Mafundisho yao juu ya Vita vya Kiroho.
Mafundisho yao juu ya Vita vya Kiroho.
Wanaigawa vita ya kiroho katika ngazi tatu. Kwanza, kuna kile
wakiitacho mapambano ya “ngazi ya chini”, ambayo wanamaanisha kutumia mamlaka
ambayo Mungu amelipatia kanisa lake kuwatoa mapepo toka kwa mtu mmoja mmoja.
Hii imetolewa mfano wake vizuri katika Injili na Matendo ya Mitume na hivyo
siyo jambo lenye kuleta hoja kwetu. Aina ya pili inaitwa mapambano ya “ngazi ya
kishirikina” ambavyo wanamaanisha kuwa ni kukabiliana na kuzifunga roho za
uchawi, dini ya kishetani, ibada za sanamu, na kadhalika, mambo ambayo kwa
kawaida yanaleta athari zake ovu kupitia kwa mtu fulani binafsi. Ngazi ya “juu”
ya mapambano ya kiroho inaitwa mapambano ya “kimkakati” au ya “kwenye anga za
juu” ambapo maombezi yanahitajika ili kuzitambua na kuzifunga roho mbaya za
ngazi za juu, au mamlaka na nguvu, ambazo zinatawala katika maeneo makubwa ya
kijografia.
Hizi ngazi mbili za mwisho ni mambo ya kukisia na ubunifu wa
hawa waandishi wa kisasa, kama tutakavyoweza kuona. Ile ngazi ya pili haina
umaarufu mkubwa na inaingiliana kwa kiasi fulani na ile ya tatu. Kwa hiyo
nitazungumza kidogo juu ya ngazi hii ya pili, tutakapoangalia vifungu
vinavyohusiana nayo. Lakini ni ngazi ile ya tatu ambayo mafundisho yao
yanakazia, kwa hiyo kwa upana zaidi tutakuwa tunatazama ngazi ya mwisho, kwa
vile ndiyo hasa inayowakilisha udanganyifu na hatari kubwa.
Ni namna gani roho hizi mbaya zinatambulikana na watu
kukabiliana nazo? Sawa, kwa wale ambao wanaamini kuwa wameitwa ili kuhusika na
aina hii ya vita, wanatumia muda wao mwingi katika maombi kutafuta kutambua kwa
njia za karama za kiroho na “upambanuzi”, jina au aina ya roho (moja au zaidi
ya moja) iliyoshikilia eneo fulani – inaweza ikawa ni roho ya kiburi, uchoyo,
tamaa mbaya au uchafu, ndipo tena wanakabiliana nayo katika vita vya maombi na
kuzifunga nguvu zake – hii inaweza ikachukua siku kadhaa au wiki kadhaa. Ili
kutambua ni roho gani inatawala juu ya mji, wanafundisha pia haja ya kile
wanachokiita kuwa ni “kutengeneza ramani za kiroho”, kazi ambayo inahusisha
uchunguzi wa historia ya mji – hali ya mji huo kidini, kijamii na kikabila, na
historia ya nyuma, hali kadhalika kuhusu matendo maovu yaliyofanywa katika mji
huo, au kufanywa na mji huo, au yaliyofanywa dhidi ya mji huo – kurudi nyuma
miaka zaidi ya mia au kama si elfu na zaidi! Inafundishwa kwamba tendo hili
litatusaidia sana kuzitambua ni roho chafu za jinsi gani zinazoshikilia mji kwa
nguvu sana ili kwamba tuweze kuomba kwa ufanisi dhidi yake na kisha kuzifunga
nguvu zake! Nilishughulikia juu ya hoja hii ya kiushirikina katika ile makala
yangu ya kwanza.
Baadhi ya hawa wahubiri wa kisasa wanasema
kwamba hawataweza kuhubiri Injili katika eneo lolote lile hadi kwanza wawe
wametambua roho mbaya zinazotawala na wakazifunga nguvu zake. Lakini sasa Yesu hakutumia mtindo huu
katika mji wowote aliouendea. Hatusomi chochote kuhusiana na mtume
Petro au Paulo akishiriki katika aina hii ya “vita vya kiroho” kabla
hajautembelea mji wowote ule; au kuhubiri Injili hapo. Hatusomi chochote
kile kuhusiana na mtume Paulo kuzifunga roho za uzinzi, uchoyo au tamaa mbaya
kule kwenye miji ya Efeso au Korintho kabla hajaanza kazi yenye nguvu hapo. Wala
hatusomi popote kwamba katika nyaraka zao kuwa mitume hao waliwasihi
watakatifu kuomba dhidi ya roho za kimaeneo, kama hawa waandishi na wahubiri wa
kisasa wanavyotutaka sisi tufanye!
Makosa Mawili ya Kimsingi
Fundisho hilo siyo tu kwamba ni nyongeza kwa Maandiko, bali
kwa kweli linaielezea vibaya na kuidhoofisha kazi yote ya Kristo pale Kalvari
na jinsi Injili ilivyo. Na tutaanza kwa kuyatazama makosa mawili ya kimsingi
ambayo mafundisho hayo yanawatumbukiza watu ndani yake.
Kwanza, fundisho hili linakanusha au
kupunguza ushindi mkamilifu ambao Yesu aliutimiza pale msalabani. Mafundisho
yenyewe hauyakiri kikweli ushindi halisi ambao Kristo ameupata dhidi ya nguvu
zote katika ulimwengu wa roho, kwa niaba ya kanisa lake, kadhalika na kwa ajili
ya wanadamu, wala hawa walimu hawaheshimu kikweli na kujali mamlaka zote na
haki ambazo Mungu anazo za kuwaelekezea watu wake na kujenga kanisa lake.
Kabla ya pale Kalvari, Yesu mwenyewe alikuwa akitembea huko
na huko akihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu. Hali kadhalika
aliwatuma mitume pamoja na wanafunzi kuhubiri Injili ya ufalme wa Mungu
na kuwatoa watu mapepo na kuwaponya wagonjwa. Akiwa amepokea msamaha na ushindi
juu ya majeshi ya uovu pale msalabani, Kristo aliita, akatuma na akawatumia
mitume vile vile na watu wengine katika kulijenga kanisa lake. Tunajua kuwa
watu wengi waliokolewa kupitia mahubiri ya mtume Petro. Filipo alitumwa
na Mungu kuwageuza wengi watokane na dhambi na uchawi. Matendo 8. Na katika ile
Matendo 11:19-21, tunasoma kuwa, “… mkono wa Bwana ukawa pamoja nao, wao …
waliohubiri Yesu ni Bwana kwa mataifa na watu wengi wakaongezeka upande wa
Bwana”. Mtume Paulo aliitwa na Mungu, Matendo 26:13-18; katika ile Matendo 13:2
mtume Paulo alitumwa na Mungu. Watu hawa wote walihubiri neno la Mungu kwa
watu wengine, wakikiri kile ambacho Kristo amekifanya pale Kalvari na watu
wengi walimgeukia Bwana. Mitume waliwakomboa waume kwa wake pia kutokana na
roho za uovu na waliyakemea mapepo yaliyokuwa yakitenda kazi ndani ya mtu mmoja
mmoja. Matendo 13:8-11; 16:18; 19:12. Hayo yote yalitokea pasipo hata
kupata mafundisho yahusuyo na pasipo matumizi ya mtindo huu wa kisasa
ambao unaitwa “mapambano ya kimkakati”
Hebu niseme hapa kwamba inapaswa iwe wazi kwetu, kwamba sio
mahubiri yoyote na kila mahubiri huwa na ufanisi. Mtume Paulo
alikuwa makini katika kumhubiri Kristo, lakini yeye alijikabidhi mwenyewe kwa
ndugu zake pamoja na kwa kanisa, naye alikuwa tayari kurejea nyumbani kwake
katika mji wa Tarso, Matendo 9:26-31. Baadaye tunamkuta kama mmoja wa manabii
na walimu huko Antiokia, Matendo 13:1. Paulo hakuhubiri tu mahali popote pale
kulingana na mipango yake na ubunifu wake, bali akiwa na ushirika na Mungu na
akimtii Roho na kanisa, Paulo aliitwa na Mungu kuihubiri Injili, Matendo 13:1, na
alielekezwa na Roho maeneo ya kwenda na maeneo ya kutokwenda, Matendo 16:6 –
10. Hivyo mtume Paulo anasema katika Warumi 10:14 – 15. “…basi wamwaminije yeye
wasiyemsikia? Tena wamsikiaje pasipo mhubiri? Tena wahubirije wasipopelekwa?”
Mtume Paulo pamoja na wenzake walikuwa makini sana kuhusiana na wito huu wa kimungu
– 1 Kor. 9:16,17 na alikuwa makini zaidi pia kuwa angeweza kufanya kazi vizuri
tu kulingana na wito wake, 2 Kor. 10:13-18.
Ikiwa tutaenda mbali na wito wa Kimungu na karama; ikiwa
tutaenda mbali na muda wa Kimungu katika maisha yetu; ikiwa tutaenda mbali na
Neno la Mungu – basi tusitegemee kupata matunda ambayo Mungu anayategemea
kutoka kwetu. Tunapaswa kuwa watumishi wa Mungu, hii ina maana kwamba
tunatakiwa kufanya yale tu anayoyasema na kujikabidhi kwenye maelekezo yake na
muda wake katika maisha yetu. Hatutakiwi pia kwenda mbali zaidi ya karama na
wito wetu. Hii inaweza kuwa pengine ndiyo sababu wengine wanaenda pasipo
kupelekwa? Inaweza kuwa ndiyo sababu kwamba wanapata mafanikio kidogo au hawaoni
mafanikio kabisa kutokana na mahubiri yao. Juhudi ya jinsi hii ya wahubiri
wasio na subira wanatafuta sasa kutunga au kubuni mtindo fulani au mbinu ambazo
zitaifanya kazi yao iweze kufanya kazi vizuri na kuleta “mafanikio”! Inaweza
ikawa ndiyo sababu wanaenda mbali zaidi ya yale ambayo yanafundishwa na
Maandiko ili kwamba wapate haya? Ninafikiri kuwa mambo hayo pia yanachangia
katika jambo hili lote la UInjilisti wenye mafanikio pamoja na kushughulikia
“mbinu mpya”. Hii yote haimaanishi kuwa ikiwa tumetumwa na Mungu, basi siku
zote tutaona ‘matokeo makubwa’, bali ikiwa tuna shauku ya kumtumikia Mungu na
kumzalia matunda na kiukweli kupeleka Neno lake kwa watu, basi tutaenenda kwa
kufuata Neno lake na Roho wake.
Kama tusomavyo Injili na Matendo ya Mitume, tunaona kwamba
watu wa Mungu walihubiri na kushuhudia juu ya kifo chake na ufufuo katika utii
wa amri zake na maongozi yake au kwa kadiri fursa zilipojitokeza. Ijapokuwa
walifahamu kuwa Kristo ameangamiza mamlaka na uwezo, haina maana yoyote, kama tusomavyo
katika habari zao, kwa watu wa Mungu kuchukua UInjilisti “katika mikono yao
wenyewe” na kujaribu kuifanya kazi ya Mungu kwa ajili yake. Mitume
hawakufanya mambo kwa kukisia pale walipokuwa wakilitumia neno la Bwana au
walipotumia uwezo na mamlaka ambazo aliwapatia. Walimtii Mungu na Mungu
aliwarejesha wengi kwake na akadhihirisha nguvu zake kuu. Na Mungu aliupata
utukufu! Hayo yote yalitendeka pasipo hata kuzitambua au kuzifunga roho
za kimaeneo! Hawakujaribu kuongezea chochote kile juu ya yale ambayo Mungu
alisema na kuyafanya ili kuufanya uInjilisti uwe wenye mafanikio zaidi! Lakini
hawa walimu wa kisasa pamoja na wahubiri wanathubutu kuonyesha kwa mafundisho
yao, kwamba yale ambayo Kristo aliyafanya pale msalabani hayakutosha. Ndiyo,
wanatangaza kwamba Kristo alipata ushindi pale msalabani, lakini inaonekana
kana kwamba hakuzivunja mamlaka na enzi vya kutosha kwa ajili yao, kwa
sababu wahubiri hawa wanaamini kuwa roho chafu bado zina haki
kisheria kuwashikilia watu katika giza na kifungo na kuwa Injili haiwezi
kupenya katika eneo linalotawaliwa na roho hizo. Wanafundisha
kuwa mtu anahitajika kwanza kufanya “vita vya kiroho” ana kwa ana na mamlaka
hizo pamoja na nguvu hizo kwa maombi, hadi kuzishinda nguvu zake kupitia maombi
kwanza, kabla Mungu hajazirejesha roho za watu kwake! Mawazo ya aina hii kwa
hakika ni ya jamii ya kiushirika tu na yenye milki ya ulozi zaidi kuliko kuwa
na mawazo ya kimaandiko. Mtazamo huu juu ya aina hii ya roho ya kimaeneo pamoja
na uwezo wao pamoja na aina hii ya kuzingatia katika maombi dhidi ya roho ya
uovu, hayapatikani katika maandiko ya neno la Mungu. Mtazamo huu unaweza
kumtukuza ibilisi kwa namna itakayowanyima watu wa Mungu ufahamu wa kweli na
nguvu ya Kristo ndani ya watakatifu wake na kupitia kanisa lake. Inawafanya
watu wamfikirie shetani zaidi badala ya kuweka mawazo yao kwa Kristo, na kwa
jinsi hiyo wanampatia shetani uwezo zaidi na utukufu na kuwanyang’anya
watakatifu ile imani yao ya kweli katika Mungu. Maandiko yanasema kwamba,
“Ijapokuwa hatujayaona mambo yote yakitiishwa chini ya nyayo zake, lakini
tunamwona Kristo.” Amina! Lakini sasa, badala yake walimu hawa wa kisasa
wanatutaka sisi tuyaone mapepo! Ni mafundisho madhaifu na manyonge kama vile
yenyewe yalivyo si ya kibiblia. Na hao walioyahamasisha mafundisho hayo ndio
huwa wa kwanza kukubali katika vitabu vyao kwamba watu wameharibiwa walipokuwa
wanajaribu kutumia mbinu hizo. Mafundisho hayo ni kashfa dhidi ya mamlaka ya
Mungu na shambulizi dhidi ya ushindi kamili wa Kristo alioupata pale Kalvari,
ambao ndio unaomruhusu kulijenga kanisa lake kulingana uradhi wa mapenzi yake
mwenyewe. Katika uweza ambao Mungu aliutumia katika kumfufua Kristo kutoka
katika wafu. (Efe 1: 19-23)!
Ndiyo tunatambua kile kinachofundishwa na maandiko, kwamba
mfalme wa uweza wa anga ni ile roho itendayo kazi sasa katika wana wa uasi; Efe
2:2. Shetani huzungukazunguka kama simba angurumaye akiwafunga wengi kuyatenda
mapenzi yake na hafanyi lolote isipokuwa ni kuua, kunyang’anya na kuharibu.
Yeye hudanganya na kuwafunga wengi katika vifungo. Mambo hayo pamoja na
mengineyo yanafundishwa ndani ya maandiko, na wala hiyo sio hoja yetu tena
hapa. Nami sisemi hapa kwamba hatuwezi kuomba kwa Mungu, kuhusiana na mambo ya
aina hii; wakati ambapo tunajua hali na watu ambao wanahitaji neema ya Mungu,
rehema pamoja na wokovu wake. Lakini linapokuja jambo la uenezi wa Injili na
jinsi inavyoenezwa na kubadilisha maisha ya watu, ndipo tunaweza kusema kuwa
mafundisho hayo ya kisasa yameenda nje ya maandiko, na yametumbukia
katika kasoro na udanganyifu – yanawafanya watu wawe shabaha ya roho za
udanganyifu. Wanakubali kuwa Kristo amepata ushindi pale kalvari dhidi ya
shetani, lakini bado wanaamini kwamba wanatakiwa pia wapate ushindi zaidi
juu ya roho zinazotawala ju ya maeneo yote yanayokaliwa na watu.
Ni nini kinaipatia roho hizo za kimaeneo haki ya kisheria
kukamata mamlaka za aina hii juu ya watu, kiasi kwamba hata iifanye Injili
isiwe yenye mafanikio katikati yao? Haya ati wanasema ni zile dhambi zilizopita
za jumuia hiyo au mkoa na ile laana iliyowekwa juu yake kwa sababu ya dhambi
hizo! Napenda niwaambie ukweli, wanachokifanya hawa walimu wa kisasa ni
kuzijaza akili za watu wa Mungu mambo yasiyo ya kiInjili yenye ushirikina mtupu
na yenye kasoro nyingi. Kristo amezichukua dhambi za ulimwengu mzima na
amelipia gharama kubwa isiyohesabika ili kufanya hayo. Kristo ni mwenye
mamlaka zote za juu – ni Mkuu. Shetani anaweza tu akaenda pale ambapo Mungu
amemruhusu kwenda. Sawa, maandiko yanakiri kuwa ipo haja ya maombi, kuhubiri,
uInjilisti, kazi pamoja na ukombozi wa mtu mmoja mmoja kutokana na mapepo;
lakini kadiri ya haja ya kuihubiri Injili inavyohusika, bado maandiko hayakiri
kwamba kuna haja ya toleo lingine zaidi ya lile alilolinunua tayari Kristo pale
msalabani kwa ajili ya ulimwengu wala maandiko hayakiri kwamba “dhambi zile
za kihistoria” zilizopita za maeneo ndizo zinaipatia roho za kimaeneo haki ya
kisheria kuzuia Injili; wala pia maandiko hayakiri kuwa ipo haja ya
watakatifu kujiingiza moja kwa moja katika makubaliano ya kiroho na hizo roho
za kimaeneo kana kwamba roho hizo zinahitajika kufungwa kabla ya Injili
kufanyika na kuenezwa kwa mafanikio yanayopaswa ( tafadhali angalia makala
yangu ya kwanza ambamo jambo hili limeelezwa kwa undani zaidi ).
Wakati mtume Paulo alipokuwa Athene, hawakupatikana watu
wengi waliomgeukia Mungu lakini pamoja na hali hiyo, si Paulo mwenyewe wala
si maandiko ya Neno la Mungu yanapohesabu hali hiyo ya watu kutoipokea Injili
kuwa ilisababishwa na nguvu kuu na mamlaka au haki ya roho za uovu kupinga
Injili au kazi ya Mungu. Mtume Paulo hakuianza kuzishughulikia roho za
kimaeneo katika maombi kwa sababu ya kuonyesha “upungufu wa mafanikio” katika
huduma yake. Mtume Paulo alikuwa na ufahamu mkubwa zaidi na mafunuo kuliko
hawa walimu wa kisasa, lakini yeye hakukimbilia kwenye “mbinu za kiwango cha
kimkakati” ili kuzishinda “roho ya kuabudu sanamu” ambazo zilidhaniwa
“kutawala” katika mji wa Athene, katika jitihada yake ya kuushinda upungufu huu
wa mwitikio katikati ya watu. Unaona, hawa walimu wa kisasa wao wanasema
kwamba, watu kwa kweli hawapo huru kuitikia Injili hadi hapo tutakapokuwa
tumezifunga roho za kimaeneo! Mmoja wa waandishi, kwa kweli anapendekeza kuwa
roho za kimaeneo zinazotawala kule Athene, zilikuwa zenye uwezo mkubwa kiasi
kwamba zilimfanya mtume Paulo kuzishindwa na eti hiyo ndiyo sababu alipata
mafanikio kidogo sana huko! Lakini sio Paulo wala maandiko ya neno la Mungu
yanayohitimisha jambo hilo kuhusu aina hii ya “upungufu wa mafanikio”. Badala
yake, mtume Paulo yeye anaendelea mbele na safari yake kwa mapenzi yake Mungu
na mpaka anapoingia katika mji wa Korintho, hatuoni popote pale panapomuonyesha
akijishughulisha na kazi ya kuzifunga roho za kimaeneo, na bado watu wengi sana
walimgeukia Bwana. Maandiko hayaelezei sababu hasa inayofanya watu wengi zaidi
wamgeukie Bwana katika eneo moja kuliko jingine, lakini yanatupa vidokezo na
kutuelekeza kwenye kanuni fulani fulani, ambazo tutaziangalia hivi punde.
Lakini jambo moja lenye uwazi ni kwamba maandiko hawayahesabii
“mafaniko” au “kupungua kwa mafanikio” kwamba imetokana na mtu mmoja ambaye
ameweza kuzishinda roho za kimaeneo zinazotawala au la.
Ninadhani kuwa kama hawa walimu wa kisasa wangekuwepo kule
nyakati zile za Paulo alipotembelea Athene, wangeweza kushauri kuwa Paulo aweze
kuhudhuria masomo katika moja ya seminari ya Kithiolojia ili aweze kujifunza
kwanza “kanuni za kukua kwa kanisa”. Pengine wangeweza kumwelezea pia kuwa
mtindo wake anaoutumia katika UInjilisti bila shaka “haufanyi kazi” vizuri na
hivyo anapaswa kuzisomea “mbinu mpya za mafanikio” ya uenezaji wa Injili,
ambazo ndizo zimethibitishwa kuleta mafanikio! Wangeweza kumwambia kuwa yote
aliyoyafanya amekosea kwa sababu tatizo halikuwa ni Wathene binafsi isipokuwa
ni ile roho ya kieneo ya kuabudu sanamu ndiyo iliyokuwa inawazuia watu kule
wasiweze kuiitikia Injili. Mtume Paulo angelazimika kufundishwa vita vya kiroho
iwapo angependa kuona mafanikio katika kuieneza Injili! Angepaswa kujifunza
kuhusu kutambua majina ya roho chafu za kimaeneo na namna ya kuzikabili katika
kuzifunga kwa maombi! Asingetazamia kupata mafanikio hadi kwanza afahamu jinsi
ya kuyafanya mambo haya! Lakini sasa hebu fikiria jinsi Paulo alivyoweza
kuwashughulikia walimu wa uongo walionyemelea makanisa ya Galatia; sifikirii kwamba
angeweza kuvutiwa kwa vyovyote vile, badala yake angeweza kuwakemea kwa nguvu
kwa ajili ya kuichafua Injili ya Kristo.
Hii ndiyo sababu inayonifanya niseme kwamba, mafundisho hayo
wanayotuletea ni kashfa dhidi ya mamlaka na busara za Mungu, ambaye huwaita na
kuwatuma watu kwenda kuhubiri Injili kulingana na amri na mafundisho ambayo
ameyaweka kwa ajili yetu. Hawa waandishi wa kisasa wanaweka busara yake Mungu
na mamlaka za utawala wake katika maswali. Wangeweza kuiita huduma ya Paulo kwa
ajili ya watu wa Athene ni jambo “lililoshindwa”. Wako makini kutafuta
mafanikio kiasi kwamba wanadiriki kuisukumilia mbali amri ya Kristo – ya kwenda
ulimwenguni kote kuihubiri Injili – sasa kinyume chake wao wanazunguka
huku na huko wakianzisha amri zao wenyewe, na hivyo wanajiweka kinyume na
busara za mamlaka ya Mungu na utawala wake juu ya mambo haya.
Hata kama Mungu alibariki au kama aliwaruhusu waweze
kujaribiwa, hata kama kulikuwa na mwitikio mkubwa wa watu au kidogo – bado
mitume wa mwanzoni kabisa, wao pamoja na kanisa waliendelea kumwangalia Mungu;
wakijikabidhi kwake, wakimwamini yeye na kumtukuza yeye! Hivyo ndivyo
walivyofanya! Na kama hapakuwepo na mwitikio sana, hawakumtilia shaka Mungu na
kuanza kukimbia huko na kuko kujifunza na kubuni “kanuni mpya za ukuaji wa
kanisa”! Wao walikuwa wakiomba na wakihubiri na walikuwa imara katika imani na
upendo; kama vile tusomavyo katika kitabu cha Matendo ya Mitume, lakini wao pia
hawakujishughulisha katika aina ya maombi yanayohusika na kuzishambulia roho za
kimaeneo kama ambavyo inavyohamasishwa na waandishi hawa wapya.
Ijapokuwa wanakiri juu ya ushindi wa Kristo pale Kalvari,
lakini mafundisho yao hayo yanaufanya wokovu wa roho za watu uonekane kuwa
unategemea matokeo ya aina fulani ya mapambano ya ana kwa ana kati ya majeshi
ya kiroho ikiwepo roho chafu kwa upande mmoja, ikipambana na karama za Roho na
maombezi ya Wakristo kwa upande mwingine; vita hiyo inayoelezwa humo ni ubunifu
wa akili zao wenyewe tu ( ambayo wanaiazima kutoka kwenye milki za ulozi.
Vitabu vya ubunifu – kama vile kitabu cha Frank Perret ) na vinajaribu
kuongezea kitu kingine juu ya ushindi ambao Kristo aliupata pale Kalvari
(msalabani). Katika maandishi yao, wakati mwingine inatolewa mfano wa nguvu za
upinzani zilizo sawa sawa zikipigana dhidi ya roho. Wanaonyesha kuwa iwapo
hutazishinda roho za kimaeneo zilizo za kienyeji na za kimaeneo zinazomiliki
eneo fulani, basi kazi ya Injili na wokovu wa nafsi haiwezi kufanikiwa
ipasavyo. Katika kutimiza hamu yao ya kupata “mitindo ya mafanikio”, wahubiri
hawa pamoja na waandishi wao hawajikabidhi katika Neno la Mungu na maelekezo
yake ambayo Yesu ameyakamilisha pale msalabani – wanafanya hayo yote kwa ajili
tu ya kutafuta matokeo. Nasema tena kwamba mawazo hayo ni ya kuanzishwa toka
duniani, hayamtukuzi Mungu, badala yake yanatukuza mafundisho yasiyothibitishwa
ambayo husababisha machafuko na kukata tamaa, na zaidi ya yote yanamtukuza
shetani.
Mafundisho yasiyothibitishwa ambayo husababisha
kuchanganyikiwa na kukata tamaa.
Lakini hebu niseme hapa kuwa shauri lao halijathibitishwa!
Bila shaka haionyeshi kwamba wanaweza kwa kweli kuonyesha kuwa jamii
imebadilishwa kutokana na mafundisho hayo yao. Zaidi ya hayo yote, wengi wa
mashabiki wa mafundisho hayo wanaishi Marekani (USA). Je huko kwao yameleta
mabadiliko gani? Mchungaji mmoja wa kanisa moja kubwa kule New York aliwahi
kuandika kitabu kuhusu kazi za kanisa lake na jinsi Mungu alivyopambana na
mafundisho haya ya kisasa – na jinsi hata yeye alivyoumizwa katika moyo wake
kuona jinsi ambavyo dhana hii isiyo ya kibiblia inavyoweza kushikilia akili za
watu wa Mungu na inaendelezwa kufundishwa nchi nzima. Lakini analiweka swali
lile lile na linalofanana – kuelezea ni kwa nini basi, iwapo mafundisho hayo ni
ya ukweli, mbona hayabadilishi miji ya Amerika – tunaambiwa na watu wengine
kuwa California ya kusini ni mji unaowakilisha kituo cha vivutio vya matamanio
katika ulimwengu. Yako wapi basi mabadiliko hayo makubwa katika miji ya
Marekani iwapo mafundisho hayo ni ya ukweli? Lakini mtu mwingine anaweza
kuuliza hivyo hivyo kuhusu miji mingine mingi pamoja na nchi. Mafundisho hayo
hayo yamekuwa yakiendeshwa Uingereza karibu miaka 15 sasa kwa kadiri
ninavyofahamu, lakini sasa, yako wapi – basi mabadiliko hayo makubwa
yaliyoahidiwa na mafundisho hayo? Ninafikiri kuwa watu wengi wangekubali
kwamba, sio jamii tu yenye hali mbaya, isipokuwa kanisa leo limo katika hali
mbaya zaidi; kwa kusema kwa ujumla, liko katika hali mbaya kuliko ilivyokuwa
miaka 20 iliyopita. Tendo mojawapo lililosababisha machafuko, matengano,
maumivu ya mioyo, kuchanika kwa makanisa, kadhalika na kugawanyika kwa
makanisa, je huko ndiko kuzaa kwa wingi kwa imani hiyo mpya!
Mashabiki wa mafundisho hayo wametengeneza mkanda wa video,
ili kuwashawishi watu waone namna ambavyo vita hivyo vya kiroho vinavyoleta mafanikio.
Baadhi ya watu wengine ambao wamechunguza yale yanayodaiwa na mikanda hiyo ya
video, kwa kuzuru hadi kwenye maeneo hayo waliyo chukulia mkanda huo pamoja na
kupata habari sahihi za maeneo hayo, wanatuambia kuwa mambo mengi, yaliyodaiwa
ndani ya mikanda hiyo yametiwa chumvi – na mara nyingi ni habari za uongo. Wale
wanaoamini katika imani au mafundisho hayo, kwa uasili wa kutosha wanaamini
kwamba “inafanya kazi” na wanajaribu kuonyesha watu kuwa ni kutokana na mtindo
wao mpya wa kuomba dhidi ya roho za kimaeneo, ndiyo iliyoleta mafanikio makuu
pale Injili ilipobanwa katika jumuiya fulani fulani. Lakini hatuoni kuungwa
mkono na maandiko ya Neno la Mungu katika maeneo hayo; na wala haiwezi
ikaonyeshwa kuwa hilo limekuwa ndiyo “ufunguo” au “jawabu” la ufanisi wa
uInjilisti kwa namna ya kimatendo, mbali ya malalamiko ya hadithi zao.
Kwa kweli kitabu kimeandikwa ambacho nimekitaja hapo punde
tu, kwa usahihi kabisa ni kwa sababu kumekuwepo na machafuko pamoja na maumivu
ya moyo yaliyosababishwa na mafundisho hayo. Mwandishi wa kitabu hicho yeye
mwenyewe pia anaamini katika vita vya kiroho dhidi ya roho, lakini anatueleza
kuhusiana na kukata tamaa pamoja na hofu iliyowanyemelea wakristo waliokuwa na
matazamio ya hali ya juu ya mafanikio kutokana na mafundisho hayo. Lakini
hatimaye waligundua kuwa haikufanya kazi yoyote; ile kama walivyotarajia na
hata ikawasababishia majanga! Hali hiyo imewasababishia kujisikia ni watu
wawezao kunaswa na shida, hofu na machafuko! Ingawaje anajaribu kuonyesha kuwa
mambo yaliwaharibikia kwa sababu ya ongezeko na ujinga wa watu wenyewe wa
kutokujua kanuni za aina hii ya mapambano; mbali ya hayo yote kitabu hicho pia
kinakazia ukweli kwamba, upepo huu mpya wa imani sio huo ambao mashabiki wake
wamelalamikia kuwa ndio, na wala hautoi matokeo kwa namna ambayo hawa waandishi
wapya wangetupelekea sisi tuamini hivyo.
Katika kitabu chake cha “Roho za Kimaeneo”, (kurasa za 17,
18), Wagner anakiri kuwa katika hali nyingi mtindo huu hautoi matokeo
yanayokusudiwa. Anatoa sababu gani hapo? Haya, anatueleza kuwa shetani
“anapinga mwenendo wa mambo”. Je, hii ina maana kwamba huyo shetani ana uwezo
mkubwa kiasi kwamba watu hawawezi kuokolewa? Hapo haelezei kwa ufasaha. Lakini
anatuelezea kuhusu uwezo, na werevu alionao na kwamba shetani anawapinga
watakatifu, kupitia roho zenye kiwango cha ngazi tofauti; ili watu wasitambue
mapenzi ya Mungu ipasavyo! Na kwamba kwa kadiri kiwango cha roho za kimaeneo
kinavyozidi kuwa juu zaidi ndivyo nguvu zaidi zinahitajika ili kuzishinda! Hali
kadhalika anatuambia kuwa Wakristo wengi hawajajiimarisha ili kukabiliana na
aina hii ya roho za viwango vya juu. Kwa hivyo basi inaonyesha shetani anaweza
kuzuia watu kuyatambua mapenzi ya Mungu katika mapambano haya; na hata kama
watatambua aina ya roho zinazopaswa kushughulikiwa bado watu wengi hawana
msimamo wa kiroho ili kuyashinda. Jambo hili humpatia mtu utukufu na humpatia
pia uwezo mwingi shetani. Kwa hiyo hitimisho tunalolipata hapo ni kwamba wokovu
wa roho za watu unategemea aina fulani ya watu walio jaliwa kuwa na uwezo wa
kutambua mambo katika “ulimwengu wa kiroho”. Pasipo uwezo wa “kutambua” jina na
tabia ya roho za kimaeneo na pasipo uwezo wa kiroho wa mtu binafsi pamoja na
msimamo wa mtu binafsi kuyashinda hayo katika maombi – hakutakuwepo na ufanisi
wa UInjilisti! Hakika, kama utasadiki porojo hizo zisizo na msimamo wa
Kibiblia, basi wewe unaweza kuamini lolote lile! Ili kuonyesha jinsi
mafundisho haya yanavyokaribia kuingia kwenye ulozi, hebu uniruhusu ninukuu
yale anayoyasema mwishoni mwa ushauri wake hapo juu; anasema kuwa, “….
tunapogundua kuwa sisi ni muhimu katika kuzifunga (roho za kimaeneo) …..
tutafanya vema kutafiti uwezekano wa chanzo chake katika ulimwengu wa kiroho”.
Kutafuta chanzo, na sio katika maandiko, isipokuwa katika ulimwengu wa kiroho!
Je wanatutaka sisi tuwe waaguzi, wachawi au waangaliao mambo ya roho? Pasipo
kuelewa, hivyo ndivyo inavyotendeka katikati yao. Wao hawaenendi kiroho, haupo
utambuzi wa kiroho na kweli, hii sio maombi ya kiroho. Hivi sio vita vya kiroho
– huu ni udanganyifu. Wanafanya mawasiliano ya kiuharamu na yenye hatari na
ulimwengu wa maroho na hivyo hudanganyika (ninaposema ulimwengu wa kiroho
ninamaanisha kuwa wanafanya mawasiliano na maroho maovu, au kujiweka katika
hali inayoweza kuwashawishi na kudanganywa na maroho maovu). Tutaangalia zaidi
kidogo hilo hapo baadaye kidogo. Lakini sasa hapa tunaona kwamba ili kuweza
kusimulia kushindwa kwa mafundisho yao pamoja na maumivu ya moyo
yaliyosababisha – wanatafuta kiurahisi tu kubuni makosa zaidi.
Niruhusu nitaje hapa yale ambayo nimewahi kuyasema mahala
penginepo yaani, tunajua kwamba Bwana analijenga kanisa lake na anayaheshimu
mahubiri ya neno lake na hakika hujali anapoona watu wake hujinyenyekeza
wenyewe katika maombi na kuutafuta uso wake kwa mioyo yao yote. Inawezekana kuwa
Mungu anafanya kazi katikati ya watu ambao baadhi yao viongozi wao huamini
katika mafundisho haya na kuyashikilia, lakini kazi yake ya neema haiwezi
kuhalalisha mafundisho hayo yote ambayo yameshikiliwa na watu ambao wanaweza
wakawa ndio wanaoongoza kazi mahala fulani. Tunajua hivyo kutokana na historia,
pia tunaweza kuziona kanuni hizo sisi wenyewe ndani ya maandiko pia. Lakini
napenda niseme tena kuwa kule kuona Mungu akitembea katikati ya watu katika
uweza wa kuokoa, haihalalishi kila mafundisho yaliyoshikiliwa na hao wanaokuwa
katika uongozi wa sehemu fulani, na wapo mbali sana katika kuonyesha kuwa
mtindo wao huo mpya kwa kweli unafanya “kazi” au kwamba mtindo huo ndio
unaohusika katika kuwaleta watu wengi katika ufalme wa Mungu.
Katika mambo ya matukio ya kiroho ya nyuma na katika kujua
kwa nini mambo hutokea au kutotokea, mara nyingi maandiko hayatoi jibu la
maswali yetu au kufunua kila kitu. Na kutokana na hoja hiyo, Mungu anatuonya
katika Kumbukumbu la Torati 29:29 kwamba “mambo ya siri ni ya Bwana Mungu wetu,
lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele”. Hatutakiwi
kupenyeza tu katika mambo ambayo Mungu hajatufunulia kwa neno lake. Ni busara
zake Mungu, kwamba ameyaweka mambo fulani mbali na ufahamu wetu. Lakini
tunatakiwa kuyazingatia kikamilifu mambo ambayo ametufunulia tayari. Hayo
yatakuwa ni yenye kutuletea faida kwetu – katika kukuza ufahamu wa Mungu na
kuimarisha imani yetu. Lakini katika jitihada zao za kupata matokeo wakati wote
na katika sehemu zote, hawa wahubiri na walimu wa kisasa wanapenyeza kwenye
mambo yasiyoonekana – ambamo wanajigamba juu ya maono yao, mafunzo yao, na
uzoefu wao wa mambo ya juu – ambayo ni mazao ya akili zao za kimwili tu na wala
hayailetei jamii mabadiliko katika maisha yao. Kama tunavyoambiwa katika
Kolosai 2:18 na wala hawashikilii kichwa cha kanisa, Yesu Kristo. Ijapokuwa
Mtume Paulo anaongelea maalum kuhusu wale wanaotafuta kuwarejesha watakatifu
kwenye mila za kiyahudi, ile sura nzima Kolosai 2:6-19 inashauri sana juu yetu,
kuhusiana na mambo haya ya mafundisho mapya.
Ulinganifu wa kimaandiko – kanisa katika kuomba.
Nyakati za matendo ya mitume kanisa lilijiheshimu na kuomba
kwa jinsi ya tofauti kabisa ukilinganisha na hawa walimu wa kisasa
wanavyoamuru. Kulipotokea mateso kule Yerusalemu, kanisa halikukabiliana na
roho chafu katika maombi yao.
Kanisa halikukiri juu ya roho za kimaeneo kwamba ndizo
zinazowashikilia wanaume na wanawake hata wasiupokee ufalme wa Mungu. Wao
waliomba kwa Mungu na kukiri juu ya mamlaka zake na uungu wake. Kulikuwepo na
upinzani mkali wakati huo ( kuliko hata ilivyo sasa naweza kusema ) juu ya
kuihubiri Injili; naye ni nani anayeweza kupinga kwamba shetani anachochea
ugumu wa mioyo ya hao wasiotaka kuamini ili wapinge kazi ya Mungu? Lakini sasa
hebu sikiliza jinsi kanisa lilivyoomba katika Matendo 4: 24-30, kwanza
walitangaza busara kuu na uweza, wa Mungu juu ya yote mengine, wakipokea
maelekezo na hamasa kutoka katika maandiko ya neno la Mungu! Ndipo wakatangaza:
“. . . Basi sasa ee Bwana, yaangalie matisho yao, ukawajaalie
watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote, ukinyoosha mkono wako kuponya,
ishara na maajabu zikafanyike kwa jina la mtumishi wako mtakatifu Yesu”.
Hebu tazama hapo watumishi hao wametishwa, lakini maombi yao
yameelekezwa kwa Mungu, wala hawayaelekezi dhidi ya aina yoyote ile ya roho za
kimaeneo zinazotawala Yerusalemu, wanayohisia juu ya mamlaka za Mungu na za
ushindi wake juu ya mambo yanayowapata, na wanaomba sio kwa ajili ya
kukabililiana na roho za kimaeneo ili kwamba ziweze kufungwa, lakini wao
wanaomba ili kwamba waweze kulisema neno lake kwa ujasiri na kwamba Bwana aweze
kutenda kazi kwa nguvu katikati yao. Lakini hata hivyo wanakiri juu ya mamlaka
za utawala wa Mungu na ushindi wake kupitia Kristo. Hayo hayawaelekezi kufuata
mambo ya kuhisihisi – wao hawachukui kutoka kwa Mungu ule uweza wake mkuu na
kutafuta kumtumikia kwa ajili ya kutimiza matakwa yao na mipango yao kwa ajili
ya ukuaji wa kanisa. Isipokuwa wanabakia wakiwa wamejikabidhi kwa Mungu na
katika busara zake wakikiri kuwa wao ni watumishi wake tu. Hilo ndilo kanisa
ambalo linamwinua Yesu juu zaidi kuliko chochote kile. Na ijapokuwa wanadamu na
mapepo wanaweza kupanga, wao wanaendelea kubakia wakiwa wamekaza macho yao
kumwelekea Kristo- na kile alichokikamilisha kupitia kifo chake na ufufuo wake
– yote mawili katika fikara zao na maombi yao. Hawatafuti kuongezea chochote
kile juu ya ushindi kamili pale Kalvari, au kunyang’anya uwezo wake na maana
yake kwa kuhesabia uwezo huo juu ya “roho za kimaeneo” ambao hawanao! Maombi
yao yanakazia macho kwa Kristo na mamlaka zake na wanamtukuza yeye, sio shetani
au roho za kimaeneo.
( Kuhusiana na maombi na kanisa, vile vile na kuhubiri Injili
kama njia ya Mungu ya kuokoa hao waaminio, tafadhali soma sehemu ya pili ya
makala ya kwanza ya “Kutubu kwa ajili ya Dhambi za Taifa”)
Na ni kweli tunaona kwamba wanayo sababu nzuri inayowafanya
wafikiri na kuomba namna hiyo. Katika Wakolosai 2:15, tunasoma kuhusu kifo cha
Kristo pale Kalvari kwamba; “… akisha kuzivua enzi na mamlaka na kuzifanya kuwa
mkogo kwa ujasiri akazishangilia katika msalaba huo”. Na kwa hiyo Mungu alikuwa
na uwezo wa “kutukomboa kutokana na nguvu za giza na kutuingiza katika ufalme
wa mwana wake mpendwa”.
Na katika Waebrania 2:14 tunaambiwa kuwa, “Yesu Kristo
alishiriki damu na mwili vivyo hivyo;.ili kwamba kwa njia ya mauti amharibu
yeye aliyekuwa na nguvu za mauti yaani Ibilisi”.
Na mtume Yohana anakubaliana na hilo pale anaposema katika
Yoh 3:8 “… kwa kusudi hili mwana wa Mungu alidhihirishwa ili aziharibu kazi za
shetani”
Ukuu wa kimungu alilonao Kristo na mamlaka zake juu ya mambo
yote umetangazwa katika Wakolosai 1:16. ” kwa kuwa katika yeye vitu vyote
viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na
visivyoonekana, ikiwa ni vitu vya enzi au usultani au enzi au mamlaka, vitu
vyote viliumbwa kwa njia yake na kwa ajili yake.”
Haupo wito wowote kwa kanisa tena ili kuzidi kuharibu
“mamlaka na uweza” kwa kuzifunga na kukemea roho za kimaeneo kana kwamba
zenyewe zinayo haki ya kisheria juu ya nafsi. Yesu Kristo alizichukua dhambi za
ulimwengu mzima na kwa hiyo yeye ni mwokozi wa wanadamu wote (1Tim 4:10) hata
kama wanaamini na kupokea wakovu huo au hapana. Yeye amenunua msamaha na wokovu
kwa ajili ya wanadamu kwa damu yake mwenyewe na kwa hiyo imeandikwa kwamba, “Mungu
alikuwa ndani ya Kristo ……. asiwahesabie makosa yao…”. Kwa wale ambao
wangeweza kuamini Injili na wakapatanishwa na Mungu, Mungu asingeweza tena
kuyashikilia dhidi yao mambo yao maovu ya dhambi zilizopita (2 Kor 5:19)
isipokuwa yeye huwaachia na kuwasamehe bure – pasipo malipo yoyote. Wale ambao
wanaukataa na kuupinga wokovu wa bure wa Mungu na ambao wanaendelea
kuzishikilia dhambi zao, watahesabiwa kuwa wanapaswa kuhukumu.
Lakini sasa haya mafundisho yao ya kisasa
kwa kweli yanaifanya damu na dhabihu ya Bwana wetu Yesu Kristo pale msalabani
ionekane kuwa haina maana. Mafundisho hayo yanamkataa yeye aliye wa kweli na mwenye
mamlaka alizozinunua na kuzipata kama mwokozi wa wanadamu wote kupitia kumwagwa
kwa damu yake. Kristo amekwishachukua msamaha wa wale wote watakaoamini. Lakini
mafundisho haya ya kisasa yanatangua kazi ya msalaba kwa kuzihesabia roho za
kimaeneo haki ya kisheria katika kuwaweka watu nje ya ufalme wa Mungu, kwa
sababu ya kile wanachokiita wao kuwa ni “dhambi zisizoungamwa na kusamehewa za
eneo la kijografia katika mkoa au jumuia.” Wao wanafundisha kuwa roho za uovu
bado zina uwezo juu ya eneo lolote lile, ambalo mambo yaliyopita ya kijamii au
mengineyo ya uovu uliotendeka. Imani za aina hii zinashikiliwa na kizazi kipya
cha roho za wanadamu wa leo; na hapo ndipo imani ya aina hii inakotokea, kuliko
kutokea katika Biblia. Wanasema kuwa maovu yaliyopita yanahitajika yapate
“ondoleo” (toleo) lake, kwa wakristo kuungama na kuzitubia dhambi hizo, na
kutumia damu ya Yesu, kabla roho za kimaeneo hazijaweza kufungwa! Kwa hiyo
wanalundika kosa moja juu ya kosa jingine. Jambo hili limetazamwa ipasavyo
ndani ya makala yangu ya kwanza.
Ikiwa tutafuata mafundisho hayo yao, tutagundua kwamba kila
mtu katika ulimwengu huu sasa hawezi kusamehewa mara moja, wala kuokolewa na
kukombolewa kutokana na nguvu za shetani kwa sababu ya msalaba. Hapana; ni
kweli kwamba haiwi mara moja kwa haraka. Lakini Kristo akiwa amenunua wokovu
huu wa bure na mkamilifu kutokana na dhambi, kuhukumiwa na uwezo wa shetani. Biblia
inatangaza kwa nguvu sasa kuwa, “Injili ya Kristo ni uweza wa Mungu uletao
wokovu kwa kila aaminiye.” Rumi 1:16. Hivyo ndivyo maandiko yanavyofundisha;
na kwa sababu ya wokovu hutujia pasipo haja ya kuzitambua na kuzifunga hizo
zinazoitwa roho za kimaeneo – isipokuwa kama unataka kubatilisha matokeo ya
damu ya Yesu pamoja na ushindi wake dhidi ya mamlaka na uwezo.
Hata hivyo ili kuonyesha kuwa sitii chumvi ule umaana wa
jambo hili pale ninaposema kuwa mafundisho haya yanawakilisha mashambulizi juu
ya Injili ya Yesu, hebu tutazame kwa makini yale ambayo kiongozi maarufu wa
thiolojia hii mpya (George Ottis jr) anavyotangaza. Katika kutoa mhadhara wake
kwa kusanyiko la YWAM huko Tacoma, Washingtone mnamo mwaka 1981, yeye pamoja na
mambo mengine alisema kwamba:
“…Kristo hajatukomboa kwa kutupatia uzima wake kama fidia kwa
ajili ya dhambi zetu, ili kwamba apate kutuachilia. Ikiwa tutazikubali asili au
(chanzo) ambacho Kristo kikweli amenunua……wokovu wetu kwa damu yake …….. naye
alimlipa Baba. Hivyo mtindo huu kabla ya yote unamwonyesha Mungu ambaye ni Baba
kana kwamba yeye ni mwenye kulipiza mambo na ni mwenye kiu ya damu na kwa
ujumla asiye patana na msamaha utolewao na Biblia.”
“Msamaha……. ni kiburudisho cha madai ya haki…….itakuwa ni
vigumu kwa Mungu kuwa nayo kama mtunzi wa nyimbo anavyoiweka, “alilipa deni
langu na akanisamehe dhambi zangu zote”
“Manukato ya toleo la Kristo yaliendelea katika utii wake kwa
sheria za kimwili kwa niaba ya mwenye dhambi. Kristo katika maisha yake alitii
sheria za mwili kwa ajili yetu na hayo ndiyo kwa uhalisi ni manukato ya toleo.”
Ijapo kuwa mwandishi huyo haelezei kwa uwazi sana kutokana na
mpangilio huu, lakini bado hajayakana mawazo kama hayo, na wengine wanaamini
kwamba yale aliyo yaandika tangu hapo pia yamejaa mawazo yenye kukaririwa. (
Kuyatambua mambo ya hapo juu, pamoja na taarifa nyinginezo juu ya mwandishi
huyo aitwaye Ottis na mafundisho yake, hali kadhalika na mkanda wa video
nilioutaja hapa kwenye makala hii angalia http://www.Bibleguide.com.
Makala inayoitwa “George Ottis na mafundisho yake ya udanganyifu
yaliyotayarishwa na Profesa J.S Malan – yote katika lugha ya Kiingereza.)
Shirika lile ambalo linaongozwa na Ottis ndilo lililo husika na utayarishaji wa
mkanda huo wa uongo wa video. Kwa sasa wameutayarisha mkanda wa pili wa video –
ambao niliutaja mwanzoni – ambao unakusudia kuonyesha kwamba jumuia fulani
fulani zimebadilishwa kupitia mafundisho haya ya roho za kimaeneo. Ottis pia
anaheshimika kama mwanzilishi wa mawazo ya “ramani ya kiroho” ambayo nayo
tutalitazama tutakapokuwa tukifikiria Ezekiel sura ya 4. Kama nilivyokwisha
kusema, msingi wa kweli kuhusiana na maisha ya dhambi ya mwanadamu na hitaji
lake la toba, pamoja na tabia na kusudi la kifo cha Yesu pale msalabani –
inaonekana ilikuwa ni jambo lenye kutia giza (lisilo eleweka) kama si kupingwa
kwa moja kwa moja na mafundisho haya ya kisasa! Ninatumaini kwamba unaweza
ukajionea mwenyewe kutokana na maelezo ya hapo juu, kuwa hayawakilishi mambo
mawili yote kwa pamoja, yaani ni mashambulizi juu yake na kuukana wokovu ambao
Kristo amenunua kwa mapenzi ya damu yake. Ni kuyakana maisha ya dhambi ya
mwanadamu ambayo ndiyo yanayomtenganisha na Mungu na pia ni kukana hitaji na
tabia juu ya wokovu wetu wa ajabu kutokana na dhambi pamoja na milki yake.
Ni Injili Nyingine!
Hili sasa linatupeleka kwenye msingi wa pili wa makosa ya
mafundisho haya, ambayo pengine ni ya hatari zaidi kuliko jambo lingine lolote
lile kwa namna inavyodhalilisha na kushambulia moyo halisi wa Injili.
Mafundisho hayo yanaonyesha kiini cha matatizo kisiwe ni dhambi, ugumu na
kutokuamini kwa moyo wangu, bali uonekane kwamba ni majeshi ya uovu ya kiroho
ndiyo yanayonizuia mimi kushindwa kumkubali Mungu. Wanasema kwa ujumla sio
mimi mwenyewe wala sio hali ya moyo wangu ambayo ndiyo tatizo, isipokuwa ni
roho chafu ndizo zinazonizuia nisimjue Mungu na kufungika katika giza.
Chini ya mafundisho hayo, wenye dhambi sasa wamekuwa ni (wajinga) nao wamewekwa
kuwa ni shabaha ya roho za uovu na kwamba inaelezwa kuwa, sio hali ya mioyo
yao ambayo ndiyo tatizo, isipokuwa ni hizo roho za kimaeneo ambazo ndizo
zinazowazuia wenye dhambi kushindwa kuitikia! Wazidi kudai kuwa kwa sasa
haiwi tena ni dhambi za mtu binafsi kuwa ndiyo tatizo, isipokuwa sasa tatizo ni
dhambi za jumuia, au miji, ambazo ndizo zinazohusika na roho hizi za kitaifa! Kwa
sababu wao huyaamini mambo hayo, pia kuyafundisha kuwa njia kuu ya kuleta
wokovu kwa watu sio kuihubiri Injili, isipokuwa ni kwanza kuzifunga roho za
kimaeneo! Mahubiri ya Injili yanachukua nafasi ya pili na bado yanaweza tu
kufanya kazi kwa ufanisi zaidi pale tu ambapo roho za uovu zitakuwa zimefungwa
kwanza! Kwa hakika mafundisho ya jinsi hii yanawakilisha Injili nyingine –
ni mashambulio kwenye ile sababu ya kimsingi na halisi juu ya kwa nini Yesu
alikufa msalabani! Ni kukana mafundisho ya Yesu mwenyewe kuhusiana na mtu,
kuhusiana na dhambi, kuhusiana na shetani, na kuhusiana na hukumu.
Mwandishi mmoja anatuambia kuhusu kiongozi mmoja maarufu wa
kanisa huko Amerika ya kusini ambaye kwa kawaida huomba yeye mwenyewe kwa muda
wa wiki moja kabla hajaanza kampeni zake. Anafanya hivyo ili aweze kuzitambua
na kuzifunga mamlaka ya nguvu za giza juu ya mji huo ambao amekuja kuuhudumu.
Mpaka “anapojisikia” kuwa amelipata lengo lake, ndipo anapoanza kuhutubia
katika mikutano ya hadhara akiwaelezea watu kuwa “sasa” wako huru kumjia
Kristo! Watu hawa wanajiinua wenyewe pamoja na mafundisho yao, wanajiinua juu
zaidi ya Kristo pamoja na mitume ambao hawakuwahi kufanya madai ya jinsi hiyo
kwa watu waliowajia. Kristo pamoja na mitume walikuja wakihubiri habari njema
na wakiwasihi waume kwa wanawake watubu! Kwa maneno mengine, watu hao
wanafundisha kuwa tatizo halisi sio ugumu wa moyo wangu mwenyewe wala sio
dhambi, isipokuwa ni hizi roho za kimaeneo ambazo zinatakiwa kutambuliwa na
kufungwa! Sio kupinga kwa moyo wangu kuwa ndilo tatizo, isipokuwa kupinga kuwa
roho za kimaeneo ndicho kinachoniweka nje ya ufalme wa Mungu. Wanataka tuelewe
kuwa ni roho za kimaeneo sasa ndizo zenye kuhusika na kiburi, tamaa mbaya na
ugumu wa moyo wangu – kadhalika na kutokuamini kwangu?- na sio mimi mwenyewe.
Mara tu mtu akizifunga roho za kimaeneo katika jamii basi, wenye dhambi
wanakuwa wamewekwa “huru” kumjua Kristo! Mwinjilisti mwingine hawezi kuhubiri
katika mji mpaka pale watakapojisikia kuwa wamezishinda katika maombi hizi roho
za kimaeneo ambazo zinaushikilia mji huo kwa nguvu zao, na mmoja wa viongozi
maarufu wa kanisa ambaye amehamasisha makosa hayo anatangaza kuwa: “ninafahamu
vizuri pasipo shaka yoyote ndani yake, kuwa mahubiri makubwa hayawezi
kuzisababisha roho za watu kuokoka na kanisa kukua … Hapana, isipokuwa ni pale
utakapozishusha chini ( kuziangusha ) nguvu za giza zililzokuwa zinawazuia watu
kumwishia Mungu katika maisha yao; hiyo ndiyo itakayosababisha kanisa kukua“.
(Makala ya Larry Lea katika kitabu cha “Roho za Kimaeneo.” – Territorial
Spirits” – Kilichoandikwa na Wagner, ukurasa wa 91 kilichokubaliwa na “Karisma
na Maisha ya Kikristo” ã 1989, Strang Communication Company.)
Je watu hawa hawadhihaki kwa kumpinga Kristo mwenyewe?
Mwandishi wa hapo juu anasema kuwa ana uhakika mkamilifu kwamba – hata mahubiri
makubwa, hayawezi kuokoa roho za watu au kulijenga kanisa! Lakini tazama mwana
wa Mungu aliwaambia wanafunzi wake, “Nendeni katika ulimwenguni kote,
mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Yeye aaminiye na kubatizwa ataokoka”. Mk 16:
15,16. Mtume Paulo naye anaurudia usemi huo huo, “siionei haya Injili ya Kristo
kwa sababu ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye.” Rumi 1:16. Pia
katika 1Kor.1:17,18,21 kwa kuwa Kristo hakunituma ili kubatiza isipokuwa
kuihubiri Injili … kwa sababu neno la msalaba …. ni nguvu ya Mungu iletayo
wokovu …. Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuzi wa lile neno
linalohubiriwa”. Maandiko mengineyo mengi yangeweza kunukuliwa ili kuthibitisha
tangazo lake Mungu litolewalo kwa ajili ya wokovu wa hao waliopotea na
kulijenga kanisa lake, lakini sasa hawa waandishi wa kisasa wanapinga moja kwa
moja ukweli huu kwa hiyo imani yao. Kristo hakuwaagiza wanafunzi wake,
“kwenda kuzitambua na kuzifunga roho za kimaeneo ambazo zinawazuia watu
washindwe kuokoka!”
Ijapokuwa waandishi hawa wanaamini kuwa
kuhubiri Injili ni njia ya kuokoa roho za watu, bado wao huanza kwa kuzifunga
roho za kimaeneo kana kwamba hilo ndiyo tendo la mwanzo na lenye msingi katika
kanisa.
Na kule kuihubiri Injili sasa hushika nafasi ya pili katika mipango yao – na
bado Injili hiyo inategemea kikamilifu mtindo huo wao wa kuomba dhidi ya roho
za kimaeneo. Hili ni tatizo kubwa la kasoro na ni sawa na kusema kuwa, “Sawa,
ni kupitia Yesu kristo mtu anaweza kuokolewa, lakini unahitaji kutahiriwa
kwanza”. Ukumbuke kuwa katika makanisa ya Galatia waliamini mambo mengi yaliyo
mazuri na yenye haki kuhusu Kristo, na msamaha pamoja na wokovu ambao tunapata
kwa yeye. Lakini wao waliongezea mafundisho yasiyo ya kiinjili, ambayo
yalidhalilisha na kutishia uwepo wa imani yote! Mtume Paulo amesema “wamelogwa”
kwa mafundisho ya aina hiyo. Na ijapokuwa wahubiri hawa wa kisasa ambao
wanafundisha mapambano dhidi ya roho za kimaeneo, wanaweza pia wakaamini mambo
mema na yenye haki vile vile, bila kujali kiasi gani wamejiingiza katika
kujishughulisha na kazi “halisi” ya Mungu, hawajali kuwa mafundisho hayo
yahusuyo roho za kimaeneo ni uchawi wenye hila ndani yake! Inayodhalilisha
imani ya Injili.
Mafundisho haya hayaji kutoka kwa Yesu
wala kutoka kwa mitume, au tusemeje sasa? Je Yesu alishindwa kuzitambua na
kuzifunga roho zilizokuwa zinatawala Kapenaumu? Korazin na Bethsaida? Huko kulikuwa na mwitikio mdogo sana kufuatia
mafundisho yake ijapokuwa amefanya kazi kwa nguvu kwao. Mat 11:20-24. Je
tunaweza kulaumu upungufu wa mwitikio wa watu hawa katika miji hiyo kuwa
unatokana na roho za kimaeneo, au kutokana na kushindwa kuyatambua majina ya
roho hizo za kimaeneo? Au je, roho hizo za kimaeneo zilikuwa na mamlaka ya
“kuzuia” huduma ya Yesu kwa sababu alikuwa bado hajafa pale msalabani
(Kalvari)? Hapana! Hakuna lolote kati ya mawazo hayo ambalo lina ukweli wowote.
Yesu alisema kwamba, ikiwa kazi alizozifanya katika miji hiyo zingefanyika huko
Tarso na Sidon, wangekwisha kutubu siku nyingi iliyopita na hata Sodoma
ingesalia hadi leo. Yesu anawakaripia watu wa miji hiyo ya Israel kwa sababu
ya kukataa kwao kutubu. Anawakaripia kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao.
Kulingana na yote aliyoyasema na kuyafanya bado hawakuweza kuzioacha dhambi
zao. Walikataa kumwamini na kumruhusu Yesu ayabadili maisha yao. Hiyo
ilikuwa ni ugumu wa mioyo yao wenyewe na kutokuamini ndiyo iliyosababisha
upungufu wa mwitikio, na ilikuwa ni kutokana na hilo ndio maana Yesu alitangaza
hukumu kali juu yao. Walipaswa kujilaumu wao wenyewe na sio shetani wala sio
roho za kimaeneo! Ikiwa tutafuata maelezo basi haya ndiyo mafundisho halisi
ya maandiko ya neno la Mungu. Katika matendo ya mitume hatumsomi mtume Paulo
akijifungia ndani mwenyewe kwa siku nyingi ili kujishughulisha na mapambano ya
moja kwa moja na roho chafu, kabla hajahubiri katika mji – kana kwamba hiyo
ilikuwa mbinu ya lazima! Hapana. Tunajua kuwa yeye alikuwa ni mtu wa maombi,
lakini alipowasili katika miji na jiji, kwa kawaida anasema habari zake kwamba
alikuwa akienda moja kwa moja kwenye masinagogi, au sehemu za masoko kumhubiri
Yesu Kristo kwa watu. Na pale wayahudi walipoupinga ukweli wa Injili, Mtume
Paulo analaumu juu ya mioyo yao. Mtd 13: 45,46.
Mtume Paulo alipokuwa huko Athene na alipoona mji
mzima umekabidhiwa kwa masanamu kwa mara nyingine yeye hakujiingiza katika
“ulimwengu wa kiroho” ili kuzifunga roho za ibada za masanamu. Hapana, bali
yeye alienda katika masinagogi na sehemu za sokoni kumhubiri Kristo na ufufuo!
Mtd 17:16-19. Sio wengi waliookolewa kule Athene. Na baada ya kuondoka hapo
alielekea kwenye mji wa Korintho. Baadaye alipokuwa akiwaandikia Wakorintho,
aliwaambia kuwa, alifika kwao baada ya kuondoka kule Athene akidhamiria asikijue
kitu kingine chochote isipokuwa “Yesu Kristo aliyerubiwa”, 1Kor.2:2. Pengine
kudhamiria huku kwake kuliweza kuimarishwa ndani yake alipoona uhafifu wa
busara ya kibinadamu ambayo iliwashika watu wengi wa Athene, ambayo ndiyo
iliyowafanya washindwe kuupokea ukweli wa Mungu. Hata kama hiyo ni kweli au
hapana, Paulo mwenyewe analifafanua kwa ajili yetu, kwa nini iko hivyo kwamba
watu hawapokei kweli ya injili.
“Kwa kuwa Wayahudi wanahitaji kuona ishara, Wayunani
wanatafuta hekima, lakini tunamhubiri Kristo aliye sulubiwa, ambaye kwa
wayahudi ni kikwazo na kwa Wayunani ni upuuzi.”
Anaendelea kueleza kuwa sio watu wengi wenye hekima na wenye
nguvu walioitwa; 1Kor.1:22-29. Anafafanua hivyo kwa makini kuwa ni hekima za
kibinadamu au tungeweza kusema ni kiburi ndicho kinachowazuia watu kuupokea
ukweli wa Mungu – na sio roho za kimaeneo! Inashangaza kuona Biblia yenyewe
inavyofafanua vizuri mambo yake. Wayahudi wanatafuta kuona aina fulani za
ishara au miujiza na Wayunani wanatukuza hekima zao wenyewe – watu wenye
vitabia vya jinsi hiyo hawako tayari kulipokea neno la Mungu kwa moyo wa
unyenyekevu bali hujiinua wao wenyewe kinyume na kweli ya Mungu.
Katika mwangaza wa ukweli huu, sasa tunaweza kuona ni kwa
nini watu wengi hawakuweza kuitikia kule Athene. Katika ule mstari wa 18 mtume
Paulo anatangaza, “kwa kuwa mahubiri ya msalaba kwa wao waangamiao ni upumbavu
bali kwetu sisi tuokolewao ni uweza wa Mungu.” Katika ile 2Kor 4:3,4 anapanua
wazo hili kidogo; anasema Injili imefichwa kwao waliopotea, na anaendelea kuelezea
“ambamo ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikra zao wasioamini isiwazukie
nuru ya Injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.”
Katika sura hiyo anasimulia kwamba shetani anao uwanja wa
matendo yake maovu kwa sababu ya kutokuamini au ugumu wa mioyo ya watu; ni
ule ugumu wa mioyo ya watu wenyewe ambayo humpatia shetani fursa ya
kuwadanganya na kuwafanya wawe mateka wa dhambi. Hapa mtume Paulo anaelezea
hali ya kiroho ya hao wanaoipinga Injili; sura hii haiwakilishi mbinu kwa ajili
ya “vita za kiroho”. Mtume Paulo hatuambii hapa kwamba tunapaswa kumfunga mungu
wa ulimwengu huu kupitia maombi ya maombezi ili kwamba hao watu (wajinga?)
waweze “kuwekwa huru” ili waweze kuamini Injili. Ijapo kuwa katika kukubaliana
na hilo, maneno ya Yesu mwenyewe alipokuwa akiongelea kuhusu “saa yake” ambayo
inamaanisha kifo chake pale msalabani. Katika Yoh 12:31 anasema: “Sasa hukumu
ya ulimwengu huu ipo, sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje”
Ukweli huu unarudiwa tena pale Yesu anapoongea kuhusu kuja
kwa Roho Mtakatifu. Yesu anasema kwamba, Roho Mtakatifu atawahukumu wanadamu
kwa hukumu kwa sababu “…yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa”,
Yoh16:11. Bwana Yesu anaungana moja kwa moja na hukumu ya mfalme wa ulimwengu
huu ambayo alikuwa anaenda kuitimiza pale Kalvari, pamoja na hukumu ya
ulimwengu, ambayo ni hukumu ya ulimwengu huu ina maana kwamba ni ya watu
waishio ndani yake. Akizichukua dhambi za ulimwengu pale msalabani Yesu
angekinyang’anya kifo ule uwezo wake uliokuwa nao, (“uchungu wa mauti ni
dhambi” 1Kor.15:56; Tim.1:10). Na atambatilisha yeye aliyekuwa na uwezo wa
mauti, yaani huyo shetani, Heb. 2:14. Kila amwaminiye Yesu Kristo – kwake
huyo mauti pamoja na shetani wamekwishapoteza haki yao na mamlaka juu yao. Kwa
sababu mwanakondoo wa Mungu amezichukua dhambi zao – dhambi zao zote – na hivyo
akanyang’anya toka kwa mauti na shetani ile haki yote waliyokuwa nayo juu yao.
Zaidi ya hayo, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya wanadamu wote, anayo haki
juu ya wote na kwa hiyo anawaagiza watu wote mahala pote kutubu (Mtd 17:30,
tupo kule Athene Tena!). Tanga mwanzo mwa huduma yake na katika kuhubiri
Injili, Kristo alikuwa akiwasihi watu kutubu, na mitume waliendeleza ujumbe huo
huo Mk 1: 14-15; Mtd 2:38. Je, hawa waandishi wa kisasa wanasema kwamba wanaume
na wanawake hawawezi kutubu mpaka kwanza roho zile za kienyeji katika taifa
ziwe zimefungwa? Je hiyo ndiyo sababu iliyowafanya watu wa Kapenaum washindwe
kutubu kwa sababu Kristo ameshindwa kuzifunga roho hizo juu ya Kapenaumu?
Mafundisho haya hayaleti maana yoyote ile katika Agano Jipya! Yesu Kristo
alizivunja mamlaka na uwezo pale msalabani kwa sababu alibakia pasipo dhambi,
na bado akazibeba dhambi za ulimwengu wote na ufufuo wake ni muhuri kamili wa
wokovu wetu, 1Kor.15:12–22. Akiwa amemnyang’anya shetani ule uwezo wake, Kristo
sasa anaweza kupanua kwa neema ya Mungu ule uwezo wa uzima wake yeye mwenyewe
akawapa hao wamwaminio. Akiwa amewasafisha kutokana na dhambi. Yesu pia
anavunja ile milki ya dhambi katika maisha yetu kwa uwezo wa ufufuo wa uzima
wake ndani yetu.
“Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo” kwa sababu shetani pamoja
na uwezo wake wamehukumiwa na amezitangua pale msalabani. Kwa maneno mengine,
huwezi kumlaumu shetani – hakuna popote inapohesabu hivyo! Sawa ni hakika kuwa
shetani anawaweka watu katika giza, dhambi na vifungo – hiyo ina maana wale
watu ambao hawaamini. Na yeye huja kunyang’anya, kuiba na kuharibu maisha ya
watu. Lakini sasa, kwa sababu ya Kalvari huwezi tena kusema kuwa, njia ya
kumwendea Yesu imefungwa kwa watu mpaka kwanza zile roho za kimaeneo zizuiazo
ziwe zimefungwa! Jambo kama hili linabatilisha tu yale yote ambayo Kristo
alilkuja kuyafilia. Hapana, wajibu unaangukia juu yako wewe na mimi kuiamini
injili. Kama hatuamini Injili, basi kwa vyovyote vile tutakuwa tunampatia
shetani pamoja na dhambi ile fursa na uwanja wa kufanya kazi ndani ya maisha
yetu. Na katika hali yoyote ile bado shetani ni jeshi la uovu lenye nguvu
katika ulimwengu, sawa sawa kama vile maandiko yanavyotangaza. Lakini maandiko
yanatangaza kwa sauti na kwa ufasaha kwamba Yesu Kristo amezishinda dhambi,
shetani pamoja na mauti, na akiwataka waume kwa wanawake watoroke wakawe huru
kutokana na toleo la wokovu katika yeye ambalo linawakilishwa kupitia Injili.
Kwa sababu ya mambo haya pia, Yesu alisema kuwa na hii ndiyo
kazi ya Mungu, “…. kwamba umwamini yeye aliyetumwa”, Yoh 6:29. Na kwa sababu
gani roho mtakatifu atawahukumu wanadamu kwa dhambi? Yesu anasema kuwa ni kwa
sababu, hawamwamini yeye. Yoh 6:9.
Na hii ndiyo dhambi ambayo wanaume na wanawake watahukumiwa
kwayo. Dhambi zinginezo Yesu anaweza kutuweka huru kwa sababu kutokana na kile
alicho kikamilisha pale Kalvari. Lakini njia pekee ya kuupokea wokovu huu ni
kwa kumwamini yeye; na kama hatutamwamini yeye, basi tutakuwa tumepotea. Mtume
Paulo anahitimisha kwa jinsi ya ajabu kwa ajili yetu pale katika Efeso 2:8.
“kwa kuwa mliokolewa kwa neema katika imani na hii sio kwa uwezo wenu,
bali ni kwa karama ya Mungu“. Na hawa Waefeso walikuwa ni watu wa aina
gani? Haya, Mtume Paulo anatujulisha katika ule mstari wa 1-3 wa sura hii –
kuwa walikuwa wafu kwa sababu ya makosa ya dhambi zao; waliishi kwa kuzifuata
kawaida ya ulimwengu huu na mfalme wa uweza wa aga, roho yule atendaye kazi
sasa katika wana wa kuasi! Na wakawa kama wengine walivyo, watoto wa hasira. Kwa
hiyo hapa tunawaona watu ambao wanatenda dhambi kisha wanajiridhia wenyewe,
chini ya usimamizi wa shetani na vishawishi vyake kwa sababu ya kutokutii kwao;
na kwa hiyo wapo chini ya hukumu ya Mungu. Na tunaambiwa wazi kwamba hiyo ndiyo
hali ya wale wote ambao hawataki kuamini. Lakini mambo yalibadilikaje kwa hawa
Waefeso? Haya mtu yule aitwaye Paulo, alitumiwa pia huko kwa Wamataifa ili
apate “kuwafungua macho yao” na kuwarejesha kutoka katika nguvu za giza na
kuwaingiza katika nuru; na kutoka katika nguvu za shetani waingie katika nguvu
za Mungu, ili kwamba wapate kupokea msamaha wa dhambi, Mtd 26:18. Hii ilikuwa
ni sehemu ya huduma ambayo Mungu ambaye aliyashinda mamlaka na uwezo kupitia
Kristo pale Kalvari – alimpatia Paul. Mtume Paulo hakuhitaji kujitahidi au
kupigana katika kupata huduma na mamlaka kwa kuzifunga roho za kimaeneo!
Hapana, Paulo alikuwa kati ya Wayahudi kwa muda mrefu wa miezi mitatu kwanza
kule Athene halafu akawa kwa wamataifa kwa muda wa miaka miwili, akiwa
anazungumza, anajadiliana, akichunguza na kuhubiri – na watu wengi walimgeukia
Bwana! Na hawa waefeso walipataje kuokolewa? Haya mtume Paulo anatuelezea
katika ile sura ya kwanza mstari wa 13. Walimtegemea Kristo baada ya kusikia
lile neno la kweli, injili ya wokovu wao! Ilikuwa ni kupitia Mtume Paulo
aliyeihubiri Injili ya Kristo kwao na wao wakaiamini Injili, hilo ndilo
lilliowasababishia kumgeukia Mungu wakiondokana na nguvu za shetani! Mungu
asifiwe!
Kristo alipoenda kwenye nchi yake mwenyewe, Mk 6:1-6,
hakuweza kufanya kazi zenye nguvu kwenye eneo hilo mbali ya uponyaji alioufanya
kwa watu wachache. Je hii ni kwa sababu roho ya kieneo hiyo ilikuwa ni nguvu
sana? Hapana! Biblia inatupatia sababu – inasema Yesu alishangazwa na
kutokuamini kwao. Hakushangazwa na nguvu za baadhi ya roho za
kimaeneo, isipokuwa yeye alishangazwa na ugumu wa mioyo yao na kutokuamini
kwa watu hapo. Mty 13:58 anatuambia kwamba, ” … wala hakufanya miujiza mingi
huko kwa sababu ya kutokuamini kwao“. Ni ile imani katika Kristo ndiyo
iletayo wokovu na sio kule kuzifunga roho ya kitaifa; na imani inakuja kwa
kusikia neno la Mungu – Rumi 10:17! Hivyo Yesu Kristo anatueleza katika Yohana
3:18,19:
“Amwaminiye yeye hahukumiwi, bali yeye asiyemwamini amekwisha
kuhukumiwa, kwa sababu hakuliamini jina la Bwana pekee ya Mungu. Na hii ndiyo
hukumu, ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni na watu wakapenda giza kuliko nuru,
kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.”
Sawasawa na mafundisho ya Yesu, watu wale
ambao wanakataa wasimjie na kumwamini, wanafanya hivyo si kwa sababu wanazuiwa
na roho za kimaeneo, bali kwa sababu walipenda matendo maovu yao. Mafundisho
haya ya
kisasa kwa ujumla yanasababisha kuchanganyikiwa na inaleta dhihaka kwa
mafundisho ya biblia. Yanafanya maroho ya kimaeneo yaonekana ndiyo
yanayohusika na uovu wa watu pamoja na kutokuamini. Wanataka tuelewe kuwa,
iwapo tutafanikiwa kuzifunga hizi roho za kimaeneo ndipo watu watakuwa huru
kuitikia Injili. Na hivyo makanisa yetu yataongezeka kwa kiwango kikubwa
ambacho hujawahi kukiona kabla. Hii kimsingi inachafua mafundisho ya Kristo na
ya Mitume. Hawa walimu wa kisasa wanasema kuwa ikiwa mji umeshikiliwa na
matabia ya uchoyo, kiburi, ulevi na au tamaa mbaya basi hiyo ni roho ya kieneo
ya uchoyo, kiburi, ulevi au tamaa mbaya ambayo inatawala juu ya mji huo na hiyo
inahitajika kufungwa katika maombezi ya maombi. Hakuna lolote kama hilo ndani
ya biblia. Eti nini? Kukemea roho za kimaeneo au tamaa mbaya na kisha watu
wa mji huo wataachiliwa huru kutokana na dhambi hizo? Eti nini? Kwamba tatizo
halisi sio mioyo ya watu bali ni uwezo wa roho za kimaeneo? Haya si mafundisho
ya kibiblia. Biblia inatambua tatizo halisi kuwa ni moyo wa mwanadamu mwenyewe
– au ndani ya moyo wa mwanadamu mwenyewe ndiko liliko tatizo. Tatizo sio kuwa
tunatawaliwa na roho za kimaeneo za nje yetu – hapana – bali tatizo halisi ni
dhambi iliyomo ndani ya moyo wangu mwenyewe na kule kujipenda. Tatizo halisi ni
ugumu wa moyo wangu mimi mwenyewe. Hawa walimu wa kisasa wanafikiri kuwa iwapo
utafunga “roho ya ulevi” katika eneo au jumuia ndipo nguvu ya kupendelea ulevi
itavunjwa katika jumuia na kuwawezesha watu wote kuwa huru kutokana na ulevi.
Huwezi kuifukuzilia mbali roho ya “ulevi” kutoka kwenye eneo kana kwamba hiyo
ndiyo inayowashikilia watu katika dhambi hiyo! Watu hawa wanafikiri nini?
Wanajaribu kulihamisha lengo la Injili lisieleweke kwa jamii; na lengo la Mungu
kwa ulimwengu mzima pale wanapopotosha ukweli wa Injili. Wanajaribu kung’oa
mwelekeo wa Mungu kwa wanadamu, kwa kuichepusha ile kweli. Lakini sasa unaweza
ukaihubiri Injili kwa watu wote na ikiwa kwa neema ya Mungu watu binafsi
wataitikia na kuokoka. Ndipo bila shaka utaweza kuona kupungua kukubwa kama sio
kutoweka kabisa kwa ubaya wa aina fulani kama matokeo ya watu wakigeuka kutoka
katika dhambi wakimgeukia Mungu! Mtd 19:19, 23-27. Huko Efeso watu wengi
walichoma moto vitabu vyao vya uchawi na kuabudu sanamu ya Diana yalitoweka
kimchezo tu – lakini hiyo ilitokea kama matokeo ya watu wengi kugeuka kutoka
katika dhambi zao kupitia mahubiri ya mtume Paulo (mstari wa 26)! Katika Biblia
nzima neno la Mungu huja moja kwa moja kwenye mioyo ya watu wa kuliona tatizo
halisi pamoja na kupinga limelala hapo, yaani ndani ya mioyo ya watu. Tunaweza
kutaja Yeremia 4:1-4 na Lk.13:34,35, pamoja ni mifano miwili kati ya mingi
iliyomo katika Biblia.
Ijapokukwa watu wa Mungu walipaswa kumuombea, lakini hakuna
chochote kile cha kuzifunga roho za kijiografia kana kwamba hizo zinawakilisha
jeshi linalowaweka watu katika vifungo na kuwakataza wasimpokee Mungu.
Hii tena ni msingi mwingine wa kasoro za mafundisho haya ya
kisasa – ni hatari izidiyo. Tatizo la wema na ubaya linaonekana kama ni
jitihada kati ya mambo mawili ya ulimwengu mzima au nguvu za roho
zinazopingana; na hazionekani kama zinahusika na chaguo ambalo mtu anaweza
kulifanya kama yale yaliyoumbwa kwa mfano wa Mungu! Inaonekana kana kwamba
wenye dhambi wenyewe sio tatizo halisi na hawafikiriwi kuwa wao wanabeba sehemu
muhimu katika kuokoka kwao. Hapo inaonesha kwamba mapambano hayamo ndani yao au
kwa ajili ya mioyo yao, bali ni sehemu fulani huko “angani”. Haionyeshi pia
kuwa ni dhambi zangu binafsi na kule kutokuamini kwangu, hilo ndilo tatizo,
bali inaonekana kama ninashikwa juu kwenye mashindano ya majeshi ya kiroho. Na
mimi nipo pale katikati, karibu sawa na mlengwa mjinga. Ninahitaji tu nguvu za
roho zilizo kubwa zaidi ili kuzidisha nguvu za roho ndogo ndogo kunifanya niwe
huru! Ni huzuni ya jinsi gani hiyo; kuchanganya mafundisho kwa udanganyifu kwa
jinsi gani huko? Injili ya Kristo ni uweza wa Mungu kwa kila aaminiye. Wokovu
wa roho za watu hautegemei kule kuzishinda roho za kimaeneo! Lakini hawa
walimu wa kisasa, sasa wamebuni Injili mpya ya ukombozi kupitia vita vya
kiroho!
Kama nilivyokwisha kusema katika zile makala zangu mbili, na bado
nazidi kukazia tena kuwa mafundisho hayo ni ya kimwili yanakazania kwenye mambo
ya nje na siyo mambo ya kweli ya ndani. Wanamfananisha shetani kama anayetaka
kuichukua nchi anayofikiri kuwa kama yake. Na wao wamesema kuwa hiyo ndiyo nchi
ya kijiografia! Shetani ni mungu wa dunia hii maadam hii ndiyo mazingira ya
kazi yake. Lakini kwa vyovyote vile viwavyo, iwe ni roho za kimalaika, mamlaka
za uweza uwao wowote, bado maandiko yanaiweka wazi kwamba uwanja ambao ibilisi
anapenda kuumiliki ni mioyo yetu, akili na nafsi zetu! Mapepo hawahamii kwenye
“vumbi” kavu, bali wao wanapenda kupata makazi ndani ya binadamu Mty 12:43-45.
Hawapati pumziko kwenye maeneo makavu, isipokuwa wanapenda kuishi ndani ya
watu. Na hii ndiyo “nchi” ambayo Yesu aliifilia na akamwaga damu yake ili
kutafuta nafasi ya kukaa yeye pamoja na Baba! Yoh 14:18-23. Tunatakiwa tuwe
makazi ya Mungu kwa Roho, Efe 2: 22. Kwa kupitia kuiamini Injili ya Kristo sisi
tumesamehewa na tumeingizwa ndani ya Ufalme wa Mungu kwa uzao mpya! Bali
Shetani anataka kutufanya sisi tuwe ni makazi ya roho zake, sio kupitia nguvu
za ziada za roho ya kitaifa, isipokuwa kwa kututaka sisi tuamini uongo wake
ambao anaupendekeza kwetu kwa kutujaribu ili tusimwamini Mungu na kisha
tujipendeze wenyewe. Huo ndio uwanja wa mapambano. Na katika huo uwanja wa
mapambano mioyo yetu pamoja na dhamira zetu, Mungu alionyesha pendo lake
mwenyewe kwetu sisi kwa kumtuma mwanae pekee afe kwa ajili yetu na kututaka
tugeuke mbali na matendo maovu na tuupokee wokovu wake wa bure. Hiki ni kipawa
cha Mungu!
Lakini madanganyo ya mafundisho hayo yanazidi kutumbukia
ndani zaidi. Baada ya kuwa wameamini kuwa wamekwisha kuzifunga roho za kimaeneo
zitawalazo juu ya mji, wengine wao wanawachagua “walinzi wa milangoni.” Eti
hao ni watu ambao wanapaswa kuomba ili kuzuia roho za uovu zisiweze kuingia
katika miji – hatimaye, watu hao watasimama pia kwa mbinu fulani ndani na
karibu na mji – kwenye barabara kuu ndani na nje ya mji na kuendelea! Kwa
kufanya hivyo, wanazihesabia roho za mikoa yaani wanazipatia uwezo wa kutawala
jumuia yote kana kwamba watu hawana chaguo lao katika mambo – na kwa kiasi
kwamba Injili ya Kristo haiwezi kuwafikia kwa ufasaha na kuwaokoa! Hivyo siyo
Injili ya Kristo – wanacheza michezo ya ulozi pasipo kutambua! Kwa hivyo, wao
kwa vyovyote wanaamini kwamba ikiwa utaweza kuzifunga roho hizo, basi roho ya
Mungu itatawala juu ya mkoa, basi hapo sasa watu wapo huru kuitikia Injili na
kisha Wakristo wanaweza kuanzisha utawala wa Mungu katika taratibu za jamii ya
kienyeji – kwenye mifumo mbali mbali ya serikali na jamii katika mji! Hii
inaonekana kama uanzishaji wa ufalme wa Mungu hapa dunianli na “kurejesha” nchi
kutoka katika mikono ya shetani. Hawa waombezi wapya wanachokifanya hapo
wanapigana ili kupata ardhi, vumbi na dunia ambayo ndiyo
wanayoisemea kuwa inapaswa kurejeshwa kutoka katika mikono ya shetani. Baadhi
ya hao waandishi wanayo mafundisho mengine yanaweka kwa urahisi yanaeleza
kwamba, kwa sababu ya dhambi zake katika bustani ya Adeni – Adamu alipoteza
milki ya mipaka ya nchi kwa shetani kwa kufanya hivyo, wanazipatia haki roho za
mikoa yaani wanazipatia uwezo kutawala sio tu nchi bali pamoja na watu
wanaoishi katika nchi hiyo. Wanasema kuwa Yesu alikufa pale msalabani ili
kurejesha milki juu ya vumbi hili na dunia – pamoja na mipaka ya kijiografia.
Lakini tunaelezwa zaidi na hawa waandishi wa kisasa kwamba, pale msalabani
hapakuharibu mamlaka zote pamoja na uweza wake. Hapana, tunatakiwa kutumia
uwezo ambao Bwana ametupatia sasa, ili kuzifunga roho hizi chafu zitawalazo juu
ya mkoa na kisha watu wa mkoa ule watakuwa huru kuupokea utawala wa Mungu! Hiyo
ni injili yao ya kimwili. Kulingana na mafundisho hayo, pambano la msingi sio
kwa ajili ya nafsi za watu (wauume kwa wake) isipokuwa ni mavumbi – yaani,
sehemu ya kiografia! Na mara tu tunapokuwa tumezifunga roho hizo zinazotawala
juu ya kipande hicho cha vumbi na ardhi, kwa watu wanaotembea au kuishi juu ya
kipande hicho cha vumbi au ardhi, watakuwa huru kuipokea Injili na kuingia
katika ufalme wa Mungu. Mafundisho haya ya kimwili yote yanawafunika macho watu
wasiijue kweli ya maandiko, ihusuyo asili ya dhambi, wokovu na ufalme wa Mungu.
Hebu niseme hapa, kwamba, ninafikiri sote tunajua kwamba eneo
fulani fulani au jumuia inaweza ikaingiwa na tabia fulani ya dhambi maalumu
inayoonekana kumiliki eneo hilo. Na kwa vyovyote vile, mtu yeyote anayezaliwa
katika mazingira ya aina hii, anaweza akashawishika. Na desturi hii ya dhambi
katika jumuia, na desturi hii ya dhambi bila mashaka yoyote yale, inakuzwa na
Ibilisi na anaweza kuwatumia kuchanganya upinzani wa Injili ndani ya wale
wasioamini, Mtd.19:23-28. Lakini hali hii ndivyo haswa iliovyokuwa katika
jumuia nyingi na miji ambayo mtume Paulo alitembmelea. Kulikuwepo na zinaa
inayoendelea katika miji mingi. Dini za Ulozi na Uchawi zilishikilia jumuia
fulani fulani. Kulikuwepo na uchoyo, kiburi, na uchafu. Koritho ilikuwa ni
sehemu iliyozoelea mambo ya aina hiyo. Lakini sasa kupambana na roho za
kimaeneo ili kuwaweka huru watu kutokana na tabia zao za uzinzi, mambo ya
kimwili au uchawi, jambo hili hamna msingi wowote ule wa Kibiblia.
Kwa hakika, mtume Paulo anachagua maneno kwa makini pale
anapoyaulizia makanisa ya kule Galatia – “Ni nani aliyewaloga? Mafundisho hayo
yanafanana kama ulozi na kadiri mtu anavyoendelea kujifunza mafundisho haya ya
kisasa ndivyo mtu anavyoona kwa urahisi kuwa yanafanana na kile ambacho mtu
anaweza akafikiria kuwa ni mafundisho na mtindo wa ulozi au wa Uaguzi. Kadiri
mafundisho haya yanavyozidi kuenea ulimwenguni kote, bila shaka yanaweza
kutengeneza vijitabia vyake kutoka nchi fulani hadi nyingine kadiri watu
walivyo na shauku ya mambo mapya; na katika njia tofauti. Kwa mfano; yapo
magazeti ambayo yanawahamasisha na kuwasihi wakristo wote kuomba dhidi ya roho
za kimaeneo juu ya baadhi ya miji na jiji fulani; magazeti hayo
yanajishughulisha sana katika kutafutia aina fulani ya dhambi nyingi hasa
Uchawi, ambao umefanywa katika nchi. Na kisha huyatangaza matokeo waliyoyapata
ili kwamba wakristo waweze kuomba maalumu dhidi ya roho hizi za kimaeneo,
ambazo zinafikiriwa kuhusika na matatizo ya dhambi hizi zote. Hata pia
wanawasihi wakristo watembelee maeneo fulani fulani ya kijiografia katika jiji
huku wakikemea roho chafu. Lakini vitabu vinavyoongoza ambavyo vimeandikwa
kuhusu somo hili kwa ujumla haviwahamasishi wakristo kuingia katika “vita vya
kiroho” dhidi ya roho za kimaeneo. Kinyume chake, wanaonya juu ya hayo na
watuambia kuwa ni wakristo wale waliokomaa, “na wenye karama rasmi” na wale
walioitwa ndio wanaopaswa kuingia katika mapambano hayo. Ijapokuwa bado
wanasema kwamba vita hivyo ni vya lazima kwa ajili ya kuleta mafanikio
ya uenezaji wa Injili. Zaidi ya hayo bado wanakubali kuwa jambo hili ni
kujitumbukiza katika matatizo ya bure na yenye kuogofya na ni mapambano ya
hatari yenye kuwapatia wengi misiba. Hayo yote ni sawa na kubatizwa katika
mambo ya ushirikina na udanganyifu.
Vita vya Kiroho – ni Matendo yenye Hatari?
Lakini sasa kwa nini “vita hivyo” viwe ni mambo “yenye
hatari”, kuogofya na kukuletea matatizo? Haya, wanasema kwamba wakristo “wa
kawaida” huwa hawana mamlaka na nguvu zilizo katika kiwango cha “madaraka ya
juu” ya roho za kimaeneo. Na wanazidi kutuambia kuwa kumewahi kutokea na
itaendelea kuleta msiba katika “vita” hivyo! Waandishi hawa wanatuambia juu ya
wachungaji ambao wameanguka katika dhambi “kwa sababu” ya kujiingiza kaika
“mbinu ya kiwango cha mapambano ya kiroho” (strategic – level spiritual
walfare)! Waandishi hawa wanatuelezea kuhusiana na kuvunjika kwa ndoa,
magonjwa, mambo ya kimwili, watu wanajifanyia uvunjifu juu ya Imani zao na hata
juu ya kifo – kwa sababu ya kujihusisha kwao katika aina hii ya vita! (Ikiwa ni
kweli kuwa matatizo hayo yamewazukia kwa sababu ya watu wenyewe kujihusisha
katika aina hii ya mapambano, basi litakuwa ni swali lingine lenye kuhojiana).
Kumekuwepo na michanganyiko mingi pamoja na maumivu ya moyo kutokana na
mafundisho haya kiasi kwamba kiongozi wa aina fulani ya huduma huko Amerika
ameandika kitabu kuhusiana na jambo hili kiitwacho (Needless Casualties of
War”; “Misiba isiyo ya Lazima katika Vita”, kilichoandikwa na John Paulo
Jackson, Kingsway Publications. Copyright John Paul Jackson 1999). Yeye pia
anapendelea mapambano dhidi ya maroho, lakini katika kitabu chake anaeleza
jambo fulani zuri na anaonya kuhusu kutokuwa na kiasi, ambako analaumu kuwa
ndiko kunako husika na majanga ya kutisha katika maisha ya wakristo. Lakini
sasa kule kuamini kwao juu ya imani ya kufunga roho za kimaeneo, kinawafanya
waandishi hawa wote wawe vipofu juu ya ukweli uliofunuliwa katika maandiko, nao
huuacha ukweli huo kirahisi tu na hawaonyeshi kuhusika kihalisi kwa yale
yanayofundishwa na Biblia ili wahalalishe makosa yao. Wanaeneza mafundisho
yenye kasoro, na watu wengi wanayafuata mafundisho hayo na mara zote hutumbukia
katika matatizo ya kutisha. Kwa hiyo waandishi hawa wanabuni kasoro ili waweze
kuzielezea ni kwa nini misiba hiyo! Kwa hiyo, hata mwandishi niliyemtaja
hapo juu, anaelezea kwamba “kwa kawaida” wakristo huwa ndani ya Kristo Yesu,
Kolosai 3: 3, lakini kama tutajihusisha katika aina yoyote ile ya mapambano ya
kiroho, basi hapo tutakuwa tumejiweka wazi kama shabaha kwa nguvu za mapepo na
tunaweza kudhuriwa na kuharibiwa na mapepo yale!
Anasema kwamba hata kule kuomba tu kwa Mungu kuhusiana na
nguvu za mapepo ni mtindo wa mapambano ya kiroho! Inafanana kama mbwa mwitu
kuweka kichwa chake nje ya tundu lake la usalama, hiyo inamfanya aonekane ni
chambo cha mnyang’anyi anayezurura! Hii ni aina fulani ya udanganyifu ambao
unaenezwa na hawa waandishi. Hayo ni mashambulizi juu ya mafunuo ya mandiko
kuhusiana usalama wetu na wokovu katika Kristo! Eti mimi? “Kwa kawaida” tupo
ndani ya Kristo, isipokuwa tunapojishughulisha na mapambano ya kiroho “hatuwi
tena ndani ya Kristo” au “hatuwi kabisa ndani ya Kristo”, isipokuwa tunakuwa tu
“sehemu ndani yake?” Eti mimi? Na kwamba eti tunaweza tukawa ni “shabaha”
ya roho chafu anayeweza kusababisha uvunjifu wa ndoa, maradhi na kifo ikiwa
tutakuwa si waangalifu?! Hii si kitu kingine isipokuwa ni ubatizo katika mambo
ya ushirikina na mafundisho ya ulozi. Agano jipya linafundisha kinyume cha
hayo yote; yaani inafundisha kuwa ni kwa njia ya kuenenda katika silaha
zote za Mungu tu na kupigana vita vizuri vya imani, hapo tunakaa kwa Usalama
kutokana na michezo yenye maumivu ya shetani – hivi ni vita vya kweli vya
kiroho na vinapaswa kuhusika na mwenendo wetu kiroho – na wala sio katika
kupambana dhidi ya roho za uovu katika maombi kama tutakavyoona baadaye katika
Efs.6:10 –18.
Maandiko hayafundishi wala kuhamasisha udanganyifu huu; wala
hawawezi kuingiza aina hii ya woga ndani ya moyo yetu. Tunaambiwa kuwa “yeye
aliye ndani yetu ni mkuu kuliko yeye aliye ulimwenguni” na kwamba “hakuna kitu
kinachoweza kututenga na upendo wa Mungu uliomo katika Kristo Yesu.” Na hii
Inajumlisha mamlaka zote na uwezo! Tumeketi pamoja katika Kristo Yesu mbinguni
na Uhai wetu umefichwa katika Kristo ndani yake Mungu” – mambo mengi ni yenye
kutia moyo na ahadi zake Mungu akituthibitishia Usalama na baraka zaidi ya
kingine chochote kile pale tunapotunza neno lake na kumwamini yeye. Hatusomi
chochote kihusucho kushambuliwa na maroho machafu au maisha yetu kuharibiwa kwa
sababu tu, tunaomba kama maandiko yanavyo tushauri kuomba. Biblia haikiri aina
yoyote ile ya misiba kati ya wale wanaoomba. Au je! Unaweza kupata mausia
yoyote ya maombi katika Biblia yanatuonya juu ya uwezekano wowote ule wa
misiba. Au Biblia inaelezaea kukumbukia wapi ili kuonyesha kikundi maalum na
teule cha Kikristo, ambacho wao pekee waliitwa kwenye vita maalum kwa sababu tu
kwamba mapambano hayo ni yenye hatari sana kwa wakristo wa kawaida
kuyashiriki?! Hivyo ndivyo wao wanavyofundisha, lakini hii pasipo ugumu wowote
ni kuwatumbukiza watu ndani ya nyumba ya matope ya ushirikina na makosa.
Mausia yote ya kuomba katika Agano jipya,
ni kwa waamini wote na hakuna hata mausia yanayohusu maonyo kwamba inawezekana
ikawa ni “hatari” kuomba, na kwamba aina fulani ya maombi inapaswa kushirikisha
aina fulani tu ya waamini wenye wito maalum!
Lakini hii karama maalum ni kitu gani ambacho hawa waombezi
wanamaanisha kuwa nazo kulingana na mafundisho hayo? Tunaelezwa kuwa wanapaswa
kuwa ni wakristo walio komaa na haswa wawe na karama ya kutambua majina na
tabia ya roho za kimaeneo na uwezo wa kusikia toka kwa Mungu, ambaye
huwasiliana nao ili kujua ni aina gani ya roho inaweza na inahitajika kufungwa.
Karama hizi zinafikiriwa kuwa ni za lazima katika vita vya kiroho. Kwa hiyo
waombezi hao wanaweza kutumia masiku na mawiki katika maombi wakiwa na shabaha
ya kutambua jina au aina ya roho za kimaeneo zinazotawala juu ya jiji na
wanasubiri toka kwa Mungu ili kuwaonyesha ni aina gani ya roho inayostahili
kukabiliwa katika maombi yao. Wengine wao wanashuhudia kuwa wanajisikia kuwa
wanaingia katika milki nyingine ambako wanakabiliana na roho chafu. Wakati
mwingine eti wanaweza kuziona hizi roho chafu labda kama katika maono, au
dhahiri. Yanaweza kujitokeza kama kiumbe cha kutisha, nasi tunaambiwa kuwa
“mivutano” inaweza wakati mwingine ikawa kwa nguvu. Mchungaji mmoja alivutana
ili kutia changamoto roho ya kieneo kuhusu mitaa mingapi katika mji inapaswa
kuachiliwa. (Inaonekana kuwa mitaa hiyo ambayo huyo roho mchafu aliiachilia kwa
washujaa wa maombi, basi watu katika eneo hilo wangeweza kuitikia Injili,
lakini kwa bahati mbaya mitaa ambayo roho mchafu hakuiachilia kwa washujaa wa
maombi, watu waliopo pale hawakuweza kuokoka! Au tufikirije?!). Baada ya
kufungwa kwa roho za kimaeneo (kama wanavyofikiri), mhubiri huyo anaita
mikutano ya Injili akiwaambia watu, eti sasa wamewekwa huru waitikie Injili!
Comments
Post a Comment