KUFUNGA NA KUOMBA KUNAKO ONGEA MBELE ZA MUNGU UTANGULIZI



KUFUNGA NA KUOMBA KUNAKO ONGEA MBELE ZA MUNGU
UTANGULIZI
Kufunga na kuomba kunako ongea ni kufunga na kuomba kunakotoa sauti inayopenya hadi kitini pa Mungu na kuleta mabadilko ya kudumu katika ulimwengu wa mwili. Tunaweza kusema Kufunga na kuomba kunakoongea ni atomic bomb katika ulimwengu wa roho kwa sababu hutoa matokeo makubwa bila kumuumiza anayetumia silaha hiyo.
Mifano ya watu waliojihusisha na kufunga na kuomba kunakoongea ni:
1. Yesu Kristo
2. Yohana Mbatizaji
3. Daniel
4. Ester nk
.
NB: Kufunga na kuomba ni kanuni ya ulimwengu war oho (uwe wa nuru au giza) wa kuhuisha nguvu za kiroho ili kufanya jambo lililokusudiwa.
AINA ZA KUFUNGA.
Zipo aina tano (5) za kufunga.
1. TOTAL FAST (FUNGA KAVU).
a. Absolute fasting (Funga iliyo sahihi) Hii ni funga ya kutokula chakula kabisa wala kunywa maji kwa siku zisizo zidi tatu (3) kama (Esta 4:16).

b. Supernatural Fasting (Funga ya Kiungu).Funga ya kutokula chakula kabisa wala kunywa maji kwa siku zaidi ya tatu (3) kama Musa (Kumb.9:9 & 9:18) kwa siku 40.
2. PARTIAL FASTING (FUNGA NUSU)
a. Yohana Mbatizaji aliamua kufunga maisha yake yote akila asali na Nzige tu. Dan. 10:2-3 Kuacha kula aina maalumu ya vyakula ambavyo ungevipenda.

b. Funga ya milo miwili au mmoja kwa siku.

c. Funga ya kawaida (Normal fasting).Kunya maji tu.
3. FUNGA YA KULAZIMISHWA (IMPOSED FAST).
Matendo 28:1 Safari ya Paulo akielekea Rumi.Kwasababu ya misukosuko ya mawimbi majini watu wanashindwa kula.Pia kama mtu anaumwa unakosa hamu ya chakula.Mala nyingine tunapata misukosuko kama sehemu ya Maisha kiroho pia.
4. FUNGA YA WAZI/KANISA, HADHARA AU TAIFA. (PUBLIC AND NATIONAL/CHURCH FASTS).
Hii inakuwa funga ambayo inatangazwa na inakuwa wazi kwa kila mtu.Sio za siri.Yona 3:6.

5. Funga ya mtu binafsi
Hii hufanywa na mtu mmoja kwa siri na mungu wake hapana anayejua mtu huyo kama amefunga.
SIFA 7 ZA KUFUNGA NA KUOMBA KUNAKOONGEA
1.     Huongozwa na roho wa Mungu Marko 1:12-14, Yesu aliongozwa na roho kufunga nyikani ndio maana hakutenda dhambi katika kufunga na kuomba kwake.
2.     Lazima iwe katika kweli ya Mungu. Kama funga na kuomba huko hakuko katika roho hakuwezi kuwa katika kweli kwa kuwa roho wa mungu hatenganishwi na kweli ya Mungu. 2samwel12:16-17 Daudi alijaribu kufunga na kuomba ili mtoto aliyezaliwa katika zinaa asife hakufanikiwa kwa kuwa Mungu tayari alisema atakufa hakika. Hata alipokuwa ameshakufa daudi aliendelea kufunga hii inadhihirisha kuwa hakuwa rohoni kwa sababu alijua anachoomba siyo mapenzi ya Mungu. Angekuwa rohoni roho angemjulisha aache kuomba kwa kuwa Mungu amekataa.

3. Lazima funga ifanywe katika unyenyekevu wa hali ya juu wa rohoni. Mtu anayefunga kwa kiburi cha uzima hawezi kupata matokeo yaliyokusudiwa. Mfano unafunga ili ujilipizie hasira yako kwa mtu anayekudharau au kutesa, unataka kushindana na wengine, unataka kuonesha kwamba wewe ni mwamba kanisani kwenu nk.
Soma isaya 58:3-4) “Husema mbona tumefunga lakini huoni, mbona tumejitaabisha nafsi zetu lakini huangalii? Fahamuni siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu, Tazama ninyi mwafunga mpate kushindana, kugombana na kupiga ngumi ya uovu”

4. Lazima ifanywe katika furaha ya roho mtakatifu na siyo kwa kujilazimisha na kunung’unika
Ukifunga kama andiko la isaya 58:3 inavyosema (mbona tumefunga lakini huoni, mbona tumejitaabisha nafsi zetu lakini huangalii? Hutapata matokeo yaliyokusudiwa. Badala yake fanya funga na maombi yaliyojaa furaha ya roho mtakatifu.Mathayo 6:16-18 “tena mfungapo msiwe kama wanafiki, wenye uso wa kukunjamana, maana hujiumbua nyuso zao ili waonekane na watu kuwa wanafunga, amini nawaambia wamekwishakupata thawabu yao. Bali wewe ufungapio jipake mafuta kichwani, unawe uso ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na baba yako aliye sirini na baba yako aonaye sirini atakujazi” linganisha andiko hilo na isaya 58:5

5. Lazima kufunga kuambatane na kuomba na kuutafuta uso wa bwana 2nyakati 7:14,

6. Lazima kufunga na kuomba kufuate kanuni ya upendo na si ubinafsi. Yaani kumpenda Mungu na jirani kama nafsi yako mwenyewe.
Matendo ya upendo kwa mungu na watu ni kama
1. hicho ambacho ungekula mpe Yesu ale. Unadhani Yesu anapatikana kanisani? Hapana, msikie mwenyewe anapatikana wapi katika mathayo 25:34-40 “Kisha mfalme akawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, njooni mliobarikiwa na baba yangu, urithini ufalme muliowekewa tayari tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu kwa maana nalikuwa na njaa mkanipa chakula, nalikuwa na kiu mkaninywesha, nalikuwa mgeni mkanikaribisha, nalikuwa uchi mkanivika, nalikuwa mgonjwa mkaja kunitazama, nalikuwa kifungoni mkanijia………………………………………amini nawaambia yoyote mliyowatendea mmojawapo ya hao ndugu zangu walio wadogo mlinitendea mimi”
NB Linganisha andiko hilo na isaya 58:6a, 7 je swaumu niliyoichagua mimi siyo ya namna hii?…………….je siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani mwako? Umwonapo mtu aliye uchi umvike nguo, wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe”
2. Ombea watu wengine kama familia, jamii yako, familia na taifa kwa nguvu ileile unayotumia kuombea mahitaji yako binafsi. Isaya 58:6, 2 samweli 22: 25-26. “ kwa mtu mwenye fadhili utakuwa mwenye fadhili, kwa mkamilifu utajionyesha kuwa mkamilifu, kwake ajitakasaye utajionyesha kuwa mtakatifu na kwa mpotovu utajionyesha kuwa mkaidi” soma pia nehemia 1:1-11 jinsi Nehemia alivyolia na kutubu kwa habari ya mabaya yaliyoipata Israel na Yeusalem hakujali kuwa alikuwa mahali salama. Danieli 9 ona jinsi alivyolia kwa Mungu kwa habari ya wayahudi hata kama yeye mwenyewe alikuwa ikulu akiheshimika sana. Au Ester ambaye alikuwa mke wa mfalme Ahusueoro angeweza kubaki alivyo lakini alifunga na kupomba kwa ajili ya ndugu zake

SABABU /FAIDA 12 ZA KUFUNGA NA KUOMBA KATIKA KANISA (MTU AU USHIRIKA)
1. Tunafunga kuonyesha utii kwa neno la Mungu (Yoeli 2:12)
Biblia kuanzia agano la kale hadi agano jipya inaonyesha umuhimu wa kufunga. Watumishi wote wa Mungu walikuwa wanafunga katika siku za maisha yao hivyo unavyofunga unaonyesha utii katika kulifuata neno la Mungu na kuliamini. Yesu Pia alisema kuwa siku zinakuja ambapo tutalazimika kufunga. (Mathayo 9:15)

2. Tunafunga ili kujinyenyekeza mbele za Mungu na kupata nguvu na neema yake. Tunahitaji neema ya Mungu siku zote ili tuweze kuishi, na ili kuipata inatubidi kujinyenyekeza chini ya mkono wake ulio hodari, Ebrania 4:16, Yakobo 4:10. Ezra aliwaamuru watu wafunge ili wapate kujinyenyekeza mbele za Mungu na kupata neema yake kwa ajili ya taifa lao, Ezra 8:21.

3. Tunafunga ili kuomba rehema
Yesu alichukua dhambi zetu zote msalabani, inawezekana kuna jambo unaona unashindwa kuacha na umejaribu sana. Hapo unatakiwa kufunga na kuomba rehema ili Mungu akuwezeshe kushinda. Pia unafunga kuomba rehema kwa ajili ya wengine mfano familia, jamaa na taifa pia. Daniel alifunga na kuomba rehema kwa ajili ya dhambi za taifa la Israeli na kubeba uovu wao mbele za Mungu. Danieli 9:3-5. Taifa la Ninawi walifunga na kuomba rehema kwa Mungu kutokana na uovu wao. Yona 3:5-10

4. Tunafunga ili katika udhaifu wetu Nguvu ya Mungu ionekane
Unapofunga unakuwa umeikana nafsi na kumchagua Mungu, uankuwa umedhamiria moyoni kutaka kuona nguvu ya Mungu ikionekana na sio nguvu yako. Zaburi 109:24-28, 2Korintho 12:9-10

5. Tunafunga kupata msaada wa Mungu katika kukamilisha kusudi lake
Viongozi wa kanisa la Antiokia walifunga na kuomba kabla ya kuwatuma Paulo na Barnabas. Walifanya hivi ili waweze fanya uchaguzi sahihi chini ya uongozi wa Mungu. Na Paulo na Barnabas walikuwa wakifanya hivyo katika miji waliyotembelea kila walipokuwa wanataka kuchagua viongozi. Kutokana na jambo hili makanisa yale yalizidi kusonga mbele maana walimshirikisha Mungu kwa kufunga katika maamuzi yao yote. Matendo 13:3-4, 14:23

6. Tunafunga wakati wa taabu
Mordekai na Esta walitangaza kufunga kwa wayahudi wote pale ilipofahamika kuwa kuna mpango wa kuwateketeza wayahudi wote, na kupitia kufunga na kuomba huku wayahudi walisalimika. Ester 4:15-16. Wakati wa taabu ni wakati wa kufunga na kumlilia Mungu na hakika Mungu ataonekana. Mfalme Yehoshafati pia alitangaza kufunga pale walipokuwa wamevamiwa na maadui wengi na wao hawakuwa na uwezo wa kupigana nao. 2Nyakati 20. Tumeona kwa uchache jinsi kufunga kulivyo muhimu katika maisha yetu ya kila siku.

7. Kufunga hunoa Imani (ili iwe kali) na huongeza ujasiri.
Esta 4:16.Huyu mama asingefunga alikuwa hana ujasiri wala imani ya kuingia kwa mfalme kinyume cha sheria – kwasababu adhabu yake ilikuwa ni kifo.Ndio maana aliomba wayahudi wote walio kuwa shushani wambebe kwa maombi.

8. Kufunga huleta unyenyekevu mbele za Mungu. Luka 14:11 & 18:14 Ezra 8:21.Mungu huwapa wanyenye kevu neema,na kuwainua.(1Petro5:5-6).Ukitaka kuwa mnyenyekevu mbele za Mungu basi jifunze kuwa mfungaji.

9. Kufunga huongeza/huleta nguvu ya Maombi na kuondoa ukame wa kiroho.Zaburi 35:13 Kufunga ni kama 4WD ya maombi.ISAYA 40:31 na Mithali 20:13.

10. Kufunga hufanya ulimwengu wa roho uwe wazi.
Daniel 10:14.Baada ya Danieli kufunga siku 21 alianza kuonyeshwa na Mungu mambo ya siku za mwisho za dunia ambako hata

11. Kukuza kanisa na huduma ya Mungu
a. Hili tendo lililofanywa sana na mitume na wafuasi wao.Act 14:22.Kukua kwa Kanisa la kwanza kulitegemea Maombi ya kufunga.
b. Ushuhuda wa Paulo kuhusu maisha yake.Akafanikiwa sana kwa sababu ya maombi ya kufunga.2Koritho 6:4-6.

12. Kutiisha miili yetu ipate kumtii Kristo. Miili yetu siku zote hupingana na Roho Mtakatifu.Galatia 5:16-17.nia ya Mwilini uadui dhidi ya Mungu Rumi 8:7-8 hivyo inabidi tuiitiishe kwa kufunga 1Kor.9:27.

Post a Comment

1 Comments