Baba
yetu wa Mbinguni … anajua kwamba tunajifunza na kukua na kuwa imara
tunapokabiliana na kushinda majaribio ambayo lazima tunayapitie.
Katika
shajara yangu usiku wa leo, mimi nitaandika, “Hiki kimekuwa mojawapo wa vikao
vyenye maongozi zaidi vya mkutano mkuu wowote ambao nimeshahudhuria.
Ndugu
na kina dada, miezi sita iliyopita sisi tulipokuwa tumekutana katika mkutano
mkuu wetu, mke mpendwa, Frances, alikuwa amelala hosptalini, akiugua kwa sababu
ya kuanguka sana siku chache mapema. Katika mwezi mei, baada ya kupambana kwa
ujasiri kushinda majeraha yake, alisonga katika milele. Kumpoteza yeye kulikuwa
na uzito mwingi. Yeye nami tulioana katika Hekalu la Salt Lake mnamo Oktoba
7, 1948. Kesho ingekuwa sherehe ya maadhimisho ya ndoa yetu ya mwaka wa
65. Yeye alikuwa kipenzi cha moyo wangu, mwandani wangu wa kuaminika, na rafiki
yangu wa dhati. Kusema kuwa ninamkosa sana haiwezi kuanza kuwasilisha hisia
zangu za kina.
Mkutano
huu unaadhimisha miaka 50 tangu mimi niitwe katika Jamii ya Mitume Kumi na
Wawili na Rais David O. McKay. Kupitia hii miaka yote sijahisi chochote
bali uhimili kamili wa mwenzi wangu kipenzi. Dhabihu zisizohesabika alizofanya
ili kwamba mimi niweze kutimiza wito wangu. Kamwe sijasikia neno la kulalama
kutoka kwake kwa vile nilikuwa nitumie siku nyingi na wakati mwengine wiki
nyingi mbali na yeye na watoto wetu. Alikuwa malaika kwa kweli.
Ningependa
kutoa shukrani zangu, pamoja na za familia yangu, kwa mtiririko wa ajabu wa
upendo ambao umekuja kwetu tangu Frances kuaga. Mamia ya kadi na barua
zilitumwa toka duniani kote zikionyesha upendo kwake na rambirambi kwa familia
yetu. Sisi tulipokea madezeni ya mapambo ya maua ya urembo. Tunashukuru sana
kwa michango mingi ambayo ilitolewa katika jina lake katika Hazina Kuu ya
Umisionari ya Kanisa. Kwa niaba ya wale wetu ambao alituacha nyuma, ninatoa
shukrani za kina kwa ukarimu wenu na maonyesho ya kutoka ndani ya moyo.
Faraja
kuu kwangu wakati huu wa kipindi kigumu cha kuachana imekuwa ni ushuhuda wangu
wa injili ya Yesu Kristo na elimu niliyonayo kwamba mpendwa wangu Frances bado
anaishi. Mimi najua kwamba utengano wetu ni wa muda. Sisi tulifunganishwa
katika nyumba ya Mungu na mtu aliye na mamlaka ya kuunganisha hapa ulimwenguni
na mbinguni. Mimi najua kwamba sisi tutaunganishwa siku moja na kamwe
hatutatenganishwa tena. Hii ndiyo elimu ambayo inayonihimili.
Ndugu
na kina dada, inaweza kudhaniwa kiusalama kwamba hakuna mtu yeyote aliyeishi
huru na mateso na huzuni, wala haijapata kuwa na kipindi katika historia ya
binadamu ambacho hakikuwa na sehemu yake ya vurugu na dhiki.
Wakati
mapito ya maisha yanafanya mkujo dhalimu, kuna majaribu ya kuuliza swali “Kwa
nini mimi?” Nyakati zingine zinaonekana kuwa hamna nuru huko mwisho wa upenyo,
hamna cha machweyo ya kumaliza giza la usiku. Tunahisi kuzongwa, kuvunjika moyo
kwa ajili ya ndoto zilizovunjika na huzuni wa matumaini yaliyotoweka.
Tunaunganika katika kusema ombi la kibiblia, “Je! Hapana zeri katika Gileadi?
?”1 Tunahisi
kutelekezwa, kuvunjika moyo, wapweke. Tunapendelea kuona dhiki yetu binafsi
kupitia kioo potoshi cha shaka. Sisi tunakosa subira kwa suluhu za shida zetu,
kusahau kwamba kila mara sifa za uvumilivu za mbinguni zinahitajika.
Ugumu
ambao unaotujia sisi unatuletea sisi mtihani halisi wa uwezo wetu wa kuvumilia.
Swali la msingi linabaki kujibiwa na kila mmoja wetu: Nitajikwaa, au
nitakamilisha? Wengine hujikwaa wanapojipata hawawezi kusimama juu ya
changamoto zao. Ili kumaliza inajumuisha kuvumilia hadi mwisho wa maisha
yenyewe.
Tunapotafakari
matukio ambayo yanayoweza kutuangukia sisi, tunaweza kusema pamoja na Ayubu wa
kale, “Mwanadamu huzaliwa ili apate mashaka.” 2 Ayubu
alikuwa mtu “mkamilifu na mwelekevu,” mtu “aliyemcha Mungu, na kuepukana na
uovu.”3 Mwema
katika mwenendo wake, mfanisi katika mali yake, Ayubu alikabiliwa na mtihani
ambao unaweza kumwangamiza mtu yeyote. Mali yake ikapotea, akakejeliwa na
marafiki zake, akapatwa na mateso, akavurugwa na kupoteza familia yake,
aliambiwa “Umkufuru Mungu, ukafe.”4 Yeye
alikataa majaribu haya na kutangaza kutoka kwa kina cha nafsi yake tukufu:
“Tazama,
shahidi wangu yuko mbinguni. Na huyo atakayenidhamini yuko juu.”5
“Mimi
najua ya kuwa mteteaji wangu yu hai.”6
Ayubu
alifanya imani. Nasi tutafanya vivyo hivyo tunapokabiliana na changamoto ambazo
zitakuwa zetu?
Wakati
wowote tunapendelea kuhisi kulemewa na mapigo ya maisha, acha tukumbuke kwamba
wengine wamepita njia hio hiyo, wakavumilia, na kisha wakashinda.
Historia
ya Kanisa ni hivi, kipindi cha ujalivu wa nyakati kimejaa matukio ya wale ambao
wamepambana na hali wamebakia imara na wenye shangwe. Sababu ni nini?
Wameifanya injili ya Yesu Kristo kuwa kitovu cha maisha yao. Hiki ndicho
kinachotusukuma bila kujali kile kinachokuja katika njia yetu. Sisi bado
tutakabiliana na changamoto kali, lakini tutaweza kukabiliana nazo, kukumbana
nazo ana kwa ana, na tutaibuka washindi.
Kutoka
kwa kitanda cha machungu, kutoka mto uliolowa na majonzi, tunainuliwa kuelekea
mbinguni na lile hakikisho takatifu na ahadi ya thamani: “Sitakupungukia Wala
Sitakuacha.”7 Faraja kama
hiyo ni ya thamani kubwa.
Ninaposafiri
kwa marefu na mapana kote duniani kutimiza majukumu ya wito wangu, nimepata
kujua mambo mengi---ikujumuisha kwamba huzuni na kuteseka ni kawaida. Mimi
siwezi kuanza kupima machungu ya moyo na huzuni ambao nishashuhudia ninapoongea
na wale wanaokumbana na dhiki, ugonjwa, wapambana na talaka, wanaosumbuliwa na
mwana au binti mpotevu, au wanaoteseka kama matokeo ya dhambi. Orodha inaweza
kuendelea na kuendelea, kwani kuna shida chungu mzima ambazo zinatukabili.
Kutaja mfano wa kipekee ni vigumu, na ninapofikiria juu ya changamoto, fikira
zangu zinamwendea Ndugu Brems, mmoja wa walimu wa Shule ya Jumapili wa uvulana
wangu. Yeye ni mshiriki mwaminifu wa Kanisa, mtu mwenye moyo wa dhahabu. Yeye
na mkwewe, Sadie, wamekuwa na watoto wanane, wengi wao ni wa rika moja na wale
wa familia yetu.
Baada
ya Frances nami kuoana na kuhama kutoka kwa kata, tuliwaona Ndugu na Dada Brems
na wanafamilia wa familia yao katika harusi na mazishi, na pia katika miungano
ya kata.
Mnamo
1968, Ndugu Brems alimpoteza mkewe, Sadie. Wawili wa watoto wao wanane pia
wameshaaga dunia miaka iliposonga.
Siku
moja karibu miaka 13 iliyopita, mjukuu mkubwa wa kike wa Ndugu Brems alinipigia
simu. Alinielezea kwamba babu yake amefika siku maadhimisho ya 105 ya kuzaliwa
kwake. Alisema, “Yeye huishi katika kituo cha utunzaji kidogo lakini yeye
hukutana na familia yote kila Jumapili, ambapo yeye huwasilisha somo la
injili.” Anaendelea, “Jumapili ile iliyopita Babu alitutangazia sisi, ‘Wapendwa
wangu, mimi nitaaga dunia wiki hii. Tafadhalini mpigieni simu Tommy Monson.
Yeye atajua cha kufanya.’”
Mimi
nilimtembela Ndugu Brems jioni hio hiyo iliyofuata. Nilikuwa sijamuona yeye kwa
muda. Singeweza kuongea naye kwani alikuwa amepoteza kusikia. Singeweza
kuandika ujumbe kwake asome, kwa sababu alikuwa amepoteza kuona. Niliambiwa
kwamba familia yake iliwasiliana naye kwa kuchukua kidole cha mkono wa kulia na
kisha kuandika katika kiganja cha mkono wa kushoto jina la mtu anayemtembelea.
Ujumbe wowote ungewasilishwa kwa njia hio hiyo. Mimi nilifuatia utaratibu huu
kwa kuchukua kidole chake na kuandika “T-O-M-M-Y M-O-N-S-O-N,” jina ambalo yeye
daima alikuwa ananijua mimi nalo. Ndugu Brems akachangamka na, kuuchukua mkono
wangu na kuuwekelea juu ya kichwa chake. Mimi nilijua hamu yake ilikuwa ni
kupokea baraka ya ukuhani. Dereva ambaye alikuwa amenileta kwenye kituo cha
utunzaji aliungana nami tulipokuwa tunamwekelea mikono kwenye kichwa cha Ndugu
Brems na kupatiana baraka iliyotamaniwa. Baadaye, majonzi yalitiririka kutoka
machoni mwake yasiyoona. Aliishika mikono yetu kwa nguvu kwa shukrani. Ingawa
yeye hakuwa amesikia baraka tuliyompatia, Roho ilikuwepo kwa nguvu, na mimi
naamini alipata mvuvio kujua sisi tulikuwa tumepatiana baraka aliyohitaji. Huyu
mtu mwema hangweza kuona. Hangeweza kusikia. Alikuwa anakaa ndani ya chumba
kidogo katika kituo cha utunzaji. Na hali tabasamu katika uso wake na maneno
yeye aliongea yaligusa moyo wangu. “Asante,” yeye alisema, “Baba yangu wa
Mbinguni amekuwa mwema sana kwangu.”
Katika
wiki moja, kama vile Ndugu Brems alikuwa ametabiri, yeye aliaga dunia. Kamwe yeye
hakulilia kile ambacho hakuwa nacho; badala yake, yeye daima alikuwa na
shukrani sana kwa ajili ya baraka zake nyingi.
Baba
yetu wa Mbinguni, ambaye hutupatia sisi mengi sana ya kufurahia, pia anajua
kwamba tunajifunza na kukua na kuwa imara tunapokabiliana na kushinda majaribio
ambayo lazima tunayapitie. Tunajua kwamba kuna nyakati ambapo tunapata huzuni
ya kuvunja moyo, wakati tutahuzunika, wakati tunaweza kujaribiwa karibu
kushinda viwango vyetu. Hata hivyo, shida kama hizo zinaturuhusu sisi kubadilika
na kuwa bora, kujenga upya maisha yetu katika njia Baba yetu hutufunza, na kuwa
kitu tofauti kutokana kile tulicho---bora kushinda tulivyokuwa, waelewa zaidi
kushinda tulivyokuwa, wenye huruma kuliko tulivyokuwa, na ushuhuda thabiti
kuliko tuliyokuwa nao mapema.
Haya
yanapaswa kuwa madhumuni yetu---kustahamili na kuvumilia, ndio, lakini pia kuwa
tumetakaswa zaidi kiroho tunapopita katika kiangazi na huzuni. Kama
pasingekuwepo na changamoto za kushinda na shida za kutatua, tungebakia karibu
kama vile tulivyokuwa, maendeleo kidogo au hamna katika kusonga kwenye malengo
yetu ya uzima wa milele. Mshairi alionyesha wazo kama hilo hilo katika maneno
haya.
Mbao
nzuri haikui kwa urahisi,
Upepo
mkali, miti thabiti.
Mbali
anga iliko, ukubwa wa urefu,
Dhoruba
ilivyo kali, nguvu zaidi.
Kwa
jua na baridi, kwa mvua na theluji,
Katika
miti na wanadamu, mbao nzuri hukua.
8Bwana
tu anajua uzito wa majaribio yetu, uchungu wetu, na mateso yetu. Yeye pekee
hutupatia amani ya milele katika nyakati za dhiki. Yeye pekee hugusa nafsi zetu
zilizoteseka kwa maneno Yake ya faraja:
“Njoni
kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
“Jitieni
nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo;
nanyi mtapata raha nafsini mwenu.
“Kwa
maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”
9Hata
ikiwa ni nyakati bora au nyakati mbaya, Yeye yupo pamoja nasi. Yeye ameahidi
kwamba hii haitabadilika kamwe.
Ndugu
na kina dada, na tuwe na sharti kwa Baba yetu wa Mbinguni kwamba hio
haitabadilishwa na mtirirko wa miaka au majanga ya maisha yetu. Hatupaswi
kupatwa na shida ndiyo sisi tumkumbuke Yeye, na hatufai kudhalalishwa kabla
sisi kumpatia Yeye imani yetu na utegemeo wetu.
Natujitahidi
daima kuwa karibu na Baba yetu wa Mbinguni. Kufanya hivyo, ni sharti sisi
tuombe Kwake na kumsikiliza Yeye kila siku. Kwa kweli tunamhitaji Yeye kila
saa, hata ikiwa ni masaa ya kiangazi au ya mvua. Na ahadi Yake daima iwe neno
letu la shime: “Sitakupungukia Wala Sitakuacha.”10
Kwa
nguvu zote za nafsi yangu, mimi nashuhudia kwamba Mungu yu hai na anatupenda,
kwamba Mwanawe Mpendwa wa Pekee aliishi na kufa kwa ajili yetu, na kwamba
injili ya Yesu Kristo ni nuru ipenyayo ambayo hung’aa katika giza la maisha
yetu. Na iwe hivyo, mimi naomba katika jina takatifu la Yesu Kristo. amina.
0 Comments