Mwisho wa somo ili utagundua
nguvu iliyopo nyuma ya kusamehe. Kuna watu wanapitia kwenye matatizo na
magonjwa kwasababu ya kutokusamehe.
Mathayo 6:9-12 “basi ninyi salini hivi…12 msipowasamehe
wengine makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu” Zaburi 103:3 Hapa tunaona kuwa kanuni ya
Mungu ni kusamehe kwanza kabla ya kuponya. Na ndio maana waweza kumwona mtu
anasema ameokoka lakini bado yupo kwenye ugonjwa kwasababu ya kutokusamehe.
KWANINI UMSAMEHE ALIYEKUKOSEA:
Kumsamehe mtu aliyekuumiza sio
jambo la mzaha, na ndio maana kuna watu wanasema kuwa wamesamehe lakini ndani
ya mioyo yao bado hajasamehe. Tunatakiwa
kusamehe kwasababu kuna nguvu iliyopo nyuma ya mtu aliyekukwaza au kukuumiza.
Watu wengi wanashindwa
kusamehe kwasababu hawajui nguvu iliyopo
nyuma ya yule mtu aliyewakwaza. Emu tuangalie mfano wa gari; Gari linapomgonga
mtu serikali haishtaki gari bali anayeshtakiwa ni dereva. Vivyohivyo ukiumizwa
unatakiwa uangalie ile nguvu iliyopo nyuma ya aliyekuumiza. Kimsingi kuna nguvu
inayotenda kazi nyuma ya aliyekuumiza na usipoijua hiyo nguvu utajikuta
unashindwa kusamehe.
VITU VITATU AMBAVYO NI VIPIMO KAMA UMESAMEHE AU BADO
HUJASAMEHE:
1. Ukimsamehe mtu utamwongelea
vizuri:
Kama kweli
umemsamehe mtu utamwongelea vizuri mbele za watu, kama unasema umemsamehe mtu
alafu bado unamwongelea vibaya ujue bado hujasamehe kutoka moyoni mwako.
Ukimkuta mtu anaongea mabaya kuhusu mtu aliyemkwaza basi ujue ndani ya moyo
wake kuna madabahu ya makwazo na machungu. Na kwasababu hiyo kuna watu
wamefukuzwa kazi, wamepigwa kwasababu ya kushindwa kuwanenea watu mazuri.
2. Ukimsamehe mtu utamwombea:
Ishara
nyingine kuwa ya kuonyesha kuwa umesamehe ni kumwombea mwingine mazuri; na ndio
maana Eliya alipotaka kujenga madhabahu ya
Mungu alibomoa kwanza madhabahu ya baali, hata leo huwezi kujenga
madhabahu ya Mungu ya amani kama bado moyoni unamadhabahu ya kutokusamehe. Watu
wengi wamejikuta wakiomba mabaya kwa watu waliowakosea na kwa namna hiyo
wanashindwa kupokea majibu ya matatizo yao.
3. Ukimsamehe mtu utawasiliana kwa
uzuri:
Ukimsamehe mtu utawasiliana
naye kwa uzuri, nah ii ni kwenye madhabahu ya moyo wako. Hata kama amekujibu
vibaya wewe mjibu kwa uzuri. Ni kweli kuwa ukisamehe Yule mtu atakudharau
lakini ni muhimu kujua kuwa tunasamehe si kwa ajili ya waliotukosea bali kwa ajili
yetu.
Watu wengi wanashindwa
kusamehe kwasababu ya kukosa nguvu ya uwezesho ya kuweza kusamehe. Kila mtu
aliyeokoka anayo nguvu ya uwezesho ya kusamehe, nayo ni Roho Mtakatifu. Kila
mtu aliyeokoka ana Roho Mtakatifu naye hutuwezesha kusamehe, kuokoka kunakupa
nguvu ya uwezesho kusamehe. Bila kusamehe huwezi kupokea kutoka kwa BWANA.
MAOMBI YA KUSAMEHE:
Baba katika Jina la Yesu
Kristo ninaomba nguvu ya msamaha wako; leo nimetambua kuna nguvu inayotenda
kazi nyuma ya mtu aliyenikwanza, leo ninawasamehe wote walionikwaza katika Jina
la Yesu. Ninatangaza msamaha, ninavunja madhabahu ya makwazo na kutokusamahe
ndani yangu katika jina la Yesu Kristo.
Baba ninaomba uniponye na
matatizo yaliyoingia ndani yangu kwasababu ya kutokusamehe katika Jina la Yesu.
Leo ninabadilika katika Jina la Yesu. Mimi ni mzima na nimeponywa katika Jina
la Yesu.
UFUFUO NA UZIMA (THE GLORY OF
CHRIST (T) CHURCH)
0 Comments