MATHAYO 26;41 Kesheni, mwombe, msije mkaingia
MAJARIBUNI.roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.
Unaweza Ukaomba Mungu
asikuingize majaribuni nawe
ukakwepeshwa ukajikuta hauingii
..Pia unaweza ukaomba ukiwa ndani ya jaribu Mungu akupe
mlango wa kutokea na Mungu akakupa mlango nawe
ukatoka humo 1KOR 10:13
Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya
wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo;
lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili..
Pia unaweza ukaomba usiingie au ukaomba Mungu akupe mlango
wa kutoka ktk jaribu lakini usipewe badala yake Mungu akaamua kupita na wewe
ktk hilo jaribu hadi mwisho
YAKOBO1;1-2 Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu,
mkiangukia katika majaribu mbalimbali, mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani
yenu huleta saburi.
Hivyo wakati mwingine unapita ktk bonde lenye uvuli wa
mauti unatakiwa usiogope maana yeye bado yupo na wewe mnapita wote ktk hayo
mateso
.Anao uwezo wa kukukwepesha usiingie ktk hilo jaribu
lakini ameamua kupita na wewe ili kukufundisha kitu,na mwisho wake ni ushindi
nawe utapewa heshima mmoja wa askari wa Kiroho..Na pia Mungu anaruhusu uingie
ili ajipatie utukufu kwa jamii za wanadamu wajue kweli Mungu yupo na anaokoa
..Ndo maana Kina
Meshaki, Shadraka na Abednego
walipotupwa ktk moto hawakuwa peke yao naye akawa ndani ya moto na
kuwaokoa mwisho wa siku Mungu akajipatia utukufu kwa mfalme Nebukadreza
(DANIELI 3;28) Mungu wao akatukuzwa ktk jamii yote ndiye Mungu aokoae..
Hata Danieli
alipotupwa ktk tundu la simba
wakali ndani ya tundu la simba Danieli hakuwa peke yake malaika alikuwa naye
akamlinda na simba hawakumdhuru..Akatoka salama na Mungu wa Danieli akatukuzwa
ktk jamii YOTE YA DUNIA kuwa ndiye Mungu aponyaye, aokoaye na kutenda
ishara na maajabu..(DANIELI 6;25)
Unapopita ktk jaribu nawe ukishinda Mungu wako anapata
sifa kwa jamii na kutukuzwa ndo maana wakati mwingine lazima upite ktk jaribu
ili Mungu wako apate kutukuzwa nawe pia unaposhinda unapandishwa cheo ktk ulimwengu wa roho huwi vilevile,Yesu
aliposhinda alipewa mamlaka mbinguni na
Duniani..
Basi km Mungu akiruhusu uingie ktk jaribu usidhani km
utapita peke yako naye atakuwepo,utatembea naye ktk hilo jaribu mwisho wake
ushindi,sifa na utukufu zitamwendea Mungu wako aliyekushindia..
MBARIKIWE.
0 Comments