ulitende, unaweza kujiuliza kwanini ROHO hakusema wakati hawakufunga
na kuomba?
Maombi
ya kufunga ni muhimu sana.
7.
Utakuwa na nguvu za MUNGU.
Mathayo
11:12 ‘’Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana
kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.‘’
-Ndugu,
watu wenye nguvu tu ndio wanaouteka ufalme wa MUNGU. nguvu zinazozungumzwa hapa
sio nguvu za miili ila ni nguvu za rohoni ambazo hupatikana kwa kujifunza neno
la kulijua, kuishi maisha matakatifu, kumtumikia BWANA YESU na kuomba sana. na
maombi ya kufunga ndio maombi ambayo yatakufanya uwe na nguvu zaidi za rohoni
hata shetani asikurudishe nyuma.
''Kama
ningaliwaza maovu moyoni mwangu, BWANA asingesikia. Hakika MUNGU amesikia;
Ameisikiliza sauti ya maombi yangu-Zaburi 66:18-19''
-Ndugu,Naamini
umejifunza na utachukua hatua njema ya kumpokea BWANA YESU kama hujaokoka ili
awe BWANA na MWOKOZI wako tangu leo na utaanza kuishi maisha matakatifu
KAMA
UNATAKA KUTUBU RUDIA MANENO HAYA KISHA TAFUTA KANISA LA KIROHO UKAJIUNGE NA
KUANZA KUISHI MAISHA MATAKATIFU.
''BABA
katika jina la YESU KRISTO Niko mbele zako mimi mwenye dhambi, lakini leo
nimetambua kosa langu na naomba unisamehe dhambi zangu zote, nisamehe dhambi
ninazozikumbuka na pia zile ambazo sizikumbuki. futa jina langu katika kitabu
cha hukumu na uliandike jina langu katika kitabu cha uzima. Neno lako katika
Warumi sura ya 10 Mstari wa 9 na wa 10 Neno lako linasema ''Kwa sababu,
ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako ya
kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata
kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu '' . BWANA YESU mimi
nimekuamini leo na hivyo naamini sasa napokea wokovu wako na hakika nimeokoka.
Kuanzia leo Naufunga ukurasa wa dhambi na ninaufungua ukurasa wa matendo mema
na matakatifu. BWANA nipe ROHO wako Mtakatifu ili aniwezeshe kushinda dhambi na
anasa zote za dunia. Kuanzia leo mimi nimeokoka na ni mtoto wa MUNGU mwenye
haki zote. ninafuta laana zote na kila roho ya shetani inayonifuatilia
naiharibu kwa jina la YESU KRISTO kama neno la MUNGU linavyosema katika Yeremia
sura ya kwanza mstari wa 10. BWANA YESU nakushukuru sana kwa kuniokoa. Yote
haya kwa imani nimepokea na niko tayari sasa kwa ROHO MTAKATIFU kunitumia.
Katika jina la YESU KRISTO nimeomba na kupokea Amen.''
Kama
umetubu toba ya kweli hakika wewe kuanzia sasa ni mshindi na ni shujaa. Kwa
sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.
ulishindwa kumpokea BWANA YESU nafasi yako bado ipo na muda wa kumpokea ni leo
wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na
utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na
wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
MUNGU akubariki sana .
0 Comments