-Watambue Wababe Walioko Langoni
Wababe wawili wanaolinda lango la kuingilia
kwenye nchi ya ahadi hata leo wanaitwa hofu na kukata tamaa. Ikiwa sasa unasikia
sauti zao, na kuhisi msukumo wa ushawishi wao, basi ujue kwamba upo karibu sana
na ahadi zako.
Katika kipindi hiki muhimu, kama ilivyokuwa
kwa Yoshua, unapaswa kuwa hodari na moyo wa ushujaa na kusonga mbele katika
neema anayokupa Mungu (Yos 1:9).
Elewa Kinachoendelea
Katika 2Kor 4:16,17 Paulo anasema tusilegee
kwa sababu kwa kupitia dhiki yetu utu wetu wa ndani unafanywa upya. Anasema
dhiki yetu nyepesi na iliyo ya muda mfupi tu, inatufanyia kitu chema katika
Mungu.
Tumaini Kwa Mungu
Hata kama imani yako ni ndogo, bado unaweza
kumtumaini Mungu na kuamini kwamba Mungu wa amani atamseta Shetani mara chini ya
miguu yako (Zab 42:5) (Rum 16:20).
Kiri Hitaji Lako, Mshirikishe Mwenzako Kisha
Mwombe
Katika Mhu 4:12 tunaona kwamba uwezo wa watu
wawili ni mkubwa kuliko wa mtu mmoja. Usihifadhi tu mawazo yako, mshirikishe
mwenzako na halafu mwombe pamoja, na kumfunga Shetani.
Pokea Kutoka Kwa Mungu
Fungua moyo wako na umwachie Roho Mtakatifu
akuhudumie kwa habari ya saburi na faraja ya Mungu, tumaini, furaha na amani
(Rum 15:5, 13).
Shughulikia Sababu Za Asili
Wakati Eliya alipokuwa amechoka na kukata
tamaa, Mungu alimpelekea chakula na pumziko kabla hajashughulika na sababu
zenyewe na kumpa neno jipya, mwelekeo mpya, na tumaini jipya (1Fal 19:3-18).
Simama Kwenye Ahadi Ya Mungu
Petro anatuasa kuwa wanyenyekevu chini ya
mkono wenye nguvu wa Mungu, kumtwika Yeye fadhaa zetu, kuwa na kiasi, kumpinga
Shetani na kuwasaidia wengine wanaoteseka. Anatupa tumaini kubwa kwa kusema
kwamba Mungu wa neema yote atatujia mara ili kututengeneza, kututhibitisha na
kututia nguvu (1Pet 5:6-11).
0 Comments