Soma mfano huu wenye mafundisho
Bill Gates aliandaa usahili mkubwa kwaajili ya kumpata
meneja mpya Wakatokea watahiniwa 5000 na wakawekwa kwenye ukumbi mmoja
🔴Mmoja wa watahiniwa hao ni Onyango, Mkenya anayeishi
Marekani
🔴Bill Gates akawashukuru watu wote waliojitokeza, na
akasema "Kama kuna mtu hajui programu ya Java tafadhali aondoke"
🔴Watu 2000 wakaondoka
🔴Onyango akawaza "Ni kweli sijui Java lakini nikibakia
nitakuwa nimepoteza nini, Ngoja nitajaribu,"
🔴Bill Gates akasema kama kuna mtu hana uzoefu wa kuongoza
watu zaidi ya 100 tafadhali ondoka
🔴Watu 2000 wakaondoka
🔴Onyango akawaza "ni kweli sijawahi kuwa kiongozi hata
wa mtu mmoja, zaidi ya kujiongoza mwenye lakini nikiendelea kubakia nitakosa
nini, je nini kitanitokea
Akabakia tena
🔴Bill Gates akasema" Kama unajijua elimu yako hata
Diploma ya utawala huna tafadhali ondoka"
🔴Watu 500 wakaondoka
🔴Onyango akawaza tena "Elimu yangu ni darasa la saba,
lakini nikiendelea kubakia nitakosa nini" Akaendelea kubakia ndani ya
chumba
🔴Mwishowe Bill Gates akasema "kama hujui lugha ya
Serbia kwa ufasaha tafadhali ondoka"
🔴watu 498 wakaondoka
Onyango akiwaza "Hiyo lugha hata kuisikia sijawahi
hata Neno moja sijui, la nikibakia nitakosa nini"
akaamua kubakia na akajikuta wamebakia watu wawili tu
🔴Bill Gates akawasogelea na kuwaambia "Hatimae
nimewapata watu niliokuwa nawatafuta watu pekee wenye uzoefu na elimu
ninayotaka na vile vile Mnajua kuongeza lugha ya Serbia, Tafadhali sitaki
kuwasikia mkiongea lugha hiyo maana naichukia
🔴Taratibu kwa uoga Onyango akamnong'oneza Mwezie"
Heshima kwako unazo sifa zote hizi hongera kwa kufaulu "
🔴Mwenzake akajibu" sina sifa hata moja nimekomaa
tu"
👉🏽Kumbuka Mungu huwaita watu wasio na sifa kisha huwapa sifa
hizo
Tafadhali usikate tamaa
Comments
Post a Comment