Nguvu ya maombi ni nini?



Dhana kwamba kuna nguvu katika maombi ni mojawapo maarufu sana. Kulingana na Biblia, nguvu ya maombi kwa ufupi kabisa, ni nguvu ya Mungu, ambaye husikia na kuyajibu maombi. Fikiria yafuatayo:

1) Bwana Mwenyezi Mungu anaweza kufanya mambo yote; hakuna lisilowezekana kwake (Luka 1:37).

2) Bwana Mwenyezi Mungu Anakaribisha watu wake kuomba kwake. Maombi kwa Mungu yanapaswa kuwa yakuendelea (Luka 18:1), pamoja na kushukuru (Wafilipi 4:6), katika imani (Yakobo 1:5), ndani ya mapenzi ya Mungu (Mathayo 6:10), kwa utukufu wa Mungu (Yohana 14:13-14), na kwa moyo ulio safi kwa Mungu (Yakobo 5:16).

3) Bwana Mwenyezi Mungu anasikia maombi ya watoto wake. Anatuamuru kuomba, na ameahidi kusikiliza wakati tunaomba. "Katika shida yangu nalimwita Bwana na kumlalamikia Mungu wangu. Akaiskia sauti yangu hekaluni mwake, kili changu kikaingia masikioni mwake"(Zaburi 18:6).

4) Bwana Mwenyezi Mungu anajibu maombi. "Ee Mungu, nimekuita kwa maana utaitika, utege siko lako ulisikie neno langu" (Zaburi 34:17).

“Walilia, naye Bwana akasikia akawaponya na tabu zao (Zaburi 34:17).

Wazo jingine maarufu ni kwamba kiasi cha imani tunayo huamua kama Mungu atajibu sala zetu au atakosa. Hata hivyo, wakati mwingine Bwana anajibu maombi yetu licha ya ukosefu wetu wenyewe wa imani. Katika Matendo 12, kanisa linaomba kwa ajili ya kutolewa kwa Petro kutoka gerezani (mstari wa 5), na Mungu akajibu maombi yao (vv. 7-11). Petro anaenda hadi mlango wa mkutano wa maombi na kugonga, lakini wale ambao wanaomba wanakataa mara ya kwanza kuamini kwamba kweli ni Petro. Waliomba ili aachiliwe, lakini walikosa kutarajia jibu kwa maombi yao.

Nguvu ya maombi haitoki kwetu; sio maneno maalum sisi huyasema au namna ya kipekee tunayasema au hata jinsi tunayasema mara nyingi. Nguvu ya maombi msingi wake si mwelekeo fulani tunaangalia au nafasi fulani ya miili yetu. Nguvu ya maombi haitokani na kutumia michoro au sanamu au mishumaa au shanga. Nguvu ya maombi inatokana na mwenye nguvu Yule anasikia maombi yetu na kuyajibu. Maombi hutuweka katika mawasiliano na Mwenyezi Mungu, na tunapaswa kutarajia matokeo matakatifu, kama Anachagua kuruzuku maombi yetu au kukataa maombi yetu. Jibu lolote kwa maombi yetu, Mungu ambaye tunaomba ndiye chanzo cha nguvu ya maombi, na Yeye anaweza na atatujibu, kulingana na mapenzi na majira yake kamili.

Post a Comment

0 Comments