SOMO KOMBOA NDOTO ZAKO
KOMBOA NDOTO ZAKO
Nini maana ya ndoto?
Ndoto ni hali fulani inayokuja kwa mtu akiwa amelala
usingizi yaani viungo vyote vya mwili vinakuwa havina ushirikiano.
Tafsiri ya pili
Ndoto ni malengo au matarajio anayokuwa nayo mtu na wakati
huo huo anakuwa ana akili timamu yaani akiwa macho hajalala usingizi, vilevile
ni mipango ya mtu.
Wakristo wengi wana ndoto lakini wameshindwa
kuzifikia ndoto zao, kwasababu wameyakataa maarifa ya Neno la Mungu.
(Jambo hili ni la kuwa nalo makini sana jinsi ninavyopwaya
katika Neno ndivyo nitakavyopwaya katika mafanikio, kwahiyo lazima niweke bidii
katika kutafuta maarifa ya Neno la Mungu)
Mithali 1:25-33.
(Nikipwaya kwenye Neno udhaifu nilio nao utanidhalilisha,
hii yote inatokana na kukosa ufahamu wa Kimungu).
Chanzo cha ndoto zangu nilizo nazo kupoteza mwelekeo ni
pale ambapo ninaukataa ufahamu wa Neno la Mungu.
Ninapoukataa ufahamu wa Neno la Mungu maana yake
nimeukataa mwonngozo wa Roho Mtakatifu, vilevile nisipotoa muda wa kusoma
Biblia kwa siku maana yake moyo wangu sijautendea haki ya kuzungumza na
Roho Mtakatifu.
Nikisoma Biblia ninapata nguvu ya rohoni , kwahiyo
ni rahisi ndoto nilizo nazo zikatimia bila kuathiriwa na adui.
Sababu kuu ya kutokusikiwa na Bwana wakati wa maombi
inatokana na mimi kwa kutokujiwekea utaratibu wa kuyaishi Maandiko Matakatifu.
Ndoto zangu zitatimia iwapo nitafanya mambo makuu mawili:-
1)Nikiruhusu hali ya kuwepo kwenye uwepo wa Mungu mara kwa
mara.
2)Nikiruhusu hali ya kujisomea Neno la Mungu wakati
wowote lakini isipite siku sijasoma.
Katika haya mambo mawili yatasababisha kibali cha Kimungu
kuyavaa maisha yangu, kwahiyo nafasi ya upendeleo itakuwepo tu hata iweje.
Nikiweka mikakati ya usomaji wa Biblia na usikilizaji wa
Neno la Mungu ,kwa maana zaidi kutokuruhusu hali ya kukosa kwenye uwepo wa
Mungu ndoto zangu nitakuwa nimeziokoa.
Ikiwa nina ndoto na ninajifahamu kwamba nina ndoto za
siku zijazo inatakiwa niziatamie ndoto hizo ndipo zitapata wepesi wa
kutimia.
Ndoto niliyo nayo itatimia iwapo maarifa ya Biblia
yataniongoza, maarifa ya Biblia (Neno la Mungu) ,ndiyo yanayoshinikiza imani ya
mtu kufika kile kiwango cha kuamuru jambo na likatimia.
NAMNA YA KUSIMAMIA
NDOTO ZANGU
Ili niweze kutambua ni namna gani ya kuzisimamia ndoto
zangu inatakiwa nijifunze kwa walionitangulia ambao ninawasoma kwenye
Maandiko Matakatifu (Biblia).
Mfano mzuri ambao tunaweza kuutumia ukatusaidia tunaupata
kwa Yusufu Mwanzo 37:5-----.
Upofu wa kiroho mara nyingi husababisha ndoto za mtu
kutotimia , mara nyingi hii inatokana na mwamini kushindwa kupambanua
pale ambapo Mungu anasema naye.
Watu wengi ndoto zao zimeathiriwa kwasababu
wanashindwa wao kama wao kusimama kuziatamia bali wanashirikisha watu wengine
wasiokuwa na maharifa nayo, kinachotokea ni nini , hiushia katika kukatishwa
tamaa na kuvunjwa moyo , ndiyo maana Mungu akasema kupitia Ezekieli 2:1.
Mungu anazungumza na mkristo ambaye ameamua maisha yake
kuwa chini ya mwongozo wa Neno lake.
Wakristo wengi wasiposimama vizuri katika Maandiko
Matakatifu, yaani katika kulisikiliza Neno la Mungu kwa undani mwisho wa siku
watazikuta ndoto zao zimezimika .
Ndoto za wakristo zinazimika kwasababu asilimia kubwa ya
waamini hawana msimamo katika suala zima la kumcha Mungu.
Mwamini mwenye uwezo wa kumsikia Mungu akisema huyo ana
uwezo wa kuatamia ndoto zake mpaka zikatimia.
Kama simsikii Mungu akisema na mimi uwezo wa kuatamia
ndoto zangu ni mdogo mno. Kwasababu ili ndoto za mwamini zitimie zinahitaji
mwongozo wa Neno la Mungu.
Hii inasikitisha sana ndoto za waamini wengi
zimeishia njiani yaani hazijatimia hii imetokana na waamini kushindwa
kuziatamia ndoto zao kupitia Neno la Mungu.
Neno la Mungu peke yake ndio lina uwezo wa kusababisha
ndoto za mtu zikatimia.
Katika Mwanzo
37:11b pale anaposema ‘baba alilihifadhi neno hili’’, ni ufahamu
kwangu leo kwamba kila nitakayoiota ninahitajika kuandika yaani kuweka
kumbukumbu mpaka siku itakapotimia.
Kila jambo linalotokea kwenye maisha yangu ukweli ni
kwamba Mungu alishanieleza kwenye ndoto shida inakuja kwamba kushindwa
kupambanua vilevile kutokukumbuka, ndio maana inatakiwa kila ndoto niiandike
kwa kumbukumbu siku za usoni.
JINSI YA KUZILINDA
NDOTO ZANGU ZISIATHIRIWE
Ili niweze kuzilinda ndoto zangu zisiathiriwe inatakiwa
niikuze mamlaka italazimisha hali ya utiisho katika kila roho
inayopambana na mimi, ndio maana Biblia ikazungumza Isaya 54:17.
Silaha ya shetani inakosa nguvu kwa mwamini mwenye mamlaka
ya Neno la Mungu ndani mwake.
Hali ya kushindwa kwa mwamini inatokana na mamlaka
aliyonayo imeshapoa yaani imepoteza uwezo.
Mwamini aliyepoteza mamlaka sanasana hukumbukwa na mambo
yafuatayo:-
i)
Hana kabisa ulinzi wa Mungu juu yake, ndio maana waweza kuwa kituo cha magonjwa
, kwahiyo katika hili huwa tunapata matokeo ya mwamini kudhoofika kiafya.
ii)
Asili ya udhaifu alionayo kwenye mwili wake huwa inainuka , sasa
basi hapa inategemea ni udhaifu gani alionao Mfano:Muongo, Mzinzi, Mlevi, Tapeli, na mengine mengi yanayofanana
na haya.
iii)
Shetani humwibia ufahamu wa kile anachosikia kuhusu Mungu, vilevile
utayari wa kukaa chini kufundishwa, ndio maana inaweza ikatokea mwamini
asije kanisani asiwe na kazi maalumu hiyo yote inatokana kashaibiwa
ufahamu.
iv)
Maisha yake hufanywa jalala la kila matatizo.
Ndoto za mwamini zinalindwa kutokana na jinsi
mwamini anavyozidi kukua kiroho yaani kuongezeka zaidi kimaarifa, maarifa ndani
ya mtu yakiongezeka kina cha ufahamu wa rohoni hufunguka na mtu huyo
mbekle za uwepo wa Mungu huitwa mtu wa imani.
Silaha itakayoweza kuyalinda maisha ya mkristo ni ile roho
ya kupambanua itakayoyavaa maisha yake.
ANGALIZO :Nikiwa ni mkristo
mwamini na wakati huohuo sina uwezo wa kupambanua ni vigumu kuvishinda vita vya
kiroho , ndani ya kupambanua ndipo tunapopata ufahamu wa kujua sauti ya Mungu
ni ipi na sauti ya roho zidanganyazo ni zipi, tofauti na hapo hutoki kwenye mtego.
Kutimia kwa ndoto za mwamini kutokana nay eye
anavyoongezeka kiukaribu kati ya yeye na Mungu.
NINI KIFANYIKE ILI
NDOTO ZANGU ZIZAE MATUNDA:
Ili ndoto zangu ziweze kuzaa matunda haitakiwi nitoke nje
ya kanuni za Neno la Mungu, hata inapotokea nimekosea inatakiwa nijirudi haraka
ili nisitoke nje ya ule mfumo wa Baraka za Mungu, ndio maana Yoshua alipewa
maagizo katika Yoshua 1:7,8.
Jambo hili ni la kuwa nalo
makini sana
Shetani anapitia katika lile jambo ninalolipenfda
kuyaathiri maisha yangu.
Ili niweze kuidhibiti hali hiyoiliyozungumzwa kwenye
point ya juu inatakiwa ufahamu wangu niulazimishe kumheshimu Mungu ndipo
nitakapopata uwezo wa kuyatambua mapenzi ya adui kabla hajaniumiza.
Comments
Post a Comment