NDOA ni shule pekee ambayo unapata
cheti kabla ya kuanza masomo. Ni shule ambayo kamwe hauwezi kuhitimu.
Ni shule ambayo unatakiwa kuhudhuria
siku zote za uhai wako. Ni shule ambayo hakuna likizo ya kuumwa au sikukuu.
Ni shule ambayo iligunduliwa na Mungu
katika misingi ifuatayo;
1. Msingi wa upendo.
2. Kuta za shule zimejengwa kwa
"uaminifu"
3. Madirisha yametengenezwa kwa
"uvumilivu"
4. Samani zimetengenezwa kwa
"msamaha"
5. Na ikaizekwa kwa "Imani"
Ukumbuke kuwa wewe ni mwanafunzi tu
na sio mkuu wa shule ya NDOA. Mungu ndio Mkuu wa Shule.
Hata wakati wa mapito, majaribu,
kimbunga na misukosuko ya hapa na pale usikimbie nje ya shule.
Kamwe usiende kulala kabla hujamaliza
homework yako. Kamwe usisahau kusoma somo la mawasiliano. Wasiliana na
mwanafunzi mwenzio pamoja na Mwalimu mkuu.
Kama utaona kuna kitu kwa mwanafunzi
mwenzako ambacho kimsingi haukipendi, basi ukumbuke mwenzako nae ni mwanafunzi
na sio mhitimu mwalimu Mkuu bado hajamalizana nae. Hivyo ichukulie ni
changamoto na muifanyie kazi kwa pamoja.
Msisahau kusoma kitabu kitakatifu
kilicho kwenye mtaala wa shule ya Ndoa (Biblia). Najua kuna muda unaweza
ukajisikia kutokuhudhuria darasani lakini unatakiwa uhudhurie tu.
Utakapojaribiwa kuacha shule jipe ujasiri
wa kuendelea na shule. Najua mitihani mingine ya muhula au nusu muhula inaweza
kuwa migumu isiyo na majibu kwako.
Lakini kumbuka Mwalimu Mkuu anayo
majibu tayari na anafahamu unaweza ukakabiliana nayo na anaona hiyo ndio shule
nzuri kwako kuzidi nyingine.
Ni moja ya shule nzuri kabisa katika
ulimwengu huu. Furaha, amani, na upendo husindikiza masomo ya kila siku.
Masomo mbalimbali hutolewa katika
shule hii, ila somo kuu kuliko yote ni UPENDO.
Baada ya miaka yote ya kusoma kwa
nadharia, ukijiunga na shule hii utasoma kwa vitendo.
Kupendwa ni kitu kizuri, lakini
kupenda ni upendeleo wa vyote. Ndoa ni sehemu ya furaha. Inatakiwa kufurahia
tofauti zenu na sio tofauti zenu ziwe chanzo cha kutoelewana.
Mimi nawatakia kila la kheri wote
mliopo kwenye hii shule takatifu. Na wale ambao bado tumuombe mwenyezi Mungu
ambae ni Mkuu wa Shule atuchagulie wanafunzi wenzetu walio bora ambao tutaweza
kujiunga nao katika hii shule nzuri hapa Duniani.
Mkuu wa Shule (MUNGU) awabariki.
0 Comments