KUOKOKA LEO NDIO KUTENGENEZA MAISHA MAZURI YAJAYO.

KUOKOKA LEO NDIO KUTENGENEZA MAISHA MAZURI YAJAYO.

Na Mtumishi Peter Mabula.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Kila jambo duniani lina mwisho wake.
Dunia ina mwisho na kila kiumbe kina mwisho wake.
Lakini Matazamio ya watakatifu ni mbingu mpya na nchi mpya ambayo haki ya MUNGU yakaa ndani yake.

2 Petro 3:12-13 ''mkitazamia hata ije siku ile ya MUNGU, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka? Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.''


Kuna mbingu mpya kwa ajili ya watakatifu.

Kuna uzima wa milele kwa ajili ya watakatifu.
Watakatifu ni wale waliompokea BWANA YESU kisha wanaishi maisha matakatifu. Nafasi ya mtu yeyote kuwa mtakatifu ipo leo.
Jinsi ya kuwa mtakatifu ni kumpokea BWANA YESU kisha kuanza kuishi maisha safi ya wokovu.
Kuna mwisho na mwisho huo upo.
 Mwisho wa kila kiumbe upo lakini watakatifu baada ya mwisho wa dunia tutaanza mwanzo wa milele wenye furaha kuu ambao BWANA YESU ameuumba mwanzo huo uitwao uzima wa milele.

Vitu vizuri vyote vinavyoonekana vitapita na kuishi.

Wakolosai 3:2-10 ''Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na KRISTO katika MUNGU. KRISTO atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu. Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu; kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya MUNGU.  Katika hayo ninyi nanyi mlitembea zamani, mlipoishi katika hayo. Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu. Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake; mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba.''

Aliye na KRISTO anatakiwa ayafikiri yaliyo juu sio yaliyo duniani.
Aliyeokoka anatakiwa ajitenge na dhambi na ajitenge na kila uovu wa duniani.
Hakuna mtu asiyejijua alivyo. Muovu anajijua na mtenda mema anajijua.
Kuna mbingu mpya kwa watakatifu lakini pia kuna ziwa la moto kwa waovu.
Salama ya kila mtu atakaye usalama iko na BWANA YESU.

Kuokoka ni leo ndugu yangu.

Mathayo 3:2 ''Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.''

Heri mwenye dhambi mmoja atubuye kuliko wenye dhambi 199 wasio na haja ya kutubu.
Heri mchawi mmoja atubuye kuliko wachawi 199 wanaoendelea na uchawi.
Heri mzinzi mmoja atubuye kuliko wazinzi 199 wasio na haja ya kutubu.
Heri fisadi mmoja atubuye kuliko mafisadi 199 wasio na haja ya kutubu.
Heri mwenye dhambi mmoja atubuye kuliko wenye dhambi 199 wasio na haja ya kutubu.
Heri mlevi mmoja atubuye kuliko walevi 199 wasio na haja ya kutubu.
Kumbe inawezekana kabisa mwenye haki mmoja akawa na thamani kuliko wenye dhambi 199 wasio na haja ya kutubu. Kuwa mwenye haki inawezekana kwa kila Mtu kupitia kumpokea YESU kisha kutubu kisha unaanza kuishi maisha matakatifu.

Isaya 55:6-7 '' Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa MUNGU wetu, Naye atamsamehe kabisa. ''

 Kuna Watu Hubadilishwa Na Maneno Mabaya Ya Watu Na Kufanya Ubaya. 
Kuna Watu Hubadilishwa Na Neno La MUNGU Na Kuanza Kuishi Maisha Matakatifu. 
Ni Heri Sana Kubadilishwa Na Neno La MUNGU Kwa Kuanza Kuishi Maisha Matakatifu Kuliko Kubadilishwa Na Maneno Mabaya Ya Watu Na Kuanza Kutenda Mabaya. 
Ni Heri Kulitafuta Neno La MUNGU Kuliko Kutafuta Maneno Ya Wanadamu. 
Ukiamua kumpokea YESU hapo unakuwa unatafuta uzima wa milele.Ukiamua kumpokea YESU unakuwa uanalifanyia kazi Neno la MUNGU kwa usahihi wake.
Ndugu. Kuokoka leo ndio kuitengeneza kesho yako yenye furaha.
Kuokoka leo ndio kufanyika mtoto wa MUNGU.
Yohana  3:16-21 ''Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU. Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa. Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika MUNGU.''


Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichaka chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.

Post a Comment

0 Comments