Mwl. Christopher Mwakasege
|
Semina ilifanyika Biafra
- Dar es Salaam 19/02/2012
Habakuki 1: 1 – 4 … Ee BWANA, nilie hata lini, wewe
usitake kusikia? Nakulilia kwa sababu ya udhalimu, ila hutaki kuokoa. Mbona
wanionyesha uovu, na kunitazamisha ukaidi? Maana uharibifu na udhalimu u mbele
yangu; kuna ugomvi, na mashindano yatokea. Kwa sababu hiyo sheria imelegea,
wala hukumu haipatikani; kwa maana watu wabaya huwazunguka wenye haki; kwa
sababu hiyo hukumu ikipatikana imepotoka.
Nilie hata lini
wewe hutaki kusikia
Habakuki
inatueleza habari za mtu ambaye aliomba na Mungu akanyamaza lakini hakuacha
kuomba
- Alipokuwa anamuoma Mungu ondoa UOVU/ UDHALIMU/ MASHINDANO ailitegemea asubuhi asivione lakini kulipokucha akaviona bado vipo, kwa muda mrefu havijaondoka!
- Akarudi kwa Mungu kuuliza kwa nini hajiondoka
V.4 sheria
imelegea/ wala hukumu haipatikani! Kesi zinahairishwa, na hukumu ikipatikana
imepotoka.
- Habakuki hakunyamaza ila Mungu alinyamaza na Habakuki akauliza kwa nini hukujibu maombi (Habakuki 2: 1)
- Kutokujibiwa maombi kuna zaa malalamiko usipojifunza kurudi kwa Mungu na kuuliza – badala ya kurudi kwa Mungu kuuliza kwa nini sikujibiwa!
- Ndio maana wakati mwingine unaingia katika maombi na unaanza kulalamika, wewe unadhani unaomba lakini kumbe unalalamika kwa sababu ya maombi unayoomba muda mrefu bila majibu.
Mathayo 17: 19
… MBONA SISI HATUKUWEZA KUMTOA…
Wanafunzi
wamejaribu kukemea pepo wakashindwa lakini Yesu akamkemea akatoka; unaona
kabisa wakipewa malaka ya kukanyaga nyoka na ng’e na kukemea pepo; sasa hawa
wamefuata maagizo.
- Wanafunzi wakarudi kwa Yesu kuuliza kwa nini sisi hatukuweza japo tulishapewa mamlaka, amri na maagizo juu ya pepo wachafu. Wangeweza wakanyamaza!
- Ukishindwa kukemea pepo nenda faragha umuulize Bwana Yesu kwa nini pepo hakutoka; maana jibu atakalokupa linaweza kuwa msaada kwako na kwa wengine.
- Yesu akawajibu kwa sababu ya upungufu wa imani! Ni kweli ukiwa na imani kama chembe ya haradani unaweza kuhamisha milima; lakini tena akaongeza hii hata kama una imani haitoki, mpaka KUFUNGA NA KUOMBA.
(2Samweli
12: 15 – 20) Daudi kampa mimba mke wa askari, Mungu katuma mtumishi
kumueleza Daudi na adhabu kuwa mtoto atafariki. Daudi alikuwa amepakwa mafuta
lakini akaomba na kufunga kwa siku 7, lakini mtoto akafa; baada ya mtoto
kufa akaoga akavaa nguo zake akala akaenda hekaluni. Lakini haukuona Daudi
akimuuliza Mungu kwa nini mtoto hakupona?
- Usije ukafunga na kuomba kwa muda mrefu ukaona haujibiwi ukakata tama.
- Swali ni kwa nini Mungu alinyamaza na hakumjibu Daudi. Watu watasema ni kwa sababu mtoto alizaliwa nje ya ndoa! Je ni watoto wangapi wamezaliwa nje ya ndoa lakini hawajafa lakini wa Daudi afe? Ni wanawake wangapi wamezaa nje na watoto wao wanakua lakin mtoto wa Daudi ndio afe?
- (Zaburi 51: 5) … mimi naliumbwa katika hali ya uovu, mama yangu alinichukua mimba hatiani/dhambini
- Watoto waliochukuliwa mimba dhambini, ile dhambi ni juu ya wazazi. Lakini mambo ya kuishi au kufa ni juu ya Mungu, kwamba ile tu unaishi ni kwa ajili ya Bwana. Kwa nini mtoto wa Daudi afe?
- Jizoeze kumuuliza Mungu kwa nini sijajibiwa!
Bwana Yesu pia
anaombi moja ambalo lilikataliwa …ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke…
- Cha muhimu hapo sio kutojuibiwa ili kufahamu kwa nini Mungu hakukujibu maombi yako
- Paulo aliachwa na Mjumbe wa shetani na alimuomba Mungu mara 3 na akajibiwa kwa neema yangu yakutosha na mahusiano yake na Mungu hayakudhurika
Hii ni Semina ya Mwl.Mwakasege nchini Uingereza iliyoandaliwa na CITE
|
Mtumishi wa
Mungu kama haendi mbele za Mungu nakuulilza kwa nini alipokuombea hayo maombi
hayajajibiwa itasababisha uhusiano wako na Mungu uwe duni na ukuaji kwako
udumae.Ndio maana
mahusiano mengine na Mungu yanakwama
Mmoja anaombewa
na kupona na mwingine haponi, Mungu ni huyo huyo, madhabahu ni hiyo hiyo na
biblia ni ile ile. Niliionja ile furaha ya mmoja kupona na pia nikaonja ila
huzuni ya mwingine kutokupona, sasa utapata picha mchanganyiko wa chumvi na
sukari! Inasumbua sana na usiporudi kwa Mungu kuuliza na Mungu
asipokusemesha unapata shida sana na kukwama, ni muhimu Mungu akusemeshe kwa
nini hajakujibu ili mahusiano yako na Mungu yawe mazuri
Baba yangu
alifariki mwaka jana, Bwana alinisemesha 2010 nikaomba aahirishe akakataa! Mungu
alimuonyesha mpaka mahali pa kumzika. Tukagawa vitu akiwa hai, akasaini na
baada ya hapo, nilikuwa naomba tu, mwezi wa 8 tar 24 akafa! Tukiwa
hosipitali tunaenda kushughulikia death certificate, wakati tunatoka saa 6
usika mama mmoja akaja kwetu akasema POLE SANA NIMESIKIA KITU AMBACHO
KIMETOKEA.
Lakini mtoto wangu kesho asubuhi anafanyiwa operation naoma
umuombee, asubuhi saa 11 Roho Mtakatifu akanikumbuka, na nikaomba tukiwa kwenye
msiba. Sasa Mungu asingekuwa ameniambia kwa nini baba ameondoka, unafikiri
ingekuwa rahisi kumuombea Yule mtu wakati unaona kabisa kwa maombi yako
hayajajibiwa!
Ni kitu ambacho
kingeweza kutuletea mkwaruzo na Mungu rohoni. Wengine wameacha wokovu wengine
wameenda kwa waganga kwasababu walipoombewa hawakujibiwa! Ukishaona namna hiyo
uhusiano wako na Mungu haujakaa sawa. Ukiona Mungu hajajibu maswali yako na
mahitaji yako, huhitaji kulalamika ila unahitaji kurudi kwake na kuuliza kwa
nini!
Mwl. Christopher Mwakasege
0 Comments