Hadithi nzuri ya kufundisha



Kulikuwa na mfalme  na mtumishi wa kiume ambaye kila mara alimwambia mfalme "Mungu ni mwema na kila afanyalo ni kamilifu" Basi ikatokea wakaenda kuwinda mwituni, ghafla akatokea simba na kuwavamia, mtumishi akafanikiwa kumuua simba lkn hakufanikiwa kumnusuru Mfalme asipoteze kidole kimoja. Kwa hasira mfalme akamfokea mtumishi; ikiwa Mungu ni mwema kwanini hakuzuia nisipoteze kidole?

Mtumishi akajibu kuwa bado Mungu ni mwema na kila afanyalo ni kamilifu. Mfalme akakasirika na kuamuru mtumishi afungwe gerezani. 

Mfalme akaenda peke yake kuwinda na huko akakutana na majitu katili ambao hutoa watu kafara kwa miungu yao. Yakamkamata ili kumtoa kafara lkn wakati yamemweka kwenye madhabahu yao mara yakabaini kwamba hana kidole kimoja hivyo hafai kwa kafara, yakamwachia. 

Mfalme akastaajabu na kuamuru mtumishi atolewe haraka gerezani. Mfalme akamwambia; rafiki yangu KWELI MUNGU AMEKUWA MWEMA KWANGU, ilikuwa niuawe lkn nimepona kwa kukosa kidole kimoja. Lakini nina swali; kama kweli Mungu ni mwema kwanini aliruhusu uwekwe gerezani? Mtumishi akajibu bado Mungu ni mwema na kila alifanyalo ni kamilifu; kama nisingefungwa gerezani tungeenda wote mwituni na hivyo tungekamatwa wote, mimi ningetolewa kafara maana ningeonekana sina upungufu wa kidole. Mungu ni mwema na kamwe hakosei.

Huwa tunalaumu kwa matatizo yanatukabili lakini tunasahau kwamba kila kitu hutokea kwa mpango maalum.

++++++++++++++
Ukipenda kumkumbusha rafikio juu wa wema wa Mungu msukumie ujumbe huu.
++++±++++++++

Omba Mungu akuondolee hofu maana kila afanyalo ni jema na kamilifu

Post a Comment

0 Comments