NAMNA AMBAVYO NAWEZA
KUSHINDA MAJARIBU
- Inafahamika wazi majaribu ni aina fulani ya vipingamizi
au vikwazo vinavyo jipenyeza kwa siri au kwa uwazi katika maisha ya mwamini kwa
lengo la kuathiri mahusiano ya mtu na baraka za Mungu.
- Jambo hili ni la kuwa nalo makini sana, lengo kuu la
majaribu katika maisha ya mtu ni kuathiri mfumo wa Imani ya mkristo katika
kumtafuta Mungu, ndio maana wakristo ambao bado hawajaimarika kiufahamu
wanapoingia katika kipindi cha kujaribiwa humuasi Mungu, mara nyingi hii
huwatokea wakristo ambao hawana kina cha Neno la Mungu katika maisha yao ya
kiroho.
- ( Mkristo ambaye bado hajairimarika katika msingi wa
Neno ni vigumu kupenya katika majaribu atashindwa tu, kwa sababu ili kushinda
jaribu kunahitajika nguvu ya Neno la Mungu katikati, kwa hiyo katika hili
kunahitajika bidii ya ziada kuhudhuria mafundisho).
- Ili nijitambue kwamba nimeisha anza kudhoofika kiroho
kuna mazingira haya yatajionyesha dhahiri katika maisha yangu :-
( i ). Kushindwa
kusoma Biblia, yaani nikianza kusoma Biblia nasikia hali ya mwili kuchoka,
kupiga miayo, vile vile kusikia usingizi, wakati mwingine kazi zisizo maalumu
kujitokeza ili mradi nikose muda
( ii ). Uvivu wa
kwenda kanisani au kushindwa kuhudhuria vipindi vya mafundisho ya Neno la
Mungu
-( watu wengi wanaoshindwa katika maisha inatokana
na kushindwa kuonyesha msimamo kwenye uso wa Mungu Kibibilia watu hawa huitwa
wapunga pepo Matendo 19:13.)
- ( nikiwa ni mkristo nisiye kuwa na msimamo katika maisha
yangu ya wokovu nitaitwa nyumba ya matatizo (majaribu) )
- ( Jaribu likiwa zito kwangu inatakiwa niongeze bidii ya
kuomba vilevile ya kujifunza Neno la Mungu )
- ( Majaribu hayakwepeki mpaka siku naingia kaburini, kila
siku majaribu yatakuwepo tu cha msingi ni kujiimarisha katika misingi ya Neno
la Mungu ili nipate ujasiri wa kukabiliana nayo )
- Wakristo wengi wanashindwa na majaribu kwa sababu ya
ufahamu mdogo wa kumjua Mungu
- Mkristo aliyejiimarisha katika ufahamu wa Neno la
Mungu hauwezi kumkuta anakata tamaa hata siku moja kwa sababu moyo wake
unafahamu wazi kwamba hakuna lisilowezekana kwa Mungu sambamba na Neno katika
Luka 1:37
- (Ni vigumu kuvuka katika majaribu ninayo kutana nayo
kama moyo wangu haujamjua Mungu).
- Ninapo uandaa moyo wangu katika kumjua Mungu maana yake
natengeneza mtiririko wa baraka za Mungu zipate mahali pa kupitia,vile
vile ninapo unyima moyo wangu uhuru wa kumjua Mungu kupitia Neno lake kwanza
kabisa kina cha maarifa ya rohoni kinajifunga, Pili baraka za Mungu zitakosa muunganiko
na mahali pa kupitia, kwa hiyo mtu huyo hawezi kutoka katika tabu alizo nazo
milele hata akiombewa.
- Kama moyo wangu umejaa Imani ya Yesu Kristo utatoa
upendo, utatoa kuwasaidia maskini, utatoa huruma.
- Kama moyo wangu umejaa mawazo mabaya utatoa hila,
utatoa chuki, utatoa tamaa, utatoa majivuno, utanirithisha hali ya
kushindwa.
NGUVU YA KUSHINDA MAJARIBU
- Kwanza kabisa inabidi nifahamu nguvu ya majaribu ni nini
na inatokana na nini?
Jibu: Ukweli ni kwamba
nguvu ya majaribu ni dhambi
- Majaribu yanapata nguvu ya kutesa maisha ya mtu kwa
sababu ndani mwake yanakutana na dhambi, kwa hiyo ile dhambi inayokuwa ndani ya
mtu ndiyo msingi wa majaribu yale
- ( nikitaka majaribu yaondoke kwangu inatakiwa nitubu
dhambi kwanza )
- Majaribu yanapo iona dhambi katika maisha ya mwamini na
mwamini huyo asipopata ufahamu atajikuta anaishi maisha ya majuto siku zote,
kwa sababu kazi ya majaribu ni kudhalilisha utu wa mkristo siku zote.
- ( Mkristo ambaye atakuwa na tahadhari na maisha yake
ataweza kuyalinda maisha yake yasinajisike ).
- Tahadhari ni ya muhimu sana katika kila maisha ya mcha
Mungu.
- Ili niweze kupata nguvu ya kushinda majaribu inatakiwa
nijifunze kwa Yesu Kristo asilimia mia moja
SWALI: Je nini maana ya kujifunza kwa Yesu Kristo ?
Jibu : Yesu kristo ni nabii peke yake katika Biblia ambaye
hakutenda dhambi wala udhalimu kuonekana katika maisha yake, ndio maana Yesu
Kristo akawa sababu ya wokovu wetu
- ( Nikijifunza kwa Yesu Kristo nitayashinda majaribu, hii
inaonekana wazi hata katika maandiko matakatifu Luka 4:
- Silaha ya kwanza ya kuyashinda majaribu au kupata wepesi
katika majaribu ni kuishi na Roho Mtakatifu
- Nikiishi na Roho mtakatifu ataniongoza katika mambo
yafuatayo :-
a ). Kunipa ufahamu
wa kumsogelea Mungu
b ). Kunipa nguvu
ya kushinda dhambi
c ). Kunipa uwezo
wa kuomba zaidi, hapa kupata hali ya mtiririko
- Mkristo anayekutana na majaribu ikiwa hana Roho
Mtakatifu ndani mwake anaweza akamkufuru Mungu jumla kwamba hamsikii kumbe
ndani mwake hana muunganiko wowote, wakristo wa aina hii maisha yao ya ucha
Mungu huishia kwenye kutangatanga kwenye makanisa na kwenye sehemu za maombezi
lakini mwisho wa yote hubaki sifuri vile vile bila jibu
- Nikitaka kushinda kila aina ya jaribu linalo jitokeza
kwenye maisha yangu inatakiwa niishi maisha ya ukweli na maisha hayo ndiyo
humfanya Roho Mtakatifu kuweza makazi ndani ya mtu.
-( Kuishi maisha ya ukweli kuna gharama, na gharama
yenyewe ni kuikana nafsi kwa ajili ya Kristo).
- Na majaribu yanaogopa mlango wa mwamini anayeishi
katika kweli na haki
- Jambo la kukumbuka inatakiwa nidhibiti udhaifu nilio nao
ili mlango wa majaribu kutumia madhaifu nilio nao usiwepo.
0 Comments