SOMO: KOMBOA LANGO LA MUDA WAKO ILI UPATE ULICHOPOTEZA

SOMO: KOMBOA LANGO LA MUDA WAKO ILI UPATE ULICHOPOTEZA

*NA MWL CHRISTOPHER E.A.  MWAKASEGE*
*TAREHE 11 SEPT 2016*.
*SIKU YA 8*
*KOMBOA LANGO LA MUDA WAKO ILI UPATE ULICHOPOTEZA*
Bwana Yesu asifiwe, neno lilotuongoza ni kutoka waefeso 5:15-17 _‘’Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; *MKIUKOMBOA WAKATI KWA MAANA ZAMANI HIZI NI ZA UOVU*. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana’’_
~~Mistari hii tumekwenda nayo sana kwa siku ya siku zote nane na msisitizo ukiwa kwenye mstari wa 16 *MKIUKOMBOA WAKATI KWA MAANA ZAMANI HIZI NI ZA UOVU*.  Katika biblia kuna wakati unatakiwa ukombolewe ambao ndio umebeba mapenzi ya Mungu na pia biblia imesema *zamani hizi* maana yake ni muda ambao umebeba uovu. Kwa hiyo ili tuweze tembea katika mapenzi ya Mungu inatakiwa tuwe na muda wa kwetu yaani tuukomboe muda na huo muda ukishakombolewa unatakiwa utumike katika kutembea katika zamani hizi.
~~Katika kibabu cha Mwanzo 1;1 Biblia inasema hapo mwanzo Mungu aliumba ulimwengu. Na maana hapo bilia inaposema mwanzo maana yake ni kuwa kuna lango la Muda lilifunguliwa kwa sababu Mungu aliikata hali ya umilele na akaweka muda. Mungu kaweka muda ili mwanadamu aweze kutembea kwayo. Na Yesu yeye ni alfa na omega maana yake ni mwanzo na mwisho. Katika hali ya kawaida Yesu anaishi kwenye umilele ila yeye kuwa alfa na omega ni ili tupate pa kwenda maana yeye anaishi kwenye umilele lakini katika kuishi kwenye umilele lakini bado yeye ndiye anayeucontrol muda maana yeye ni alfa na omega na yeye ndiye anatusaidia tuweze kutembea kwenye huo muda.
~~Muda unafanya kazi na vitu vingi kama Fikra, sheria, muda wa kuabudu, muda wa kulelewa na ni maeneo mapana sana tumepita huko kama hukuwepo pata kanda sikiliza na kusikiliza na utapata kitu cha kukusaidia. *Lengo la semina hii kukuonesha kuwa muda wako umetekwa na unakatikwa kukombolewa kwa kuwa muda huo umebeba aina Fulani ya maisha*  . Na Kwa kuwa hutembei katika mapenzi ya Mungu na ina maana kuna vitu unakosa maana muda umebeba aina ya maisha ya mwanadamu. 
~~Leo nataka tungalie kipengele kingine
*MUDA WA TAIFA UNALOISHI NDANI YAKE*
Leo nataka tuangalie kwa mtiririko wa mambo yafuatayo.
*1* *Kila taifa limebeba kuishi kwa kufuata nyakati zilizopangwa juu yake kwa ajili yake*
*Matendo ya mitume 17:26-28*  _wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu cho chote; kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote. *Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao*; ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu. Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake_
~~Kila Taifa limeubwa kuwa liishi kwa kufuata nyakati, na ukisoma vizuri maandiko utaungana na mimi kuwa nyakati ziliumbwa kabla ya Taifa. Pia kila muda uliumbwa kabla ya mwanadamu na hivyo muda kwa MUngu ni kitu cha muhimu sana.
*2* *Siku ambayo Taifa linazaliwa ni lango la nyakati za aina ya maisha zilizoamriwa juu ya Taifa hilo*
Isaya 66:8 Ni nani aliyesikia neno kama hili? Ni nani aliyeona mambo kama haya? *Je! Nchi yaweza kuzaliwa siku moja?* *Taifa laweza kuzaliwa mara?* Maana Sayuni, mara alipoona utungu, Alizaa watoto wake.
~~Kuna Tofauti kati ya Taifa na Nchi.  *Nchi ni ardhi yenye mipaka halali ya kiumiliki, hii ni kwa mujibu wa Biblia*. Na Taifa *ni  mkusanyiko wa watu waliokubaliana  na waishi kwa pamoja chini ya utawala Fulani* Taifa kuzaliwa ni ishara ya kuwa kuna lango linafunguliwa , sasa kuna tofauti kati ya nchi kuzaliwa na taifa kuzaliwa.
~~Biashara inapozaliwa ina maana kuna lango Fulani la maisha linazaliwa ili kuingiza kwenye mfumo wa maisha yaliyoko kwenye biashara hiyo. Ndivyo ilivyo unapozaliwa mara ya pili ina maana unahamishwa kutoka kwenye ufalme wa giza na kuhamishiwa kwenye ufalme wa Mungu.
~~Kuna tofauti kati ya Taifa kupata uhuru na nchi kuzaliwa. Tofauti kati ya kuzaliwa Israel na siku ya kuingia kwenye nchi yake. Na kuna wengine hawajui Taifa la Israel lilizaliwa lini. Ngoja nikuoneshe Kitabu cha *Mwanzo 49:1,28* _‘’ Yakobo akawaita wanawe, akasema, Kusanyikeni, ili niwaambie yatakayowapata siku za mwisho. *Hizo zote ndizo kabila za Israeli kumi na mbili*. Na hayo ndiyo aliyowaambia baba yao, na kuwabariki; mmoja mmoja kwa mbaraka wake aliwabariki_
~~Hapa tunaona kuwa familia ya mzee Yakobo iligeuka na kuwa taifa la Israel, na huu ndio muda ambapo Taifa lilizaliwa na kumbuka kuwa Taifa la Israel lilikuwa kati nchi ya Misri. *Kumbu kumbu ta Torati 4:34*  _Au Mungu amekwenda wakati gani akajitwalia *taifa toka kati ya taifa lingine*, kwa majaribu, na kwa ishara, na kwa maajabu, na kwa vita, na kwa mkono hodari, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa maogofya makuu, kama vile Bwana, Mungu wenu, alivyowatendea ninyi katika Misri, mbele ya macho yenu?_
~~Taifa la Israel lilikuwa ndani ya taifa la misri lilipokuwa linazaliwa.  Na unapokuwa upo kuomba kwa ajili ya taifa inatakiwa kuwa makini kidogo maana kuna umuhimu sana wa kujua kuwa taifa lilizaliwa lini. Lazima utofautishe kati ya kupata uhuru wa Tanganyika na kuzaliwa kwa Tanzania. Kwa maana hii ya kupata uhuru ina maana hii nchi ilikuwepo bali ilikuwa chini ya utawala Fulani. Na Tanzania ilizaliwa  baada ya matokeo ya Muunganiko wa Tanganyika na Zanzibar. 
~~Kwa hali ya kiroho taifa la Tanzania halijawahi kutawaliwa, maana Tanzania haijawahi kupata uhuru.
~~ *Jana nilipokuwa nafanya maombi ya kuombea Uchumi wa watu jana niliuliza kuwa watu wangapi wana Uchumi mbaya. Na pia niliuliza kuwa ni watu wangapi wameona watu katika eneo hilo hilo wamefanikiwa na wao hawajafanikiwa. Sasa Kama jana hukunielewa leo tega sikio*
~~Kama ni katika nchi hiyo hiyo kuna baadh ya watu wanafanikiwa lakini wewe hufanikiwi ina maana hujajiconnect na Uchumi wa eneo wa nchi. Kwa sababu kila nchi inakwenda kwa hatua zake ina maana kuna tofauti kati ya hatua zako na hatua za Uchumi wa nchi.
*3* *Ili maisha ya mtu yafanikiwe katika Taifa analoishi inabidi Nyakati zake ziendane pamoja na Nyakati za Taifa hilo*
*Zaburi 139:16* _Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; *Chuoni mwako ziliandikwa zote pia*, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado_  Mtu huyu siku zake ziliandikwa kwenye kutabu na ina maana mtu anapozaliwa ukurasa mpya unafunguka.  Sasa unganisha na *Matendo ya mitume 17:26* _ Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha *kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao*_
~~Kwa hiyo inatakiwa kuwa kwa kila hatua anayoishi mtu yaani majira na nyakati inatakiwa yaendane na mazingira ya kiroho ya eneo nchi husika. Sasa zikiendana tofauti tofauti ina maana kunakuwa na shida Fulani na mtu atakayeishi katika taifa hilo hataweza kufaidi maendeleo ya uchumi ya nchi hiyo. Wageni wakijua mahali taifa linapita na wakajiconnect na Uchumi wa hilo eneo basi uwe na uhakika ya kuwa watafanikiwa kuliko wenyeji.
~~ Mungu alituma mtu mbele yao  na alipewa nafasi ya kuwa kiongozi wa nchi na ona ndugu zake walipokuja FARAO aliwauliza kuwa je wanajua kazi gani  ili aweze kuwaconnect na muda wa Taifa hilo. Ghafla wakaanza kuwa watawala wa taifa hilo, Wamisri walipata shida na spidi ya kufanikiwa kwa wana wa Isreal maana walikuwa wanaenda kwa spidi kwa sababu ya  walijua namna ya kujiconnect na Uchumi wa eneo la Misri.
~~Kaangalie habari za Isaka, Isaka alifanikiwa katika taifa lile la wafilisti na akapanda na akavuna japo wenyeji hawakuweza na alifunua na visima ambavyo vilikuwa vimefukiwa na baada ya mtu wakagombania. Baada ya kuendelea wenyeji waliona wivu kwa sababu ya maendele ya spidi ya Isaka.
~~Uchaguzi wa jiji la London wa mayor wa jiji, alipatikana mhindi. Na iliwapa shida kidogo waingereza pale walipoona mhindi anakuwa mayor. Na Tunajua kabisa wahindi ni wageni uingereza. Na kama ni wageni ina maana kuwa wazazi wake walikuwa wamemuandaa na aliweza kujua namna ya kujiconnect na nyakati za taifa hilo. Sasa jiulize Yusufu aliwezaje, na Daniel alitokea wapi, hawa watu walijua namna ya kuingi akwenye majira na Nyakati za eneo.
*4* *Ombea Mipaka ya Taifa kieneo kwa maana hali ya mipaka inaamua hali ya muda wa kiroho ya taifa*
*Kutoka 19:12* ‘’ _Nawe utawawekea mipaka watu hawa pande zote, ukisema, Jihadharini, msipande mlima huu, wala msiuguse, hata mapambizo yake; kila mtu atakayeugusa mlima huu, bila shaka atauawa_
~~Mpaka unaowekwa kwa jinsi ya mwili ni mipika ya kiroho kwanza unaotenganisha aina ya maisha kati ya hao watu/baina ya pande mbili kati ya hali ya kiroho. Katika kitabu cha kutoka tunaona ya kuwa watu hawa walikuwa na Mungu yule yule lakini upande wa Musa alikuwa na aina Fulani ya maisha kwa sababu ya eneo alikuwa amekaa na nje ya mipaka ya lile eneo nako walikuwa na maisha tofauti kwa sababu ya Matendo ya Mitume 17:26 ‘’ *Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao*
~~Mipaka ya nchi au Taifa Fulani ni mipaka inayoamua hali (maisha) ya kiroho ya sehemu hata ya kiuchumi kwa sababu imepewa majira na nyakati na miapaka yake
~~Mipaka ya taifa inaashiria mipaka ya muda wa aifa na kazi yake moja wapo ni kuunganisha muda wa watu husika na muda wa taifa hilo ambalo watu wanaishi. Nchi nyingi sana zinaishi kwenye sheria na kutokea kwenye sheria mama yaani katiba lengo lake ni kuweka kuishi kwenye mfumo Fulani wa maisha.
~~Mpinga kristo anapotaka kuleta vitu vyake kwanza lazima atabadilisha majira na sheria  ili kuweza kuwabana watu watakao kuwepo wakati huo waweze kuwa na mfumo Fulani wa maisha . Na ndio maana biblia inasema pasipo maono watu huacha kujizuia maana ana heri mtu anayetii sheria. Na kazi moja wapo ya sheria ni kukufanya uweze kuishi kwenye maono Fulani na kuweza kukufanya uweze kujua matumizi ya muda ambao ndio umebeba maisha.
~~Biblia inasema njozi hii ni kwa wakati uliomriwa na ijapokawia biblia inasema ingojee. Watu wengi wanaona tabu sana kutii sheria na kwa kuwa hawana waono na hata kama wanayo hawajui kuwa yanawapeleka wapi. *Isaya 10:13* * Kwa maana amesema, Kwa nguvu za mkono wangu nimetenda jambo hili, na kwa hekima yangu; maana mimi nina busara; nami nimeiondoa mipaka ya watu, nikaziteka akiba zao, nikawaangusha waketio juu ya viti vya enzi kama afanyavyo shujaa.*
~~Maana yake ni hali ya mipaka inaamua hali ya kichumi  ya eneo na biblia imetumia akiba na akiba maana yake ni Uchumi wa baade unaotegemea sasa. Kwa hiyo mipaka inashikilia muda na muda  na muda unapitisha maisha na inakuwa na sauti juu ya hali ya maisha ya watu waliochini ya mipaka hiyo.
~~Kwa mfano hapa kwetu Tanzania hapa. Na tuanze na huu mpaka kati ya Tanzania na Kenya wakati Fulani ulipata shida kidogo na kilichotokea kuna vitu tuligawana na mpaka leo shirika letu na halijainuka mpaka leo na linasua sua pia angalia na reli iliyokuwepo pale nayo ilikufa afu cheki na Wafanyakazi waliokuwa wa EAC zamani zile wengine hawana kazi hadi leo na hata wale wastaafu hawajaweza kulipwa mpaka leo. Shida ni iko kwenye mpaka na hapo ndipo tulipobanwa na tokea mpaka huo umepata shida hata maisha ya watu na nchi yaliyotegema mpaka huo yalivurugika kabisa. Haya na mambo ya rohoni usigombane na serikali bali omba Mungu kuhusu hili eneo.
~~Pia endelea kuombea mpaka wa mashariki mwa nchi yetu ili ukae sawa na uweze kupitisha maisha ambayo Mungu kayakusudia.  Cheki pia mpaka wa Uganda na Tanzania kipindi kile cha Idd Amini na kwa kweli angekuwa anasoma biblia asingegusa kabisa ule mpaka maana kuna vitu vilitakiwa kuwa ule mpaka upishe na ambavyo ulivurugwa ukaraibu kabisa maeno ya eneo lile na nchi yao kwao na ya kwetu ilipata shida maana kuna aina Fulani ya maisha yanayoamriwa na mpaka yakakosekana.
~~Pia angalia mpaka wa Msumbiji na Tanzania kipindi kile Taifa na Msumbiji iko chini ya ukoloni, na ona ilivuraga kabisa ule mpaka wa kusini na isababisha maisha ya ile mikoa ya kusini kuwa nyuma ya wakati na fananisha na leo kwa kweli iko nyuma. Na sababu kuu ni mipaka ilipoguswa ilivurugwa na kama Biblia ianvyosema Isaya 10:13 “ *nami nimeiondoa mipaka ya watu, nikaziteka akiba zao* maana yake Uchumi wa maeno ulivurugwa na *Uchumi* hapa limefichwa kwenye neo *akiba*
~~Pia kumbuka kuombea mpaka kati ya Tanzania na Malawi, maana nao unataka kuleta shida kwa sababu nao una sauti ya maisha ya watu wa kusini wanaoutegemea huo mpaka. Haya mambo ni ya ndani sana na ni neema tu ya Mungu ameamua kuyateremsha kwa staili hili.
~~Mfano wa Jumuia ya ulaya  na kujitoa kwa uingereza. Uingereza umejitoa Umoja wa ulaya alafu inataka kutumia mpaka kwa ya Umoja wa ulaya na Umoja wa ulaya inajaribu kweka mashart kwa uingereza kuwa uingereza inataka kutumia mipaka ya Umoja wa ulaya kupisha tu Uchumi na sio watu. Kwa maana hiyo inakuwa ni ngumu sana kuchagua kitu gani mpaka upitishe maana mpaka huo unaopitisha Uchumi ndio huo unapitisha  na watu sasa uingereza inapokuwa inataka kuchagua kupitisha tu aina Fulani ya maisha inakuwa ni taabu kidogo. Sasa hapa ndipo hekima inahitajika sana kwa nchi zote ambazo zitakuwa zinategema mipaka ya uingereza na mipaka ya Umoja wa ulaya kibishara maana zisipojua cha kufanya Uchumi utayumba, kwa mujibu wa Isaya 10:13.
*5* *Muda wa taifa unaweza kukwamisha kwa watu wa taifa hilo kutokuandaliwa kwa ujio wa mabadiliko ya nyakati ya mbele yao*
*Mwanzo 15:13-16*  _Bwana akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa muda wa *miaka mia nne*. Hata na taifa lile, watakaowatumikia, nitawahukumu; baadaye watatoka na mali mengi. Lakini wewe utakwenda kwa baba zako kwa amani, utazikwa katika uzee mwema. Na kizazi cha nne kitarudi hapa, maana haujatimia uovu wa Waamori bado_
*Kutoka 2:23-25*  _Hata baada ya siku zile nyingi mfalme wa Misri akafa; wana wa Israeli wakaugua kwa sababu ya ule utumwa, wakalia; kilio chao kikafika juu kwa Mungu kwa sababu ya ule utumwa. Mungu akasikia kuugua kwao, *Mungu akakumbuka agano lake alilolifanya na Ibrahimu na Isaka na Yakobo*. Mungu akawaona wana wa Israeli, na Mungu akawaangalia_
*Kutoka 12:1-2, 37-42*  _Bwana akanena na Musa na Haruni katika nchi ya Misri, akawaambia, Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu. Wana wa Israeli wakasafiri kutoka Ramesesi mpaka Sukothi, walipata hesabu yao kama watu sita mia elfu watu waume waliokwenda kwa miguu, bila kuhesabu watoto. Na kundi kubwa la watu waliochangamana mno wakakwea pamoja nao; na kondoo na ng'ombe, wanyama wengi sana. Nao wakaoka mikate isiyochachwa ya ule unga waliouchukua walipotoka Misri, maana, haukutiwa chachu, kwa sababu walitolewa watoke Misri, wasiweze kukawia, nao walikuwa hawajajifanyia tayari chakula_
_Basi wana wa Israeli kukaa kwao, maana, muda waliokaa ndani ya Misri, ulikuwa ni miaka mia nne na thelathini. Ilikuwa mwisho wa miaka hiyo mia nne na thelathini, ilikuwa siku ile ile, ya kwamba majeshi yote ya Bwana yalitoka nchi ya Misri. Ni usiku wa kuangaliwa sana mbele za Bwana kwa sababu ya kuwatoa katika nchi ya Misri; huu ndio usiku wa Bwana, ambao wapasa kuangaliwa sana na wana wa Israeli wote katika vizazi vyao_
~~Ukiangalia kitabu cha Mwanzo ukaona kuwa muda wa agano wa kukaa Misri ulikuwa ni miaka 400 ‘’ . _nao watateswa muda wa *miaka mia nne*_ una unakuta muda wa mateso ulikuwa umeisha na ndio maana walipoanza kulia haikutakiwa tena waendelea kulia pale  na ndio maana Mungu alilikumbuka agano. _*Mungu akakumbuka agano lake alilolifanya na Ibrahimu na Isaka na Yakobo*_  . na ndio maana Mungu alianza mapema kumuandaa Musa kwa ajili ya kuja kuwaokoa wana wa Israel ili waweze kuondoka katika taifa Misri.
~~Muda wa taifa unaweza ukatekwa na ukakwamisha kabisa watu na wana wa Israel walipolia kwa Bwana, Mungu alilikumbuka agano lake alilolifanya na Ibrahimu. Wana wa Israel walipokuwa wanaomba walikuwa wanaomba maisha yao yabadilishwe maana hawakuwa wanaomba ili waweze kuondolewa katika taifa hilo. Lakini agano linasema kuwa baada ya miaka 400 wanakuwa hawana uhalali tena wa kuweza kuishi chini ya Utawala wa Farao na ilitakiwa waweze kuondoka.
~~Na maana ya agano lilokuwepo lilikuwa linasema hibi  baada ya miaka 400 Mungu alikuwa hahusiki tena na wao wakiwa Misri na ndio maana Mungu alimbebesha Musa majira na nyakati ili aweze kulitoa taifa lileMisri, na una mpaka wakakubali iliwachukua miaka 30, walipokuwa wanajadiliana namna ya kutoka huko Misri.  Na ina maana kila kitu kilistop kwa muda wa miaka 30 walipokuwa wanavutana.
~~Baada ya kukubali kuondoka tena iliwachukua miaka 40 kuweza kuingia katika nchi ambayo Mungu waliwaambia kwa sababu ya kubishana tena njiani. Na ukijumlisha jumla ni miaka 70 yaani ile 30 wakati wanabishana kutoka misri na miaka 40 wakati wakiwa safarini.  Na kwa maana hiyo muda wa agano wao wa kukaa katika nchi ya kwao ulikuwa nyuma kwa miaka 70. Umewahi fikiria kwa muda wote huo ni mambo mangapi yalistop.  Sasa jumlisha na ule muda waliokaa Misri yaani miaka 400 yote na jumla na hii ni 470 ina maana yote ilistop kabisa.
~~Angalia *Kutoka 23: 23,28-30* _ Kwa kuwa malaika wangu atatangulia mbele yako, na kukufikisha kwenye Mwamori, na Mhiti, na Mperizi, na Mkanaani, na Mhivi, na Myebusi; nami nitawakatilia mbali. Nami nitapeleka mavu mbele yako, watakaomfukuza Mhivi, na Mkanaani, na Mhiti, watoke mbele yako. *Sitawafukuza mbele yako katika mwaka mmoja* nchi isiwe ukiwa, na wanyama wa bara wakaongezeka kukusumbua. *Nitawafukuza kidogo kidogo mbele yako, hata utakapoongezeka wewe, na kuirithi hiyo nchi*_
~~Anazungumzia kipindi kipi, ni kipindi wanapojiandaa kwenda Kanani. Na walipovuka Jordan walianza kupamba na kitu kingine na spidi ya kuwatoa ilikuwa inategemea sana maandalizi waliyokuwa wanayafanya  maana halikuwa suala la la kuwatoa wale watu waliokuwa wanatakiwa kuondolewa bali ni suala la wao kujiandaa.
~~Hata baada ya wao kuweza kujiandaa na kuingia ile nchi na Joshua aliwowarithisha watu wote wakasema sisi na nyumba zetu tutamtumikia Bwana. Na kizazi chao wote waliweza kumtumikia Bwana kwa muda wao hadi kizazi chao kilipoisha.  Na ndipo kiliinuka kizazi kingine kisichomjua Bwana na hiki ni kipindi cha Waamuzi.
*Na leo nataka nikupe agenda za maombi ya kuombea ili taifa letu liweze vuka hapa mahali*
*1*  *Omba Mungu awasaidie viongozi wanapotaka kuleta mabadiliko kwenye taifa, familia, siasa, kanisani au eneo lolote lile ambalo Mungu anataka mabadiliko*.
~~Musa alipewa upako lakini kuweza kuleta mabadiliko  lakini ilimchukua miaka 30 na kama tungesema ni vipindi vya siasa tungesema ni awamu tatu maana ni miaka 10 bado tu mabadiliko hayajafikia na pia ongeza na miaka mingie 40 yaani bado wanabishana tu. 
*2* *Mungu ainue watu kuwahimiza na kuwalinda watu ambao Mungu kawaandaa kwa ajili ya kubeba muda wa kiroho ili kuwasaidia watu kubeba muda wa taifa wa kiroho ili kuwasaidia watu kuishi muda huo*
~~ *Musa* alizaliwa ili aweze kubeba majira na nyakati za kulibadilisha taifa na Israel ili litoke Misri na linekee Kanani. Na alishindwa kufika kwa sababu ya kushindwa kuchukuliana na watu wale. Katika wakolosai 4:5 biblia inasema enendeni kwa hekima na watu walio nje. Omba Mungu atoe hekima hii kama alivyotoka kwa sulemani ya kujua namna ya kuwaongoza watu.
~~Naongea na watu kama akina *Joshua* ambao Mungu anawatafuta kwa ajili ya kuwarithisha watu wake urithi ambao Mungu kakukusudia
~~Naongea na wana wa *Isakari wanaojua Nyakati na mambo yanayotakiwa kufanyika katika nyakati hizo*
~~Naongea na watu kama  *Esta* wa kulikomboa taifa lote, watu kama *Daudi* wenye kuleta uchaji na ufalme wa Mungu katika nchi. Maana Daudi ndiye aliyeleta kiti cha enzi cha Bwana na sanduku la Bwana.
~~Watu kama *Samweli* maana samweli alipitisha watu wawili mikononi mwake Daudi na Sauli. Na omba Mungu awafanye hawa watu washike zamu zao na hata kama walikuwa wamejificha wapi Munguatawafuata hata kwa vichaka vya moto ili walifanye kusudi la Bwana.
*3* *Mungu awape kuelewana watu waliopewa muda wa kitaifa kwa kufanana na ili kwamba katika hali hiyo ya kila mtu kuwa na majukumu tofauti lakini waweze kuelewana*
~~Musa na Haruni walikuwa na majukumu tofauti na Haruni ndiyo alikuwa anaisema ndoa ya Musa na Mungu akamkasirikia sana Haruni na isingekuwa Musa kuomba Mungu akifanya kitu kibaya sana. Omba watu  hawa waelewane ili kusitokee ufa, maana Taifa la Israel lilisimama kwa siku 7  ili kutatua huu mgogoro.
~~Yusufu  na Faro waweze kuelewana ili kazi ya Bwana iweze kufanyika. Na kisiwepo izuizi
~~Daudi na wana wa Isakari ili waweze kutumia muda vizuri sawa sawa na kusudi na Bwana.
~~Samweli na Sauli waweze mtii Bwana na kulifanya taifa lilipie kipindi kizuri na isitokee tena Ikabodi maana yake utukufu kwa Bwana kuondoka katika Taifa.
~~Elia na Ahabu waweze elewana na taifa liache kuabudu miungu mingine na limrudie Bwana.
~~Esta na Ahusero ili kuweza kulisaidia taifa. Modekai walikuwa anamuambia Esta kuwa yupo kwenye muda wake lakini walikuwa hawambebi kwenye maombi ili ndoa yake ikae vizuri maana ndiyo ilibeba maisha ya kwao. Na iliwagharimu siku tatau kufunga na kuomba ili kuerejesha suala hili mahali pake baada ya kuharibika.
~~Daniel na watawala wa Babeli ili nchi ikae vizuri.
*4* *Mungu awape kuelewana kati ya aliyebeshwa muda wa kiroho wa taifa na watu wake*
~~Joshua na wana wa Isarel, japo walimzoe sana Musa lakini Mungu alitaka pia Joshua amtumikie na akamilishe kusudi lake maana muda wa Musa ulikuwa tayari umeisha.  Na wawe na kibali machoni pa watu wote wa Bwana.
~~Elia na Ahabu, maana Elia alikuwa ameibuka tu na watu kama hawa wapo tukiomba Mungu anawaleta na atawaibua, japo Elia alibeba majira na Nyakati za taifa. Japo Elia alikuwa na mamlaka juu ya muda ila japo alisimamisha muda bado lakini na yeye alipata shida maana miaka 3 ya ukame alilishwa na kunguru.
~~Mikoani ninakopita huwa naona watu kiu waliyonayo na naomba Mungu sana ili Mungu ainue waalimu wa kuweza kutusaidia taifa hili liweze pata neno la Bwana maana hatuwezi tumika sisi wenyewe katika taifa zima la Tanzania lakini watu wana kiu sana ya neno la Mungu. Na ukiona kiu ya neno la Bwana inaongezeka basi ujue kuwa ni Mungu anataka kuwapa melekezo watu wake kwa ajili ya kutembea katika majira yake na nyakati zake.
*HIZI NI AJENDA ZA MAOMBI NA OMBEA SANA MAANA KUPONA KWA TAIFA NI KUPONA KWAKO*
Napenda kumshukuru Mungu sana kunisaidia kuandika semina hii kwa siku zote nane. Na Pia Mwl Mwakasege na huduma yote ya Mana kwa utumishi wako.
Tuonane tena siku nyingine Mungu akitupa kibali.
Ratiba ya Semina za Mwalimu C. Mwakasege
4 - 11 Septemba 2016 - Arusha (Uwanja wa Reli)
18 - 25 Septemba 2016 - Dar ( Uwanja wa Chuo Kikuu - UDSM)
29 Sept - 2 Oktoba 2016 - Njombe Mjini
10 - 16 Oktoba 2016 - Mbeya Mjini (Uwanja wa Otu)
19 - 23 Oktoba 2016 - Iringa Mjini ( Uwanja wa Gangilonga)
4 - 6 Novemba 2016 - Birmingham, Alabama USA
11 - 13 Novemba 2016 - Washington DC USA
Kumbuka kuziombea semina hizi,kusudi la Mungu lifanyike. Mbarikiwe!!
Kusoma Zaidi Mafundisho ya Mwl Mwakasege tembelea
*Facebook*
https://www.facebook.com/Christopher-Diana-MwakasegeMana-Ministry-132462780111984/
Youtube
https://www.youtube.com/channel/UC4p4lrpgpNd-9bHPgHJ4xWw
Ustream
http://www.ustream.tv/channel/mwakasegemanaministry
website
www.mwakasege.org na kama umeokoka kupitia mafundisho haya soma somo la Utangulizi katika link hii http://www.mwakasege.org/mafundisho/hongera/utangulizi.htm

Post a Comment

0 Comments