Kadri
siku zinavyokwenda ndivyo mambo MAPYA yanaibuliwa ili kusindikiza imani!
Katika
suala la maombezi, hasa nchini Tanzania, ilikuwa mtu anaombewa tuu kwa kuwekewa
mikono na kwa IMANI anapokea uponyaji na anaondoka amepona.
Mambo
yaliendelea hadi ikafikia mtu anapewa kitambaa, mafuta, bangiri au kitu
chochote kinachobebeka kwa urahisi, kwamba UPONYAJI WAKE UKO NDANI YA HICHO
KITU. Anapewa na kuelekezwa namna ya kukitumia!
Mambo
yameendelea na sasa, kwa mfano, Watu inabidi Wapite, wakanyage mafuta au wapite
kwenye beseni la maji, kwamba kwa kufanya hivyo watapokea UPONYAJI au Majibu ya
mahitaji yao. Na mengine mengi!
Jee,
Katika Hali ya namna hii bado kweli IMANI IPO au sasa TUNAENENDEA KWA KUONA?
Ni wapi
ambako Ukristo Unaelekea?
Haya
mambo yanayofanyika wakati wa maombi, mfano wa hayo yaliyotajwa hapo juu, LENGO
LAKE NI ZURI au BAYA?
0 Comments