MAHUSIANO YA SADAKA,
BARAKA, MAFANIKIO NA ULINZI.
- Wakristo wengi tunajitahidi kutoa sadaka kwenye uso wa
Mungu lakini ukweli ni kwamba hatujui maana halisi ya tunacho kifanya kwenye
uso wa Mungu, kwa sababu
kama ningelijua nguvu iliyoko ndani ya sadaka katika
maisha yangu ningelitoa kipaumbele katika utoaji wa sadaka.
- Sadaka ni ulinzi wa mambo yafuatayo katika maisha ya mtu
anaye mtegemea Mungu :
i). Afya
ii). Uchumi
iii). Familia
- Kinacho leta shida katika maisha ya Wakristo
hawajajua usahihi wa sadaka katika nyumba ya Mungu, na jambo hili shetani
amepofusha macho ya watu wengi ili wasitambue uthamani,kwa sababu chanzo cha
baraka za mwamini ni madhabahuni.
- Maisha ya watu wengi wanaomwamini Mungu yanaathirika kwa
sababu ya kutokutii agizo ambalo Mungu analizungumza katikati yao kupitia
madhabahu.
- Ufalme wa Mungu umesimama ndani ya madhabahu kwa sababu
matamko ya baraka, matamko ya kuponywa, matamko ya kufunguliwa hayatoki nje na
madhabahu bali yanatoka ndani ya madhabahu, kwa hiyo madhabahu ni kitu
cha kuheshimiwa sana kuliko kitu chochote.
- Sadaka ina nguvu kubwa ya ushawishi ndani yake, kwa hiyo
nikitaka mambo yangu yafunguke kiwepesi kila jambo ninalo lifikiria kulifanya
nilitolee sadaka kwa sababu
Malaki 3:10b, inadhibitisha
maneno haya.
- ( Nikiombewa bila mimi kufuata kanuni bado sitapata
mpenyo, kwa sababu kanuni ndizo zinazo fungua baraka )
- ( Mungu anajaribiwa na sadaka kwa sababu sadaka ndio
inayo gusa moyo wa Mungu )
- Sadaka ina uwezo wa Kukata rufaa ya maisha ya mtu
akaendelea kuishi hata kama muda wake umeisha.
2 Wafalme 19 : yote na 20: yote .
- Sadaka ina uwezo wa kuugeuza moyo wa Mungu akamuwazia
mtu tofauti na alivyo kuwa anamuwazia mara ya kwanza.
- ( Waamini walio wengi hawaoni umuhimu wa sadaka kwa
sababu macho ya kiroho yamepofuka ).
HII NI
TAHADHARI:
- wachungaji wanapo fundisha utoaji wa sadaka
makanisani waumini wengi wanaanza kujenga hoja tofauti hiyo ni laana.
- Sadaka ni hatua ya mwisho ambayo Mungu anaitazama na
kutimiza baraka katika maisha ya mtu, hili jambo liliwakuta wana wa Israeli
wakati wamezidiwa nguvu.
1 Samwel 7: 1-11
- Katika 1Samwel
7:6, sababu ya wana wa Israel kuingiwa hofu mpaka kufika kiwango cha
kuwaogopa wafilisti ni kwa sababu ya dhambi, na kawaida ya dhambi huwa inaondoa
ujasiri kabisa katika moyo wa mtu anaye mtegemea Mungu.
- Sadaka ina nguvu ya kukata na kubomoa laana inayo tembea
na maisha ya mtu ili mradi tu muhusika awe mwaminifu katika utoaji.
- ( Ndani ya sadaka kuna nguvu ya msamaha, hili jambo
tunaliona wazi katika 1 Samwel 7:9
).
- Mwamini akiwa ajatoa sadaka kwa Mungu ya kujitenganisha
na roho ya dhambi hata kama ametubu dhambi ile roho haita ondoka mitaani mwake,
nini kifanyike?
Inatakiwa nitoe sadaka ya kujitenganisha na dhambi
ndipo niwe huru jumla
- Maisha ya mtu yanabadilika pale ambapo mtu anaamua
kufuata kanuni za Mungu zilizo andikwa kwenye maandiko matakatifu.
- Kama ninahitaji maisha marefu chini ya Mbingu inatakiwa
nielekeze nguvu zangu katika sadaka, kwa sababu sadaka ndio nafasi ya mwisho
ambayo Mungu anaitazama katika maisha ya mtu, ili liko wazi kwa maana jinsi hii
Mungu alimtoa mwanae wa pekee Yohana
3:16
- Sadaka ya Agano ina nguvu kubwa sana ndani yake ya
kulinda maisha ya mtu anaye mwamini Mungu yasiathiriwe na uvamizi wa nguvu za
giza kwenye ulimwengu wa roho, hili jambo tulitazame hata katika Biblia. 2 Samwel 24:yote
- Nguvu iliyoko ndani ya sadaka inayo uwezo mkubwa wa
kutiisha hata mauti, ndio maana inaonekana wazi katika 2 Samwel 24: 25- Sadaka ya Daudi iliharibu nguvu ya mauti iliyo
kuwa imekuja kwa njia ya tauni.
- Hatuwezi kuiepuka adhabu yoyote iliyoko mbele yetu
isipokuwa tunaweza kuibadilisha kwa njia ya sadaka, ndio maana suala la
sadaka inatakiwa liwe ni tendo endelevu katika maisha.
1 Comments
Ubarikiwe sana
ReplyDelete