Nikijiona ninashindwa kusahau jambo ambalo nimemsamehe mtu
hiyo ni picha wazi kwamba bado sijamsamehe, kwasababu kitendo cha
kukumbuka nilicho kisamehe kitanifanya
maumivu kurudi upya, hapo utakuwa mwanzo wa moyo wangu kuishi katika maumivu ya ndani kwa ndani .
(Maumivu ya ndani kwa ndani yanayotokana na kutokusamehe ndani ya moyo yanaathiri utendajikazi wa
imani).
Mkristo anayeshindwa kusahau jambo ambalo amemsamehe mtu haishi na Roho mtakatifu, kwa maana zaidi
ni mkristo kwa nje yaani kimwili, kiroho ni mpinga kristro , na hao ndio
wamejaa katika makanisa ya kiroho.
Hakuna majibu ya maombi yoyote yale yatakayo toka kwenye
uso wa Mungu nakuja kwenye maisha ya mwamini kama moyo wake hajautakasa usiwe na hila na mtu yeyote , ni kitu ambacho
hakiwezekanikani .
(Nikitaka Baraka za Mungu inatakiwa nitakase moyo
wangu inatakiwa moyo wangu usiwe na visasi na watu walioumbwa kwa mfano
wa Mungu).
(Wakristo wengi wanashindwa kupokea Baraka za Mungu
kwasababu mioyo yao inakuwa mizito kuachilia na kusahau waliyotendwa).
Nikisamehe na kusahau maumivu niliyotendwa ninaonyesha uhai wa Mungu waziwazi katika maisha
yangu ya wokovu,hata katika kitabu cha waebrania limethibitishwa jambo hili
sura ya 8:12,
( Nikiamua kuvaa vazi la wokovu inatakiwa nijikane
waziwazi nafsi yangu)
( Yesu nisaidie kwenye maisha yangu mimi siku zote niitwe
haki )
Yesu Kristo ndiye mwanzilishi wa kusamehe na kusahau ndio
maana anatusisitiza sana juu ya kusahau tuliyoyasamehe kwa watu, hata katika
kitabu cha Nabii Isaya enzi za babu zetu wakina Ibrahimu, Isaka na Yakobo
walilisoma andiko hili Isaya 43:18.
Muda ninaotumia kukaa chini kuhojiana mambo yasiyokuwa na
utukufu kwenye uso wa Mungu ni bora ningeutumia muda huo kusoma angalau kurasa
mbili za Biblia kitu kipya kitazaliwa katika maisha yangu.
Imani za wakristo zimeathiriwa sana na mambo yasiyo kuwa
na maana wanayoyaruhusu kuingia kwenye mioyo yao, hapa inabidi nipate ufahamu
wa ziada wa kupambanua kwa sababu nikiruhusu moyo wangu kuvaliwa na mambo
yasiyokuwa na utukufu kwa Mungu ndio mwanzo wa kujeruhika kiroho.
Msingi wa kuijenga imani ni kusamehe na kusahau, hapo
ndipo unapofunguka ukurasa mpya wa ushindi katika maisha ya ucha Mungu.
ANGALIZO
NO. 1
Ninapoamua
kuokoka maana yake nimeamua kuyaishi maisha ya Yesu Kristo aliyoishi katika
mwili , kwa hiyo lazima nijikane kwelikweli bila kutazama mazingira
yaliyonizunguka au ninayo yapitia yaani hapa ni kutimiza sheria yote ya Mungu
hata kama ndani yake kuna maumivu “ Ee Yesu nisaidie ’’
Ninasisitizwa kusamehe na kusahau kwa sababu darasa la
Roho Mtakatifu lina mambo mengi sana.
Bila kupita kwenye darasa la Roho Mtakatifu maono
niliyonayo ni vigumu kutimia kwa sababu darasa la Roho Mtakatifu ndilo
linalotuimarisha katika misuli ya imani.
Kila hatua ninayo ipitia katika maisha yangu ya imani
haijalishi ni ugumu wa aina gani hilo ni darasa la kunijenga kwa ajili ya
kustahimili makubwa zaidi yatakayo jitokeza kesho.
2
Timotheo 3:12
Maandiko kutimia katika maisha ya mwamini ndiko kunako
sababisha mpenyo kutokea.
Yesu Kristo alipotangaza msamaha wakati yuko msalabani
alikuwa akifundisha wazi ulimwengu maisha ya visasi hayana Baraka.
KINACHOFANYA MWAMINI ASHINDWE KUSAMEHE
Kinachofanya mwamini ashindwe kusamehe ni udhaifu alionao
katika imani ya kumwamini Mungu, kwa sababu mtu anaye mwamini Mungu lazima awe
na asili moja na Mungu, kwa hiyo suala la yeye kusamehe ni lazima ili asifarakane
na uwepo wa Mungu, mbona Biblia imesema wazi katika wakorinto ?
1
wakorinto 6:17 .
Kama kweli ninamcha Yesu Kristo suala la kusamehe
halitanisumbua kichwa, lakini kama ni muigizaji kwenye uwepo wa Mungu kamwe
siwezi kusamehe na kusahau.
MBINU ZA KUMJUA MTU AMBAYE HANA TABIA ZA KUSAMEHE NA
KUSAHAU
i.
Hawezi kuomba, mtu wa aina hii akiingia kwenye maombi ile hali ya maumivu ya
kutendwa ndiyo inayo jidhihirisha ndio maana utamkuta anaishia kulia na kupiga
kelele, sikwamba Roho Mtakatifu anakuwa amemshukia hapana bali kumbu kumbu ya
kutendwa ndio inayo kuja ndani mwake.
MBINU YA KUMFAHAMU MTU MWENYE HILA NA ROHO YA VISASI NDANI
YAKE.
i.
Picha ya mtu mwenye hila na roho ya visasi ndani mwake hujidhihirisha kwa njia
ya kinywa, namna ambavyo hutoa maneno ya uchochezi, uchonganishi, uzushi, uongo
watu wa aina hii hata Mtume Paulo alikutana nao, Yesu Kristo alikutana nao,
Musa Nabii alikutana nao, ndio maana 2 Timotheo 3: Nikiisoma yote nitaona namna
ambavyo walizusha mambo mengi kuhusu watumishi wa Mungu, ndio maana Paulo Mtume
anatoa tahadhari dhidi ya watu kama hao 2 Timotheo 3: 6-9, vilevile Timotheo
alitoa tahadhari sanasana 2Timotheo 2:16-18 .
0 Comments