NAMNA YA KUSIKIA NA KUIELEWA SAUTI YA MUNGU ILI IKUSAIDIE KATIKA KUFANYA MAAMUZI
Mada: Mambo mhumu kujua kuhusu sauti ya Mungu
Katika sehemu ya kwanza ya ujumbe huu niliandika kuhusu mambo matatu ambayo ni kujenga mahusiano na Roho Mtakatifu, kuongeza ufahamu wako kuhusu alama za mawasilano na tatu ujue namna ya kutofautisha sauti ya Mungu na isiyo ya Mungu. Ili kusoma sehemu ya kwanza bonyeza link hii https://sanga.wordpress.com/2015/04/02/namna-ya-kusikia-na-kuielewa-sauti-ya-mungu-ili-ikusaide-katika-kufanya-maamuzi-sehemu-ya-1/ Sasa fuatana nami tuendelee na mabo mengine muhimu kujua:
- Vifahamu vikwazo vinavyopelekea kutokusikia sauti ya Mungu
- Ongeza ufahamu wako kuhusu njia anazotumia Mungu kuzungumza
- Unahitaji kufahamu umuhimu wa Mungu kuzungumza/kusema nawe
Lengo lake katika kusema na wewe ni kukuongoza katika njia sahihi kwa kukuondoa kwenye makusudi ambayo yapo nje na mapenzi yake kwenye maisha yako maana imeandikwa ‘Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam hata mara ya pili ajapokuwa mtu hajali, ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi’ (Ayubu 33:14, 17).
- Ongeza ufahamu wako kuhusu ulimwengu wa roho
Hivyo kuwa na ufahamu wa ulimwengu wa roho hususani namna ya kuishi na kuwasiliana katika ulimwengu huo ni muhimu sana kwa mwamini mwenye kutafuta kujua na kuisikia sauti/mawazo ya Mungu katika maisha yake kwa kuwa Mungu ni roho kama alivyo na Shetani pia. (Rejea 2 Wafalme 6:8-17 na Waefeso 6:10-12).
Mpenzi msomaji usiruhusu yale unayoyapitia au yale ambayo watu /mazingira yanasema juu yako yabadilishe au kuongoza maisha yako, bali tafuta kuijua na kuielewa sauti ya Mungu kwenye maisha yako. Na ndiyo maana somo hili limekuja ili kukusaidia kufika mahala ambapo utaweza kuyatenda mapenzi kamili ya Mungu kwenye maisha yako.
Baada ya kuwa tumeangalia mambo haya saba ambayo ni muhimu kujua kuhusiana na sauti ya Mungu, katika sehemu ya tatu nitaanza kuandika kuhusu njia mbalimbali ambazo Mungu hutumia kusema na wanadamu. Somo litaendelea….
Na: Patrick Sanga
Comments
Post a Comment