Roho Mtakatifu ni nani?



Roho Mtakatifu ni nani?

Roho Mtakatifu ni Mungu, mwenye nguvu zote, maarifa yote, anayepatikana kila mahali. Yeye anayo nafsi na ameamua kuishi ndani ya mwili wa mwanadamu. Kusudi kubwa la ujio wake ni kuwa Msaidizi wa mwanadamu kwenye ulimwengu huu wa mwili, ili kumsaidia kuishi katika mapenzi ya Mungu.

Roho Mtakatifu amemamua kuishi ndani ya mwili wa mtu kwa sababu, Mungu ana namna ya  kutawala kwenye ulimwengu wa kimwili bila kuwa na mwili wa damu na nyama, kwa kuwa yeye ni Roho (Yohana 4:24). Hivyo hana budi kuingia kwenye mwili wa mtu na kufanya makao yake hapo, ili kutawala na kumuongoza mwanadamu katika mapenzi yake. (Yohana 14:23, Yohana 14:18, Ufunuo 3:20, 1Wakorinto 3:16-17, 6:19).

Kinachotusaidia kujua kwamba Roho Mtakatifu ana nafsi, ni tabia zake, maana kwenye kila nafsi kuna hisia, nia, kumbukumbu, akili nk. Baadhi ya sifa na tabia za Roho Mtakatifu ni; anapatikana kila mahali (Omnipresence), Zaburi 139:7, ana maarifa/anajua yote (Omniscient, Intelligence), 1 Wakorinto 2:10-11, ni mwenye nguvu zote/wa umilele (Omnipotent),Mwanzo 1:2, ni Mtakatifu, Luka 11:13, ana hisia (Waefeso 4:30, Mwanzo 6:3) – Wala msimuhuzunishe Roho wa Mungu…, Roho yangu haitashindana na Mwanadamu milele, ana nia (will), 1Wakorinto 12:11 – Hutenda kazi kama apendavyo.

 Kazi za Roho Mtakatifu

1.Kufundisha, Mwalimu (Yohana 14:26) … Atawafundisha yote…
2.Kuongoza, Kiongozi (Warumi 8:14, Yohana 16:13) – Atawaongoza awatie kwenye kweli yote, wote wanaoongozwa na Roho hao ndio … Mfano (Matendo ya Mitume 13:4, Acts 8:29)
3.Ni mfunuaji wa mambo/mafumbo/siri za Mungu (1Wakorinto 2:10) – Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote. Usipoteze muda kumtaka Mungu akufunulie siri zake, wewe mwambi Roho Mtakatifu hiyo ndiyo kazi yake.
4.Muombezi (Warumi 8:26) – Roho hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.
5.Mtoa/mpasha habari za mambo yajayo (Yohana 16:13f) – Na mambo yajayo atawapasha habari yake.
6.Ni msemaji wa mambo ya Mungu/Yesu (Yohana 15:26, 2 Petro 1:21) – Yeye atanishuhudia (he will speak about me), Wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
7.Ni mtetezi/msemaji wa mambo yetu (Marko 13:11) – Kwa maana si ninyi msemao, bali ni Roho Mtakatifu.
8.Ni mkumbushaji wa yale uliyojifunza au uliyoagizwa na Mungu (Yohana 14:26)… Atawakumbusha yote niliyowaambia.
9.Kutia/kuwapa nguvu watu wake nguvu/uwezo (Matendo1:8) – Lakini mtapokea nguvu akisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu…
10.Kuuhakikisha (convict, make aware, sadikisha) ulimwengu kwa habari ya dhambi, haki na hukumu (Yohana 16:8) e.g unajuaje kwamba kuna hukumu? Warumi 8:16
Summary

Naam kazi hizi za Roho Mtakatifu zinatufikisha mahali pa kujua kwambajukumu lake kubwa ni kuwa Msaidizi wa mwanadamu. Kufanyika msaada wa mwanadamu katika mambo hayo hapo juu pale mwanadamu atakapohitaji msaada huo.  Hivyo ni jukumu lako kumpa nafasi kwa kuboresha mahusiano yako na yeye ili akusaidie. Hata hivyo Roho Mtakatifu kuitwa Msaidizi haina maana kwamba ndio umvunjie heshima, bali fahamu kwamba, Roho Mtakatifu ni Msaidizi kwa namna ambayo bila yeye mimi na wewe hatuwezi kutenda neno lolote.

Kazi hizi zinatupa kujua kwamba Roho Mtakatifu yupo tayari kutusaidia katika kila eneo la maisha yetu. Ni jukumu letu kumpa  nafasi hiyo na kutambua kwamba bila msaada wake sisi hatuwezi lolote. Watu wengi leo hawaoni msaada wa Mungu kwao kwa sababu ya kutokumpa Roho Mtakatifu nafasi ya kuwasaidia katika maisha yao na pia kwa kutokujua maeneo ya kumtumia Roho Mtakatifu kama Msaidizi.

Je, unahitaji msaada wa Roho Mtakatifu eneo gani la maisha yako?, ni ndoa, kazi, madeni, huduma, kanisa, utawala nk mpe nafasi akusaidie, akufundishe na kukuongoza katika kweli yote. Kumbuka yeye ni Mungu ambaye ni Mwalimu na Kiongozi pasina yeye mimi na wewe hatuwezi neno lolote. Unataka kumjua Mungu, kuwa na maombi yenye matokeo mazuri na kufanikiwa katika maisha yako kiroho na kimwili pia mwambie Roho Mtakatifu akusaidie.

Msaada wa Roho Mtakatifu hauna mipaka maadam unahitaji msaada katika yale ambayo ni mapenzi ya Mungu. Hivyo haijalishi unapita katika jambo gani mpe nafasi Roho Mtakatifu akusaidie. Na ili uweze kuthamini msaada wa Roho Mtakatifu jifunze siku zote kufikiri kwa dhana kwamba bila msaada wake wewe huwezi lolote, na kwa sababu hiyo utaona umuhimu wa yeye kukusaidia katika maisha yako.

Usisubiri mambo yako yaharibike au usiachague mambo unayofikiri magumu ndio umshirikishe akusaidie, yeye anataka kuwa Bwana wa maisha yako, akusaidie kwa kila kitu hata mambo madogo kabisa kwenye maisha yako. Kina-muumiza Mungu kuona watoto wake chini ya jua wanahangaika katika maisha yao, wakati yeye amemleta Roho Mtakatifu ili awasaidie katika maisha hayo. Tumia vizuri fursa ya Roho Mtakatifu sasa maadam anapatikana, kuna wakati hatapatikana.

Jinsi ya Kumpokea na kujazwa Roho Mtakatifu.

Unapokwisha kutubu na kuokoka inabidi uombe ili Roho wa Mungu aje juu yako. Kuna njia mbili za maombi ya kujazwa Roho Mtakatifu.

 Kuomba mwenyewe

Ukishaokoka unaweza kuchukua hatua ya imani na ukaomba mwenyewe ili ujazwe Roho Mtakatifu. Kitabu cha Luka 3:21-22 imeandikwa hivi “Ikawa watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, naye anaomba, mbingu zilifunuka; Roho Mtakatifu akashuka juu yake…” Hapa tunaona kuwa Yesu baada ya kubatizwa alichukua hatua ya kuomba mwenyewe, na alipokuwa katika kuomba ndipo mbingu zikamfunukia Roho Mtakatifu akaja juu yake.

Luka 11:13 imeandikwa hivi; “Basi ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba yenu wa mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?”Maneno haya yanatufundisha kuwa ujazo wa Roho Mtakatifu ni kipawa unachoweza kukiomba kwa Baba wa mbinguni. Unauhuru wa kimaandiko kusimama mwenyewe na kujiombea ujazwe Roho Mtakatifu.

 Kuombewa na watumishi waliopakwa mafuta

Mungu ameweka utaratibu wa watu kujazwa Roho Mtakatifu kwa kuombewa na watumishi wa Mungu waliopakwa mafuta kwa huduma ya Roho Mtakatifu. Matendo 19:1-7, inatuonyesha kuwa kubatizwa bila kumpokea Roho Mtakatifu haitoshi kukukamilisha kwa ajili ya ufalme wa Mungu. Paulo aliwakuta watu ambao tayari walishabatizwa kwa maji, lakini hawakujazwa Roho Mtakatifu. Paulo anawauliza; Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini?
Ni swali ambalo linamhusu kila mtu anayeamua kumfuata Yesu Kristo. Hebu na wewe jiulize swali hili; je ulipokea Roho Mtakatifu ulipoamini? Watu wa kipindi kile cha akina Paulo walijibu wakasema hata kusikia kuwa kuna Roho Mtakatifu hatujawahi. Leo hii wengi sana tumesikia habari za Roho Mtakatifu lakini ni wachache sana ambao wamejazwa Roho Mtakatifu na wanatembea naye.

 Kufunga

Ishara za (kumpokea) na kujazwa Roho Mtakatifu
1.    Kunena kwa Lugha
2.    Utakuwa tayari kwa ajili ya vita vya kiroho dhidi ya ulimwengu (1 Yohana 2: 15-17); dhidi ya mwili (Wagalatia 5: 16-17); na dhidi ya Shetani (1 Petro 5: 7-9; Waefeso 6: 10-13)
3.    Maisha yako kuonyesha zaidi na zaidi ya tunda la Roho (Wagalatia 5:22, 23) na itakuwa zaidi na zaidi kufanana na Kristo (Warumi 12: 2; 2 Wakorintho 3:18) 
4.    Maisha yako ya maombi na kujifunza Neno la Mungu litakuwa na maana zaidi. Wewe uzoefu nguvu zake katika kushuhudia (Matendo 1: 8).
 
1.Mungu ni No1 katika maisha yako. Unaweza kuwa mtumishi wa Mungu na mawazo yako ya kila siku, harakati na vitendo shaka kuwa reflection ya kwamba. Mungu atakuwa No1, hakuna maelewano. Wewe wanaweza au kuwa na ufahamu wa hayo, lakini wengine hasa wale walio karibu na wewe. Badala ya kulenga binafsi wewe ni kufahamu kwamba wewe kuwa chombo juu ya dunia hii kwamba yeye ni kufanya kazi kupitia kufikia nje ulimwenguni katika hali ya kimwili.(Warumi 10:13 Kwa kuwakilaatakayeliitia jina la Bwana, ataokolewa.),( Yohana 14:26
Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisheni kila kitu, na kuwakumbusha yote niliyowaambia, yo mimi nimewaambia ninyi.)
 
2. Mabadiliko ya Maisha Kabla na Baada kuna tofauti. Mambo na mwenendo wa njia zako za zamani kuanguka mbali. utu mpya itakuwa na njia tofauti ya kuona mambo na kuwa na malengo tofauti na malengo. mabadiliko inaweza kuwa makubwa au inaweza kuwa polepole, kila hali ni tofauti.( 2 Wakorintho 5:17
 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya, mambo ya kale yamepita; tazama, mambo yote yamekuwa mapya.)
 
3. Zawadi. Karibu wote watakuwa na Utambuzi. Hii ni kutolewa na ni bidhaa muhimu katika akiba ya Mkristo alieokoka ambaye ana Roho Mtakatifu. wengine itakuwa moja au baadhi au labda yote ya yafuatayo: Teaching, kuhubiri, unabii
, kuponya, Kunena Kwa Lugha. Jambo moja utakuwa kupokea bila kujali ni huwezi kuwa na hofu ya kifo! (2 Timothy: 1: 7
Kwa maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi., Yohana 10:28Na mimi nawapa uzima wa milele; nao hawatapotea milele, wala hakuna mtu atakayeweza kuwatoa mkononi mwangu.)
 
3. Moyo uliopondeka. You kuhisi maumivu na mateso ya wengine. Utakuta ni vigumu kutembea nyuma mtu anayeishi kwenye mitaa bila angalau kutambua yao. Utakuwa kilio au hata kulia zaidi kuliko alivyofanya kabla na wakati mwingine juu ya mambo ya ajabu. moyo waliotahiriwa tajwa katika kale na jipya(Wagalatia5: 24. Na hao walio wa Kristo wameisulubisha mwili pamoja na upendo na tamaa.)
 
4. Mateso. Watu watajaribu kukuweka wewe chini au mbaya kwa utii wako wazi kwa Mungu mwingine ila wewe itaendelea kufuata Bwana hata kama wewe wanakabiliwa taabu au udhalimu kwa kufanya hivyo, hata kifo. Roho Mtakatifu nitakupa imani kabisa unshakable kuvumilia matukio kama hayo
 
5. Ushirika. Utakuwa kutafuta ushirika wa watu wengine walio kama wewe mwenyewe, kwa sababu wewe kutambua mambo unaweza kufanya na kusema na mambo unaweza kuona itafanya watu wengi kuhisi wasiwasi, kwa hiyo kushirikiana na wakristo ambao ni kama wewe mwenyewe ni kuhitajika na muhimu.
 
6. Uelewa kwamba miili yenu ni hekalu: Kama ungekuwa mla chakula Junk, utakuwa tena ukata au kuepuka chakula kama au hata kupoteza ladha kwa ajili yake. Utakuwa dhahiri kufahamu kwamba mbinu utakatifu mwili wako na akili lazima kama safi kama iwezekanavyo.( 1 Yohana 4: 13
Hili tunafahamu ya kuwa tunakaa ndani yake, naye ndani yetu, kwa kuwa ametushirikisha Roho wake.)
 
7. Uinjilisti: Utakuwa inaendeshwa kueneza na kushiriki Neno katika sura yoyote au fomu. Wale ambao ni bila kufafanua nia utakuwa na maswali na kutafuta nje na kuwa inayotolewa na wewe, kutafuta majibu maisha bila hata kujua kwamba wewe ni Mkristo. Kimsingi wewe kutembea kama Yesu alitembea, ushahidi mwingine kwamba wewe ni waliojawa na Roho Mtakatifu!
 
8. Maombi na Ibada. Utakuwa na juhudi sana kuwaomba kuabudu na kumtukuza Bwana juu ya angalau kila siku, mara nyingi hata wakati wa mchana. maisha ya maombi: Unaweza kuona Bwana wa wazima msukumo wewe kuomba kwa ajili ya mambo fulani au watu na kujibu maombi yako. Utakuwa na uhusiano binafsi na Bwana, mtu hawezi kubadilishwa na mtu yeyote alifanya huduma kusema maneno kabla ya     scripted(Muswada) (Yohana 10:27 Kondoo wangu huisikia sauti yangu, nami nawajua, nao hunifuata)
 
9. Hofu ya Bwana: Unaweza kuwa na Mtumishi wa Mungu lakini pia ni ufahamu wa hofu overpowering yake kama huna kufuata sheria zake, amri na sheria ambazo ni pale kwa sababu nzuri, lakini pia kufahamu yeye siku zote inatoa onyo wakati wewe ni kupotea kutoka "njia nyembamba("John: 3: 24
Naye azishikaye amri zake hukaa ndani yake, naye ndani yake. Na katika hili tunajua kwamba yeye anaishi katika muungano nasi, na Roho ambayo yeye ametupa.)
 
10. Roho anajua roho. Utatambua wengine walio na Roho na wao kutambua wewe. Wewe kuja kutambua kuna si kama wengi duniani kama watu wengi wanadhani na itakuwa kama mkutano familia wa karibu ambaye hawajaona katika miongo kadhaa.( 1 Yohana 4: 6
Sisi ni wa Mungu Yeye amjuaye Mungu atusikia; yeye asiyetokana na Mungu hatusikii. Katika hili twamjua Roho wa ukweli na roho wa uongo.),(Wagalatia5:25. Kwa kuwa tunaishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.)
 
 
 
 
 
 
 



Post a Comment

0 Comments