MFALME ALIYEKUWA NA MBWA
WAKALI KUMI
Kulikuwa na mfalme mmoja aliyekuwa na mbwa kumi wakali
sana. Alipenda kuwatumia mbwa hawa pindi akitaka kumuadhibu mtumwa aliyekosea.
Mbwa hawa waliwatesa watumwa kwa kuwararua na meno yao makali! Wakati mwingine
watumwa waliokutana na adhabu hii walipoteza uhai.
Siku mtumwa aliyemtumikia mfalme kwa miaka kumi alitoa
wazo baya ambalo halikumpendeza mfalme, ikaamriwa akamatwe na kutupwa katika
banda la mbwa. Mtumwa alinung'unika na kusema :"nimekutumikia kwa miaka
10, na leo wanitenda hivi? Naomba unipe walau siku 10 kabla hujanitupa baniani!
" Mfalme akakubali.
Katika siku izo 10, mtumwa alimfuata mlinzi wa banda la
mbwa na kumuomba ampe nafasi kuwahudumia mbwa wale. Mlinzi alistaajabu ila
akakubali. Mara moja mtumwa akaanza kazi ya kuwapa mbwa chakula, kuwaogesha na
kila aina ya faraja ambazo wanyama huhitaji.
Siku 10 zikaisha, mfalme akaamuru mtumwa atupwe bandani
kutumikia adhabu yake. Hilo likafanyika kwa haraka, lakini cha kushangaza mbwa
walianza kulamba miguu ya mtumwa na si kumrarua kama ilivyotegemewa. Mfalme
akastaajabu, akasema:"Nini kimewasibu mbwa wangu? ",. Mtumwa akajibu
:" nimewahudumia mbwa hawa kwa siku 10 tu ila hawajasahau fadhila zangu.
Ila nimekutumikia miaka 10 lakini umesahau yote kwa sababu ya kosa moja tu!
" Kufikia hapo mfalme akatambua kosa lake na akaamuru mtumwa aachiwe huru.
FUNZO: Katika maisha kuna watu husahau mambo mema
waliyotendewa pindi wakikosewa. Kamwe usiruhusu historia nzuri kufutika sababu
ya jambo moja usilolipenda! Tembea katika msamaha! Bw. Wetu Yesu mwenyewe aliwasamehe
waliomtesa; alibeba mzigi ambao hakuustahili kutwikwa.
Binafsi natambua Mema yako mengi uliyonitendea na unayonitendea ktk
Maisha yangu, Wewe ni mtu wa muhimu sana
kwangu, kwa familia yangu, na kwa huduma
Mungu Baba ktk Kristo YESU Aliyoweka ndani yangu. Asante sana kwa kuwa mwema kwangu. MUNGU AENDELEE KUKUTUNZA NA KUKUFANIKISHA KTK
KILA ENEO MAISHANI MWAKO.
Uwe na wakati mwema.
[3:41 PM, 6/2/2016] Venlov: *MFALME ALIYEKUWA NA
MBWA WAKALI KUMI*
Kulikuwa na mfalme mmoja aliyekuwa na mbwa kumi wakali
sana. Alipenda kuwatumia mbwa hawa pindi akitaka kumuadhibu mtumwa aliyekosea.
Mbwa hawa waliwatesa watumwa kwa kuwararua na meno yao makali! Wakati mwingine
watumwa waliokutana na adhabu hii walipoteza uhai.
Siku mtumwa aliyemtumikia mfalme kwa miaka kumi alitoa
wazo baya ambalo halikumpendeza mfalme, ikaamriwa akamatwe na kutupwa katika
banda la mbwa. Mtumwa alinung'unika na kusema :"nimekutumikia kwa miaka
10, na leo wanitenda hivi? Naomba unipe walau siku 10 kabla hujanitupa baniani!
" Mfalme akakubali.
Katika siku izo 10, mtumwa alimfuata mlinzi wa banda la
mbwa na kumuomba ampe nafasi kuwahudumia mbwa wale. Mlinzi alistaajabu ila
akakubali. Mara moja mtumwa akaanza kazi ya kuwapa mbwa chakula, kuwaogesha na
kila aina ya faraja ambazo wanyama huhitaji.
Siku 10 zikaisha, mfalme akaamuru mtumwa atupwe bandani
kutumikia adhabu yake. Hilo likafanyika kwa haraka, lakini cha kushangaza mbwa
walianza kulamba miguu ya mtumwa na si kumrarua kama ilivyotegemewa. Mfalme
akastaajabu, akasema:"Nini kimewasibu mbwa wangu? ",. Mtumwa akajibu
:" nimewahudumia mbwa hawa kwa siku 10 tu ila hawajasahau fadhila zangu.
Ila nimekutumikia miaka 10 lakini umesahau yote kwa sababu ya kosa moja tu! "
Kufikia hapo mfalme akatambua kosa lake na akaamuru mtumwa aachiwe huru.
FUNZO: Katika maisha kuna watu husahau mambo mema
waliyotendewa pindi wakikosewa. Kamwe usiruhusu historia nzuri kufutika sababu
ya jambo moja usilolipenda! Tembea katika msamaha! Bw. Wetu Yesu mwenyewe
aliwasamehe waliomtesa; alibeba mzigi ambao hakuustahili kutwikwa.

0 Comments