MAGONJWA YA KICHAWI

MAGONJWA YA KICHAWI

Na Askofu Mkuu Josephat Gwajima

Zaburi 27:“Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani? Watenda mabaya waliponikaribia, Wanile nyama yangu, Watesi wangu na adui zangu, Walijikwaa wakaanguka. Jeshi lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea, Hata hapo nitatumaini. Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana, Na kutafakari hekaluni mwake. Mradi atanisitiri bandani mwake siku ya mabaya, Atanisitiri katika sitara ya hema yake, Na kuniinua juu ya mwamba. Na sasa kichwa changu kitainuka Juu ya adui zangu wanaonizunguka. Nami nitatoa dhabihu za shangwe hemani mwake; Nitaimba, naam, nitamhimidi Bwana.”
 
Mungu huinua watu duniani kwaajili ya kutimiza makusudi mazuri ama ya ubaya`,Historia inatuonyesha Mungu aliwainua kina Petro, Paulo na mitume 120 wakatenda makusudi yao wakati wao ukapita. Baadaye Mungu akainua mtume muhamad kwaajili ya kusudi lake akasimama wakati wake na kusudi lake akapita. Akazaliwa Martin Luther king ambaye alianzisha imani ya kkkt inayoitwa (Lutheran) kanisa ambalo limeenea dunia nzima mpaka leo watu wa mataifa mbalimbali wanaabudu, alikua ni padre wa kanisa katoliki ambaye aligundua kasoro fulani ndiomaana akaanzisha imani hiyo na Mungu alimtumia sana kipindi hicho.
Lakini Mungu baadaye aliinua mfalme aitwaye Henry ambaye alianzisha kanisa, akaja mtu mwingine anaitwa Moldovan akaanzisha kanisa leo hii linaitwa Moldovans, akaja mtu mwingine anaitwa Joseph mtu mweusi alianza kule marekani alianzisha kunena kwa Lugha kulikomalizwa na baadhi ya watu.
 
CHANZO IMANI YA KIKRISTO
Imani ya kikristo imezaliwa msalabani kwenye miiba kichwani, kwenye misumari mikononi na miguuni, imezaliwa kwenye mkuki uvavuni imezalwa kwenye aibu kubwa na mateso yaliyoishia msalabani ndiomaana mpaka leo inapatwa na msukosuko bado inasonga mbele kutimiza kusudi la aliyeianzisha Yesu Kristo.
ASILI YA MAGONJWA YA KICHAWI
Kuna magonjwa yanayosemekana ni kwasababu ya kibaolojia, mtu anaweza kusema sababu hizo ni moja wapo ya magonjwa, kuna magonjwa ya kichawi ambayo yameandikwa kwenye Biblia yanatokana na nini na ikumbukwe lolote la kichawi ndilo hilohilo la kishetani, tunasema magonjwa ya kichawi sababu yanatokana na shetani na wakala zake.
 
Mathayo 4:“ Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa hawawezi, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.”
Mapepo mengi yanauhusiano ma magonjwa ya akili, ama laana, ama mikosi, ama magonjwa ya moyo, asili ya magonjwa ni mashetani yawe ni majini, mizimu au mapepo yote hayo yanaweza kusababisha magonjwa.
 
Mathayo 17:15 "Bwana, umrehemu mwanangu, kwa kuwa ana kifafa, na kuteswa vibaya; maana mara nyingi huanguka motoni, na mara nyingi majini.16 Nikamleta kwa wanafunzi wako, wasiweze kumponya. Yesu akajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa pamoja nanyi hata lini? Nitachukuliana nanyi hata lini? Mleteni huku kwangu. Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile."
Mtu huyu mtoto wake ana Kifafa alikwenda kumwomba Mungu ili amrehemu na Yesu hakuangaika na kifafa bali alimtoa pepo na mtoto akapona. Matatizo kama kifafa, balaa, presha yote haya yanatokana na chanzo.
Marko1:26 "Yule pepo mchafu akamtia kifafa, akalia kwa sauti kuu, akamtoka. Wakashangaa wote, hata wakaulizana, wakisema, Nini hii? Ni elimu mpya! Maana kwa uweza awaamuru hata pepo wachafu, nao wamtii!"
 
Mapepo yanaweza kumtia mtu kifafa, akawa mgonjwa wa kansa, akawa na laana, akawa na mikosi, balaa. Mashetani yanaweza kutumwa na mtu yakaambiwa nenda ukaingie ndani ya mtu fulani umwekee balaa, kifo na ajali. Unaweza kumwona mtu anaugonjwa wa moyo kumbe mtu huyo amewekewa ugonjwa huo na mashetani.
Marko 9:20 “Wakamleta kwake; hata alipomwona, mara yule pepo alimtia kifafa; naye akaanguka chini, akagaa-gaa, akitokwa na povu. "26" Naye Yesu akiona ya kuwa mkutano unakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena. Akalia, akamtia kifafa sana, akamtoka; naye akawa kama amekufa; hata wengi wakasema, Amekufa. Lakini Yesu akamshika mkono akamwinua naye akasimama."
 
Kazi ya pepo wanaweza kukuangusa chini, ukashanga umepatwa na ugonjwa wa harufu mdomoni au sehemu nyingine hata ukinawa vizuri sababu asili ya pepo ni uchafu ndiomaana wanaitwa pepo wachafu, mtu anaweza akawa anatokwa na mate mdomoni, au mwoga, maana yake yanaweza kumfanya mtu aonewe na asiweze kufanya maamuzi ya kujitetea akakaa kimya. Hii ndio kazi ya mapepo
Unaweza ukawa umewekewa magonjwa sana, unaweza kuwekewa na roho ya kukataliwa na watu ukawekewa sana mapepo ya ugonjwa lakini usiogope sababu Mungu yupo anaweza kukufungua kwa jina la Yesu.
Ukiri
“Kwa jina la Yesu kuanzia leo kila ugonjwa wa kishetani hauna nguvu juu yangu”

Pepo hubwaga chini. Pepo anaweza kutumwa akabwage chini mahusihano ya ndoa, pepo anaweza kubwaga chini biashara. Kila anguko unaloliona linasababu yake.
 
WALIOTUMWA
Duniani Kuna watu walikuja Duniani kwasababu maalum, hata leo hii kuna watu wametumwa kwaajili ya kuanguka kwa wengi kulingana na jinsi watakavyowatendea na kuinuka kwa wengi kulingana na jinsi watakavyowatendea. Mungu huwa anatuma watu miaka baada ya miaka, watu hao huja duniani kwaajini ya kusudi maalum, watu hao wana majina kama wengine, wanaongea kama wengine lakini wametumwa kwaajili ya kusudi fulani na watu hao hawawezi kufa mpaka kusudi lao liwe limetimia.
 
MAPEPO YA MAGONJWA
Kuna magonjwa yanayotokana na uchawi na ushirikina mtu anaweza kuwekewa bila yeye kujua.
Mathayo 9:32 "Hata hao walipokuwa wakitoka, tazama, walimletea mtu bubu mwenye pepo. Na pepo alipotolewa, yule bubu alinena, makutano wakastajabu, wakasema, Haijaonekana hivi katika Israeli wakati wo wote."
Huyu mtu alikua anamatatizo mawili, kwanza alikua bubu na pili alikua kipofu. Pepo alipotolewa ule ububu wake uliondoka, Yesu hakuangaika na ububu wake bali alihangaika na Pepo la ububu, tunajifunza kumbe kuna mtu anaharibu mimba kumbe amewekewa mapepo ya kutoa mimba ile. Kuna uwezekano kabisa mtu anakutumia mashetani ili yakuharibu wewe na maendeleo yako, mfano kwa kukutenganisha na watu wa muhimu wa kukusaidia. Unaweza kutumiwa pepo ambalo linaweza kukutenganisha na ndoa yako.
“Kwa jina la Yesu nakataa mapepo yote yaliyotumwa kwenye maisha yangu na ndoa yangu”.
Ukishughulika na matokeo ya matatizo huwezi kuyamaliza matatizo yakaisha, ukitaka kuua mti wa maembe huwezi kuumaliza kwa kukata matawi yake na kuvuna maembe yake, unatakiwa uchimbe mti mzima uungoe mizizi yake yote.
Marko 9:17 - 25
Mtu anaweza akawa na jini na hili jini anatumiwa na wasiompenda likasababisha ububu, kimwi, kansa, kupooza, lakini tumeona jinsi Yesu alivyomtendea huyu pepo ndani ya mtu huyu kwa kumtambua na kumwamuru amtoke. Kumbe tunaona magonjwa ya kichawi yapo na mapepo haya yakitolewa uzima unapatikana kabisa.
Luka 11:14 "Naye alikuwa akitoa pepo bubu; ikawa pepo alipotoka, yule bubu akanena, makutano wakastaajabu."
 
Jini anaweza kumwingia mtu, akimwingia mtu, mtu huyo aweza akashindwa kuongea, anaweza akapatwa na kansa, ukimwi, kupooza n.k
Luka 13:“ Siku ya sabato alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo. Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu muda wa miaka kumi na minane, naye amepindana, hawezi kujinyosha kabisa. Yesu alipomwona alimwita, akamwambia, Mama, umefunguliwa katika udhaifu wako. Akaweka mikono yake juu yake, naye akanyoka mara hiyo, akamtukuza Mungu. Basi mkuu wa sinagogi alikasirika kwa sababu Yesu amemponya mtu siku ya sabato, akajibu, akawaambia mkutano, Kuna siku sita zifaazo kufanya kazi, basi njoni mponywe katika siku hizo, wala si katika siku ya sabato. Lakini Bwana akajibu akasema, Enyi wanafiki, kila mmoja wenu, je! Hamfungui ng'ombe wake au punda wake siku ya sabato katika zizi, aende naye kumnywesha? Na huyu mwanamke, aliye wa uzao wa Ibrahimu, ambaye Shetani amemfunga miaka kumi na minane hii, haikupasa afunguliwe kifungo hiki siku ya sabato? Aliposema haya wakatahayari wote walioshindana naye; mkutano wote wakafurahi kwa sababu ya mambo matukufu yaliyotendwa na yeye.”
 
MAPEPO YA UDHAIFU
Mapepo yanayoleta udhaifu yanaweza kumwingia mtu yakakaa ndani yake mda wa miaka 18. Mtu unakua mdhaifu hujui unaumwa kichwa au mwili mzima, mtu anakua hajiskii vizuri hana raha kumbe anapepo la udhaifu, (kwenda kanisani haina umuhimu bali cha muhimu unakwenda wapi) ni lazima ukutane na Yesu kanisani ili akusaidie.
 
KUTANA NA YESU AKUPONYE
Zakayo alikua mfupi sana alishindwa kumwona Yesu akaamua kupanda kwenye mkuyu ili amuone Yesu, bahati nzuri Yesu alipita kwenye mkuyu ule akamwambia atakua mgeni wake, Tunajifunza Jambo la muhimu ni kujua ‘mkuyu’ upi Yesu anapita leo sababu ‘mikuyu’ ipo mimngi duniani, (Ufufuo na Uzima ni mkuyu ambao Yesu yupo na anasaidia watu wote bila kubagua.)
Tumeona huyu mwanamke ambaye amepindishwa udhaifu wake.

Ukiri
“kwa jina la Yesu mahali popote ambapo kwenye maisha yangu pamepinda napanyoosha kwa jina la Yesu”
 
KUFUNGWA KICHAWI
Mtu anaweza kufungwa bishara kichawi asifanikiwe, mtu anaweza kufungwa kichawi kazini akabaki palepale, mashetani wanaweza kufunga, majoka wanaweza kufunga, mizimu inaweza kufunga mtu na maisha yake, majini pia yanaweza kufunga na kuharibu maisha ya watu.
Anakuwepo mtu ambaye hakupendi ambaye yeye mwenyewe ni mshirikina, unapokuwa vizuri unafanya kazi ya Mungu kuna watu lazima utawagusa na kuharibu kazi zao. Matendo 16 Paulo aliponya watu ambao walikua wakitumika kuwanufaisha wafanya biashara wa miji kupata fedha, walitaka kumuua kwasababu aliharibu madhabahu zao za kupatia fedha, leo hii Kuna watu ukiwaona utajua wataenda mbali sana au wataangamia kwa jinsi walivyo na wanayoyafanya.
Ibrahimu alikua hazai yeye na mkewe wakaja wakazaa baaada ya miaka 90 akazaliwa Isaka na Yakobo na Uzao wa Israeli ukatokea kwao, kuna mwingine amezaliwa ana kipawa cha kusaidia watu akikitumia kwaajili ya utukufu wa Mungu anafanikiwa na hata asipokitumia kwaajili ya utukufu wa Mungu bado kitafanya kazi sababu Mungu akikupa kipawa hakunyanganyi lakini utakutana naye siku moja katika hukumu.
Mtu mwingine anaona kwenye tumo lako kuna nyota ya kuzaa mtoto wa aina Fulani, anatuma mashetani ukiwa bado mdogo ili usifanikiwe kuzaa mchungaji au mfanya biashara mkubwa au kiongozi wa nchi. Kama ilivyokua kwa Ibrahimu aliambiwa atamzaa Isaka akiwa bado kijana lakini alikuja kumzaa akiwa mzee.
Kuna mashetani yanaweza kutumwa kwa mtu ili kumfunga asifanikiwe kufanya kusudi lake hapa duniani, mtu mkubwa hawi mkubwa bali anakua tayari amezaliwa ili aje awe mkubwa kutokana na asili ya kipawa chake.
 
USHAURI KWA WASICHANA AMBAO HAWAJAOLEWA
“Ukitaka kuanza maisha angalia mtu mwenye akili nzuri ambayo inamaono mbele usiangalie mtu mwenye mafanikio tayari ana gari na nyumba na kilakitu, kwa mfano ukila yai na mwingine akila kuku yupi ambaye amekula zaidi? Jibu ni aliyekula Yai sababu amekula mpaka manyoya ya kuku, amekula mpaka utumbo wa kuku na kinyesi chake lakini Yule aliyekula kuku amekula nyama peke yake, hivyo kuna watu wanaishi kwa staili ya kula kuku. Usihangaike na watu wenye mafaniko tayari bali simama na mtu mwenye kesho nzuri, mtu mwenye akili nzuri ya kesho yake. Ukianza kuangalia huyu ananini basi mtu yule ataanza kukutengenezea sura ya yale unayoyataka ili akuoe baada ya mda mfupi unakuta yote aliokufanyia ni maigizo na kilichounganishwa na Mungu mwanadamu asikitenganishe unabaki na kidonda cha maisha yako, simama imara usihangaike Mungu yupo pamoja na wewe” 
 
VIFUNGO VYA SHETANI
Kwahiyo shetani anaweza kufunga uso. Shetani na malaika zake na wachawi wanaweza kuona ubunifu ulioko ndani yako wakakufunga ushindwe kuwaza, kila mtu anacho cha kipawa ama kwenye mikono, au kwenye moyo, au kwenye miguu ama kwenye kinwa, Mungu ameweka Baraka kwenye mikono ya watu, lakini unakuta mtu mgonjwa wa mikono, mikono inakua inatoka jasho hawezi kuandika, inatetemeka unakuta mtu anaugonjwa ambao hauponi hospitalini kumbe amewekwa mapepo, lakini Yesu alikuja duniani ili kuvunja kazi hizo zote za shetani na kuwaweka watu huru.
Kuna miguu ya watu wengine imebarikiwa wakifatilia jambo lazima wapate kile wanachokifatilia, watu waliobarikiwa miguu wengi huwa wanafungwa miguu yao inakua inauma sana, ni lazima wafungue kwa kusema kwa vinywa vyao kwamamlaka ya jina la Yesu.
 
NAMWACHIA MUNGU
Hakuna neno namwachia Mungu kwenye Biblia, Mungu ametupa sisi mamlaka yote ya kutenda hapa duniani, ukitamka neno linakua vilevile kama ulivyosema, wewe ndiyo tawi la Ufalme wa Mungu hapa Duniani, ukikanyaga wewe amekanyaga Mungu, ukingoa amengoa Mungu, ukiteketeza wewe ameteketeza Mungu, ukiponda wewe ameponda Mungu, ukitamka wewe ametamka Mungu, kwenye nyumba ya Ufufuo na Uzima hakuna neno ambalo linasema namwachia Mungu sisi ni majeshi ya Bwana tunayo mamlaka ya kungoa, kubomoa, kuharibu na kujenga na kupanda tunayo mamlaka ambayo Yesu ametupa .
 
ROHO YA MAGONJWA
Majini ama mashetani wanakua wametumwa na watu kuharibu maisha ya watu wengine, yeyote yule unayemwona mgonjwa anadhiki au shida nyuma yake kuna roho imetumwa ya kumwangamiza, haiwezekanin mtu amesoma shule akamaliza elimu yake isimsaidie kuendeleza vipawa vyake akafanikiwa, ni mtu amemtumia mapepo wachafu waharibu kichwa chake asiweze kuchangamka akapata kazi au akafanya biashara, haiwezekani mtu ameharibiwa maisha yake na mizimu ya familia ili asifanikiwe abaki vilevile akienda kaisani ni lazima watu wawe huru kutoka kwenye vifungo hivyo kwa jina la Yesu.
Kuna watu wanakuloga sio kwasababu wana uadui na wewe hapana, bali kuna kitu kikubwa Mungu ameweka ndani yako wanazuia kisitimie kwasababu kitaonekana na kuwa msaada kwa watu wengine wanaogopa na kuona wivu.
 
MUNGU HAPENDI TUWE MASKINI
2 Wakorintho 8:9 Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.
 
MUNGU WA IBRAHIMU NDIYO MUNGU WETU
Mwanzo 13:2 "Naye Abramu alikuwa ni tajiri sana kwa mifugo, kwa fedha, na kwa dhahabu."
Isaya 45:3 "nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni Bwana, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli."
Zaburi 24:1 "Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake. "
 
MATESO YOTE YANAYOWAPATA WATU HAYAJATOKA KWA MUNGU
Maombolezo 3:31 Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu Hata milele. Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake. Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha."
 
TAMKA KWA KINYWA CHAKO
 
Shetani kazi yake ni kufunga na kuwatesa wanadamu lakini Mungu hapendi mtu ateseke kwenye biashara, kwenye ndoa bali yupo anaye asababisha mateso yale. Unatakiwa ukate hali uliyonayo kwa kutamka kwa mamlaka ya Jina la Yesu. Mungu hutendea kazi kile unachokisema kutokea kwenye kinywa chako, Desturi ya Mungu atakachokisikia unasema ndicho atakacho kitenda, akikusikia unasema kwa jina la Yesu Sitalogwa, nitafanikiwa, nitasafiri, nitapata mtaji, sitaonewa, sitataabishwa, nitaolewa/oa nitasimama basi itakua vilevile kama ulivyotamka kwa jina la Yesu. Sisi tumeubwa kwa sura ya Mungu, Mungu aliumba dunia kwa kusema na ikawa, sisi ni watoto wa Mungu tunachokisema kwa vinywa vyetu ndicho Mungu anakitenda, ndiomaana ukitamka kwa kinywa chako Yesu ni Bwana na mwokozi wa maisha yao unakua umeokoka kutoka kwenye Ufalme wa giza na kuingia kwenye Ufalme wa nuru kwa kutamka tu.
 
FARASI NA MPANDA FARASI
 
“Ukimuua mpanda farasi ukamwacha Farasi baadaye atakuja mtu mwigine kumpanda huyo farasi, vilevile ukimwangamiza farasi na mpanda ukamuacha baadaye atapanda farasi mwingine lakini Ukumuua mpanda farasi na farasi utakua umemaliza kazi. Akili kubwa kuliko zote duniani ni kujua cha kufanya, wakati wa kukifanya na nini cha kufanya kwa wakati huo.”
 
KUSUDI LA KUISHI
 
Kila mtu anayosababu ya kuishi hapa duniani kulingana na kipawa alichopewa na Mungu akitumie kimnufaishe atajirike, wengine wamepewa moyo, wengine akili, wengine mikono, wengine sura, wengine miguu, wengine vinywa wote hao wamepewa vipawa hivyo ili viwanufaishe, wengine hawajui vipawa vyao ndivyo vitakavyowafanya waweze kufanikiwa wanahangaika na mambo mengine.
Yesu anasema adui wa mtu ni Yule wa nyumbani mwake, Musa alikua na ndugu yake anaitwa Miriam huyu ndiye alipanga mpango mbaya juu yake, Daud alikua na mtoto wake aitwaye Absalom huyo ndiye aliyemsaliti, Dothan, Abiram na Kora hawa walikua chini ya Musa wakamsaliti, Yesu kristo alikua na mitume 12 na kati yao alitokea mmoja aitwaye Yuda aliyekua karibu yake sana akamsaliti na wote hawa mwisho wao ulikua wa kufanana, ndiomaana Yesu akasema adui mkubwa wa mtu ni Yule wa nyumbani mwake.
 
MAMA JUSI WA MASHARIKI
 
Mathayo 2:
Hao mamajusi walitokea mashariki ya mbali walimfuata Yesu wakasema wameiona nyota yake, hapa tunajifunza kwamba kila mtu ana nyota yake, pia nyota ya mtu inaweza kuonekana, pia nyota ya mtu inaweza kufuatwa, pia nyota ya mtu inaweza kuibiwa,pia nyota ya mtu inaweza kurudishwa kama imeibiwa. Nyota ya mtu ni kama kipawa, kazi ya shule ni kuendeleza kile kipawa ulichowekwa na Mungu ndani yako, mafanikio hayapatikani kwenye elimu sababu ingekua hivyo waalimu wangekua matajiri sana mafanikio ni kujua kipawa chako ni kipi na kukitumia.
Ukiri
“Kwa jina la Yesu Bwana nifungue macho nimjue anayenitumia mashetani ya magonjwa“.

Wachawi wanauwezo wa kuona nini kipo ndani ya mtu wakakiiba au kukizuia kisidhihirike kama mtu hajaokoka. Wanakua wanafunga tumbo au mikono au macho au akili, wanaweza wakaachia kila kitu kikaenda sawa lakini wakazuia kipawa kisikufanikishe ubaki vilevile. Leo hii simama urudishe vyote vilivyoibiwa na kuharibu magonjwa ya kichawi kwa jina la Yesu.
 
MUNGU NI MUNGU WA KURUDISHA

Wana wa Israeli walichukuliwa utumwani Misri Miaka zaidi ya 400 Mungu akawarudisha, Wana wa Israeli walichukuliwa utumwanin miaka sabini Mungu akawarudisha, wana wa Isralei walichukuliwa utumwani nchi za ulaya Mungu akawarisha wakawa taifa kamili mpaka leo hii wapo, Mungu anasema “Nitakurudishia miaka yako iliyoliwa na nzige na madumadu na tunutu” Mungu anasema

“Nitakurudishia afya yako” usiogope simama imara utapona kwa jina la Yesu. Simama kwa ujasiri tamka kwa kinywa chako haribu magonjwa ya kichawi juu yako na familia yako kwa jina la Yesu Amen.
 
 

Post a Comment

0 Comments